Hope Chanell ya wasabato wekeni watu waliobobea kwenye vipindi vya afya ili msivuruge watazamaji wenu

Hope Chanell ya wasabato wekeni watu waliobobea kwenye vipindi vya afya ili msivuruge watazamaji wenu

Cashman

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2018
Posts
3,333
Reaction score
5,845
Kuna somo linaendelea sasa hivi kuhusiana na ugonjwa wa kisukari.
Nasikitika kwamba mtaalamu mliyemuweka kufundisha somo hilo,anatumia rejea ya elimu za kizamani sana ambazo zimepitwa na wakati.

Kusema mtu mwenye kisukari aepuke kula nyama na mayai kwamba umeng'enyaji wa protini hizo ni mgumu na kwamba mfumo wa umeng'enyaji wa mtu kwenye kisukari umeshaarika.
Jambo hili sio sahihi.Maana vyakula vya wanga ndivyo hasa vinaweza kuwa na changamoto kwa mtu mwenye kisukari kwa sababu ndivyo kwa kiasi kikubwa vinategemea insulin.

Pia amekataza ulaji wa mafuta na huku akishauri watu wanywe juisi za matunda walizotengeneza wenyewe.
Hii inaweza kuwa hatari zaidi kwa mtu mwenye kisukari.
Juusi ya matunda ina sukari nyingi sana kiasi kwamba ni bora ule tunda lenyewe kuliko unywe juisi unaweza kujikuta umekula machungwa sita kwa wakati mmoja kupitia juisi tu.

Mafuta ya wanyama ni mazuri hasusan nyama yenye mafuta kwa sababu inaleta kujisikia kushiba na kutopata njaa upesi.
Pia mafuta hayasababishi ongezeko kubwa la insulini kama ilivyo kwa sukari na wanga.

Nashauri mtu akipewa kipindi kama hicho kiwe mubashara watu waulize maswali.Mtu kama hajajipanga asije kwenye kipindi
 
Back
Top Bottom