Hongera Waziri Ummy Mwalimu kwa mkakati mpya wa kupambana na COVID19

Hongera Waziri Ummy Mwalimu kwa mkakati mpya wa kupambana na COVID19

Be careful, nitakupoteza!

Nitamuomba Mungu upigwe BAN ya 24hours
Usipige ngumi ukuta..wenye mawazo hayo ni haki yao ila wapotezee.

Turudi kwenye mada, Huu ni ugonjwa wa mlipuko tofauti na magonjwa mengine.
Suala la kujua idadi ya walioambukizwa ni la muhimu sana ili kuiwezesha serikali kujua namna ya kukabiliana nao.

Pia wananchi watahamasika kuongeza bidii katika kujihadhari.

Toeni takwimu ya walioambukizwa na pia ni maeneo gani yameshambuliwa zaidi. Hii itatusaidia tunaoishi vijijini kuweka umakini zaidi kwa wageni wanaotoka maeneo hatarishi
 
Naipongeza Sekta ya Afya nchini kwa jitihada kuntu inazozichukua katika kukabiliana na mlipuko wa COVID-19 tangu kuingia kwake hapa nchini. Ni wazi wataalam wa Afya wameonyesha "Commitment" itokayo mioyoni mwao huku wakiitendea haki mikataba yao ya ajira katika kipindi hiki kigumu.

Kutokana na majukumu wanayoendelea kuyatekeleza katika kipindi hiki, wataalam hawa hawana budi kujengewa uwezo zaidi ili kuyatekeleza majukumu hayo si tu kwa weledi wa hali ya juu, bali pia kwa ufanisi mkubwa.

Ni wajibu sasa wa Serikali kuchukua hatua zifuatazo;

(i). Kuhakikisha vituo vyote vya Afya nchi nzima vina vifaa/zana za kutosha katika kukabiliana na janga hili.

(ii). Kuwajenga kisaikolojia wahudumu wote wa Afya nchini ili kuwaondolea hofu pindi wanapokabiliana na wagonjwa wa COVID-19.

(iii). Kuwapa motisha ambayo ni nje ya mishahara ama marupurupu wanayoyapata kila mwezi.

Aidha, huu ndio muda muafaka wa kutumia vifungu vya tahadhali na dharura (Miscellaneous and Emergency Iterms) ili kuokoa maisha ya watanzania na si vinginevyo. Ni changamoto kubwa pale Mhudumu wa Afya anapomkimbia mgonjwa akiogopa kuambukizwa COVID-19. Hali hii itasababisha hata wagonjwa watakaougua magonjwa mengine kukimbiwa kutokana tu na hofu waliyonayo hawa wataalam. Nini hatma yake.

Nasubiri kuona Wawakilishi wetu wana sura gani wanapojadili na kuidhinisha Bajeti ya Sekta hii muhimu katika kipindi hiki kigumu.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni ombi langu kuwa watumishi wa afya wote watumie mask za N95. Hats kama mask za Vitambaa zimeruhusiwa kwenye jamii kwa ujumla ukweli ni kwamba mhudumu wa afya kumpàtia mask za vitambaa ni sawa na kumpa rungu askari aliyeko mstari wa mbele kwenye mapambano badsla ya machine gun.

Rsis Magufuli aliposhauri watu wajitengenezee mask za vitambaa hakumaanisha kuwa amebariki madaktari na manesi wapewe mask hizo!! Kuna taarifa ya baadhi ya hospital kuwapa watumishi wao mask za vitambaa!! Huu utakuwa ni upotoshaji mkubwa sana wa kauli ya Rais.

Napendekeza Wizara itoe tamko rasmi la kuzuia wahudumu wa afya kupewa mask za vitambaa.

Rais alishauri mask za vitambaa kwa jamii kwa sababu hali halisi hairuhusu kila mtu kumudu mask rasm. Hata Marekani wameruhusu mask za vitambaa lakini si kwa watumishi wa afya walioko mstari wa mbele kwenye vita hii.
It sounds rais hakosei😀😀 eti upotoshaji ! !

Kwani hakusema mavitambaa yashonwe mask?
Yakishahonwa nani ayatumie kama wakiyatumia wauguzi ngoma inapenya sasa unataka wananchi ndio wakaambukizane mtaani huko?
Kama rais akiupata huu ugonjwa kisha akapona atajifunza kuacha ujeuri.
 
Mi nafikiri idadi ikiwekwa bayana itasaidia watu kujua ukubwa wa tatizo na kuchukua hatua madhubuti za binafsi kujilinda. Kwa hali ilivyo sasa watu wameuchukulia ni ugonjwa wa kawaida sana na hata tahadhari wanayoichukua ni ya kawaida sana na ndio maana unakuata kwenye daladala wengine wamevaa mask na wengine hawana,mikusanyiko mikubwa watu wachache wana mask na wengine hawana, unakuta watu kama 10 mtaani wanapia story wamekaribiana sana bila hata kuvaa mask, watu hao unaweza kusema wanauchukulia ugonjwa huo kwa uzito unaostahiki?

Serikali itafute namna ya kuwafanya watu wauchukulie ugonjwa huu kwa uzito mkubwa ili waweze kujizatiti ipasavyo lakini bila kuleta panic.
 
Kuhusu DAMU salama waombeni CHADEMA wawaombe wananchi wajitokeze kuchangia damu tatizo litaisha fumba na kufumbua!
Muwe mmejiandaa kwa social distancing maana watakuja wananchi kama wote.
 
Back
Top Bottom