Hongereni Uongozi wa JamiiForums kwa kutoweka Hadharani Zawadi zetu Nono kwani Wengine Simu zetu sasa zinaisha Chaji tu kwa Kukopwa

tetesi mtapewa toyo na vi-swaswadu
 
Hamu yangu ni kuwajua wachache nisiowajua ila kaka Mohamed Said huyo namjua ukimtaka nenda youtube tafuta vipindi UTV kipindi Zumari utamuona huyo mzee kwa hilo jina .

Mdogo wangu Mshana Jr huyu nenda kwenye uzi wa selfika page ya kwanza utamkuta kwa sura yake kabisa .

Wakili Pascal Mayalla huyu tafuta vipindi vya IPP huko Youtube utampata kwa sura kabisa .

Bwana charistmatic fella , entertainer ndugu GENTAMYCINE huyu usihangaike kama uliangali mechi ya Simba iliyopita hapo taifa , tizama dakika ya ishirini na nane kuna muda mtangazaji aliwataja wachezaji wakongwe waliokuwa jukwaani huyu bwana alikuwa miongoni mwao kwa mavazi yake na sura yake .

Sikutajii alivaaje ila nakutuma uhangaike kuwajua wachezaji wakongwe ukishawajua utajua fika kuwa Genta ni yupi kwakuwa ni miongoni mwao ila sio kwa kuwa mkongwe mpirani .

Ahsanteni , wewe GENTAMYCINE usiwasahau wanao wa kawe na makongo hata kwa kidogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…