Tujikomboe Finance
JF-Expert Member
- May 8, 2013
- 212
- 81
Leo mchana niliingia dukani hapo kununua dawa, bahati mbaya nilikuwa na bahasha yenye pesa kama 450,000 nikaisahau pale cash counter. Nilienda hadi Mlimani city ndio nikagundua sinayo ile bahasha moja kwa moja nikajua niliiacha pale Nakiete. Tukafanya hima kurudi pale, lakini nilijua hata nisipoipata sitawalaumu wale wafanyakazi maana nitakuwa nimeacha sehemu ambayo iko exposed sana na ni rahisi mteja anayelipia dawa kuichukua bila wale staff kuiona.
Jambo la kufurahisha nilipofika pale na kuwaeleza wakanieleza ile bahasha ipo, wakaniuliza amount nikataja na kuwaeleza maandishi juu ya ile bashasha basi wakanirudishia. Mimi na familia yangu tukafurahi sana na kuwashukuru na kuwapongeza wale staff.
Nimeona niandike hapa maana tumezoea kuandika mabaya tu, lakini pia kama recognition kwa staff wale wa Nakiete. Once again, thanks a lot, keep it up. Nitakuwa mteja wenu, naa word of mouth promoter.