Hospitali zituheshimu wateja, mnatuibia sana

Utaratibu ni kusign fomu ya bima baada ya matibabu na sio vinginevyo.
 
Utaratibu ni kusign fomu ya bima baada ya matibabu na sio vinginevyo.
Soma tena
Hawakukuandikia fomu nyingine ya kupata hizo dawa kwenye Pharmacy ya Bima mtaani?

Endapo hizo dawa wanazosema hawana halafu baadae wazijaze watakipwa na Bima. Hapo ndipo upigaji maana watalipwa kitu ambacho hawajakitoa
Hawakuniandikia kabisa yaani niliondoka tu kuepusha shari maana nilikuwa na mtoto
 
Du kweli Kuna haha ya kuratibu baadhi ya gharama Kama consultation na registration fee
 
Hiyo hospitali nilienda last week SAA tatu usiku nilitoka saa saba na robo usiku wagonjwa wengi then kulikuwa na daktari mmoja. Nimetoka nakuta Malaya kama wote pale stendi ya bajaji
 
kuna hospitali moja iko dar mjini ya kina chakorii,aisee hata kama ukiwa na maleria moja ukienda pharmacy lazma upewe dawa mpaka 10 za kumeza na wengine unakuta mpka dawa 15 yani ukiumwa mara 20 kwa miez 6 basi unafungua pharmacy
 
Hahahaa
 
na hii tabia ya ku sign kabla naona ipo Sana unasign kabla ya matibabu
 
Ekenywa kumuona daktari nililipa 40,000 halafu baada ya daktari kunihudumia akaniambia kuna kipimo natakiwa nikapime ili ijulikane nina tatizo gani gharama za hicho kipimo ni 100,000. Na hawakutaja ni kipimo gani mimi nilisepa kimyakimya
 
[emoji122][emoji119][emoji119][emoji120]barikiwa mkuu siku hizi udaktari sio wito ni business[emoji26][emoji26]
 
Sahihi kuna kipindi nilipeleka binti wa kazi kupata matibabu nikaandikiwa dawa. Hizo dawa alikuwa anywe kwa miezi miwili alikuwa na tatizo la upungufu wa damu unaojirudia mara kwa mara. Kwa sababu nilipungukiwa hela ikabidi nilipie dawa za wiki mbili. Baada ya dawa kuisha nikaona uvivu kurudi hospital nikaenda phamarcy dawa nilizouziwa Tsh 22000 nikanunua kwa Tsh 8000.
Ukweli hospitali zinatupiga hela sana.
 
Sijaelewa hapa kwenye kumuona Daktari 46000/-

Au unamaanisha ni pamoja na Vipimo na Dawa??
agha khan kildaktari unayemuona kutokana na sifa zake ana bei yake.

kuna dr specialist wa tumbo kumuona ikikuwa 54k au 56k kama sikosei. Ila sikujuta kumuona yule dk kwa kweli......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…