Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,817
Tuwe wa kweli kabisa kama Kofi Olomide angefanya alioyafanya Kenya yaani kumpiga kumdhalilisha Mwanamke hapa Tanzania asingefukuzwa kwanza jamii yetu ya Kitanzania ndiyo ingemgeukia yule Mwanamke na kumwita majina yote Duniani kwamba ni Malaya, amejitakia badala ya kumtetea!
Kumbu kumbu zangu zinaniambia kuna kipindi Wazungu walimdhalilisha dada yetu wa ya Kitanzania kwa kumlazimisha afanye mapenzi na Mbwa jamii yetu (sehemu kubwa, ingawaje siyo yote) ya Kitanzania badala yakuwa upande wa ndugu na dada yetu ikawa upande wa Mzungu na kumuita dada yetu Malaya na majina yote, nakumbuka ishu ya Saro iliyotokea maeneo ya Kimara ambapo Mwanaume kwa hasira zake akaamua kupiga risasi na kuuwa watu, jamii yetu (sehemu kubwa siyo yote) ikawa upande wa muuwaji na kumtenga mama Saro hivyo historia hii inaniambia kwamba WatanZania Wanaume kwa jinsi wanavyopenda miziki ya Kongo kukata viuno stejini wangeandamana kumtetea Kofi Olomide na kumuadhibu Mwanamke kwamba alijitakia, kwani Mwanaume wa kitanzania ana matatizo ya kisaikolojia na huona Mwanamke ndiyo wa kumtolea matatizo yake yote na humlaumu Mwanamke kwa kila kitu, hata tu akipata mtoto mlemavu humlaumu Mwanamke kwa hilo na hatimaye kumkimbia!
Hivyo kwa hili nasema Hongereni sana Kenya kwa kuonyesha mfano mzuri wa kutetea wanyonge na wanaonewa, hivi sasa Kofi Olomide yuko Lupango!

Mungu Awabariki kwa Hilo!