Hongereni Simba kwa kupata ushindi mnono ugenini

Hongereni Simba kwa kupata ushindi mnono ugenini

Tariq f

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2021
Posts
233
Reaction score
347
Salute wakuu.

Napenda kuwapongeza wanalunyasi kwa ushindi mnono walioupata dhidi ya Waangola, hakika kweli SIMBA nyie ni wakimataifa.

Napenda kuchukua nafasi hii kuwakilisha pongezi zangu zote Simba kwa niaba ya Wanayanga wote.

Hakika mmetanguliza mguu mmoja kwenye hatua ya makundi.

Ila nasikitishwa sana na baadhi ya Wanayanga wenzangu wabishi wasiotaka mabadiliko ndani ya klabu yetu. Najiuliza Je, hawaoni wivu jinsi Simba anavyotusua anga?

Akili zetu zilivyo za kipumbavu tunataka tuifunge Simba tu ndiyo mioyo yetu inaridhika!!
Kiukweli sipendi kuongea mengi mno kuhusiana na mambo mengi nayoyajua yanayoendelea kwenye klabu.

Hata mtu mjinga unashindwa kujiuliza kwa nini kila siku sisi? Yaani tuwe vizuri ndani ila nje majanga? Namungo wa juzi atupite viwango vya CAF?

HAIINGII AKILINI KABISA!
Kuna refa mmoja wa ligi kuu nafahamiana naye (namuhifadhi kwa jina kuepusha uzi kufungiwa) na huwa nawasiliana nae sana, kiukweli ananimbia uchafu mwingi unaofanywa na kigogo mmoja wa timu yetu kwa kumhonga refa huyo kila achezeshapo mechi ya yanga! [emoji17][emoji17]
SIKUAMINI MPAKA AKANIONESHA SMS ZA UCHAFU NA MIAMALA YA PESA!

Nimeamua kuongea tu ukweli kuhusiana na hali halisi kuhusu yanayoendelea klabuni jamani.

KAMA KUNA YANGA NITAKUWA NIMEMKOSEA ANISAMEHE TU MAANA NIPO KWENYE KUJENGA NA SI KUBOMOA. NAUMIA NA SUALA HILI.

Sipendi uchonganishi na wala sipendi kuiongelea vibaya Yanga ila kiukweli niseme imetosha Yanga kufanya huu uchafu ipo siku nyie viongozi mtakuja kuumbuka

TUACHIENI YANGA YETU, YANGA SI KITEGA UCHUMI!

#𝙝𝙚𝙧𝙨𝙞 𝙤𝙪𝙩
#𝙣𝙖𝙗𝙞 𝙤𝙪𝙩
 
Aisee kiukweli, yanga watakuwa wanaharibu soka la Tanzania kama watakuwa wanafanya hivi

TUWEKE USHABIKI PEMBENI, HUU NI UHUNI
 
Mie hapo kwenye kuhonga sina shaka nalo.

Mie ni Shabiki wa Simba. Jana nilienda kwa Mkapa na nikakaa na mashabiki wa Yanga tena wale vindakindaki wanaojua mipango ya timu yao.

Wanalalamika jinsi uongozi ulivyoshindwa kuwatafuta referees ili wawahonge.

"Inamaana viongozi wameshindwa kujua hawa marefa wamefikia hoteli gani?, kama wangewatafuta lile goli la Mayele la offside lingewekwa kati" Alisema shabiki mmoja.

Kiukweli jana ndio nimejua mengi sana under the carpet.
 
Mie hapo kwenye kuhonga sina shaka nalo.

Mie ni Shabiki wa Simba. Jana nilienda kwa Mkapa na nikakaa na mashabiki wa Yanga tena wale vindakindaki wanaojua mipango ya timu yao. Wanalalamika jinsi uongozi ulivyoshindwa kuwatafuta referees ili wawahonge...
Aiseee
 
Inasikitisha sana kwakweli
Hili suala lichunguzwe kwa kina na TFF
kwani linashusha hadhi ya mpira wetu na
Pia linaondoa ubora wa ligi yetu

Pindi huu mchezo wanaoucheza ukigundulika ligi itashuka hadhi yake na hata kufungiwa kimataifa
 
Mie hapo kwenye kuhonga sina shaka nalo.

Mie ni Shabiki wa Simba. Jana nilienda kwa Mkapa na nikakaa na mashabiki wa Yanga tena wale vindakindaki wanaojua mipango ya timu yao. Wanalalamika jinsi uongozi ulivyoshindwa kuwatafuta referees ili wawahonge...
Mmh! noma sana kwakweli!
 
Ndio mana linapokuja suala la kimataifa wanashindwa kufanya vizuri, ila kwenye ligi za ndandi wanatoboa kwa ushindi wa kununua, ila kama wamerizika na magumashi yao sio mbaya, kupanga ni kuchagua
 
Mambumbumbu wenzangu toka MAKOLOKOLO FC chonde chonde tusijisahau sana maana mwisho wa safari yetu hauko mbali sana [emoji28]
 
Inasikitisha sana kwakweli
Hili suala lichunguzwe kwa kina na TFF
kwani linashusha hadhi ya mpira wetu na
Pia linaondoa ubora wa ligi yetu

Pindi huu mchezo wanaoucheza ukigundulika ligi itashuka hadhi yake na hata kufungiwa kimataifa
Inabidi mashabiki wa yanga tupambane vilivyo ili kuondoa huu uhuni, na si kingine bali ni kuuondoa uongozi madarakani
 
Jamaa anaongea ukweli, mashabiki wasimame kidete kutetea klabu yao maana hali hii inatishia uwezo wa timu
Kabisa yaani timu haichezi kwa uwezo wake, ila kwa kubebwa tu ,linapokuja swala la mechi zisizo na mbeleko wanaangukia pua
 
Ndio mana linapokuja suala la kimataifa wanashindwa kufanya vizuri, ila kwenye ligi za ndandi wanatoboa kwa ushindi wa kununua, ila kama wamerizika na magumashi yao sio mbaya, kupanga ni kuchagua
Kweli kabisa nashangaa kwa nini yanga wanashindwa kuligundua hilo
 
Mimi kama shabiki na mwanachama wa Yanga nasema adui yetu mkubwa ni Hersi na jopo lake wanaopambana kuhonga waamuzi badala ya kuiandaa team kiushindani. Tumefanya usajili mkubwa kwaajili ya michuano ya kimataifa na si kombe la mbuzi.
#HersiOut
 
Hivi mkuu we ni kolo mwenzangu au mwananchi unajua sijakuelewa we jamaa????manake wananchi pia hawata kuelewa ila kama we ni yanga basi una akili sana na una maisha marefu kwa kukataa unafiki
 
Back
Top Bottom