mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,897
- 18,477
Tutumie uzi huu kuipongeza Simba kwa kumpatia Mgunda nafasi ya kuwa kocha mkuu wa Simba. Naamini kabisa kuwa Mgunda almaarufu kama Gurdiola Mnene ataifanyia Simba maajabu ambayo hatujawahi kuyapata kwa makocha Wazungu.
Angalizo langu ni kuwa isitokee hata kidogo kuwa simba wamempa nafasi hiyo kama namna ya kubana matumizi kwa kumpa mshahara mdogo!
Hiyo itakuwa ni laana. Kama ambavyo mishahara ya makocha wa kigeni huwa inawekwa wazi (na huu ndiyo utamaduni wa kwenye soka), tunaitaka Simba iweke hadharani mshahara wa mgunda kama Kocha Mkuu wa Simba! Tusisikie eti mnampa vi milioni 10 - 20 huo utakuwa ni uchawi na kutaka kunyanyasa makocha wazawa! Napendekeza kuwa Mgunda apewe mshahara si chini ya kocha yeyote wa kigeni aliyeifundisha Simba hivi karibuni!
Nawasilisha!