Mama saamia anajua wazi kuwa anapaswa kuweka mazingira sawia kwenye baadhi ya maeneo ya nchi ili kurahisisha kuendelea kuyashikilia maeneo husika kisiasa,tulio wengi tunaungalia uteuzi wa mama kwenye angle moja tu ya utendaji na kuziacha zingine mbili muhimu yaani angle ya kisiasa na ulinzi.
mnao shangaa kumuona chalamilla Mwanza basi mmekuwa vipofu kwenye angle ya kisiasa,kuondoka kwa mwenda zake kunaifanya kanda ya ziwa kuwa eneo linalo elea, linaweza kulalia kokote kisiasa yaani upinzani au CCM.
Na kwa historia ya eneo hili huwa halina lelemama majimbo yote mawili ya mwanza kurudi upinzani sio ishu,nampa pole ndugu yangu chalamilla ajipange amefika kunako.
Watu wa eneo hili sio wababe kama Mbeya ila wanajua jinsi ya kumkamata nyoka na kumuua bila maumivu anakufa huku anatabasamu, wajua kushambulia kwa dharula, kwa kushitukiza bila taarifa huku ukijiamini kuwa uko sawa kumbe sio sawa yaani kwa ujumla ni wanadipromasia wazuri hawatataki marumbano wala tambo ila wanajua kutenda wanapokuwa na hasira.
Kabla ya utapeli wa wizi wa kura hauja komaa waliwahi kuishanga CCM kule Bariadi,Magu na Mwanza mjini. nadhani mlio wengi mnanielewa CCM inahitaji watu wa aina gani kanda ya ziwa, Chalamilla wa Mbeya sio Chalamilla utakayemuona mwanza,Chalamila utakeyemuona mwanza ni Chalamilla mwanasiasa na anaetumia busara.
wakati ni mwalimu tusubiri.