Hospitali zituheshimu wateja, mnatuibia sana

Hospitali zituheshimu wateja, mnatuibia sana

Mwezi December kijana wa shamba alilalamika kichwa kuuma sana sana.nikaenda shamba nikamchukua na kumpeleka dispensary ndogo.nimefika pale nakuta doctor yanki tuu yupo njee anapiga story nikaingia reception nikalipia kumuona doctor na kujisajil bei (10,000) tuu cha ajabu nipo njee kwenye bench napiga upepo doctor akanifata nadhani aliniona wakati naingia na kuniambia jumla ya dawa itakuwa 12,000 kwa dawa nne.nikashangaa ana sema nimpe pesa akashughulikie dawa .kwa kuwa muda ilikuwa unaenda nawahi mtoto mdogo (saa moja kasoro usiku).na poleni mi kubwa ya kusubiri dawa Nikampa.nikamuitia boda kijana nami nikaondoka. Kwenye mida ya saa nne Usiku nikampigia kijana na kumsisitiza kunywa dawa zote nne bila kuacha(huwa anaumwa mara kwa mara Malaria)ananiambia kapewa 3 na yule doctor.kha kesho asubuhi nikawazukia nikamuulizia naambiwa shift yake imeisha.nikawaambia shida yangu wakaanza kuitana kuangalia karatasi(walibaki nayo)inaonesha dawa ya 4000 aliikata.nikawaambia wakati ananionesha hiyo karatasi dawa haikukatwa.wakaanza kujitetea pale nikawaangalia nikawaambia nipeni dawa nisepe na sirudi tena hapa. dispensary kapya kijana anapiga pesa dah.
 
Ukihudumiwa kwa bima Bei inashuka kidogo?

Ishu sio bima Bali kwanini wanafanya huu udhalimu wa kuweka magharama makubwa tofauti na uhalisia,

Yaani wanafurahia kuumwa kwako ili wakupige,

Kuna ki dispensary kimoja kipo sinza karibu na mlimani city,ukienda kufanya vipimo doctor (ndio mmiliki) anakuambia ungechelewa kidogo tulikuwa tunakupoteza yaani Figo zako zinaelekea kufeli,au anakuambia una UTI Kali kiasi Cha kwamba kizazi chako kipo hatarini.

Ukishatetemeshwa ndio anakupiga kwenye gharama za matibabu..

Hospital nyingi binafsi siku hz zimeendekeza njaa
duh.hiv mzee yupo pale bado?
 
Kwa ushauri wangu ambao mie sio mtalamu wa afya lakini ninawaombeni mkipata ugonjwa please jaribuni hospital za serikali. Jaribu kuwa rafiki wa daktari kule Kama nyekundu ni nyekundu Kama ni kijani ni kijani.
Ila huku jamani utabambikiwa ugonjwa smt Kama hivi vimabara havipimi wanakuambia tu unayo uti yaani wanakariri common diseases among society Fulani kwa lifestyle tuliyonayo.
Ni ushauri fuata ama usifuate wewe nenda huko kisa unazo hela nyingi.
Ni sawa kusomesha mtt kulipa Ada kubwa unadhani kuwa ndo ubora wa elimu.
Ila soda ni Ile Ile Kuna sehemu inauzwa 3000 na dukani kwa muha ni 500
 
Jana nimeenda hospital moja hapa Tegeta kibaoni, na imeshajijua maana ipo peke yake pele kibaoni. Waanapiga bei kubwa sana wateja wao, kujiandikisha tu pale ni 7,500/= na sijui ni yanini maana hata file hupewi mambo yote yapo kwenye system za computer. Baada ya hapo anakwambia inachofuata ukamuone daktari, kumuona daktari ni 15,000/=. Dokata anakupa vipimo ukafanye, achana na gharama za vipimo hizi sibishani nazo.

Noma ilikuja baada ya vipimo vyote tukaandikiwa sindano 3 na dawa za kutuliza maumivu. Tuliambiwa gharama za sindano moja ni 37,000/= Hapo ndio kengele ikalia kichwani na kujua hapa kuna shida. Nikaomba niandikiwe ni sindano gani ili nichome mbele kwa mbele, hapo dokta akaanza kukataa anasema harusiwi kutoa hicho kitu inaweza kumletea shida kikazi, ilileta ubishi mkubwa sana kwakuwa mimi nimeshalipa kukuona na kila kitu kitoka kwako nimeshalipia na gharama za vipimo hapa niandikie hizo dawa mi niondoke, ndio kwa mbinde nikapewa majina ya hizo dawa.

Nikaenda pharmacy ipo opposite tu na hiyo hospital hizo dawa hapo wanauza 7,000/= tu na lile bomba la sindano ni 500/= Nikamlipa nesi 3000 nikachomwa sindano yaani 10,000/= nikawa nimepata tiba ambayo ilibidi nilipe 37,000/=

HOSPITALI MUWE NA HURUMA NA WATEJA WENU, MTU AKIUMWA ISIWE NAFASI YA KUMPIGA, SIO POA KABISA
Jana nimepigwa 47,000/= Agakhan Polyclinic, ikiwa katika mnyumbuliko huu.

Kusajiliwa 1,000/=
Kumuona Dk 46,000/=

Mungu aendelee kutuponya
 
Huo uspecialist wako labda uwe katika hospital yako binafsi ndio unaweza kuonana bure na wagonjwa,lakini ukiwa umeajiriwa hauwezi kuonana na wagonjwa bure tu unalipwa mil 3 halafu uonane na wagonjwa bure tu?
Private Hospital zote consultation fee ya kuonana na specialist ,super specialist sio chini ya elfu 50 hutaki kutoa pesa nenda ukaonane bure na Clinical officers
hv mm ndo kilaza sana au mbona hii ua super specialist ndo naisikia leo jamn?? Kumbe kuna specialist na super specialist ?
 
Sijaelewa hapa kwenye kumuona Daktari 46000/-

Au unamaanisha ni pamoja na Vipimo na Dawa??
Hapo ni kumuona Dk kwenda kumueleza shida yako, endapo kama atahitaji kutumia vipimo vya maabara ili kubaini tatizo itahitaji ulipie vipimo hivyo vya maabara.

Dawa ukiandikiwa utalipia tena gharama yake
 
Kuna hospitali wanaitwa wauguzi wanaulizwa mbn dawa hizi na hizi hamziandiki zimejaa store tu. Kuna siku et jamaa kaandikisha cheti wanapigiana simu huyo anapesa fanya kweli. Hivi hii ethic kweli?.
Mtu unaenda unasema unaumwa kifua unaambiwa upime UTI na Malaria, hujasema unaumwa kichwa wala kupandisha homa.
Kuna dogo nilimpeleka hospital ana vipele mwilini, but aliambiwa apime UTI na Malaria.

Sent from my Infinix X623 using JamiiForums mobile app
Wakat mwingine muwe mnawa challenge hao ma dr mkuu, haiwezekani niwe nakohoa tu unaniambia nipime mkojo na malaria.
 
Hapo ni kumuona Dk kwenda kumueleza shida yako, endapo kama atahitaji kutumia vipimo vya maabara ili kubaini tatizo itahitaji ulipie vipimo hivyo vya maabara.

Dawa ukiandikiwa utalipia tena gharama yake
Dohhhh..... Pole sana. Mbona inakuwa too much.... Dohhhh..... !!

Alikuwa ni Specialist au ni General Practitioner??
 
Jana nimeenda hospital moja hapa Tegeta kibaoni, na imeshajijua maana ipo peke yake pele kibaoni. Waanapiga bei kubwa sana wateja wao, kujiandikisha tu pale ni 7,500/= na sijui ni yanini maana hata file hupewi mambo yote yapo kwenye system za computer. Baada ya hapo anakwambia inachofuata ukamuone daktari, kumuona daktari ni 15,000/=. Dokata anakupa vipimo ukafanye, achana na gharama za vipimo hizi sibishani nazo.

Noma ilikuja baada ya vipimo vyote tukaandikiwa sindano 3 na dawa za kutuliza maumivu. Tuliambiwa gharama za sindano moja ni 37,000/= Hapo ndio kengele ikalia kichwani na kujua hapa kuna shida. Nikaomba niandikiwe ni sindano gani ili nichome mbele kwa mbele, hapo dokta akaanza kukataa anasema harusiwi kutoa hicho kitu inaweza kumletea shida kikazi, ilileta ubishi mkubwa sana kwakuwa mimi nimeshalipa kukuona na kila kitu kitoka kwako nimeshalipia na gharama za vipimo hapa niandikie hizo dawa mi niondoke, ndio kwa mbinde nikapewa majina ya hizo dawa.

Nikaenda pharmacy ipo opposite tu na hiyo hospital hizo dawa hapo wanauza 7,000/= tu na lile bomba la sindano ni 500/= Nikamlipa nesi 3000 nikachomwa sindano yaani 10,000/= nikawa nimepata tiba ambayo ilibidi nilipe 37,000/=

HOSPITALI MUWE NA HURUMA NA WATEJA WENU, MTU AKIUMWA ISIWE NAFASI YA KUMPIGA, SIO POA KABISA
Na ukute hayo maradhi walokwambia wala Huna na wala hukutakiwa kuchoma hayo masindano. Yaani tunakamuliwa Fedha then tunauliwa.
 
Noma sana kuna kahospital kwanza kapo maeneo ya pamba road karibu na msikiti hiyo hospitali ukienda na bima wanalipisha kisha wanalipisha na cash, wanakuambia dawa walizokupa hazipo kwa bima hivyo ulipie cash kumbe unalipa mara mbili sikua na muda sana ila huu ndio wizi mpya mjini.

USHAURI
hospitali nyingi za binafsi na vituo vya afya kwanza ni wezi, wanatisha wagonjwa kusudi wafanye vipimo vingi, wanaandika madawa mengi bila kufuata miongozo.
fikiria mtu anachomwa tramadol 2cc, anapakwa diclofenac jell, anachomwa dexamethathol, anapewa predinisol, anapewa, loratidine....yaani tatizo la kungatwa na tandu ndio upewe dawa za kutuliza maumivu bila mpangilio!!!! Unaweza kujikuta figo na ini vinafeli kwa ujinga wa manesi kujifanya madaktari, pumbavu kabisa hawana madaktari waliosajiliwa, ukipata shida utahudumiwa na manesi na huenda ukapoteza maisha kwa kukosa daktari ni vyema kwenda hospitali za serikali hata kama dawa hazipo utapata vipimo na matibabu mengine ni hayo tu. Vituo vya afya vya serikali ndio sehemu ya kukimbilia private nyingi ni upumbavu mtupu na wizara bado inawachekea hata BIMA wanatakiwe wasiruhusiwe kabisa
 
Ndipo umuhimu wa bima ya afya huonekana
Yaani wamefanya kamtaji ukiwa na cash tabu kwenye Bima nao wanapiga juzi nimemaliza kusikilizwa na daktari napewa nisaini zile karatasi zao nawauliza hizi nasaini baada ya kumaliza matibabu na kuchukua dawa iweje nipewe now? tukabishana kidogo nikaona nisaini nafika pharmacy dawa kama tatu hazimo na nimeshazisaini nikawarudia wazitoe wakagoma ili kuepusha shari nikaacha lipite tu since my 1st twin alikuwa ana homa ila kuna baadhi wanaiba huko Bima pia.
Ndipo umuhimu wa bima ya afya huonekana
 
Naomba nitetee kwa upande wa gharama za dawa hapo. Katika soko huria kuna brand mbalimbali za dawa ambazo zinatofautiana bei. Dawa inaweza kuwa ni ya aina moja let's say CEFTRIAXONE INJ ya India na ile ya German (Denk) zinatofautiana bei. Its obvious muuzaji wa Denk atacharge zaidi kutokana na ubora. Asante.
 
Dohhhh..... Pole sana. Mbona inakuwa too much.... Dohhhh..... !!

Alikuwa ni Specialist au ni General Practitioner??
Ana Master(Ndio Uspecialist unaanzia hapa).

Hela imeenda na msaada sijapata zaidi ya kusema katumie dawa fulani jambo ambalo sijaridhika nalo kabisa kwani kiini cha tatizo kashindwa kuniambia
 
Yaani wamefanya kamtaji ukiwa na cash tabu kwenye Bima nao wanapiga juzi nimemaliza kusikilizwa na daktari napewa nisaini zile karatasi zao nawauliza hizi nasaini baada ya kumaliza matibabu na kuchukua dawa iweje nipewe now? tukabishana kidogo nikaona nisaini nafika pharmacy dawa kama tatu hazimo na nimeshazisaini nikawarudia wazitoe wakagoma ili kuepusha shari nikaacha lipite tu since my 1st twin alikuwa ana homa ila kuna baadhi wanaiba huko Bima pia.
Hawakukuandikia fomu nyingine ya kupata hizo dawa kwenye Pharmacy ya Bima mtaani?

Endapo hizo dawa wanazosema hawana halafu baadae wazijaze watakipwa na Bima. Hapo ndipo upigaji maana watalipwa kitu ambacho hawajakitoa
 
Back
Top Bottom