KERO Hongereni TRC ila zingatieni ustaarabu wa Abiria wanaopiga muziki kwa Spika za Bluetooth, ni kero

KERO Hongereni TRC ila zingatieni ustaarabu wa Abiria wanaopiga muziki kwa Spika za Bluetooth, ni kero

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Niwaombe TRC waongeze mishahara kwa wafanyakazi wao ,sio kuwavalisha tu uniform ila mishahara kiduchu...Wajaribu hata kuwapa mafunzo ya nje mara kwa mara ,wakubwa wasiwabanie watendaji wa chini .
Mishahara yao kiasi gani,ili tujue kama ni kiduchu kweli au la?
 
Kwanza kabisa napenda kuwapongeza TRC kwa kuendesha SGR mwaka mzima kwa ufanisi na kiwango kile kile mlichoanza nacho. Kwa hili mnastahili pongezi.

Pamoja na huduma zenu nzuri kuna kitu mnakifumbia macho ila sio ustaarabu na inaondoa starehe ya kupanda treni kwa watu wanaopenda utulivu na amani. Ni hii tabia ya baadhi ya abiria kupanda na yale maspika makubwa sijui ndio yanaitwa Bluetooth.

Hawa watu hawana ustaarabu hata kidogo . Wanafungulia miziki yao kwa sauti kama wako bar au wako kwenye vyumba vyao huko wanakoishi. Mbaya zaidi unaweza kuta wako zaidi ya mmoja kila mtu na muzii wake,huyu singeli huyu Bolingo yaani ni vurugu kama kwemye zile nyumba za kupanga uswahilini.

Tabia hii imekithiri sana hasa ukisafiri na kundi la watu wanaotoka au wanaokwemnda kwenye marathons. Hatukatai watu kusikiliza muziki ila iwe kistaarabu. Hii ni public transport kuna watu wa aina nyingi. Kuna wazee,watoto wagonjwa sio wote wanaweza kusikiliza makelele ya muziki.

Tunaomba TRC iweke utaratibu wa kudhibiti hawa wapiga muziki kwemye treni au kama utaratibu upo tunaomba ukaziwe maanake mara nyingi tuliripoti kwa wahudumu wa TRC ila hakuna kilichofanyika.
Pia TRC sometimes mnakosa umakini. Juzi nilipanda behewa eti tunaondoka ndio wanatuomba radhi kuwa lina hitilafu. Tulikaa gizani na bula hewa kutoka Dodoma hadi Dar. Ingekuwa nchi nyingine mngeshtakiwa na mngelipa fidia.
 
Bila hewa una maana mlisafiri Dom to Dar bila AC? How?
 
Kwanza kabisa napenda kuwapongeza TRC kwa kuendesha SGR mwaka mzima kwa ufanisi na kiwango kile kile mlichoanza nacho. Kwa hili mnastahili pongezi.
Kweli, wamejitahidi sana. Sikutarajia kutokana na asili yetu ya ubabaishaji. Ila, waongezee bidii kwenye usafi wa vyoo. Wakati mwingine harufu uwepo kutoka vyooni.
 
Back
Top Bottom