Hongereni wanawake mnaotukataa kistaarabu, pale tunapowatongoza kistaarabu, amini mko wachache sana

Hongereni wanawake mnaotukataa kistaarabu, pale tunapowatongoza kistaarabu, amini mko wachache sana

Tafuta pesa mwanamke hatongozwi siku hizi, anatolewa out analishwa executive meal, wine, champagne, beer whatever yeye ndio atafeli hata Kama Ana bwana atakupa chiu tu usisahau kumpa handsome money for repetitive business [emoji120]
 
Tafuta pesa mwanamke hatongozwi siku hizi, anatolewa out analishwa executive meal, wine, champagne, beer whatever yeye ndio atafeli hata Kama Ana bwana atakupa chiu tu usisahau kumpa handsome money for repetitive business [emoji120]

Mi nashangaa bado vijana wana tabia za kukimbizana na wadada bara barani.
 
Nakumbuka nikiwa enzi za kupevuka kuna bidada nilimuelewa enzi hizo. Mimi nipo form 1 yeye form 2. Nilijikaza nikamface na kuomba nafasi ya kuongea nae ili nimwage mistari.

Hakuwa na maringo na alikuwa mzuri balaa. Ni wale mademu wa geti kali wazuri na kila mtu anaogopa hata kuwasalimia, akipita sehemu kila mtu anajistukia kuwa ni mchafu unaogopa asikuongeleshe.

Akanikubalia akapanga appointment tuonane. So tukaonana akanambia kwa sauti ya upole kuwa ananisikiliza. So tukaanza kuongea. Nikwamwaga mistari hadi moyo ukaridhika.

Akanambia amenielewa na huwa anapata barua zangu za mahaba na huwa zinamvutia sana maneno yangu matamu sana anajizuia tu kujibu maana anahofia kuhusu yeye na boyfriend wake.

Akanambia flan si unajua ni boyfriend wangu na nipo nae. Me nikamwambia kwan hauwezi kuwa na mimi na yeye asijue, akaniuliza, so kwa mfano nakukubalia, wewe utajiskiaje mimi nikiwa na boyfriend mwingine nje yako?

"Niambie tu kama hiyo ni sawa kwako, huoni kama nitakuwa sijafanya fair kwake kukukubalia na wakati nipo na yeye" dah nikaona hii hoja ni ya msingi amenikataa kisayansi sana hapa na hapa sina hoja ya kujibu mashambulizi wacha niachie kombe tu hizi point za uandishi mzuri wa barua na maneno matamu zinananitosha kwenye kulinda heshima yangu.

Nikamuuliza sasa mimi haya mapenzi juu yako napeleka wapi? Akanambia kama mimi pia nakupenda but tumekutana wakati mbaya sana nikiwa na mtu mwingine. Kama MUNGU amepanga tuwe pamoja then tuombe atuonyeshe njia, kama itakuwa sio mpango wake then tutamshukuru pia. But i promise you, u will always be special to me and I wont leave you alone. Please usiache kunitumia barua nzuri kama ulizokuwa ukinitumia, and i promise nitakujibu.

Dah sijawahi pigwa kibuti kitamu kama kile aisee. Yule binti akawa kila jumapili ananipitia akienda kanisani kunisalimia kitu ambacho alikuwa hafanyi kabla sijaongea nae kumtokea. Nikawa natumia kadi za sikukuu zote pasaka, Christmas, mwaka mpya. Hadi leo nikimuona huwa sijisikii chuki wala kuhisi alinichomolea.

Aiseee mtu mwenye moyo mzuri huwa anajali hata anapofanya jambo negative linakuwa tamu unajikuta hauna chuki nae
 
Back
Top Bottom