Elections 2015 Hongereni tena Segerea: Nina furaha tele na sijatetereka

Elections 2015 Hongereni tena Segerea: Nina furaha tele na sijatetereka

Joined
Jun 20, 2009
Posts
45
Reaction score
225
HONGERENI TENA SEGEREA: NINA FURAHA TELE NA SIJATETEREKA!

Na. Julius Mtatiro,

Ndugu zangu, nimejulishwa na mtu muhimu sana kwamba jimbo la Segerea limeachwa chini ya CHADEMA lakini ndani ya UKAWA, nimeshazithibitisha taarifa hizi kwa viongozi wangu.

Kwanza niwapongeze viongozi wote wa UKAWA kwa kufikia makubaliano hayo muhimu, mimi ni muasisi wa UKAWA na nimekuwa Katibu wa UKAWA katika Bunge Maalum la Katiba, naipenda UKAWA na naamini katika UKAWA; Kama viongozi wameweza kukubaliana jambo hili mimi bila KINYONGO chochote kile naunga mkono mapendekezo na maamuzi yao.

Pili nawataka wananchi wa Segerea, wanachama wa CHADEMA, CUF, NCCR na NLD na vyama vingine vyote waende kwenye vituo vya kupigia kura tarehe 25 Oktoba na kuchagua Diwani, Mbunge na Rais aliyesimamishwa na chama chochote cha UKAWA bila kujali mambo mengine, huu ni mwaka wa mabadiliko na lazima tuyasimamie.

Tusikubali kupumbazwa na janja za CCM kuwa angekuja Mtatiro huku Segerea tungewaunga mkono! CCM ni ileile na mtu yeyote anayegombea kupitia CCM anakwenda kuimarisha mfumo uleule uliochoka, unaonuka na kukumbatia rushwa na ufisadi, wagombea wa CCM ni walewale wanaotetea mfumo uleule ambao umelifikisha taifa letu hapa tulipo. CHAGUA vyama vya UKAWA hapa Segerea na nchi nzima bila kujali kuwa MTATIRO siyo mgombea tena.

Kwa sababu siasa siyo ajira mimi ntajikita katika masuala mengine ya ujenzi wa taifa langu ikiwemo kuelimisha wananchi katika uchaguzi na kusimamia kampuni yangu na kisha ntajipanga kuingia bungeni mwaka 2020. Nataka kuwaonya wale wenzangu na mimi ambao wako katika siasa kwa ajili ya KUTAFUTA MKATE WA KILA SIKU watambue kwamba SIYO MAHALI PAKE na kwamba wataumbuka! Ukifanya siasa usiitegemee kama sehemu ya kipato chako hata siku moja ili usijekuathirika sana kila unapokosa fursa kama nilivyokosa mimi pale Segerea.

Natoa wosia na wito kwa wagombea wote wa vyama vya UKAWA nchi nzima ambao hawatapitishwa kuwa wagombea kwenye uchaguzi huu washirikiane na wagombea waliopo ili tutafute ushindi, huu ni mwaka wa mabadiliko na mwaka wa maamuzi, shiriki kuleta mabadiliko hayo.

Na wale watakaotimkia ACT, ADC, CCM na kwingineko kwa sababu hawakupata majimbo ndani ya UKAWA nawatakia kila la heri na kuwakumbusha kuwa KIMBUNGA CHA UKAWA kitawasambaratisha kokote kule waliko bila kujali walipewa nyadhifa gani.

Nawaahidi kuendelea kusimamia ukweli na kulipigania taifa langu hadi mwisho wa maisha yangu.

Julius Mtatiro – B.A, M.A, LLB,
Mtia nia atakayewaunga mkono wagombea wa UKAWA jimbo la Segerea na nchi nzima,
Mapambano yanaendelea, ‪#‎IKISHINDA_UKAWA TUMESHINDA_SOTE‬!
 
Mkuu vyovyote,ila unataka kumaanisha hutagombea ubunge?kama ni hivyo ntajutia kukukosa mjengoni
 
Heshima Kwako Mkuu, Hakika Taifa Linahitaji Watu Kama Nyinyi Wenye Uwezo Wa Kujitoa Kwa Ajili Ya Taifa Na Wala Si Maisha Yao Binafs, Nami Nasema Mungu Akutangulie Katika Kila Jambo Unalolifanya, Akuongee Hekima Na Maarifa Katika Shughuri Zako
 
Hekima kubwa sana hii...!!!

Mtatiro hongera sana Comrade, Siasa inataka mwanasiasa kuwa na kiasi, Na wewe umeonyesha hasa siasa inavyotakiwa kuchezwa. Mungu akubariki sana. Na ninakuona ukifika mbali wana kwa moyo huu ulionao, Vijana wa lika lako wanayomengi sana ya kujifunza kutoka kwako.

Heko sana sana Kamanda wangu Mtatiro!!

BACK TANGANYIKA
 
Rafiki yangu Julius,Hongera sana kwa ukomavu huu uliouonyesha.

Naamini tutaendelea kushirikiana kuhakikisha mfumo huu kandamizi unang'oka

Jambo kubwa la Msingi ni kujipanga kisawasawa kuhakikisha pia ndoto yako inatimia. Umepiga hatua moja kubwa zaidi. Sote tutashinda

Soldier on my comrade!
 
Nimeipenda hoja yako I wish u da best Mtatiro
 
Hongera Mkuu,Allah akuongoze usije kengeuka kama wakina fulani wa kuanzia Kanda ya Kati hadi kanda ya Ziwa,freedom is coming!!
 
Back
Top Bottom