Hospitali ya Muhimbili izingatie weledi katika kutoa taarifa wakati wa Majanga!

jingalao

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Posts
36,197
Reaction score
29,717
Nasikitika kuona "kiherehere" cha hospitali ya Taifa ya Muhimbili katika kutoa Taarifa zinazohusu majanga bila kuzingatia chain of command.

Sio afya kwa hospitali hii as an entity kukimbilia kwenye media na kutoa taarifa bila kuzingatia taratibu za uhabarishaji umma wakati wa tukio la majanga.

Nilitegemea kuona strictly taarifa zinatoka kutokea kwa mamlaka zilizokasimiwa kutoa taarifa wakati wa majanga.

mfano:Mganga Mkuu wa Serikali...Mkuu wa Mkoa,Mkuu wa Wilaya au Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaamu.

Haitakiwi kuwa na taarifa zilizo vipande vipande bali taarifa moja tu kutoka kwa relevant authority...sasa kama tunaanza kuwa na taarifa za Muhimbili,Amana,Mnazi mmoja n.k hii ni chaos ...tuzingatie weledi bana!!

Maoni yangu :Tupunguze kukurupuka linapokuja swala la majanga na dharura na tuzingatie weledi !

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!
IMG-20241116-WA0036.jpg
 

Attachments

Kwanza Muhimbili siyo kazi yao kutoa taarifa. Taarifa zinatolewa na Mkuu wa jeshi la polisi wa eneo husika, na watu wenye mamlaka ya uokoaji ambao ni jeshi la zima moto.
 
Nasikitika kuona "kiherehere" cha hospitali ya Taifa ya Muhimbili katika kutoa Taarifa zinazohusu majanga bila kuzingatia chain of command...
Najua watu watakunanga ila upo sahihi kabisa. Hii nchi suala la kufuata utaratibu imekuwa tatizo sugu. Sasa Janabi anaenda na lile coat lake Jeupe la nini? Halafu ndiyo mkurugenzi.. Napata mashaka makubwa!
 
Najua watu watakunanga ila upo sahihi kabisa. Hii nchi suala la kufuata utaratibu imekuwa tatizo sugu. Sasa Janabi anaenda na lile coat lake Jeupe la nini? Halafu ndiyo mkurugenzi.. Napata mashaka makubwa!
kunangwa sio tatizo...mimi huwa nasimama na miongozo na weledi siku zote.atakayechukia achukie tu kwani ni haki yake kuchukia .Ila utaratibu ni muhimu kufuatwa na wote...awe anayejua,au asiyejua
 
Wenye mamlaka ya kutoa taarifa ni hospital husika ila kwasababu nchi yetu inaendeshwa kisiasa ndio maana unaona wanasiasa ndio wenye haki ila sio kweli.
 
Back
Top Bottom