Hongereni 'Mortuary Attendant' wa Tanzania, ila usiombe Nduguyo afie India halafu uje uipokee Maiti yake waliyoiandaa Wao huko

Hongereni 'Mortuary Attendant' wa Tanzania, ila usiombe Nduguyo afie India halafu uje uipokee Maiti yake waliyoiandaa Wao huko

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
8,018
Reaction score
16,802
Kuna Maiti nimetoka kuipokea na kwenda Kuihifadhi Hospitali fulani Jijini Dar es Salaam ila baada ya Kuifungua ili ianze kuwa treated ikitokea nchini India alikofia kiukweli nimeamini Waafrika tunadharaulika mno na hawa Wahindi siyo Watu japo hapa Tanzania tunawapenda na hata Kuwanyenyekea vile vile.

Huko nyuma pia niliwahi kubahatika katika Kushughulikiwa Mwili ( Maiti ) iliyokuwa ikiandaliwa ( treated ) tayari kusafirishwa kwenda nchi fulani na kiukweli Mortuary Attendant wa Tanzania ( katika Hospitali husika ) waliuandaa Mwili vizuri kabisa, Kiutaalam, Kiupendo na Kiutu kabisa na naamini hata Walioupokea huko ulikoenda walishukuru na kuridhika nao.

Mwili ( Maiti ) niliyoipokea leo kutoka nchini India ( nilikoamini kuwa kuna Watu makini na Weledi ) baada ya kufika na kuikagua tayari kwa Kuiandaa kwa Kuagwa Kesho imenifanya niamini kuwa kumbe Waafrika ( hasa Watanzania ) ambao ni Mortuary Attendant wana Utu, Hekima na Ustaarabu sana katika Kuandaa Miili ya Marehemu Wetu lakini imenifanya nianze Kuwachukia Wahindi na kuamini kuwa kumbe ni Watu wenye Roho Mbaya na hawana Ubinadamu.

Ushauri wangu ( na silazimishi ) kama utakuwa na Ndugu yako nje ya nchi hasa nchini India kama mkiona dalili za Kupona hazipo tafadhali upesi sana mrudisheni tu Tanzania aje afie huku ili apate treatment nzuti ya Mortuary Attendant wa Kitanzania ila mkiacha wafie nje ( hasa huko India ) wakija huku katika Jeneza ( ambalo hugeuka kuwa Cargo ) tegemeeni kukutana na Makwazo na Uchungu mkubwa pale mkiupokea.

R.I.P Marehemu wote nchini Tanzania.
 
Wahindi huwa wanachoma moto marehemu hivyo inawezekana wana uzoefu mdogo sana kwenye uhifadhi wa miili ya binadamu haswa ikiwa ninkwa madhumuni ya kusafirisha.

Japo suala la ubaguzi linaweza kuhusika pia.
 
Sawa tumeelewa kuhusu utu, heshima na ustaarabu. Sasa hebu tueleze ulichokiona maana kwa ishu kama hii hatuwez kuomba kapicha ka kusindikiza. We shusha maelezo chap chap
😃😃😃 Kumbe mnachagua uzi wa kuomba picha,, mwambieni mwamba atume tu picha maana kuna wadau watasem bila picha uzi ni batili
 
Umepokea? Marehemu mia kutoka india au mmoja?

Inawezekana huyo tu ndio kakutana na mabalazuri wakamuandaa vibaya mkuu .. sio waindi wote wanaweza fanya hivyo mkuu

Sio watu wote duniani ni wabaya mkuu
 
Wammwandaa vipi mbona ktka maelezo yote sijaona? Au wamemkata baafhi ya viungo ili kumpumguza uzito?
Hili la Kumpunguza Viungo vyake vya ndani kwa Maiti yoyote ile inayosafirishwa kutoka nchi za mbali ni la Kawaida kwani vikiachwa Maiti itanuka vibaya kwakuwa hivyo Viungo huoza kwa haraka sana.

Concern yangu ni Mwili kuandaliwa kwa Kulipua lipua, Kutokuujali na kuupa tu treatment ya kutimiza wajibu kiasi kwamba inaibua Hisia kuwa huenda Wahindi wanatudharau sana Sisi Waafrika.

Nimesikitika mno.
 
Mbona hujaeleza kimetokea nini ????
Mwili umekatwakatwa, tobo la Mpira aliokuwa akiutumia Kulia Chakula halikuzibwa vizuri, Mishono mingi isiyo ya Ulazima huku Dawa ikiwa si nyingi.

Bahati nzuri hata Mortuary Attendant wa Tanzania aliyeupokea Mwili husika katika hiyo Hospitali tuliyomuhifadhi nae alishangaa na Kusikitika mno huku akiwalaani vikali Wenzake wa huko nchini India Mwili ulikotokea.
 
Back
Top Bottom