DOKEZO Hospitali ya Aga Khan yadaiwa kufunga baadhi ya Vituo vyake Tanzania, Mamia wadaiwa kupoteza Ajira

DOKEZO Hospitali ya Aga Khan yadaiwa kufunga baadhi ya Vituo vyake Tanzania, Mamia wadaiwa kupoteza Ajira

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kwamba hiyo sheria ni dhaifu?
Umesomea kipengele Cha mwisho kwenye fair termination?
Lakini unajua maana ya Kampuni kufilisika kweli? Achana na hizi za serikali.... It's sad
Vituo vingu vya Aga Khan visingefanya vizur on the go hata walivyoanza tu..
Bunda, Mabibo, Kahama (at least) nk

Kingine ni ku set premier pricing wakati wananchi wengi ni masikini sana ...
It's more of a business knowledge kuliko Kaz perse...
Good intention but bad idea from the inception....
 
View attachment 3067994
KUNA taarifa za kufungwa Kwa baazi ya vituo vya kutolea huduma ya afya vilivyopo chini ya Taasisi ya Aga Khan,Tanzania kwasababu za changamoto za kiuendeshashaji.

Fununu hizo zinaeleza kuwa Taarifa zimetokana na mkutano uliofanyika na mtendendaji mkuu wa Taasisi hiyo nchini,Kupitia mtandaoni na kuhudhuliwa na baazi ya wafanyakazi.

Mtendendaji huyo amesema kwamba kutokana na changamoto za kiuendeshaji, Taasisi inalazimika kufunga baazi ya vituo na kupunguza wafanyakazi.

Hata hivyo,Kwa mujibu ya mmoja wa wafanyakazi wa Taasisi hiyo akizunguumza Kwa faragha na Mdau TZ,amekili kuwa Taarifa hizo ni za kweli na zoezi la kufunga vituo hivyo limeshaanza na mwisho wa uendeshaji wake inatarajiwa ni mwishoni mwa wiki hii ambapo itakuwa Tarehe 15/8/2024.

Mtoa Taarifa huyo amesema kwamba tayari baazi ya wafanyakazi waliokuwa wakifanya kazi katika vituo vinavyofungwa na wale wanaopunguzwa kutoka kwenye vituo vinavyosalia wameshapewa barua za mualiko wa majadiliano ya kuachishwa kazi.

MY TAKE.

KATIKA Hili waajili wengi wanatumia udhaifu wa Sheria ya Kazi inayotumiKa nchini katika kuwachisha kazi wafanyakazi wao pindi tu Taasisi inapopitia changamoto kidogo.

Sheria imempa wigo Mpana mwajili wa kufanya maamuzi bila ya kujali hali ya mwajiliwa.

Pia kutokana na urahisi waliopewa katika kipengele Cha kupunguza wafanyakazi hasa Kwa sababu za kiuendeshaji.

Ni wakati wa mamlala hisika kufikiria kufanya mabadiliko ya sheria hii ili kuwapa ulinzi na uhakika wa ajira kwa wafanyakazi.
Mleta mada ulitaka muajiri hapo afanye nini ikiwa mzigo wa kuendesha taasisi umemshinda?
Kama mwajiri ataamua kuwashisha kazi kwa kufuata sheria basi hana kosa lolote, huwezi kumlaumu chochote na wafanyakazi hawapaswi kulalamika kwa chochote maana walijua huo utaratibu hata kabla ya kuajiriwa.
 
Kuhudhuliwa na baazi✖️
Kuhudhuriwa na baadhi✔️
Amekili✖️
Amekiri✔️
Waajili✖️
Waajiri✔️
Mwajili✖️
Muajiri✔️
Mwajiliwa✖
Muajiriwa✔️
Cha msingi umepata taarifa acha mambo ya ajabu watu waliopata F ya hesabu mna shida sana
 
Mleta mada ulitaka muajiri hapo afanye nini ikiwa mzigo wa kuendesha taasisi umemshinda?
Kama mwajiri ataamua kuwashisha kazi kwa kufuata sheria basi hana kosa lolote, huwezi kumlaumu chochote na wafanyakazi hawapaswi kulalamika kwa chochote maana walijua huo utaratibu hata kabla ya kuajiriwa.
Wana retrench wazawa tu. Ma expatriates wanaokula mishahara mikubwa hawaja guswa. Ni ubaguzi full-time.
 
Mleta mada ulitaka muajiri hapo afanye nini ikiwa mzigo wa kuendesha taasisi umemshinda?
Kama mwajiri ataamua kuwashisha kazi kwa kufuata sheria basi hana kosa lolote, huwezi kumlaumu chochote na wafanyakazi hawapaswi kulalamika kwa chochote maana walijua huo utaratibu hata kabla ya kuajiriwa.
Ma expatriates wanaokula mishahara mikubwa hawaja guswa na zoezi hilo. Ni wazawa tu ndiyo wanaachishwa kazi.
 
Hii ni dalili kuwa mazingira ya wafanyabiashara na watoa huduma nchini ni mbaya sana.kodi na tozo lukuki zinawafanya wawekezaji waanze kufunga shughuli zao.serikali kaeni chini,acheni kubambika tozo na kutumia kikosi kazi Cha kijambazi Cha TRA kusumbua wawekezaji.Nchi hii shida sana.
 
Kuna ya taarifa za kufungwa kwa baadhi ya vituo vya kutolea huduma ya afya vilivyopo chini ya Taasisi ya Aga Khan, Tanzania kwa sababu za changamoto za kiuendeshashaji.

Fununu hizo zinaeleza kuwa Taarifa zimetokana na mkutano uliofanyika na mtendendaji mkuu wa Taasisi hiyo nchini, kupitia mtandaoni na kuhudhuliwa na baadhi ya wafanyakazi.

Mtendendaji huyo amesema kwamba kutokana na changamoto za kiuendeshaji, Taasisi inalazimika kufunga baadhi ya vituo na kupunguza Wafanyakazi.

Hata hivyo, kwa mujibu ya mmoja wa wafanyakazi wa Taasisi hiyo akizunguumza kwa faragha na Mdau Tanzania, amekili kuwa Taarifa hizo ni za kweli na zoezi la kufunga vituo hivyo limeshaanza na mwisho wa uendeshaji wake inatarajiwa ni mwishoni mwa wiki hii ambapo itakuwa Tarehe 15/8/2024.

Mtoa Taarifa huyo amesema kwamba tayari baadhi ya wafanyakazi waliokuwa wakifanya kazi katika vituo vinavyofungwa na wale wanaopunguzwa kutoka kwenye vituo vinavyosalia wameshapewa barua za mualiko wa majadiliano ya kuachishwa kazi.

MY TAKE
Katika hili waajiri wengi wanatumia udhaifu wa Sheria ya Kazi inayotumiKa nchini katika kuwachisha kazi wafanyakazi wao pindi tu Taasisi inapopitia changamoto kidogo.

Sheria imempa wigo Mpana mwajili wa kufanya maamuzi bila ya kujali hali ya mwajiliwa.

Pia kutokana na urahisi waliopewa katika kipengele cha kupunguza wafanyakazi hasa kwa sababu za kiuendeshaji.

Ni wakati wa mamlala hisika kufikiria kufanya mabadiliko ya sheria hii ili kuwapa ulinzi na uhakika wa ajira kwa wafanyakazi.

View attachment 3068018
Mzanzibari nchi imemshinda aondoke tu
 
udhaifu wa Sheria ya Kazi inayotumiKa nchini katika kuwachisha kazi wafanyakazi

Sera mbovu za huduma ya afya na mifuko ya bima za afya inayovuja, kukopwa, kushindikizwa kuwekeza fedha za bima ktk miradi yenye msujumo wa kisiasa bila kusahau mifuko ya bima kukosa usimamizi mzuri nchini ni suala la serikali kuu, hili nalo linafaa kupewa shutuma.

Yatokanayo na hayo madhaifu ndiyo kunapatikana masuala mtambuka watu kukosa hata huduma bora za kulipia au zilizokatiwa bima, vituo vya afya kufungwa na wafanyakazi kupunguzwa n.k


Wizara ya Afya
https://www.moh.go.tz › mifumo-...
mifumo isomane kuleta matumizi sahihi ya fedha za mifuko ya bima ...


11 Oct 2023 — “Tunahitaji kufika mahali mifumo ya afya isomane katika ngazi zote itasaidia kupuguza matumizi mabaya ya fedha za mfuko wa bima....
 
Kampuni inatakiwa iendeshwe kwa faida.

Inatakiwa kwamba kama mwezi huu imetengeneza 10K mwezi ujao itengeneze kuanzia 15K, unaofuatia iwe kuanzia 17K n.k.

Ikiwa hivi maana yake faida ipo na mtaendelea kulipana mishahara, ila ikiwa kinyume itabidi gharama za uendeshaji zipunguzwe.

Bahati mbaya gharama za uendeshaji humgusa anayekesha kuhakikisha huduma zinaenda wakati wakuu wa idara n.k. ambao hata hawajahi kuovertime hawaguswi.

WaTz wachache tumefanya kazi kampuni ambazo zinakupa target na ukizishindwa unakua terminated nafikiri ndiyo maana mleta uzi analalamika.

Anyway, swali kuu "Kampuni hua haiwezi kupredict kwamba kwa mwendo wa sasa tutarajie anguko?" "Waliajiri BDM?" "Alikua competent?"
 
retrench wazawa tu. Ma expatriates

Pengine expatriates ndiyo wenye utaalamu unauhitajika Aga Khan Hospital iishi, ila hali mbaya ya kisera ya serikali kuhusu huduma ya afya ni suala la muda tu nao expatriates watatupiwa virago au watakimbia wenyewe kwenda nchi zingine kwa kuwa wana utaalamu unaofukuziwa duniani kote.

Utasikia wataalamu expatriates wakikimbia Tanzania, wamepata ajira Dubai, Qatar, Namibia, Australia n.k
 
Back
Top Bottom