Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

Alialikwa na Msigwa
 
M

Mkuu, with due respect, sisi wengine tunaomfahamu Paschal hatukubaliani kabisa na unayoyasema hapo juu. Give due where it belongs. Paschal ni mmoja kati ya waandishi wazuri sana hapa Tanzania. Lakini hapa wengi tunamsifu kwa sababu ameuliza maswali ya msingi kabisa. Nafiriki kama mwanasheria, ameuliza maswali yanayolenga pia kuondoa dukuduku la yeye kutoelewa (Kama Mwanasheria) mamlaka anayotumia Rais yanatoka wapi katika Katika ya nchi. Ni maswali yake ni ya msingi (Objective) kwa sababu majibu yake ni lazima yawe na references (toa quote kwenye katiba ambayo umeapa kuilinda). Lakini kwa sababu ya ubabaishaji wetu, tunataka kila kitu kuingiza siasa za maji taka.
 
Kwa hiyo tunaweza kusikia kuwa katika kesi zinazopelekwa mahakama ya mafisadi inaweza kutokea kesi yenye maslahi makubwa kwa nchi akaamua kuwa yeye atakuwa Jaji kwa vile yeye ni kila kitu?
 
Hongera sana kiongozi. Wewe ndo nimekuelewa sana... tofauti na wale wengine
 
IQ za watu zipimwe jaman ha ha ha ha ha ha kiklichoulizwa hakujibiwa mayalla oyeee Pascal Mayalla umekandamiza mwanawane kwa tulioenda shule tumepata feedback nyingi sana katika irrelevant answers !!hana mshauri na akiambiwa hawasikilizi watu mbaya zaidi nchi inataka iongozwe kwa utashi wake na sio katiba
 
Safiiii jamaa kauliza bila uwoga kuhoji anatumia mamlaka yapi cha ajabu anajibu kwa vijembe
kwa tulioenda shule ukifungua tu mdomo kujibu tunapata feedback nyingi sana ,kwanza jamaa anadhani nchi inaenda kwa utashi wake na sio katiba ,pili inaonyesha anashauriwa ila hawasikilizi watu ndo maana ali panic sana aliposikia swali in short ni irrelevant answers
 
Christine Amanpour na wa aina hiyo, hao ni wa kimataifa sana. leo walikuwa wa kitaifa,,
 
Hizi ni akili uchwara kamwambie basi huyo kwanza aanze kuwanyoosha wachochezi Wastaafu akina Warioba, Mwinyi na Butiku.
Hivi mkuu BAK, kama DU kashindwa kujibu maswali ya mtu kama Paskal anayeuliza kwa nidhamu na ka woga kidogo ataweza kweli kukabiliana na waandishi makini kama wa CNN au BBC ambao huwa hawana woga wala unafiki kama alivyokuwa anajibishana nao Ben? Naanza kujisikia aibu kabla hajaenda
 
Reactions: BAK
KUMBE RAISI ANALIDHIBITI HATA BUNGE, SASA LINAISIMAMIAJE SERIKALI WAKATI LIKO CHINI YA RAISI.
 
Nahisi Paskall Mayalla atakuwa amejihisi vibaya sana
 
Ningelkuwa mshauri wa Rais, ningemshauri mambo mengine apige kazi kimya kimya. Nchi hii iko nyuma sana. Hapaswi kutoa uhakikisho kwa jambo lolote kwani ana miaka 10 tu. Ajenge misingi mizuri ya uchumi endelevu, lakini si kutoa uhakikisho kwamba ataacha nchi ya viwanda. Pili, ningemshauri pia awe Rais wa wote. Kwa sasa anaonekana ni Rais wa wana CCM zaidi. Hata anapoongea anaonekana wazi bado na ile "Sisi" na "Wale" huku wakati huo huo akisisitiza uchaguzi umekwisha na yeye ni Rais wa wote. Pengine anafanya hivyo kwa kuwalenga akina Mbowe, Lissu n.k, lakini kwa maoni yangu, kama Rais wa nchi, hapaswi kuonyesha kitu hicho kabisa. Hiyo awaachie akina Kinana na Sendeka.
 
mayala oyeeeeeeee zizonje ali sema baada ya kujibu swali kisanii
 
kwa jinsi alivyo jibu ni dhahiri kwamba Mh. rais anatumia madhaifu ya katiba yetu inayompa mamlaka makubwa kufanya chochote wakati wowote so kwa nn hataki katiba mpya tena ya warioba!?
 
Though alijibiwa kisiasa sana ila aliuliza swali la msingi sana
 

..inaelekea jpm haelewi dhana ya separation of powers ya hii mihimili mitatu.

..yes, serikali ndiyo yenye vyanzo vya fedha. Lakini serikali haiwezi kutumia fedha hizo bila bajeti kupitishwa na BUNGE.

..Vilevile bunge linatunga sheria. Lakini mhimili wa MAHAKAMA ndiyo unaotafsiri sheria hizo na kutoa haki kwa wananchi.

..matatizo mengine yanatokea kwa kutokuelewa taratibu za kikatiba na kisheria. Kwa hili tunapaswa kumuombea.

Cc Pasco, Nguruvi3
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…