Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

Swali ni hilohilo Pascal alitafsiri tu ndomana mkuu hakujishughulisha na hiyo part b ya pascal kwa kuwa alishajibu
 
Wana JamiiForums,

Nimejaribu kutafakari mantiki ya RAIS kuelezea maana ya neno "MAYALA" kwamba ni "NJAA" badala ya kujikita kwenye kujibu swali, lengo lilikua ni kulipunguza nguvu swali au nini?
 
Swali ni hilohilo Pascal alitafsiri tu ndomana mkuu hakujishughulisha na hiyo part b ya pascal kwa kuwa alishajibu
Kabisa mkuu, ila sasa doubt ya wadau inakuja eti Mh. Kashindwa kujibu swali la pili na kumpa credit zote Mayalla.
 
Kumekuwa na dhana kuwa mtu pekee aliyeuliza swali la msingi kwa Mh. Rais ni Mayalla pekee. Ni kweli anastahili pongezi kwa swali lake bora kabisa.

Lakini pia kuna mtu mmoja aliuliza swali ambalo ukikaa na kufikiri zaidi ni suala ambalo ndilo lililo hot kwa sasa, na wapinzani pamoja na wanaharakati wamekuwa wakilipigia kelele. Swali liliulizwa na mwandishi wa BBC "SAMI AWAMI" Lilikuwa liki dai "INAONEKANA RAIS ANATUMIA KUKANDAMIZA DEMORASIA KWA EXCUSE YA MAENDELEO, HASA BAADA YA KUZUIA MIKUTANO YA WAZI YA VYAMA VYA SIASA"

Leo hii tumesahau na huku tulikolalamika kila kukicha kuwa rais anakandamiza uhuru na haki ya kufanya siasa, uhuru wa kujieleza, Uhuru wa kutoa maoni.

Mimi kwa upande wangu nilimuelewa sana huyu mtu. Nadhani Pasco amekuwa popular kwa kuwa tu alijinasabisha kuwa ni member wa JF, ndio maana leo tumesahau watu wengine makini kama hawa kuwapa credit na kutoa airtime zaidi kujadili hoja zao.

Nawasilisha.
Kwani swali la pili la Pasco ambalo halikujibiwa ni lipi ??
 
Wana jamii forum nimejaribu kutafakari mantiki ya RAIS kuelezea maana ya neno "MAYALA" kwa mba ni "NJAA" badala ya kujikita kwenye kujibu swali ,lengo lilikua ni kulipunguza nguvu swali au nn??
Lengo ni kutafsiri fullstop hayo mengine ni mawazo yako binafsi!
 
Wana jamii forum nimejaribu kutafakari mantiki ya RAIS kuelezea maana ya neno "MAYALA" kwa mba ni "NJAA" badala ya kujikita kwenye kujibu swali ,lengo lilikua ni kulipunguza nguvu swali au nn??
Duh, ile ya 4:1 inathibitika kila kukicha.
Kuna formula yoyote ya kujibu lile swali?? Ebu watanzania tujaribu kujiongeza na tuache ujinga maana hii ni makusudi sasa.
 
Uko sahihi kabisa kwamba Pasco (Paschal Mayala) amekuwa popular kwa kuwa alieleza kuwa ni mwana JF...sasa baadhi ya wanaJF wanamuona kuwa eti yeye ndiye aliyeuliza swali zuri kuliko wote...na hii pia ni kwa sababu wako baadhi ya wana JF wanaoona kuwa JPM anakiuka katiba na 'kuiburuza' mihimili mingine....Lakini kwa maoni yangu waandishi wa habari wote waliuliza maswali mazuri kabisa...Dk. Rioba kwa mfano na hata Tido maswali yao yalikuwa mazuri kabisa. Lile la Dk. Rioba la kumtaka/kumuomba JPM ajipime mwenyewe kuhusu utendaji wake katika kipindi cha mwaka mmoja na pia jambo.mambo gani yanamuumiza kichwa yalikuwa mazuri kabisa...hata yule dada aliyekuwa amekaa karibu na Suzan Mungy/Mongi??? naye aliuliza maswali mazuri kabisa moja likiwa la human interest linalomtaka/linalomuomba Rais aeleze jambo gani anapendelea (baada ya saa za kazi?)....maswali kuhusu nchi ya viwanda nayo yalikuwa mazuri kama la Joseph Kulangwa...na maswali yote ya Tido Mhando yalikuwa mazuri likiwemo lile la kinachoitwa tendency ya udikteta ya Rais...kwa ujumla maswali yalikuwa mazuri kwa wote na hata la comrade Muhanika wa MOAT...

Isipokuwa binafsi nimekuwa disappointed namna magazeti 'yalivyopotezea' maelezo ya Rais kuhusu swali la Muhanika....kimsingi katika swali la Muhanika maelezo ya Rais yalikuwa kama ifuatavyo: Tuache Bunge wajadili muswada huo yeye hawezi kuingilia; Muswada huo ukipitishwa yeye ataupitisha/kusaini siku hiyo hiyo kuwa sheria (Rais hakuonyesha unafiki kabisa katika hili); wadau wamekuwa nao suala la muswada huu since 2011 lakini bado tu wanataka miezi mingine mitatu; wako watu wakiwemo wamiliki wa vyombo vya habari wanaoshinikiza kukataliwa kwa muswada huu na baadhi yao wanafahamika na wanatumia fedha na tunawafahamu, waandishi wa habari waache kutumika; muswada huu ni kwa maslahi yao waandishi wa habari....
Kama anawafahamu na yeye ndio mkuu wa nchi kwann asiwaagize takukuru wawashughulikie?. Maana hiyo ni rushwa,akili za kumbiwa ..........?
Kwani Pascal Mayalla anasifiwa humu tu JF??
Hujaona kwenye vijiwe vya kahawa, FB, Twitter kote huko akisifiwa??
Au nako alijinasabaisha kua anafanya kazi huko??
 
Hakuwa na majibu na lile swali lakini pia lile swali lilimuudhi sana.
Kifupi swali lilimvua nguo hadharani.
Kumbukeni rais wetu ni mtukufu huwa hapendaji maswali ya kuudhi.

Na tukiendelea kuuliza uliza tusishangae Pascal Mayalla akikamatwa kwa uchochezi.
 
Paschal anasifiwa kwa kuwa aliuliza swali kwa kiswahili bali Awami kwa kiingereza! Paschal alieleweka vizuri bali Awami hakueleweka kwakuwa wabongo wengi kiingereza chaliiiiii! Ngumbaru irudishwe!

Mh!!!! Bora nikalale
 
Kumekuwa na dhana kuwa mtu pekee aliyeuliza swali la msingi kwa Mh. Rais ni Mayalla pekee. Ni kweli anastahili pongezi kwa swali lake bora kabisa.

Lakini pia kuna mtu mmoja aliuliza swali ambalo ukikaa na kufikiri zaidi ni suala ambalo ndilo lililo hot kwa sasa, na wapinzani pamoja na wanaharakati wamekuwa wakilipigia kelele. Swali liliulizwa na mwandishi wa BBC "SAMI AWAMI" Lilikuwa liki dai "INAONEKANA RAIS ANATUMIA KUKANDAMIZA DEMORASIA KWA EXCUSE YA MAENDELEO, HASA BAADA YA KUZUIA MIKUTANO YA WAZI YA VYAMA VYA SIASA"

Leo hii tumesahau na huku tulikolalamika kila kukicha kuwa rais anakandamiza uhuru na haki ya kufanya siasa, uhuru wa kujieleza, Uhuru wa kutoa maoni.

Mimi kwa upande wangu nilimuelewa sana huyu mtu. Nadhani Pasco amekuwa popular kwa kuwa tu alijinasabisha kuwa ni member wa JF, ndio maana leo tumesahau watu wengine makini kama hawa kuwapa credit na kutoa airtime zaidi kujadili hoja zao.

Nawasilisha.
Sami alisema inaonekana au kusemekana. Kuanza na lugha yoyote hapo ni uoga tayari. Pasco Mayalla hakuchepusha lugha, aliuliza moja kwa moja kuwa ulipata wapi na kwa sheria ipi ambayo aliapa kuilinda ilimwambie azuie mikutano ya siasa na kuwazuia wabunge wasisafiri.

Ukitazama vizuri swali la Pasco lilimeza lile la Sami. Ndio maana tunampongeza Pasco. Hata Tido pia aliuliza kwa namna hiyo hiyo ya kudhani, kuonekana wakati hawakupaswa kufanya hivyo. Ukweli wa mambo upo
 
Mbona katiba inaipa bunge nguvu ya kumwajibisha rais endapo atakiuka maadili au kuvunja katiba? Ndio maana Mzee Butiku alisema hatuhitaji rais TEMBO!
Rais anaweza vunja Bunge lakini Bunge ni lazima lipitie kura na akidi 2/3 kutokuwa na imani na rais. Kwa Tanzania hii haiwezi kutokea ikiwa tumepigania Katiba mpya ili kupunguza nguv za rais halafu bado mnataka kufananisha bado nguvu za serikali na Bunge. Kiongozi wa chama ndiye kiongozi wa serikali. rais ndiye mkuu wa majeshi, ndiye humchagua Jaji mkuu na kifupi kwa njia za nyuma ndiye hata humchagua Spika kwani yeye ndiye mwenyekiti wa chama tawala. Ana kinga ya uongozi wake hata baada ya.

Kama asingekuwa na nguvu zaidi ilikuwaje UKAWA mkamtaka Magufuli amwondoe Naibu Spika Bi. Tulia? kama hana nguvu zaidi kwa nini UKAWA walitaka aingilie swala la Uchaguzi mkuu wa Zanzibar? Ikiwa hana mamlaka zaidi kwa nini JK analaumiwa kuharibu katiba mpya? In reality tunajua ukweli ni upi lakini tunataka kuzunguka mbuyu jangwani..

Hizi habari za Bunge jamani tusidanganyane. Miaka yote tumekuwa tukilalamika humu kuhusu Bunge letu lisilokuwa na meno. Na sababu mojawapo ya Kuitaka Katiba mpya ni kulipa Meno, sasa lina meno tayari kilichotakiwa kuongezwa ni nini? Wabunge wote ni wanachama wa vyama na wana kiongozi wao iwe Magufuli au Mbowe. Atakachosema Magufuli kama rais au Mwenyekiti hakuna mbunge wa chama chake atakayepindua.

Na atakachosema Mbowe (mwenyekiti wa Chadema na UKawa bungeni hakuna mbunge wa Ukawa atakaye pindua. Ukileta za kuleta unanyang'anywa tu uanachama huo Ubunge umekufa. Mifano ipo tumeshuhudia mengi tayari leo mseme ati Bunge lina mamlaka zaidi ya Serikali? Kwa nini mnachanganya sana manen haya? Kutoingiana katika shughuli zao haina maana kila muhimili una nguvu sawa...
 
Truth JPM can't take constructive criticism without getting angry. Huo ndio ukweli.
 
Hakuwa na majibu na lile swali lakini pia lile swali lilimuudhi sana.
Kifupi swali lilimvua nguo hadharani.
Kumbukeni rais wetu ni mtukufu huwa hapendaji maswali ya kuudhi.

Na tukiendelea kuuliza uliza tusishangae Pascal Mayalla akikamatwa kwa uchochezi.
kukamatwa tena...
 
Anamjua Vizuri Alivyokuwa Bingwa Wa Kutukana Humu Na Kujipendekeza Kwa Lowassa Mwaka Jana
 
Back
Top Bottom