Hongera TRL kwa Mabehewa Mapya. SGR ni Reli Mpya ya Kisasa; Je, Mabehewa Haya ni Mapya ya Kisasa? Hakuna Ubaya Kutumia Mitumba, Ila Tuambiwe Ukweli!

Chombo chochote kinachokwenda mwendo kasi ninakushauri usinunue mitumba, tatizo la mabehewa yakitumika zaidi ya muda wake mabehewa huanza kutoka na kurudi kwenye reli hii ni hatari kwa abiria, wanapokarabati wanajaribu kuaraini ili yasitoke na kurudi kwenye reli na hilo ndilo muhimu kuliko viti, vyoo na madirisha, lakini kuna lamuhimu zaidi ni viungio kati ya behewa na behewa yaani zile seheme zenye maturubai kama ya akodiani ya muziki au kwenye mabasi ya mwendokasi.
Serikali inayonunua mitumba ni serikali ya wajanja kwani bei ni ya maelewano kati ya watu wawili vivyo hivyo na muda wa matumizi haumo kwenye mkataba yaani "you buy as it is".
 
Kwahiyo watu wote ni wajina isipokuwa wewe na Msigwa ndiyo mnajua? haya ni mabehewa used ya umeme
 
Haya ni mabewa used ya umeme
 
Hua najiuliza hivi ni kitu gani hasa ambacho hapa nchini hua kina fanyika kwa usahihi wake? Kila sehemu ni ushuzi tuu
Jamaa huwa wanakaa wanabuni namna nzuri ya kuiba mali za umma bila kusumbuliwa, wanaenda kumsifia huyu bibi biashara inaisha na yeye ni mtu wa kupenda kuambiwa badala ya kuona na kufuatilia
 
Umesema vizuri sana!

Hawa wanategemea kuona Bullet train...!!

Hata maana ya Standard Gauge hawajui na hawataki kujua!

Yajayo yanafurahisha!!
 
kwa
kwa kweli umesema ukweli mtupu.hata mm ambae sijakaa huko majuu lkn tunaona kwenye mitandao mabehewa na vichwa ya treni havifanani kabisa na hivi vilivyoletwa na TRL.nilikuwa najiuliza mbona vinafana tu na vya kawaida?nashukuru P kwa kutudadavulia zaidi God bles you.
 
Gazeti la Jamhuri habari zake hazina bias, ni Kweli tupu.

Naamini Mmiliki wa gazeti la Uhuru na Jamhuri Si wamoja.
 
Hoja nzito sana hizi ndugu Pascal Mayala.

Mimi nauliza swali:
Ikiwa ndege zilinunuliwa mpya kabisa (ingawa sikubaliani na manunuzi ya ndege) na ndege zina bei kubwa sana kushinda mabehewa ya treni, nini kimewashinda kununua mabehewa mapya??

Kwa uozo huu, Je, hii na mengine hayatoshi kutuonesha kuwa Madam president is incompetent?
 
Kwani muonekano mzuri wa train unategemea speed.....!!?
 
na bado unataka ukagombee ubunge kupitia ccm. au umeahirisha?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…