Hongereni Baraza la Maaskofu (TEC) kwa tamko makini na lenye kueleweka vyema!

Hongereni Baraza la Maaskofu (TEC) kwa tamko makini na lenye kueleweka vyema!

Fumadilu Kalimanzila

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2016
Posts
1,770
Reaction score
5,423
Tumeshazungumza mengi humu kuhusu mkataba wa kilaghai wa kuchukua Bandari zetu milele na kuwakabidhi Waarabu wa Dubai.

Sa100 lazima aambiwe ukweli kwamba hata kama alikuwa na nia nzuri kuhusu uwekezaji katika Bandari lakini approach yake imekuwa ni njia isiyokuwa wazi ( hakuna ushindani ktk kumpata DP World) , hila na Mazingira yenye harufu mbaya ya RUSHWA!

Mama lazima atambue kuwa hakuna anayepinga uwekezaji wenye tija na wenye masharti Bora kwa Taifa.

Kwa huu mkataba wake na Waarabu hakuna mtu mwenye akili huru anayeweza kumuunga mkono na Sa100 atambue kuwa anaungwa mkono na kudanganywa na wachumia tumbo Wachache wasiona mbele zaidi ya matumbo yao tu!

CCM tumeuza Madini,Gesi, Mbuga za Wanyama n.k angalau tungekuwa basi na aibu tukaziacha hizi Bandari free of encumbrances ili vizazi vijavyo wazikute kama na sisi tulivyozikuta.

Tutawapa kazi sana watoto na Wajukuu wetu kuzitoa hizi Bandari mikononi mwa Waarabu na hasa kwa kuzingatia kwamba mafuta yao yanakwenda kukosa soko baada ya mapinduzi makubwa wanayofanya akina Elon Musk ya magari ya Umeme badala ya mafuta!

Sa100 ziache Bandari zetu umekuta tunaishi nazo na uwekezaji tumeshafanya mkubwa hapo!

Mwamba Hayati Rais Magufuli alikuwa na ndoto kubwa sana sana ya kuziunganisha Bandari , SGR na Umeme wa Bwawa la Mwl.Nyerere na hii Nchi ingepaa kwa Uchumi hakika!

Wewe Sa100 ni kama umepoteza dira kabisa kwani sasa unaamini hatuwezi chochote bali ni Waarabu wa Dubai ndo wanaweza kila jambo!

Hii reckless thinking sijui imetokea wapi na Kwa haraka hivi mara tu baada ya Kifo cha Rais Magufuli!

Wewe malizia hii miaka yako 2 iliyobaki na hata ukiamua kwenda kuishi Dubai wengine hatutajali ila tuachie Bandari zetu!

Ma-Baba Askofu wetu wote wa TEC pokeeni Maua yenu popote mlipo.
Nawatakieni Dominika njema hapo kesho.
Mwenyezi Mungu awabariki sana na kuwapa Nguvu muda wote.
 
Back
Top Bottom