Hongera wafanyakazi wa Nakiete Pharmacy Mwenge

Hongera wafanyakazi wa Nakiete Pharmacy Mwenge

Tujikomboe Finance

JF-Expert Member
Joined
May 8, 2013
Posts
212
Reaction score
81
Leo mchana niliingia dukani hapo kununua dawa, bahati mbaya nilikuwa na bahasha yenye pesa kama 450,000 nikaisahau pale cash counter. Nilienda hadi Mlimani city ndio nikagundua sinayo ile bahasha moja kwa moja nikajua niliiacha pale Nakiete. Tukafanya hima kurudi pale, lakini nilijua hata nisipoipata sitawalaumu wale wafanyakazi maana nitakuwa nimeacha sehemu ambayo iko exposed sana na ni rahisi mteja anayelipia dawa kuichukua bila wale staff kuiona.

Jambo la kufurahisha nilipofika pale na kuwaeleza wakanieleza ile bahasha ipo, wakaniuliza amount nikataja na kuwaeleza maandishi juu ya ile bashasha basi wakanirudishia. Mimi na familia yangu tukafurahi sana na kuwashukuru na kuwapongeza wale staff.

Nimeona niandike hapa maana tumezoea kuandika mabaya tu, lakini pia kama recognition kwa staff wale wa Nakiete. Once again, thanks a lot, keep it up. Nitakuwa mteja wenu, naa word of mouth promoter.
 
Ni habari nzuri. Inafurahisha na kutia matumaini kuwa hata ktk kizazi hiki kinachopoteza uaminifu na uadilifu kwa kasi ya ajabu bado kuna habari nzuri kama hizi za watu wasioendekeza njaa
 
Camera bhana haziongopi! !!!!
Walikuwa na option gani zaid ya kutunza???!!


Pamoja na ustaarabu wao ila camera ni kiboko ya hizi mambo nilishuhudia mteja akiwa benki kasahau simu juu ya meza mwingine akaichukua fasta na kuizima baada ya jamaa kugutuka na kuanza kujisachi mfanyakazi mmoja akatoa wazo la ku re view tukio aaaargh jamaa aibu ilimkuta!!!!!
 
aisee wanastahili shukrani kwani siku hizi kizzazi hichi kimeharibika ahakuna uaiminifu hata kidogo

tumepata funzo hapa kwakweli
 
Uaminifu ni kitu kizuri sana.Hapo wamejijengea kuwa mteja wao permanent. Hongera kwa hao staff
 
Back
Top Bottom