Hospitali ya Agakhan yasema haijazidiwa na wagonjwa wa Corona, yataka wajawazito kuhudhuria Kliniki

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Hospitali ya Aga Khan imesema siyo kweli kwamba wodi zake zimejaa wagonjwa wa Corona bali wapo wagonjwa wenye matatizo mbalimbali.

Mtendaji mkuu wa hospitali hiyo amemwambia Katibu mkuu wa wizara ya afya Prof Mchembe kwamba akina mama wajawazito wameacha kwenda Kliniki kufuatia uvumi huo na akatumia nafasi hiyo kuwataka watu wote wenye ratiba za kliniki waendelee kuja kwani hospitali iko salama.

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama
 
Kwanini ayaseme hayo baada ya kutembelewa na Katibu mkuu wa wizara ya afya? Angeweza kusema tofauti na hivyo?

Tanzania si hakuna Corona, sasa nini mantiki ya kusema wodi zao bado hazijajaa wagonjwa wa Corona?

Sasa hospitali inaita watu waende hospitali kutibiwa!!!
 
Hata mkipamba lugha johnthebaptist . Corona ipo na inakula vichwa mdogo mdogo.

Kwani uongozi wetu una tatizo gani na Corona ?!. Mpaka tujifanye kama vile ugonjwa haupo huku upo !!

Kuwa na Covid 19 si aibu
 
Je wana charge pesa nyingi au hapana hao jamaa wame chukuwa 38m na mtu kafa
 
Serekali iwe macho hawa jamaa Nina hisi wanaweza tumika kujaribu chanjo za India hapa kwetu!
 
Kwanini ayaseme hayo baada ya kutembelewa na Katibu mkuu wa wizara ya afya? Angeweza kusema tofauti na hivyo?

Tanzania si hakuna Corona, sasa nini mantiki ya kusema wodi zao bado hazijajaa wagonjwa wa Corona?

Sasa hospitali inaita watu waende hospitali kutibiwa!!!
Za kuambiwa changanya na zako
 
Hospitali ya Aga Khan imesema siyo kweli kwamba wodi zake zimejaa wagonjwa wa Corona bali wapo wagonjwa wenye matatizo mbalimbali.

Mtendaji mkuu wa hospitali hiyo amemwambia Katibu mkuu wa wizara ya afya Prof Mchembe kwamba akina mama wajawazito wameacha kwenda Kliniki kufuatia uvumi huo na akatumia nafasi hiyo kuwataka watu wote wenye ratiba za kliniki waendelee kuja kwani hospitali iko salama.

Source ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
Wee Mama

Sawa tumekupata wee Mama..
Naona unataka kutujulisha tu kwamba kliniki ya huo ujauzito wako unaenda Agha Khan.
 
Tanzania si hakuna Corona, sasa nini mantiki ya kusema wodi zao bado hazijajaa wagonjwa wa Corona?

Sasa hospitali inaita watu waende hospitali kutibiwa!!!
Maana yake ni kwamba wagonjwa wa covid19 wapo pale japo wodi hazijajaa. Anauekataa kwamba corona haipo anajidanganya na anajua anachokifanya
 
Back
Top Bottom