Hospitali ya Taifa Muhimbili yatoa neno baada ya vitanda kuonekana nje

Hospitali ya Taifa Muhimbili yatoa neno baada ya vitanda kuonekana nje

Cannabis

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2014
Posts
11,557
Reaction score
33,535
20210216_091730.jpg

IMG_20210216_091902.jpg

Hospitali ya Taifa Muhimbili imesema kuwa huwa inao utaratibu wa kupuliza dawa ya kuuwa wadudu karibu maeneo yote ya hospitali na kwamba wakati wa zoezi hilo wagonjwa hutolewa nje na kuwekwa chini ya mahema.

Kauli hiyo imetolewa kupitia ukurasa wa mtandao wa Twitter wa hospitali hiyo, baada ya picha kusambaa mitandaoni zikionesha vitanda vya hospitali hiyo vikiwa vimetolewa nje na kuwekwa kwenye mahema.

"Hospitali ina kawaida ya kupuliza dawa ya kuua wadudu mbalimbali wodini, maofisini na maeneo mengine ya nje mara mbili kwa mwaka, wakati zoezi likifanyika, wagonjwa hutolewa nje na kuwekwa chini ya mahema huku huduma nyingine zikiendelea, hili ni zoezi la kawaida na endelevu", imeeleza taarifa hiyo.
 
Kupulizia muhimu wodi wanalazwa watu wenye migonjwa ya kila namna ya ngozi ya upele ya vifua vikuu nk lazima muda upulizie dawa.Ukiingia ofisi kama za Chadema huwa hawapulizii dawa kuna siku nimeingia pale makao makuu kama mwandishi wa habari nilikohoa mfulululizo sijawahi rudi tena
 
Ha ha
 
Hili ndo tatizo kubwa la watanzania...

Wakiambiwa ukweli wa mambo kwa nn vitanda viko nnje wanapinga majibu na wanakuja na majibu yao

Dawa ni kuwadanganya au kuwapa majibu siyo....maana majibu halisi huwa wanayapinga .
 
Back
Top Bottom