Betterhalf
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 2,882
- 2,560
Habari za asubuhi wana JF. Nianzie kwa kuwatakia Jumapili njema...na pasaka njema kwa wale ndugu zetu wa imani hiyo.
Jana nilifuatilia kwa karibu sana mechi ya Azam na Mtibwa. Mpambano ulikuwa wa haja kiasi cha dakika 90 kuzishuhudia timu hizo zikiwa nguvu sawa kwenye mchezo wa robo fainali ya FA.
Hatua hiyo iliwalazimu waende kwenye mikwaju ya penalti ambapo jumla ya penalti 20 zilipigwa. Azam wakipiga penalti 10 na kupata 8 huku wakipoteza mikwaju miwili, wakati Mtibwa wakipiga penalti 10 na kupata 9 huku wakipoteza mkwaju mmoja wa Henry Joseph.
Nitumie fursa hii kuwapongeza Mtibwa kwa kupambana kwa dhati kabisa na hivyo kufanikiwa kuzima ndoto za Azam kwenda hatua ya nusu fainali.
Kwa hili, niwapongeze tena Mtibwa na niwasisitize kwamba, kwa hali ilivyo, matumaini ya wao kutwaa taji VPL ni madogo mno ikilinganishwa na nafasi ambayo wanayo kwenye FA.
Mtibwa wana nafasi kubwa ya kuwekeza nguvu kubwa kwenye FA ili kutafuta nafasi ya uwakilishi wa kimataifa hapo mwakani kwenye CAF Confederation Cup(ambako Simba wametolewa na El-Masry na ambako Yanga wamerejea baada ya kuondoshwa kwenye CAF Champions League na Township Rollers).
Ninaamini, kwenye VPL wanahitaji kupigania kutoshuka daraja tu suala ambalo naamini wana uhakika mkubwa wa kulivuka. Lakini kwenye FA kuna fursa nyingi zaidi. Jukumu walilonalo kwa sasa ni kupambana na Stand Utd kwenye nusu fainali na baadae kupambana na mshindi wa mechi ya leo kati ya Singida na Yanga.
Nawatakia Mtibwa kila la kheri...!
Nawasilisha.