KERO Hospitali ya Taifa Muhimbili (Mloganzila) Madaktari wanafunzi ni Janga. Watu wanakufa kwa uzembe

KERO Hospitali ya Taifa Muhimbili (Mloganzila) Madaktari wanafunzi ni Janga. Watu wanakufa kwa uzembe

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Hii hospitali kama serikali na uongozi hautachukua hatua za haraka watanzania wengi wataendelea kufa kwa uzembe wa madaktari wanafunzi ambao hawasimamiwi ipasavyo na wakuu wao kazi.

Nimeshuhudia mgonjwa wangu akiambiwa hana tatizo lolote la nyonga baada ya kumpeleka akiwa amepata ajali na daktari ambaye ni mwanafunzi kusoma vipimo akatuambia mgonjwa aendelee na dawa alizopewa ( tulianzia matibabu hospitali ya wilaya kabla ya kwenda hapo mloganzila)

Tulipata mashaka na tukarudi tena kuomba uchunguzi zaidi ndipo daktari msimamizi wa mwanafunzi huyo alipokuja nadhani alikua kikaoni na baada ya kupitia tena vipimo alibadilika ghafla na kuwa mkali sana na kumfokea yule daktari mwanafunzi kuwa kwanini hajaona tatizo la nyonga kuvunjika? Na ni eneo hatari sana kwa mgonjwa? Japo alikua akimfokea kwa kiingereza ila tuliweza kujuwa kuwa daktari mwanafunzi alizembea katika matobabu ya ndugu yetu.
Nashukuru tumepangiwa tarehe ya operesheni. Ila nimeondoka na maswali mengi kichwani je ni wagonjwa wa ngapi wanaopitia hali kama tuliyopitia sisi?

Naomba serikali na uongozi mzima wa hospitali ya taifa ya Muhimbili (mloganzila) kuchukua hatua za haraka kuokoa maisha ya watanzania.
Ukweli mtupu, ni nchi nzima siyo tu huko. Kuna daktari mwanafunzi mmoja ilibidi nimzuie alichokuwa akimfanyia mwanangu baada ya kugundua anajifunzia Kwa mwanangu na kumsababishia maumivu makali Kwa matibabu aliyokuwa akiendelea kumfanyia!
 
Mm nahisi matokeo ya elimu yetu ya bongo yameanza kutoka
Mwezi uliopita kuna mgonjwa alipata ajari tumeanza nae sinza Palestine kwa huduma ya kwanza kwavile ilikuwa usiku wakasema muda wa kunya x ray umeisha kwahyo tumpeleke Mwananyamala tumeenda mwanyamala kwanza nakuta madaktari wote vijana ambao wanaonekana hawana muda mrefu kazin wakamfanyia mgonjwa x ray ya kwny kiuna na kwny ankle majibu yalivyotoka naona wanashauriana hii itakufracture wakarudisha majibu kama walivyoo shauliana kesho yake mgonjwa kamiishiwa MOI majibu yametoka vingne kbsa
 
Mloganzila, a.k.a lango la kuzimu, hata tafsiri ya jina "mloga-nzila" ni jibu tosha
 
Mimi kwa kweli sitaki kubeza hospital, Maana ni sehemu pekee ambapo unaweza jikuta upo hapo na unahitaji msaada ukiwa hata hujoelewi
Hata mimi sibezi mkuu lakini lazima tuseme penye kasoro. Madaktari wanafunzi wasiachiwe kufanya kazi zenye uhitaji utaalamu mkubwa bila usimamizi wa wakuu wao wa kazi.
 
Hii hospitali kama serikali na uongozi hautachukua hatua za haraka watanzania wengi wataendelea kufa kwa uzembe wa madaktari wanafunzi ambao hawasimamiwi ipasavyo na wakuu wao kazi.

Nimeshuhudia mgonjwa wangu akiambiwa hana tatizo lolote la nyonga baada ya kumpeleka akiwa amepata ajali na daktari ambaye ni mwanafunzi kusoma vipimo akatuambia mgonjwa aendelee na dawa alizopewa ( tulianzia matibabu hospitali ya wilaya kabla ya kwenda hapo mloganzila)

Tulipata mashaka na tukarudi tena kuomba uchunguzi zaidi ndipo daktari msimamizi wa mwanafunzi huyo alipokuja nadhani alikua kikaoni na baada ya kupitia tena vipimo alibadilika ghafla na kuwa mkali sana na kumfokea yule daktari mwanafunzi kuwa kwanini hajaona tatizo la nyonga kuvunjika? Na ni eneo hatari sana kwa mgonjwa? Japo alikua akimfokea kwa kiingereza ila tuliweza kujuwa kuwa daktari mwanafunzi alizembea katika matobabu ya ndugu yetu.
Nashukuru tumepangiwa tarehe ya operesheni. Ila nimeondoka na maswali mengi kichwani je ni wagonjwa wa ngapi wanaopitia hali kama tuliyopitia sisi?

Naomba serikali na uongozi mzima wa hospitali ya taifa ya Muhimbili (mloganzila) kuchukua hatua za haraka kuokoa maisha ya watanzania.
Kweli kabisa mm pia nj muhanga WA Hilo bila specialist kuingilia kati siku hiyo nilikuwa napoteza hope kwa kada hii ya udaktari. We eti madaktari hawakujua naumwa nni wakaanza kukugoogle
 
Wakubwa wao wako busy sites za dada poa wanatafuta huduma...umkute ofisini hapo kavaa miwani yake kwny computer utajua anafanya kazi ya maana kumbe upupu...kama ni wanawake wapo busy na majungu kusemana...hii nchi Magufuli ndo aliwakomesha watumishi wa uma...kwa sbb alisikiliza kero direct na kutake actions...hapa mpk kijiji kipuputike ndo bi mdashi ataongea...
Nimeishia hapo kwenye upupu😂😂
 
Back
Top Bottom