Hongereni JWTZ na Watanzania kwa kuwa na 'Ndege Vita' nzuri zilizokuwa 'zinazurula' tu Anga la Tanzania leo Mchana

Matumizi mabaya ya Kodi zetu,ukiimarisha demokrasia na ujirani mwema uhitaji kupoteza kodi kugharamia jeshi.
Yafaa nini mtu hadi anastaafu ajawahipiga hata risasi
Nikiwa sebleni kwa shemeji yangu na king'amuzi ameshakilipia huku na subiri dada apike ugali na nyama nile..we unalipa kodi gani ya kufanya Nchi ikaachana na kugharamia Jeshi Marekani na Utajiri wake wote ana Military Base dunia nzima we umeamka hata hujui utakula nini leo unajifanya umeridhika na amani
 
Unakula vizuri,unalala kwa amani,unakunya..then unakuja kutoa pumba zako hapa,tunakulinda ndo maaana unapata nguvu ya kuandika hapa.
 
Wakati mwingine tier tunafikiri na kudadavua kwa akili pevu badala ya kukurupuka tu na kushadidia mambo ambayo hatuna upeo nao wa kina.
Hata nchi kama Marekani, Urussi, Uingereza na nchi nyingine Tajiri na zinazopigiwa chapuo kuwa ‘zenye demokrasia na utawala bora‘ zaidi wanajiimarisha kijeshi Duniani.
Ni Isuzu na uzumbukuku kubeza jitihada za taifa kuimarisha jeshi lake au kujenga uchumi na mustakabali wa wananchi wake.
 
Wata kama hao ni wa kuwapuuza tu kwani hawajui mawiwo wala machweo yao!
 
Kuwa na amani haimaanishi hao mliowataja hawana kazi ndugu zangu kuna nchi wanasema hazina jeshi ni kweli lakini kuna nchi zina mikataba ya kuwalinda ,inapaswa kujua kwamba kuna mengi yanamalizwa kimnya kimnya kwa jasho na damu tusitukane watu humu kwa sababu tumepata bia tamu ,nakumbuka kabisa nilipokua bwana mdogo kuna tukio lilitokea sikumbuki vema basi wananchi wakabebana kwenda kuchoma kituo cha polisi na walifanikiwa kukichoma bwana bwana kumbe miongoni mwa waliokua amsha popo ya kuchoma kituo walikuwepo na wezi stadi mbona tuliisoma namba na ukizingatia tulikua tunakaa pembezoni kwa mji sana na hako kakituo kwa kiasi fulani kalisaidia hivyo chunga sana hizo kauli hapo ni watu wanakua na agenda zao kwahiyo mnataka vyombo vyote vya ulinzi na usalama viache majukumu yao tukagombanie samaki feri huko alafu? 🦁
 
Mnataka jeshi lisifanye mazoezi ya utayari?

Hao hao silaha mpya zikinunuliwa mnalalamika, zikioneshwa zile kongwe mnalalamika!

Wachieni wenye kazi zao wafanye, kuna watu wako bize kulinda anga lenu wakati mpo baa mnagombania wahudumu.

Jeshi bila mazoezi ya utayari ni sawa na kikundi cha wacheza ngoma tu!

Mungu libariki jeshi letu ( JWTZ),
 

Ndege vita za tanzania we nyarwanda zinakutesea nini?
 
Watu wameweka sana nyuzi humu wakilalama kuhusu Shenyang F7 na zile MiG kuwa ni za kizamani ila umekuja ujio mpya bado tu sasa sijui wanataka nini?
 
kwa bongo issue sio hizo ndege uzionazo, issue iko kwenye mikataba iliyotumika kuzinunua na hao wazabuni....dah na CAG ndio hafikagi kule...
 
Tungeuza hii midude pesa tushughulikie mambo mengine kwanza ipo outdated
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…