Kuna siku dogo tumempeleka akapimwa malaria , sasa tulipoenda kuchukua majibu Dr akatuandikia dawa, nikamuuliza hii dawa ya nn na hii ya nn? Akasema hii ya malaria, ya maumivu na hii ya UTI nikashtuka kwani huyu si kapimwa malaria tu !!! Nikamuuliza hii UTI imetoka wap na hamjapima mkojo? Akasema sorry nimekosea hapa dah hawa jamaa wapo kibiashara tu..
Kuna kipindi dengue illizingua sana watu mwaka juz kama sikosei, mimi ni miongoni mwa wagonjwa wa mwanzo kabisa tena vipimo vya dengue vilikuwepo hospital baadh kama muhimbili na hospital binafsi chache tu zile kubwa, sasa mimi niliumwa sana nikazidiwa nikapelekwa hospital fulan kufika pale nikapimwa vipimo vyote wakasema UTI kali sana na malaria ila mimi nililazwa walionipeleka ndo waliambiwa hivo, sasa nikalazwa pale mpka saa 4 usiku nikaona na nafuu kidogo wakaniruhusu wakasema natakiwa Sindano 5 nirudi asubui.
Kesho nikarud kuchoma ila bado naumwa tu , baada ya siku mbili nilizidiwa zaidi,, tukasema twende hospital nyingine tukaenda kkoo kuna hospital fulan ya waarabu magomen , tukaeleza pale wakatuomba ile karatasi ya kule nilipotoka wakaangalia nikafanyiwa vipimo tena, wakasema nilichoandikiwa pale nitofauti na ninachoumwa, ugonjwa unaniosumbua ni dengue!!!
Wakasema hospital zenye vipimo vya dengue ni chache sana kwahyo watu wengi wanaumwa ila wakienda hospital hivo vipimo havipo wanaambiwa tu una malaria au UTI, kulikua na wagonjwa wengi sana pale wa dengue wanapokezana vitanda, ule ugonjwa hauna dawa wanachofanya wanakuwekea tu drip 2 asubui na jion 2 kama siku 5 unakuwa fresh, yaan kuanzia hapo hospital za kijnga huwa siendi kabisa, mtu unachomwa sindano za UTI alafu haumwi UTI