Relief Mirzska
JF-Expert Member
- Jun 13, 2017
- 13,992
- 22,396
Wanajamvi,
Waswahili walisema chelewa ufike. Na pia Bora nusu shari kuliko shari kamili.
Naomba nitoe pongezi zangu za dhati kwa Mheshimiwa Tundu Antipas Lissu kwa hatimae kumuelewa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania na Amir jeshi mkuu wa Majeshi ya ulinzi na usalama.
Mheshimiwa Lissu baada ya kukutana na Mheshimiwa rais na kufanya mazungumzo huko jijini Brussels nchini Belgium ameongea na kuwaelezea watu miongoni mwa agenda walizozizungumzia. Kupitia taarifa yake hiyo, Mheshimiwa Lissu ameelezea kuwa anatambua kazi aliyonayo Mheshimiwa rais ni kubwa na nzito na ameonyeshwa kuridhia kumpa mama muda wa kutosha wa kushughulikia MAOMBI yake.
Mheshimiwa rais Mama Samia Suluhu Hassan alipoapishwa tu na wakati analihutubia bunge la JMT aliwaomba Watanzania wampe muda wa kushughulikia masuala kadhaa na kuahidi kwamba atashughulika na kila changamoto inayowasibu Watanzania.
Baadhi yetu kwa kumjua Rais ni binaadam wa aina gani basi hatukuwa na mashaka na ahadi ile. Tulijua fika kwamba sasa nchi yetu imempata Rais, tulijua fika sasa nchi yetu inaenda kuendelea kwa kasi ya ajabu. Tuliijua commitment ya Mheshimiwa rais kwa Mungu nà kwa Watanzania.
Ni bahati mbaya sana wahuni wachache wakiongozwa na watu wasio na uelewa wa mambo ya management and administration walitoka wakitukana na kukebehi hoja ya Mama Samia kwamba apewe muda. Ni bahati mbaya pia mmoja wa Watu hao alikuwa ni Mheshimiwa Tundu Lissu.
Mama Samia Suluhu Hassan kwa kuwa ni mkomavu wa siasa mwenye experience ya kutosha juu ya siasa za Tanzania alijua ni karata gani atumie. Mama alijua ni button gani ya kubonyeza na sasa nathubutu kusema Mheshimiwa Tundu Lissu amemuelewa Rais wetu kipenzi japo yeye ameelewa the hard way.
Kupitia bandiko hili, namuomba Mama yetu kipenzi Samia Suluhu Hassan ayafanyie kazi mazungumzo yake na Mheshimiwa Tundu Lissu kwa manufaa ya Tanzania yetu.
Viva Mama Samia, kidumu chama cha mapinduzi. Jumbe Brown sema Kidumuuuu
Jambo la Mama ni jambo letu vijana. Mama aongoze mpaka atakapochoka.