SoC02 Hospitali za Rufaa kuwaachia majukumu yote ya kitabibu wanafunzi wa udaktari pasipo usimamizi wa kutosha - chanzo cha vifo vingi

SoC02 Hospitali za Rufaa kuwaachia majukumu yote ya kitabibu wanafunzi wa udaktari pasipo usimamizi wa kutosha - chanzo cha vifo vingi

Stories of Change - 2022 Competition

cupvich

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2022
Posts
408
Reaction score
247
UTANGULIZI
Nikiwa wodini nauguza mgonjwa wangu katika moja ya hospitali kubwa ya Rufaa nchini, Nilimsikia daktari mmoja akitumia lugha ya kiingereza kuwaambia wanafunzi wanao somea udaktari ambao walikuwa wakitoa huduma kwa mgonjwa aliyekuwa kitanda cha pembeni na alicho mgonjwa wangu maneno haya nanukuu "MMEKOSEA, HAMKUTAKIWA KUMCHOMA SINDANO HIYO". Hakika nafsi yangu iliogopa sana, Nilihisi kana kwamba amefanyiwa mgonjwa wangu, hivyo niliwaza iwapo angekuwa ni mgonjwa wangu na nimesikia maneno yale ya daktari ningechukua hatua gani. Ilinifanya kufuatilia kwa ukaribu maendeleo ya Mgonjwa yule tokea siku ile kwasababu nilikuwa pale kwa wiki moja nikimuuguza mgonjwa wangu, Baada ya siku moja nilipewa taarifa kuwa Mgonjwa yule alifariki Dunia.

Hospitali zetu za rufaa zimekuwa kimbilio kwa walio wengi katika suala zima la matibabu, hii ni kutokana na kuaminika kwamba zina wataalamu wa kutosha. Lakini pia zinaweza kutoa huduma za kibingwa. Kwa hapa kwetu Tanzania tumebarikiwa kuwa na Hospitali za rufaa za mikoa lakini pia tuna hospitali za rufaa za kanda kama vile HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA MBEYA, HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA KCMC, HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA BUGANDO pamoja na hospitali kubwa ya taifa MUHIMBILI. Hospitali hizi za rufaa za kanda zina Vyuo ambavyo hutoa mafunzo kwa wataalamu wa Afya kama vile madaktari, manesi na wafamasia. Vyuo hivyo ni MUHAS,BUGANDO, MCHAS, na KCMCo pamoja na vyuo vingine vinavyopatikana katika hospitali za mikoa na Hospitali zingine za Binafsi na mashirika ya dini.

Wanafunzi hawa wa udaktari walioko wafunzoni wamekuwa wakitumia muda mwingi kufanya mazoezi kwa vitendo katika hospitali zetu jambo ambalo ni Zuri kwani linawajenga na kuwaimarisha vyema katika Sekta hiyo muhimu ya afya. Lakini pia wamekuwa wakirahisisha utoaji wa huduma za afya kwa kuongeza wahudumu wa afya katika hospitali zetu ukizingatia kwamba vituo vingi vya afya pamoja na hospitali zetu Bado zina changamoto kubwa ya upungufu wa wataalamu wa Afya. Kwa ujumla wanataalamu hawa walioko mafunzoni hususani madaktari wanafanya kazi kubwa.

TATIZO LINAANZIA HAPA.
Kwa Bahati mbaya, hospitali zetu zimewaamini Wanafunzi hawa walioko vyuoni kupitiliza kiasi cha Kuwapangia Zamu za kuwaona wagonjwa pasipo usimamizi wa daktari mzoefu na kufanya matibabu kwa mgonjwa hata kwa wagonjwa ambao wako katika hali mbaya. Jambo ambalo ni Hatarishi kwa afya ya mgonjwa. Hii imesababisha kutokea kwa vifo vingi kutokana na kwamba wanafunzi hawa wa afya hawajawa bado na Utaalamu wa kutosha katika kutoa huduma za afya kwa kiwango kinachostahili ukilinganisha na madaktari wazoefu.

CHANZO CHA TATIZO.
Ni kweli kwamba siku hizi Teknolojia imerahisisha ufanyaji wa kazi katika hospitali zetu.Teknolojia imechukua nafasi kubwa sana katika utoaji wa huduma katika vituo vya afya na Hospitali, na ndio maana utakuta Daktari anayeingia katika zamu ya usiku anaweza kumfahamu vizuri mgonjwa aliyelazwa wodini, matibabu aliyoyapata na matibabu anayotakiwa kuyapata hivyo kumrahisishia kuendeleza matibabu kwa mgonjwa. Lakini ukuaji huu wa Teknolojia usiwe Sababu ya kuwaachia majukumu yote wanafunzi wa udaktari walioko Vyuoni kwani waliowengi bado hawajapata maarifa ya kutosha katika kutoa huduma za kitabibu. Lakini pia wingi wa hawa wanafunzi katika hospitali zetu kisiwe kigezo cha madaktari wazoefu na wenye majukumu ya kutoa huduma za afya kusahau wajibu wao wa kuwahudumia wagonjwa. Wengi wa hawa wanafunzi wa udaktari wamekuwa wakitoa huduma kwa hisia ili tu kukamilisha matakwa ya kozi wanazosomea ikiwa ni pamoja na kufanya mazoezi kwa vitendo. na hivyo kuhatarisha maisha ya mgonjwa.

ATHARI ZITOKANAZO NA TATIZO HILI.
Utakubaliana nami kuwa Siku zote Mwanafunzi atabaki kuwa mwanafunzi, hata kama ni mwanafunzi wa udaktari mwaka wa nne au wa tano. Na sifa mojawapo aliyonayo mwanafunzi ni kutokujiamini kwa asilimia mia moja, hivyo kupelekea kufanya jambo kwa Jazba na Mihemko ilimradi tu kukamilisha takwa fulani. Hivyo nilazima uongozi wa hospitali zetu uwachukulie wataalamu hawa wa afya kama wanafunzi na kuwasimamia katika huduma zote za kitabibu katika hospitali zetu kwa manufaa mapana ya mgonjwa na mtoa huduma.

Kutokana na kuwatumia madaktari mafunzoni katika hospitali zetu hizi za rufaa, Huduma katika hospitali hizi zimekuwa zikishuka kadiri siku zinavyokwenda licha ya serikali Kuwekeza kiasi kikubwa cha fedha katika kuboresha mazingira ya utoaji huduma katika hospitali hizi, ikiwa ni pamoja na Ununuzi wa vifaa vya kutolea huduma za afya, Uongezaji wa majengo ya kutolea huduma za afya na kuongeza watumishi wa afya. Jambo hili si zuri kwasababu linapunguza imani kwa wananchi hivyo kutumia gharama kubwa kupata matibabu katika hospitali za binafsi.

Usalama wa mgonjwa awapo hospitalini ni muhimu sana. Muda mwingi mgonjwa hubaki na wataalamu wa afya kwa ajili ya matibabu. Hivyo ndugu jamaa na marafiki huamini kuwa Daktari au mtaalamu yeyote wa afya ana nafasi kubwa katika kuokoa maisha ya Mgonjwa. Wote tunaamini kwamba mtaalamu yeyote wa afya anatakiwa awe na ujuzi wa kutosha katika kumhudumia mgonjwa ili kuokoa maisha yake. Iwapo mtaalamu huyo wa afya atakosa ujuzi na maarifa ya kutosha maisha ya mgonjwa yatakuwa hatarini, na hata kuwa ametekeleza majukumu yake ipasavyo. Lakini pia kukosekana kwa maarifa ya kutosha kutamfanya mtaalamu huyo kushindwa kujiamini katika kazi yake.

HITIMISHO
Madaktari walioko mafunzo pamoja na wataalamu wengine wa afya wanafanya kazi kubwa na nzuri katika kurahisisha utoaji wa huduma katika hospitali zetu, Lakini Uongozi wa hospitali zetu kwa kushirikiana na vyuo vinavyotoa wataalamu hawa wa afya hauna budi Kuwasimamia ipasavyo wakati wote wanapotoa huduma kwa wagonjwa ikiwa ni pamoja na kuwapanga pamoja na Madaktari wazoefu ili kuifanya huduma yao ya matibabu iwe salama na yenye kuleta matumaini kwa mgonjwa na Kuepukana na Vifo vinavyotokana na UZEMBE wa watoa huduma za afya.

Wenu
Mwita Ngutunyi Mohono
S.l.p 237 Mbarali- MBEYA
0762185894
mwitangutunyimohono@gmail.com
 
Upvote 49
You must be crazy, tunawaona interns wako peke yao wanahudumia wagonjwa wenye uhitaji maalum. Tunaona maana wanafunzi madaktari tunawajua, wanamwagwa kila mwisho wa mwaka .... after a pone year wanaondoka wanakuja wengine...usibishe, tunaona wanavyoachiwa wagonjwa ambao unaona kabisa hyu hajui anachokifanya.
Ahsante kwa kuliona hili mwanajukwaa. Kwakweli Hospitali hizi ambazo ni kubwa zinaendelea kupoteza imani kwa walio wengi kwasababu ya kuwaachia wanafunzi wa udaktari majukumu yote. hii inapelekea mtu kutumia gharama kubwa katika hospitali za binafsi. Ipo haja kuanza upya ili kujenga imani kwa wananchi kwasababu serikali imewekeza pesa nyingi katika sekta hii.

TAFADHARI MWANAJUKWAA USIACHE KULIKE NA KUPIGIA KURA ANDIKO HILI ILI LIFIKE SEHEMU HUSIKA. bonyeza vote
 
seems wewe ni hao hao tunaowasema maaa ulivyoshupaa...na kejeli kama Mwigulu
Ni kweli wengi wanaoweza kubisha ni wahusika wenyewe. Hata kama mimi ni mhandisi ukaeleza madhaifu katika sekta yangu bado sitakubali kirahisi.

Hivyo andiko letu Halina Nia mbaya hata kidogo. Tunathamini kazi kubwa za wataalamu wa afya. Lakini hainabudi hospitali zetu ziwe na usimamiz wa kutosha
 
Mfano hai..
Sengerema wanafunzi wakamfanyia jamaa upasuaji baada ya kupata ajali ya pikipiki..wakati wa ushonaji wakashonea mawe ndani ya ngozi

Hawa wanafunzi ndio wanaongoza kusababisha vifo hasa suala la upasuaji..

Atakaye kubishia Ni mchawi
Asante kwa kuwa shahidi. Kwakweli hali hii inaondoa imani kwa waliowengi.

Tafadhari usiache kulike na kupigia kura andiko hili.
 
You must be crazy, tunawaona interns wako peke yao wanahudumia wagonjwa wenye uhitaji maalum. Tunaona maana wanafunzi madaktari tunawajua, wanamwagwa kila mwisho wa mwaka .... after a pone year wanaondoka wanakuja wengine...usibishe, tunaona wanavyoachiwa wagonjwa ambao unaona kabisa hyu hajui anachokifanya.
Naomba Tuendelee kupigia kura andiko wanajukwaa. Na kulike pia
 
Kwanza hongera mkuu Kwa kuibua changamoto kubwa inazo zikumba jamii zetu kutokana na uzembe WA kuachiwa madaktar wanafunzi pasina uangalizi toka Kwa madaktar wazoefu......

Pili nimependa Una hekima na Busara Sana ktk kujibu hoja zako....hata pale inapoonekana kupewa changamoto lkn upo Mtulivu ktk kujibu hoja zako....hongera Sana

Nimeona maoni ya wahusika wenyewe WA Kada ya afya wakijaribu kuleta hoja na kutufahamisha utaratibu ambao unafanywa huko wodini ni Jambo zuri na binafsi nimepata elimu kubwa....lkn pamoja na utaratibu mliotufahamisha lkn bado kuna changamoto kadhaa ambazo baadhi ya wachangiaji wamezizungumzia hapa kuwa watu wameathirika kutokana na huduma walizo pewa na madaktari hao Hilo lipo na halitakiwi kutetewa penye ukweli pasemwe.

Kwa uzoefu wa watu wetu ambao sio wawajibikaji Hilo wala si Jambo la kushangaza kabisa kwasababu unakuta huyo ambaye angetakiwa amsimamie daktar mgeni ndo Kwanza anapiga Soga huko pembeni ....au anajishughisha na mambo ambayo si sehemu ya kazi yake Kwa Wakati huo kisa pale wodini kamuacha daktar mwanafunzi.....watu WA afya mjitathimini mnadili na afya za watu....hayo si magari kuwa spea hii ikiharibika utanunua nyingine....mnadili na ustawi na afya ya binadamu kwahiyo umakini wenu unatakiwa Sana.
 
Asante sana mwanajukwaa kwa kuunga mkono hoja hii. Kwakweli huo ndio uhalisia. Hivyo ni wajibu wa wahusika kuchukua ili kunusuru maisha ya watu yanayotokana na uzembe usio na sababu.

Hatusemi kwa ubaya bali ni kwa namna iliyo njema ili kuboresha huduma zetu katika hospitali hizi ambazo zinatakiwa kuwa mfano.
 
Kwanza hongera mkuu Kwa kuibua changamoto kubwa inazo zikumba jamii zetu kutokana na uzembe WA kuachiwa madaktar wanafunzi pasina uangalizi toka Kwa madaktar wazoefu......

Pili nimependa Una hekima na Busara Sana ktk kujibu hoja zako....hata pale inapoonekana kupewa changamoto lkn upo Mtulivu ktk kujibu hoja zako....hongera Sana

Nimeona maoni ya wahusika wenyewe WA Kada ya afya wakijaribu kuleta hoja na kutufahamisha utaratibu ambao unafanywa huko wodini ni Jambo zuri na binafsi nimepata elimu kubwa....lkn pamoja na utaratibu mliotufahamisha lkn bado kuna changamoto kadhaa ambazo baadhi ya wachangiaji wamezizungumzia hapa kuwa watu wameathirika kutokana na huduma walizo pewa na madaktari hao Hilo lipo na halitakiwi kutetewa penye ukweli pasemwe.

Kwa uzoefu wa watu wetu ambao sio wawajibikaji Hilo wala si Jambo la kushangaza kabisa kwasababu unakuta huyo ambaye angetakiwa amsimamie daktar mgeni ndo Kwanza anapiga Soga huko pembeni ....au anajishughisha na mambo ambayo si sehemu ya kazi yake Kwa Wakati huo kisa pale wodini kamuacha daktar mwanafunzi.....watu WA afya mjitathimini mnadili na afya za watu....hayo si magari kuwa spea hii ikiharibika utanunua nyingine....mnadili na ustawi na afya ya binadamu kwahiyo umakini wenu unatakiwa Sana.
Nakuunga mkono asimilia zote mkuu. Mimi ni shahidi wa jambo hili. Kwakweli inakatisha tamaa na kuvunja moyo.
 
Nakuunga mkono asimilia zote mkuu. Mimi ni shahidi wa jambo hili. Kwakweli inakatisha tamaa na kuvunja moyo.
Tumia muda wako kusoma andiko hili na kulipigia kura ili kufikisha ujumbe unao takiwa.
 
Mwandishi haelewi kbs system ya hosp inavyofanya kaz, pia hajui matibabu ni nn, .
.
Hawa wanafunz/interns ni maDaktari wa kupita kila mwaka, hospital hua ina staff wake ambao wako kweny roaster/ratiba ya kila sku na interns wana roaster zao, so haiwezekan intern apangiwe zamu peke ake.
.
Kila asubuhi hua kuna morning report ambapo intern pamoja na supervisor wake (permanent employee either specialist au experienced dr) watarepot taarifa za 24hrs.
.
, Then watapita kwny morning rounds kuangalia wagonjwa na kufanya maamuzi na kuandika dawa za 24hrs, na hapo matibabu yanakua yamekamilika,
.
Sasa kinachofuata ni kwenda kunywa chai then wanaoenda clinic wataenda, wanaoingia theatre wataenda, wanaorud hom wanarudi, wodini anabaki intern na nurse wa zamu, kutimiza yaliyoamriwa asubuhi,
.
Km kuna tatizo, intern atawasiliana na Supervisor/Muajiriwa permanent wa hospital alie kwny zamu, na ataelekezwa afanye nn, na tatizo likiwa kubwa itaenda kwa hatua hadi kwa super specialist,
.
Ndugu sio lazima specialist aje amchome sindano mgonjwa wako ndo ujue ametibiwa na Daktar mzoefu,
Hyo ni Common misconception ambayo ndugu wa wagonjwa hua mnayo, mkimuona intern muda wote mnajua ndo Daktar pekee anaefanya matibabu,
MKO WRONG SANA,.
.
P.S
ni rare sana mgonjwa kupewa dawa ambayo sio sahihi, na hta ikitokea hawezi kabisa kufa, maana ile sio sumu, ni dawa, one injection haiwez kua lethal,.

Pia sio jambo la kushangaza Daktar mmoja kubadili dawa alizoandika Daktar mwngne, ni swala la Kuzidiana elimu na uzoefu, na haimanishi zilizofutwa ni mbaya, ila zilizoandikwa yawezekana ni bira zaid kulingana na uzoefu.

Kingne fanya utafiti kuhus kero za wahudum wa afya na maslahi yao, sio kuwakandia tu afu baadae kuwatext kuwaomba dawa za UTI.
P.S
ni rare sana mgonjwa kupewa dawa ambayo sio sahihi, na hta ikitokea hawezi kabisa kufa, maana ile sio sumu, ni dawa, one injection haiwez kua lethal,.

👆Unaidefine vipi rare sana? What's the magnitude of very rare? It applies to whom?
So it can happen, kwa asiyejulikana. So it might be the one mentioned.

Sichukulii ukweli sana kwa yaliyoelezwa japo yawezekana; lakini maelezo hayo yanadhihirisha uwezekano wa kutokea. Hapo hujatetea chochote.
 
P.S
ni rare sana mgonjwa kupewa dawa ambayo sio sahihi, na hta ikitokea hawezi kabisa kufa, maana ile sio sumu, ni dawa, one injection haiwez kua lethal,.

[emoji115]Unaidefine vipi rare sana? What's the magnitude of very rare? It applies to whom?
So it can happen, kwa asiyejulikana. So it might be the one mentioned.

Sichukulii ukweli sana kwa yaliyoelezwa japo yawezekana; lakini maelezo hayo yanadhihirisha uwezekano wa kutokea. Hapo hujatetea chochote.
Asante mwanajukwaa kwa kupitia andiko hili.

Jambo ambalo wasomaji watakiwa kufahamu ni kwamba tunathamini sana huduma za wataalamu wote wa afya.

Lakini hatuungi mkono wanafunzi wa udaktari ambao bado wapo masomoni kuachiwa wagonjwa pasipo usimamizi wa kutosha..haya mambo yapo katika hospitali zetu hivyo ni lazima wahusika wachukue Hatua..ili kuendelea kujenga imani kwa wananchi.

Tafadhari kumbuka kupigia kura andiko hili na kulike.
 
Nimezalishwa na wanafunzi
Hongo kidogo ndo ilimleta mkunga akanisaidia.
Hatari!!!! Nadhani sasa wengi tumeshuhudia mambo haya katika hospitali zetu..ipo haja kubwa ya wasimamizi kufanya sehemu yao ili kujenga tena Imani kwa wananchi walio wengi.

Tafadhari usiache kupigia kura na kulike katika andiko hili ili Ujumbe ufike.
 
Wanafunzi wa chuo au Interns?..kama ni mwanafunzi wa chuo hilo ulilolisema haliwezekani.

Intern huwezi kumwita ni mwanafunzi..maana baada ya mwaka huo anakuwa yupo tayari kupractice..sasa unamwitaje mwanafunzi??

Nakubali inatakawa wafanye kazi kwa uangalizi lakini ulivyoandika ni kana kwamba wao ndo wanawaona wagonjwa toka mwanzo..kitu ambacho sio kweli kwenye hizi refferal hospital..

Interns wanaachiwa tu treatment plan baada ya ward rounds ambazo wapo pia na specialists na wanasimamia utekelezaji wake..kitu ambacho sio kigumu kufanya.
 
Back
Top Bottom