Hongereeni Kenya kwa hili, Mungu Awabariki!

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Posts
22,584
Reaction score
27,817
Tuwe wa kweli kabisa kama Kofi Olomide angefanya alioyafanya Kenya yaani kumpiga kumdhalilisha Mwanamke hapa Tanzania asingefukuzwa kwanza jamii yetu ya Kitanzania ndiyo ingemgeukia yule Mwanamke na kumwita majina yote Duniani kwamba ni Malaya, amejitakia badala ya kumtetea!

Kumbu kumbu zangu zinaniambia kuna kipindi Wazungu walimdhalilisha dada yetu wa ya Kitanzania kwa kumlazimisha afanye mapenzi na Mbwa jamii yetu (sehemu kubwa, ingawaje siyo yote) ya Kitanzania badala yakuwa upande wa ndugu na dada yetu ikawa upande wa Mzungu na kumuita dada yetu Malaya na majina yote, nakumbuka ishu ya Saro iliyotokea maeneo ya Kimara ambapo Mwanaume kwa hasira zake akaamua kupiga risasi na kuuwa watu, jamii yetu (sehemu kubwa siyo yote) ikawa upande wa muuwaji na kumtenga mama Saro hivyo historia hii inaniambia kwamba WatanZania Wanaume kwa jinsi wanavyopenda miziki ya Kongo kukata viuno stejini wangeandamana kumtetea Kofi Olomide na kumuadhibu Mwanamke kwamba alijitakia, kwani Mwanaume wa kitanzania ana matatizo ya kisaikolojia na huona Mwanamke ndiyo wa kumtolea matatizo yake yote na humlaumu Mwanamke kwa kila kitu, hata tu akipata mtoto mlemavu humlaumu Mwanamke kwa hilo na hatimaye kumkimbia!

Hivyo kwa hili nasema Hongereni sana Kenya kwa kuonyesha mfano mzuri wa kutetea wanyonge na wanaonewa, hivi sasa Kofi Olomide yuko Lupango!

Mungu Awabariki kwa Hilo!
 
Sijapata sababu za kwa nini huyo mwanamke alipigwa!, vinginevyo hii ya kushabikia pasi kujua kisa kwa undani ni sawa na kula ukiwa gizani..[emoji32] !!
 
Sijapata sababu za kwa nini huyo mwanamke alipigwa!, vinginevyo hii ya kushabikia pasi kujua kisa kwa undani ni sawa na kula ukiwa gizani..[emoji32] !!


Typical Mwanaume wa Kitanzania tayari umeshaelekea upande wa Mwanaume na kumlaumu Mwanamke na ndicho nilichomaanisha, hakuna sababu yoyote ile inayoweza kumpa haki binadamu kumpiga binadamu mwingine!
 

Kenya huwajui.Wanaume wengi hupigwa na wanawake hadi wana vyama vya wanaume vya kutetea wanaume wanaonyanyaswa na wanawake.Wanawake wa kenya ni wababe kwa wanaume acha tu.Sasa walishangaa kuona Mwanamke anadundwa na Kofi olomide!! Badala ya yeye Mwanamke kumdunda Kofi OLOMIDE.Wanawake wa Kenya wakasema haiwezekani mwanamme kupiga mwanamke.

Ona dume huyu Kenya alivyodundwa na mkewe
 
Da kweli wabongo c ni wapuuzi maana kuna mchina kamuua mtanzania kwenye migodi kisa kudai aongezewe hela lkn kimya sisikii chochote aise I hate to be in this poor countries
 
Da kweli wabongo c ni wapuuzi maana kuna mchina kamuua mtanzania kwenye migodi kisa kudai aongezewe hela lkn kimya sisikii chochote aise I hate to be in this poor countries
Wachina si ndiyo wale waliyobarikiwa na Mwenye nyumba na kusifiwa wana mahela Mengi? we unategemea mchina ataguswa nchi hii hata akifanya kosa?
Kwa hilo ndugu sahau kabisa.
 
Sijapata sababu za kwa nini huyo mwanamke alipigwa!, vinginevyo hii ya kushabikia pasi kujua kisa kwa undani ni sawa na kula ukiwa gizani..[emoji32] !!
Hamna justification, Hamna sababu yoyote ya mtu kupigwa hilo ni kosa la jinai!
 
Huko Kenya wanaume ndio wanaongoza kwa kutandikwa na wake zao. Walihofia kitendo cha Koffi Olomide kumpiga yule mama, kingewaletea balaa kwa wake zao.

Back to you Barbarosa, unaweza kuweka hapa link ya ile thread yako kwamba Watanzania tupo tofauti na watu wengine, sijui ulisema tu wastaarabu sana blah blah blah, na ukafika mbali kwa kusema hujawahi kubakwa kwa hiyo Tanzania ni salama?
 
Da kweli wabongo c ni wapuuzi maana kuna mchina kamuua mtanzania kwenye migodi kisa kudai aongezewe hela lkn kimya sisikii chochote aise I hate to be in this poor countries [/QUOTE]
tumia lugha unayoimudu vyema
 
We gamba Mleta uzi huu!jiulize tu kwa mfano koffie angefanya kitendo hicho hapa tanzania,
Serikali yako iliyokuwa Haiko makini,ingelichukua hatua gani?
Nasubiri jibu lako...

Ovaa
 
Da kweli wabongo c ni wapuuzi maana kuna mchina kamuua mtanzania kwenye migodi kisa kudai aongezewe hela lkn kimya sisikii chochote aise I hate to be in this poor countries
Ilaumu serikali usiseme Eto sisi wabongo,huuwezi kumlaumu mtu Yuko dar au arusha etc tukio limetokea geitaaa...
Kwanza mpaka sahvi mbungee wa geitaaa Yuko kimyaaaa
 
Ukweli ni kwamba mleta hajakosea yuko right, That's the meaning of good governance. Viva Kenya, viva the country of accountability
 
hapa si serikali pekee, hii ilifanyika sababu ya malalamishi ya wananchi kwa polisi

sikuhizi ofisi karibu zote za serikali hua ziko na account za social media, haswa twitter ambako hua ni rahisi kuongelea jambo linalokera watu kutumia hashtag moja na hapo hapo unaezajua ni watu wangani au kiasi ghani wamekereka na hilo jambo. kuna mambo mengi sikuhizi hapa kenya hulazimika kufanywa baada ya wananchi kulalamika kwa radio, mtaani au mitandaoni, serikali ya kenya sikuhizi hua haina budi ila kushughulikia jambo ambalo wananchi wengi wanatatizwa nalo, watu wengi wakilalamika kwa twitter utaona ofisi husika inajibu lwamba watashughulikia mara moja



hata hii story ya ile restaurant ya wachina ilishighulikiwa mbio mbio baada ya wakenya kutumia mitandao ku pressure serikali kuchukua hatua
No Blacks: Racist Chinese Restaurant In Kenya Closed Down
 
Typical Mwanaume wa Kitanzania tayari umeshaelekea upande wa Mwanaume na kumlaumu Mwanamke na ndicho nilichomaanisha, hakuna sababu yoyote ile inayoweza kumpa haki binadamu kumpiga binadamu mwingine!
Kenya ni nchi ya kike tunajua hivyo, wanawake wanawanyima wanaume unyumba, Kibaki kulazimishwa na mke wake kwenda media kuongelea michepuko. Kenya inaongoza wanaume kupigwa na wake zao. Kuna haja ya kuwaza zaidi ya kumhurumia mwanamke kwa ujumla. Kuna siku mtadai haki kutoka kwa wanawake.
 
Typical Mwanaume wa Kitanzania tayari umeshaelekea upande wa Mwanaume na kumlaumu Mwanamke na ndicho nilichomaanisha, hakuna sababu yoyote ile inayoweza kumpa haki binadamu kumpiga binadamu mwingine!
We utakuwa mwanamke naona. Sisi kiumeni sababu za kumfumua mwenzio zipo.
 
Wacha kusema ukweli..Watanzania wenzako watakumaliza..
 
Story zingine mnadandia tu
Jamaa umaarufu ulimponza
Nasio lingine
Kila kukicha Kenya visa kama hivyo ni vingi
Mbona hawafanyi hivyo!!

Fanyeni yamaana mambo ya kipuuzi hayo
 
Dah! Hii ngumu kumeza, yaani nashangaa mleta mada unataka kutuaminisha umeona chochote cha kusifia Kenya, maana tumezoea wewe kutuita wajinga.

Anyway yote tisa, hatua zhilichukuliwa baada ya Wakenya kupandisha hisia zao kwenye mitandao. Huyo jamaa alichokifanya sicho, hata kama mwanamke alikua na kosa, kuna njia nyingine za kumuadhibu na sio kumpiga teke tena mbele ya umati, yaani kumdharilisha kama mbwa koko vile.

Watu wakijitambua kama jamii, mambo mengi yatabadilika. Hapo awali ilikua rahisi kwa mwanaume kumpiga mwanamke ovyo tena hadharani, lakini leo hii unajikuta pabaya tena fasta. vurugu au unyanyasaji wa kijinsia haufai, iwe kwa mwanaume au mwanamke. Kama jamii tubadilike jameni, tuwapende wanawake wetu na kuwatunza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…