Hongera serikali kusikia kilio cha tozo

Pongezi kwa waanzilishi wa tozo? Hamna tatizo walilotatua hapo.
 
Kachawa tena ka damu ya mzee kama wale chawa wa zile za VIP wanafuata rangi ya pindo lake na rangi yake inakua ivo ivo. Bora chawa mweusi wa kwenye nywele nyeusi kichwani hana kigeugeu
 

Hiyo danganya toto ndio unasema sikivu? Eti tozo imetolewa kwenye muamala wa kibenki usiozidi 30,000! Katika marekebisho ya hivyo unadhani kuna wajinga wa mtawapata?

Watu wanalipa kodi, na kama ni kidogo basi ujue huo ndio uhalisia. Hizo tozo hatutaki. Kauzeni zile raslimali mnazosema tunazo mpaka wazungu wanatuonea wivu. Hayo mambo ya kulipa tizi ili mkazunguke na maVX/R hatuko tayari.

Kuanzia sasa viongozi wote waondolewe matumizi ya VX, watumie magari ya chini ya 50m, misururu ya viongozi kwenda kufanya show off ifikie mwisho. Wafanyakazi kwenye miji yenye kundi kubwa la watumishi wa serikali, waende kazini kwa mabus. Vikao visivyo na tija iwe mwisho.
 
Tozo sio mzigo, bila tozo baadhi ya miradi ya kimaendeleo haiwezi kutekelezeka, keep that in mind.

Uzeni zile raslimali, ile list ya vituo vya afya mmetoa kuhalalisha makusanyo ya tozo, ni uongo wa mchana kweupe. Tunataka jedwali la kweli likionyesha vituo vya afya vilivyojengwa wakati tozo imeanza, ikionyesha thamani ya mradi, muda wa mradi kuanza, mkoa, wilaya na tarafa mradi ulipo.

Hatuoni sababu ya sisi kukamuliwa tozo wakati tunalipa kodi kibao. Tunataka mkauze hizo raslimali mnazosema tunazo, ili kutuondolea hizi tozo zisizo na kichwa wala miguu.
 
Tozo sio mzigo, bila tozo baadhi ya miradi ya kimaendeleo haiwezi kutekelezeka, keep that in mind.

Miradi ipi nyau we[emoji23][emoji23][emoji23] madarasa? Hayo mwanzo tuliambiwa pesavza uviko au unajisahaulisha sasa hivi!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…