Naipongeza Sekta ya Afya nchini kwa jitihada kuntu inazozichukua katika kukabiliana na mlipuko wa COVID-19 tangu kuingia kwake hapa nchini. Ni wazi wataalam wa Afya wameonyesha "Commitment" itokayo mioyoni mwao huku wakiitendea haki mikataba yao ya ajira katika kipindi hiki kigumu.
Kutokana na majukumu wanayoendelea kuyatekeleza katika kipindi hiki, wataalam hawa hawana budi kujengewa uwezo zaidi ili kuyatekeleza majukumu hayo si tu kwa weledi wa hali ya juu, bali pia kwa ufanisi mkubwa.
Ni wajibu sasa wa Serikali kuchukua hatua zifuatazo;
(i). Kuhakikisha vituo vyote vya Afya nchi nzima vina vifaa/zana za kutosha katika kukabiliana na janga hili.
(ii). Kuwajenga kisaikolojia wahudumu wote wa Afya nchini ili kuwaondolea hofu pindi wanapokabiliana na wagonjwa wa COVID-19.
(iii). Kuwapa motisha ambayo ni nje ya mishahara ama marupurupu wanayoyapata kila mwezi.
Aidha, huu ndio muda muafaka wa kutumia vifungu vya tahadhali na dharura (Miscellaneous and Emergency Iterms) ili kuokoa maisha ya watanzania na si vinginevyo. Ni changamoto kubwa pale Mhudumu wa Afya anapomkimbia mgonjwa akiogopa kuambukizwa COVID-19. Hali hii itasababisha hata wagonjwa watakaougua magonjwa mengine kukimbiwa kutokana tu na hofu waliyonayo hawa wataalam. Nini hatma yake.
Nasubiri kuona Wawakilishi wetu wana sura gani wanapojadili na kuidhinisha Bajeti ya Sekta hii muhimu katika kipindi hiki kigumu.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.
Sent using
Jamii Forums mobile app