Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

Truth JPM can't take constructive criticism without getting angry. Huo ndio ukweli.
swali la jamaa wa bbc kuhusu demokrasia na la tido kuhusu udikteta kidogo yamtoe kwenye reli....alimeza mate kwanza,jasho likatoka na moyo ukadunda
 
Mkulu ni wale watu wapenda utani ambao yeye kukutania ni chochote,wewe kumtania eti unatakiwa uufanyie interview utani wako. wanaboaje!!!!!!
 
Mayala oyeee (njaa oyeee) mtegamee njaa hii awamu
 
Mkuu Kimbunga, utakuwa ama hufuatilii au umeamua tu kujenga hoja kwa kusimamia kile alichojibu rais. Si kweli kwamba watu hawakuhoji au kuuliza mheshimiwa Rais alipoipa hela mahakama. Kulikuwa na mjadala mkali sana uliojielekeza katika hofu ya Rais kuingilia uendeshaji wa kesi. Suala la kubana matumizi halia tatizo, na wananchi wanaunga mkono, wanachohoji wananchi, na bila shaka Mayala alisaidia wananchi kuhoji kiko wazi. Maswali yako ya mwisho sioni mantiki yake katika hoja ya msingi!
Siamini kama watu walihoji suala la Rais kuipa hela mahakama watu walihoji kauli ya Rais kuhusu kuiahidi mahakama kiasi fulani cha pesa ambacho kingetokana na hukumu za mahakama. Hiyo ndio ilikuwa hoja ambayo nami naikubali. Maswali yangu ya mwisho hapo ni kutaka kuonyesha kwamba Rais anaweza kuingilia kwa njia hizo ambazo zipo kikatiba. Katika nadharia ilikuwa kwamba mihimili ifanye kazi bila kuingilia hata kidogo lakini hiyo haiwezekani ndio wakaja na kitu inaitwa checks and balances. Ukisoma sheria za katiba utaligundua hilo.
 
Hilo mkuu ni tatizo la kikatiba. Katiba ndiyo inampa mamlaka rais kuteua majaji badala ya kufanyiwa vetting. Lakini rais hana mamlaka ya kumfuta jaji kazi, hilo nalo liko kikatiba. Wanaunda tume yao wenyewe ya kuwajibishana.
Asante mkuu kwa kunielewesha,nilidhani kwa kuwa ana mamlaka ya kuwateua
ana mamlaka ya kuwafuta kazi.Lakini kudhani kwangu kunatokana
na matendo ya baadhi ya majaji kuisigida taaluma kwa matakwa
ya waliowateua,kama wako huru kiasi hicho,mbona haya yanatokea?
 
Watu wanapolilia katiba mpya mnawaambia katiba haina maana yoyote
Mkuu waliokuwa wanaitetea hiyo katiba mpya
tayari wamewekwa kapuni,hapo tena kuna katiba mpya
au tutapata kitabu kipya?
 
Asante mkuu kwa kunielewesha,nilidhani kwa kuwa ana mamlaka ya kuwateua
ana mamlaka ya kuwafuta kazi.Lakini kudhani kwangu kunatokana
na matendo ya baadhi ya majaji kuisigida taaluma kwa matakwa
ya waliowateua,kama wako huru kiasi hicho,mbona haya yanatokea?
Mkuu hata mimi sielewi uwoga wao unatoka wapi! Ni kweli baadhi ya mambo hufanywa kwa kumpendeza aliyewateua. Lakini ukweli ni huo hawezi kuwafuta kazi. Unakumbuka scandal ya escrow, wale majaji waliopewa mgawo na Ruge JK alisema wazi kwamba hao wana utaratibu wao wa kuwajibishana, hata kwenye tume ya maadili hawakuitwa.
 
Mkuu hata mimi sielewi uwoga wao unatoka wapi! Ni kweli baadhi ya mambo hufanywa kwa kumpendeza aliyewateua. Lakini ukweli ni huo hawezi kuwafuta kazi. Unakumbuka scandal ya escrow, wale majaji waliopewa mgawo na Ruge JK alisema wazi kwamba hao wana utaratibu wao wa kuwajibishana, hata kwenye tume ya maadili hawakuitwa.
🙂🙂🙂 Mkuu huyu aliyepita si tunasema iliharibu!!!
 
.....
.....Moderators huu Uzi ugandishwe kwa Heshima ya member wetu kulibeba Bango LA J4 kishujaa
 
Kamuuliza kuwa kapata wapi mamlaka ya kuzuia safari za watumishi nje wakati kuna mihimili mitatu na yote inajiongoza yenyewe?

Pia kwanini mikusanyiko ya kisiasa inatambulika na katiba lakini yeye kaizuia wakati aliapa kutumikia nchi kwa mujibu wa katiba?

Kama wangekuwepo hata watano tuu wenye mwelekeo wa Pasco hakika angependa hayo masaa mawili yaishe aondoke, lakini kwa vile waliopo wengi ni makanjanja basi kawaambia waulize mpaka wachoke wenyewe.
Mmh! Navyomjua rais wetu hakika huyu jamaa teyar kashakalia kuti bovu hivyo muda wowote utaskia kapigwa chini/Katumbuliwa JIPU!

Hapo ndio utajua Ukisema kweli kwenye mambo yamsingi yakisiasa ya Taifa letu basi tambua Status yako ni lazima figisufigisu zifanyike ili ISHUKE...
Dah! Babu Seya
Yangu macho....
 
Habari za jioni wana JF wenzangu!

Naomba nichukue fursa hii adimu kujadili upande wa pili wa swali linaloonekana na baadhi ya watu kuwa NI swali bora kuliko maswali yote ya wahariri walipokutana na Mhe. Rais wa JMT Dr. Magufuli.

Kwanza naomba kusema kuwa halikuwa swali bora hata kidogo bali lilijaa mihemuko na wanaolishabikia wamejaa mihemuko. Sio analytical question hata kidogo kwa sababu zifuatazo:-

1. Halikuwa na background information ya nini kimefanyika ili uweze kukipinga vizuri
2. Halikuwa na any kind ya data kulipa backup ya mtu aliyeenda shule
3. Halikutoa madhara yoyote ya hatua za kubana safari za nje! Hivyo kukosa uhalali wa kuzitetea
4. Pascal Mayall ni kati ya watu waliomtukana Rais Kikwete kuwa ni VASCO DAGAMA kwa masafari lukuku
5. Ameshindwa kuelewa nafasi ya Mhe. Rais ktk mihimili mitatu
6. Ameonesha kuwa ni "MSEMAJI WA WAPIGA DILI"

Kwa muktadha huu, naomba sasa nije kwenye majibu ya Mhe. Rais

Rais ni kiongozi katika mihimili yote mitatu (BUNGE, MAHAKAMA, SERIKALI) kwasababu zifuatazo:-
- Kitendo cha kwenda kuhutubia Bunge na kutoa direction ya nchi
- Kitendo cha Mahakama kuomba pesa za kuendeshea kesi kinaonesha wanamtegemea kama kiongozi wao
- Yeye ni Pay Master General (PMG)
- Yeye ndie anayeteua majaji nk

Hivyo basi kitendo cha Paskali Mayalla kujinasifu kuwa ndie aliyeuliza swali bora kuliko wahariri wote ni dharau kubwa kwa waandishi wenzie wa habari.

Unafiki mkubwa wa huyu bwana unajitokeza anapowaambia wenzake hawakutakiwa kumuona kama Rais. Hivi huyu Paskali anapokaa na baba yake mzazi kuna saa anamuona kama house boy au shamba boy??????

Hivi angeuliza lile swali kwa tone ya kawaida angepungukiwa nini?? Kweni ukiongea kwa kufoka ndio vyombo vya habari vya nje vitakuona na kukupa kazi?? Huko nje wenzake wanaheshimu Ma Rais wao!!!

Huyu Ndugu ni wakupuuzaaaa!!! Jina lake ni Njaa na Njaa imepanda kichwani!! APUUZWEE NA KUSAMEHEWA!!!

Jioni Njema.

Mimi Ndugu yenu.

Queen Esther
 
Hiri ri nchi ni rikubwa sana, sijui kwann wote mnabanana kwa mtogore
 
mayala oyeeee
aisee this is a tragedy of the century. sijawahi ona kitu kama hii. acha safar za nje zisiendeke ni aibu mno.
 
Back
Top Bottom