Hospitali ya Mzena inamilikiwa na nani? Kwanini iitwe Mzena?

Hii hospitali iko pale Makumbusho kwenye makaaazi yale ya usalama wa taifa
Ukitoka Makumbusho kama unaenda Moroco mkono wa kushoto kuna njia inaingia kuna majengo kama apartment kuna ulinzi mkali sana huwezi hata kusogea hapo nd usalama wa taifa wanapoishi na ndipo hiyo hosp ilipo
Wanatibiwa viongozi wakubwa pekee
 
🤔
 

Kwa nini inaitwa Mzena?
 
Zamani iliitwa Ikulu clinic (Ikulu hospital)

Mpaka nahisi mwaka 2005 ilipobadilishwa jina na kupewa jina la Emilio Mzena Memorial hospital

Ikiwa ni kumuenzi aliyekuwa DGIS wa kwanza nchini (mkurugenzi mkuu wa usalama wa Taifa wa kwanza nchini) marehemu Emilio Mzena

Mmiliki wa hospitali ni Idara ya usalama wa Taifa

Ipo Makumbusho eneo ambalo pia ni kota za PSU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…