Wickama
JF-Expert Member
- Mar 8, 2009
- 1,466
- 1,196
presenter,Ninaitwa Athumani Ntoga, ni mtanzania na pia ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam. Wiki iliyopita tulitembelewa na ugeni mzito katika chuo chetu na nchi yetu ya Tanzania kwa ujumla. Tulitembelewa na Prof. Patrick Lumumba (P.L.O) katika kumuenzi Mwl. Julius Nyerere katika "Kigoda cha Mwalimu Nyerere" na siku hiyo PLO alikuwa mhadhiri aliyewasilisha mada. Kiukweli sikuwahi kuona mzungumzaji bora Afrika Mashariki kama Patrick Lumumba na siku hiyo alibadilisha mawazo ya watanzania wengi mno. Hakika wakenya mmebarikiwa kuwa n mtu kama PLO na ninatamani angekuwa ni Mtanzania ili tuwe tunayapata aliyonayo kila siku. Nimalizie kwa kunukuu aliyoyasema
"We are the authors of our own misfortunes"
Nilipata bahati ya kuhudhuria 2nd general assembly ya ASARECA ilifanyika mwaka jana december Bujumbura. Huyu Professor alikuwa kivutio kikubwa sana kwa washiriki toka nchi zote 11 za ECA kwa ushupavu wake wa mada na kupangilia ayasemayo.
Kwa bahati kuna professor Mtanzania anaitwa Nuhu Hatibu ambaye ni CEO wa International body (Kilimo Trust) iliyoko Uganda, huyu aliongea baada ya Lumumba. Professor Hatibu ni kivutio kikubwa na authority sana kwenye agricultural sciences/development kwenye ECA region.
Ki-ujumla afrika mashariki na kati tuna magwiji na wanataaluma wazuri sana wanaoheshimika sana na wenzetu Ulaya.
Ahsante kwa mada Athuman.
cc lawmaina78
Last edited by a moderator: