SoC02 Hospitali za Rufaa kuwaachia majukumu yote ya kitabibu wanafunzi wa udaktari pasipo usimamizi wa kutosha - chanzo cha vifo vingi

Stories of Change - 2022 Competition

cupvich

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2022
Posts
408
Reaction score
247
UTANGULIZI
Nikiwa wodini nauguza mgonjwa wangu katika moja ya hospitali kubwa ya Rufaa nchini, Nilimsikia daktari mmoja akitumia lugha ya kiingereza kuwaambia wanafunzi wanao somea udaktari ambao walikuwa wakitoa huduma kwa mgonjwa aliyekuwa kitanda cha pembeni na alicho mgonjwa wangu maneno haya nanukuu "MMEKOSEA, HAMKUTAKIWA KUMCHOMA SINDANO HIYO". Hakika nafsi yangu iliogopa sana, Nilihisi kana kwamba amefanyiwa mgonjwa wangu, hivyo niliwaza iwapo angekuwa ni mgonjwa wangu na nimesikia maneno yale ya daktari ningechukua hatua gani. Ilinifanya kufuatilia kwa ukaribu maendeleo ya Mgonjwa yule tokea siku ile kwasababu nilikuwa pale kwa wiki moja nikimuuguza mgonjwa wangu, Baada ya siku moja nilipewa taarifa kuwa Mgonjwa yule alifariki Dunia.

Hospitali zetu za rufaa zimekuwa kimbilio kwa walio wengi katika suala zima la matibabu, hii ni kutokana na kuaminika kwamba zina wataalamu wa kutosha. Lakini pia zinaweza kutoa huduma za kibingwa. Kwa hapa kwetu Tanzania tumebarikiwa kuwa na Hospitali za rufaa za mikoa lakini pia tuna hospitali za rufaa za kanda kama vile HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA MBEYA, HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA KCMC, HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA BUGANDO pamoja na hospitali kubwa ya taifa MUHIMBILI. Hospitali hizi za rufaa za kanda zina Vyuo ambavyo hutoa mafunzo kwa wataalamu wa Afya kama vile madaktari, manesi na wafamasia. Vyuo hivyo ni MUHAS,BUGANDO, MCHAS, na KCMCo pamoja na vyuo vingine vinavyopatikana katika hospitali za mikoa na Hospitali zingine za Binafsi na mashirika ya dini.

Wanafunzi hawa wa udaktari walioko wafunzoni wamekuwa wakitumia muda mwingi kufanya mazoezi kwa vitendo katika hospitali zetu jambo ambalo ni Zuri kwani linawajenga na kuwaimarisha vyema katika Sekta hiyo muhimu ya afya. Lakini pia wamekuwa wakirahisisha utoaji wa huduma za afya kwa kuongeza wahudumu wa afya katika hospitali zetu ukizingatia kwamba vituo vingi vya afya pamoja na hospitali zetu Bado zina changamoto kubwa ya upungufu wa wataalamu wa Afya. Kwa ujumla wanataalamu hawa walioko mafunzoni hususani madaktari wanafanya kazi kubwa.

TATIZO LINAANZIA HAPA.
Kwa Bahati mbaya, hospitali zetu zimewaamini Wanafunzi hawa walioko vyuoni kupitiliza kiasi cha Kuwapangia Zamu za kuwaona wagonjwa pasipo usimamizi wa daktari mzoefu na kufanya matibabu kwa mgonjwa hata kwa wagonjwa ambao wako katika hali mbaya. Jambo ambalo ni Hatarishi kwa afya ya mgonjwa. Hii imesababisha kutokea kwa vifo vingi kutokana na kwamba wanafunzi hawa wa afya hawajawa bado na Utaalamu wa kutosha katika kutoa huduma za afya kwa kiwango kinachostahili ukilinganisha na madaktari wazoefu.

CHANZO CHA TATIZO.
Ni kweli kwamba siku hizi Teknolojia imerahisisha ufanyaji wa kazi katika hospitali zetu.Teknolojia imechukua nafasi kubwa sana katika utoaji wa huduma katika vituo vya afya na Hospitali, na ndio maana utakuta Daktari anayeingia katika zamu ya usiku anaweza kumfahamu vizuri mgonjwa aliyelazwa wodini, matibabu aliyoyapata na matibabu anayotakiwa kuyapata hivyo kumrahisishia kuendeleza matibabu kwa mgonjwa. Lakini ukuaji huu wa Teknolojia usiwe Sababu ya kuwaachia majukumu yote wanafunzi wa udaktari walioko Vyuoni kwani waliowengi bado hawajapata maarifa ya kutosha katika kutoa huduma za kitabibu. Lakini pia wingi wa hawa wanafunzi katika hospitali zetu kisiwe kigezo cha madaktari wazoefu na wenye majukumu ya kutoa huduma za afya kusahau wajibu wao wa kuwahudumia wagonjwa. Wengi wa hawa wanafunzi wa udaktari wamekuwa wakitoa huduma kwa hisia ili tu kukamilisha matakwa ya kozi wanazosomea ikiwa ni pamoja na kufanya mazoezi kwa vitendo. na hivyo kuhatarisha maisha ya mgonjwa.

ATHARI ZITOKANAZO NA TATIZO HILI.
Utakubaliana nami kuwa Siku zote Mwanafunzi atabaki kuwa mwanafunzi, hata kama ni mwanafunzi wa udaktari mwaka wa nne au wa tano. Na sifa mojawapo aliyonayo mwanafunzi ni kutokujiamini kwa asilimia mia moja, hivyo kupelekea kufanya jambo kwa Jazba na Mihemko ilimradi tu kukamilisha takwa fulani. Hivyo nilazima uongozi wa hospitali zetu uwachukulie wataalamu hawa wa afya kama wanafunzi na kuwasimamia katika huduma zote za kitabibu katika hospitali zetu kwa manufaa mapana ya mgonjwa na mtoa huduma.

Kutokana na kuwatumia madaktari mafunzoni katika hospitali zetu hizi za rufaa, Huduma katika hospitali hizi zimekuwa zikishuka kadiri siku zinavyokwenda licha ya serikali Kuwekeza kiasi kikubwa cha fedha katika kuboresha mazingira ya utoaji huduma katika hospitali hizi, ikiwa ni pamoja na Ununuzi wa vifaa vya kutolea huduma za afya, Uongezaji wa majengo ya kutolea huduma za afya na kuongeza watumishi wa afya. Jambo hili si zuri kwasababu linapunguza imani kwa wananchi hivyo kutumia gharama kubwa kupata matibabu katika hospitali za binafsi.

Usalama wa mgonjwa awapo hospitalini ni muhimu sana. Muda mwingi mgonjwa hubaki na wataalamu wa afya kwa ajili ya matibabu. Hivyo ndugu jamaa na marafiki huamini kuwa Daktari au mtaalamu yeyote wa afya ana nafasi kubwa katika kuokoa maisha ya Mgonjwa. Wote tunaamini kwamba mtaalamu yeyote wa afya anatakiwa awe na ujuzi wa kutosha katika kumhudumia mgonjwa ili kuokoa maisha yake. Iwapo mtaalamu huyo wa afya atakosa ujuzi na maarifa ya kutosha maisha ya mgonjwa yatakuwa hatarini, na hata kuwa ametekeleza majukumu yake ipasavyo. Lakini pia kukosekana kwa maarifa ya kutosha kutamfanya mtaalamu huyo kushindwa kujiamini katika kazi yake.

HITIMISHO
Madaktari walioko mafunzo pamoja na wataalamu wengine wa afya wanafanya kazi kubwa na nzuri katika kurahisisha utoaji wa huduma katika hospitali zetu, Lakini Uongozi wa hospitali zetu kwa kushirikiana na vyuo vinavyotoa wataalamu hawa wa afya hauna budi Kuwasimamia ipasavyo wakati wote wanapotoa huduma kwa wagonjwa ikiwa ni pamoja na kuwapanga pamoja na Madaktari wazoefu ili kuifanya huduma yao ya matibabu iwe salama na yenye kuleta matumaini kwa mgonjwa na Kuepukana na Vifo vinavyotokana na UZEMBE wa watoa huduma za afya.

Wenu
Mwita Ngutunyi Mohono
S.l.p 237 Mbarali- MBEYA
0762185894
mwitangutunyimohono@gmail.com
 
Upvote 49
.......kiini chako Cha andiko ni kuwa,wanafunzi wa udaktari wasiachwe kwa 100% peke Yao,

Ukweli ni kuwa, huo muda unaowaona wewe may be wakitoa dawa,ndo asilimia 1% ambazo wanaachiwa,asilimia kubwa zinasalia (99%) wako under supervision,wako Darasani au wanafundishwa ....na hao unawaowajua wewe km ni wazoefu.........

Kama unafaham kuwa kukosea ni sehemu ya kujifunza,sidhani km ungefikiria kukaa na kuandika haya mawazo!! Tafuta hao wazoefu,wataalam bingwa ambao unawaaamini!! Walikuwaje wataalam bingwa!! Wakikusimulia ......nadhani utajifunza vingi ambavyo huvijui,na usingeweza kuvijua. Ambavyo ndo vimewafanya wawe wataalam
.

.
Mambo ya Afya ukitaka kuyaandikia chochote heri kwanza ukutane na watu wa afya!! Uwaulize uongee nao ujifunze ...then ndo uandike.
.
.

.

Kingine pia usisahau kuandika Uzi wa changamoto wanazokutana nazo watu wa afya wakiwa makazini,kuandika Uzi kuwapongeza wanafunzi wanaosomea udaktari kwa kujitoa na kuwasaidia wananchi wengi wanapokuwa mafunzoni.
.
Pia tukiona tukio Moja tunaandika Uzi kukosoa,tukumbuke pia kuandika Uzi kupongeza....
Maana
Wanaoenda hospital,kutibiwa na kupona ni wengi zaidi ..........
Ila Cha ajabu tukiumwa hata mafua tukitibiwa na kupona tunasahau,

Tukija kuona tukio Moja la bahati mbaya!! Tutatafuta maneno mazuri ya kukosoa ...

Amani iwe nanyi
 
Habari mwana jukwaa. Nathamini mchango mkubwa unaotolewa na wataalamu wa afya nchini wakiwemo wanafunzi wa udaktari Vyuoni.

Na ndio maana ukisoma andiko langu vizuri. Utakugundua kuwa NIMESIFIA NA KUTAMBUA kazi kubwa inayofanywa na wataalamu hawa. Na naunga mkono serikali kuendelea kuboresha maslahi yao kila siku.

Kiini cha andiko langu ni kuzikumbusha hospitali zetu za rufaa kutokuwaamini kupita kiasi wanafunzi wa udaktari ambao hawajaitimu masomo yao kiasi cha kuwaachia majukumu mengi pasipo usimamizi wa kutosha.

Hii ni kwasababu tunataka Hospitali zetu Zitoe huduma bora kila siku na kuaminiwa na wananchi.
 
Kazi kweli kweli.
Hakika ni kazi. Ipo haja ya serikali kupitia wizara ya afya kuangalia jambo hili ili kuboresha utoaji wa huduma za afya katika hospitali zetu hizi kubwa.
 
Wanafunzi wanamakosa mengi sana,kama unapesa zile hospital zenye vyuo sio za kwenda

Mwanafunz anafungulia drip ya maji kwa kasi kubwa mpaka inasababisha blood pressure kwa mgonjwa

Mwanafunz hauliz kama una pressure anakutundikia drip la kwinini ndo umefika tu unapitiliza kuzima
 
Nadhani ipo haja ya serikali kupitia wizara ya afya kuziangalia hospitali hizi kubwa nchini ili wananchi waendelee kuziamini na kuzotumia kuepuka gharama kubwa wanazozitumia katika hospitali za binafsi.
 
Usisahau kulipigia kura andiko hili mwanajukwaa.
 
Habari mwanajukwaa..naona ukipata muda upige kura katika andiko hili.
 
Asante Sana kwa andiko zuri hili..huu ndio uhalisia.
 
Asante kwa kulitambua hili mwanajukwaa. Naomba usisahau kupiga kura yako katika andiko hili
 

Hospitali ya Rufaa ya KCMC inaongoza kwa kuwaachia majukumu yote ya kitabibu wanafunzi wa udaktari pasipo usimamizi wa kutosha na imesababisha chanzo cha vifo vingi Katika Hospital hiyo Kila siku Kila saa.​

Usiache kupigia kura andiko hili kiongozi ili tufikishe ujumbe.
 
Sahihi mwanajukwaa. Ipo haja ya hospitali hizi kusimamia utoaji wa huduma ili kujenga imani kwa wananchi.
 
Hakuna mwananfunzi anaye achiwa mgonjwa hospital.
You must be crazy, tunawaona interns wako peke yao wanahudumia wagonjwa wenye uhitaji maalum. Tunaona maana wanafunzi madaktari tunawajua, wanamwagwa kila mwisho wa mwaka .... after a pone year wanaondoka wanakuja wengine...usibishe, tunaona wanavyoachiwa wagonjwa ambao unaona kabisa hyu hajui anachokifanya.
 
Mfano hai..
Sengerema wanafunzi wakamfanyia jamaa upasuaji baada ya kupata ajali ya pikipiki..wakati wa ushonaji wakashonea mawe ndani ya ngozi

Hawa wanafunzi ndio wanaongoza kusababisha vifo hasa suala la upasuaji..

Atakaye kubishia Ni mchawi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…