Hospitali binafsi siyo wa pigaji wa hela kama wengine wanavyofikiria

Hospitali binafsi siyo wa pigaji wa hela kama wengine wanavyofikiria

ZALEMDA

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2017
Posts
1,956
Reaction score
2,225
Kiukweli hospitali binafsi hazipati au kupiga hela kama wengine wanavyofikiria, tofauli na hospitali za Serikali ambazo zinapata ruzuku kutoka Serikalini pamoja mishahara kutoka hazina, private hospital zinajitegemea 100% katika kutoa huduma zote. Hakuna ruzuku yoyote wanayoipata kutoka Serikalini na hakuna msamaha wowote wanaopata kutoka kwa mamlaka za serikali kama ni VAT wanalipa zote.

Kibaya zaidi huduma za NHIF zimepangwa kimakundi kulingana na level ya kituo, unakuta kwenye level ya wilaya ukifanya upasuaji mkubwa kwa mteja wa bima unalipwa 110,000 wakati upasuaji huo ukifanyika ngazi ya hospitali ya rufaa unalipwa 700,000 lakini dakitari ni yule yule, nesi yule yule, nyuzi zile zile, kitanda kile kile, shuka ile ile,nk


Binafsi siwezi wekeza hela zangu kwenye sekta ya afya.
 
Back
Top Bottom