Simba sio ya kufungwa bao 5 hata kama mpira unadunda kiasi gani, ulisukwa mkakati wa muda mrefu baina ya wanaojiita wajanja wa mjini ambao wameondolewa ndani ya Simba na wale walioshindwa kwenye uchaguzi wakaamua kuungana na adui ili tu akina Mangungu waonekane hawana uwezo.Ukweli ni kuwa wale walioondolewa ktk benchi la ufundi na kupelekwa Simba B nao wameshiriki kwenye usaliti huo, wenyewe wanadai ndio wenye Simba yao, haya yaliyofanyika leo ndio yale yale yaliyofanyika wakati wa Yanga ya Nchunga Lyod ambapo marehem Mzee Akilimali aliisaidia Simba kuwaua Yanga bao 5 0 na siku ile alisema kabisa na ninamnukuu, "Tuone kama Simba atafungwa" mwisho wa kunukuu, Yanga akala mkono.
Leo wasaliti ndani ya Simba wamechukua mzigo wao mapema na wakaeleza A to Z kwa maadui zetu.Lengo lao warudishwe ndani ya timu ili maisha yaendelee.
Mashabiki na wanachama wala msiumie, Simba haikufungwa kimpira leo, wasaliti ndani ya timu ambao wako nje ndio wameifunga Simba leo, Yanga mtoto mdogo sana, sana tena, ila wamepewa furaha na watu wetu wasiompenda Mangungu.