Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

Swali ni hilohilo Pascal alitafsiri tu ndomana mkuu hakujishughulisha na hiyo part b ya pascal kwa kuwa alishajibu
 
Wana JamiiForums,

Nimejaribu kutafakari mantiki ya RAIS kuelezea maana ya neno "MAYALA" kwamba ni "NJAA" badala ya kujikita kwenye kujibu swali, lengo lilikua ni kulipunguza nguvu swali au nini?
 
Swali ni hilohilo Pascal alitafsiri tu ndomana mkuu hakujishughulisha na hiyo part b ya pascal kwa kuwa alishajibu
Kabisa mkuu, ila sasa doubt ya wadau inakuja eti Mh. Kashindwa kujibu swali la pili na kumpa credit zote Mayalla.
 
Kwani swali la pili la Pasco ambalo halikujibiwa ni lipi ??
 
Wana jamii forum nimejaribu kutafakari mantiki ya RAIS kuelezea maana ya neno "MAYALA" kwa mba ni "NJAA" badala ya kujikita kwenye kujibu swali ,lengo lilikua ni kulipunguza nguvu swali au nn??
Lengo ni kutafsiri fullstop hayo mengine ni mawazo yako binafsi!
 
Wana jamii forum nimejaribu kutafakari mantiki ya RAIS kuelezea maana ya neno "MAYALA" kwa mba ni "NJAA" badala ya kujikita kwenye kujibu swali ,lengo lilikua ni kulipunguza nguvu swali au nn??
Duh, ile ya 4:1 inathibitika kila kukicha.
Kuna formula yoyote ya kujibu lile swali?? Ebu watanzania tujaribu kujiongeza na tuache ujinga maana hii ni makusudi sasa.
 
Kama anawafahamu na yeye ndio mkuu wa nchi kwann asiwaagize takukuru wawashughulikie?. Maana hiyo ni rushwa,akili za kumbiwa ..........?
Kwani Pascal Mayalla anasifiwa humu tu JF??
Hujaona kwenye vijiwe vya kahawa, FB, Twitter kote huko akisifiwa??
Au nako alijinasabaisha kua anafanya kazi huko??
 
Hakuwa na majibu na lile swali lakini pia lile swali lilimuudhi sana.
Kifupi swali lilimvua nguo hadharani.
Kumbukeni rais wetu ni mtukufu huwa hapendaji maswali ya kuudhi.

Na tukiendelea kuuliza uliza tusishangae Pascal Mayalla akikamatwa kwa uchochezi.
 
Paschal anasifiwa kwa kuwa aliuliza swali kwa kiswahili bali Awami kwa kiingereza! Paschal alieleweka vizuri bali Awami hakueleweka kwakuwa wabongo wengi kiingereza chaliiiiii! Ngumbaru irudishwe!

Mh!!!! Bora nikalale
 
Sami alisema inaonekana au kusemekana. Kuanza na lugha yoyote hapo ni uoga tayari. Pasco Mayalla hakuchepusha lugha, aliuliza moja kwa moja kuwa ulipata wapi na kwa sheria ipi ambayo aliapa kuilinda ilimwambie azuie mikutano ya siasa na kuwazuia wabunge wasisafiri.

Ukitazama vizuri swali la Pasco lilimeza lile la Sami. Ndio maana tunampongeza Pasco. Hata Tido pia aliuliza kwa namna hiyo hiyo ya kudhani, kuonekana wakati hawakupaswa kufanya hivyo. Ukweli wa mambo upo
 
Mbona katiba inaipa bunge nguvu ya kumwajibisha rais endapo atakiuka maadili au kuvunja katiba? Ndio maana Mzee Butiku alisema hatuhitaji rais TEMBO!
Rais anaweza vunja Bunge lakini Bunge ni lazima lipitie kura na akidi 2/3 kutokuwa na imani na rais. Kwa Tanzania hii haiwezi kutokea ikiwa tumepigania Katiba mpya ili kupunguza nguv za rais halafu bado mnataka kufananisha bado nguvu za serikali na Bunge. Kiongozi wa chama ndiye kiongozi wa serikali. rais ndiye mkuu wa majeshi, ndiye humchagua Jaji mkuu na kifupi kwa njia za nyuma ndiye hata humchagua Spika kwani yeye ndiye mwenyekiti wa chama tawala. Ana kinga ya uongozi wake hata baada ya.

Kama asingekuwa na nguvu zaidi ilikuwaje UKAWA mkamtaka Magufuli amwondoe Naibu Spika Bi. Tulia? kama hana nguvu zaidi kwa nini UKAWA walitaka aingilie swala la Uchaguzi mkuu wa Zanzibar? Ikiwa hana mamlaka zaidi kwa nini JK analaumiwa kuharibu katiba mpya? In reality tunajua ukweli ni upi lakini tunataka kuzunguka mbuyu jangwani..

Hizi habari za Bunge jamani tusidanganyane. Miaka yote tumekuwa tukilalamika humu kuhusu Bunge letu lisilokuwa na meno. Na sababu mojawapo ya Kuitaka Katiba mpya ni kulipa Meno, sasa lina meno tayari kilichotakiwa kuongezwa ni nini? Wabunge wote ni wanachama wa vyama na wana kiongozi wao iwe Magufuli au Mbowe. Atakachosema Magufuli kama rais au Mwenyekiti hakuna mbunge wa chama chake atakayepindua.

Na atakachosema Mbowe (mwenyekiti wa Chadema na UKawa bungeni hakuna mbunge wa Ukawa atakaye pindua. Ukileta za kuleta unanyang'anywa tu uanachama huo Ubunge umekufa. Mifano ipo tumeshuhudia mengi tayari leo mseme ati Bunge lina mamlaka zaidi ya Serikali? Kwa nini mnachanganya sana manen haya? Kutoingiana katika shughuli zao haina maana kila muhimili una nguvu sawa...
 
Truth JPM can't take constructive criticism without getting angry. Huo ndio ukweli.
 
kukamatwa tena...
 
Anamjua Vizuri Alivyokuwa Bingwa Wa Kutukana Humu Na Kujipendekeza Kwa Lowassa Mwaka Jana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…