Hongereni Wakenya kwa kuwa na Prof. Patrick Lumumba

presenter,
Nilipata bahati ya kuhudhuria 2nd general assembly ya ASARECA ilifanyika mwaka jana december Bujumbura. Huyu Professor alikuwa kivutio kikubwa sana kwa washiriki toka nchi zote 11 za ECA kwa ushupavu wake wa mada na kupangilia ayasemayo.

Kwa bahati kuna professor Mtanzania anaitwa Nuhu Hatibu ambaye ni CEO wa International body (Kilimo Trust) iliyoko Uganda, huyu aliongea baada ya Lumumba. Professor Hatibu ni kivutio kikubwa na authority sana kwenye agricultural sciences/development kwenye ECA region.

Ki-ujumla afrika mashariki na kati tuna magwiji na wanataaluma wazuri sana wanaoheshimika sana na wenzetu Ulaya.

Ahsante kwa mada Athuman.
cc lawmaina78
 
Last edited by a moderator:

Si kwa ubaya. But why do you write with commas? It's very difficult to read what you write and i normally just move on. Thanks
 
Wewe unazidi kujichanganya na kufanya makosa, kwanza siyo "kwenyu" bali ni "kwenu", na hakuna kitu kama tumbo nyingi, na tatu unapaswa uandike Wanasiasa wenye tumbo lisiloshiba ndio sahihi!

:frusty::frusty::frusty::frusty:

Karudi shule jamani. Unapomkosoa mtu, kuwa na uhakika kuhusu unachokisema. Kwanza, Kwenu na Kwenyu ni mamoja. Ni kama Ninyi na Nyinyi; acha na wacha.

Pili, uwingi wa tumbo ni matumbo. Neno hili liko katika ngeli ya Li-Ya.

Tumbo lisiloshiba
Matumbo yasiyoshiba

Hata kama lingekuwa halina uwingi, basi tungeliweka katika ngeli ya I-Zi

Nyumba ile
Nyumba zile

Ndizi ile
Ndizi zile
 
Ni tumbo lisiloshiba!
Nadhani tungejikita kwenye hoja na sio kurekebishana lugha. Kimsingi na wewe umekosea kwa sababu yeye ameongelea wanasiasa wengi hivyo angekosea iwapo angesea wanasiasa wenye tumbo lisiloshiba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…