DOKEZO Hospitali ya Mloganzila inatumia wanafunzi (interns) kuhudumia wagonjwa mahututi, na manesi wana huduma mbaya, mnatumaliza

DOKEZO Hospitali ya Mloganzila inatumia wanafunzi (interns) kuhudumia wagonjwa mahututi, na manesi wana huduma mbaya, mnatumaliza

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Huduma za afya kwa mgonjwa mahututi kibongo bongo wanataka utangulize pesa mbele.
Maana wao wanajuwa ikiwa huyo ni ndugu yako na unampenda utamgharamia ingawa kiuhalisia wa maisha pesa inaweza mtu akawa hana.
 
Kuna ndugu yangu mmoja anafanya kazi Mloganzila aliniambia nikajifungue kule nilikataa nikamuambia kuna huduma mbaya watu wanakufa akaniambia shida moja wagonjwa wengi ni wa rufaa unakuta mpaka analetwa Mloganzila kashakuwa hali mbaya hawaletwi hali nzuri wnaapoteza maisha lawama kwetu sababu wanaletww critical condition.
Yaani ungeenda kujifungua ungefurahi mwenyewe.wana level za aghakhan
 
Kwa mloga kwa kuwa ni teaching hospital siwezi kushangaa sasa muhimbili usiku asilimia kubwa unakuta wanabaki intern nimewahi kushuhudia dogo anapiga sim kwa chief anamwambia hii issue ni ngumu anataka ushauri.
Sasa wanafunzi watajifunzaje??
Ila mimi nilichooona ukiingia kwa daktari.daktari anakuwepo na mwanafunzi au wanafunzi wawili wako nae pembeni.kuna ubaya gani? Na wodini madaktari wanakuja mara kwa mara.wale wanafunzi wanaweza kupita Tu ila mwenye maamuzi ni daktari bingwa.na wale wanafunzi me naona wanasaidia Sana kuliko mgonjwa ungeachwa Peke yako
 
Sasa wanafunzi watajifunzaje??
Ila mimi nilichooona ukiingia kwa daktari.daktari anakuwepo na mwanafunzi au wanafunzi wawili wako nae pembeni.kuna ubaya gani? Na wodini madaktari wanakuja mara kwa mara.wale wanafunzi wanaweza kupita Tu ila mwenye maamuzi ni daktari bingwa.na wale wanafunzi me naona wanasaidia Sana kuliko mgonjwa ungeachwa Peke yako
Ni kweli kabisa mchana haina shida ila usiku wanapobaki peke yao sometime inakuwa sio sawa umewahi kulazwa muhimbili ukaona kinachoendelea wakati wa usiku.
 

ZIPI HATUA ZA KISHERIA ZA KUCHUKUA JUU YA HOSPITALI KWA UZEMBE KWA MGONJWA?​


 
Pole sana mkuu Kuna rafiki yangu aliwahi kunambia kama nataka mgonjwa wangu afariki haraka basi nimpeleke Mloganzila
 
Pole sana ndugu....wengine wana exp safi wengine mbaya....
 
Kifo hakikosi sababu, Hakikosi wa kutupiwa Lawama.

Naamini kama siku yako bado basi Bado Tu, Binafsi naamini katika PESA huduma bora sidhani kama kuna hospital inatoa hii nchi ni ubahatike tu.

Mwl wangu alifia Mloganzila, Alikua anapungua damu na hawajui zinavujia wapi.

Anaongezwa damu leo pakikucha damu imeshuka

Anaongezwa asubuhi jioni imeshuka, inakaa stable siku mbili siku ya tatu inaporomoka..

Mloganzila wamechemkaaa Mtu akaenda..wamempma kila kipimo ila holaaa...

Naamini mimi ni PESA tu otherwise upate ugonjwa wa kawaida ndio utaisifia mloganzila ila magonjwa pasua kichwa yanayohitaji PESA,VIFAA,PROFESSIONALS asee heri ya MUHIMBILI sio.mloganzila.
 
Kuna mdogo wangu alilazwa pale aliandikiwa kwenda kufanyiwa kipimo cha MRI mpaka anafariki hakufanyiwa hicho kipimo kisa hakuna wa kumpeleka kwenye hiyo machine,labda useme wewe una mtu wa kukushika mkono
Mimi nilimpeleka mama pale MRI ilichukua siku tatu MRI mbovu ilipokuja kuwa sawa na kupimwa daktari wa kusoma hayupo na hata majibu yalipotoka na yalivyosomwa na kuambiwa arudi tena kwa ajili ya clinic majibu hayakuonekana wala hawakuwa na taarifa kuwa warudi. Mgonjwa wangu alikuwa na stroke analalamika kichwa kinamuuma hakuna nesi wala daktari anayefanya kitu , unawafuata unawaambi hawatake any action , inabidi sasa kumfuata umsimamie ampe dawa za maumivu. Hiyo hospitali inashida kubwa
 
Back
Top Bottom