*****SORY MADAM*****(42)
AGE....................................................................18+
WRITER.............................................................EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA
Gafla macho yangu yakagongana na mume wa Madam Mery ambaye siku zote ni adui yangu na mara ya mwisho nakumuka nilimpiga kichwa na akanitolea bastola na jamaa sura yake ikabadilika gafla akanitazama kwa umakini kisha macho yake akayahamishia kwa mtoto aliye bebwa na mfanyakazi wake
ENDELEA
"Waooo ni muda sasa sijakuona naona umekuja kuchukua kiumbe chako si ndio?"
Mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio huku nikimtazama mume wa Madam Mery na kajasho kembamba kakaanza kunimwagika
"Nipe huyo mtoto"
Mfanyakazi wa ndani akamkabidhi mume wa madam Mery mtoto ambaye tayari nimegundua kuwa ni mwanangu.
"Nenda ndani?"
Mfanyakazi wa ndani akaondoka na kutuacha na mume wa Madam,Japo ninamaumivu ya mkono nikajaribu kunyanyuka ila niweze kujiokoa,mume wa madam Mery akamshika mwanangu kichwa chini miguu juu na kumfanya mtoto kuanza kulia kwa sauti
"Kaa hapo hapo la sivyo huyu paka wako ninamwangamiza mbele ya macho yako"
Nikamangalia jinsi mtoto wangu anavyolia na kujikuta roho ya huruma ikinitawala na nikakaa chini nikimtazama mume wa Madam Mery,Akatoa simu na kuipiga
"Njoo nyum bani"
Jamaa akakata simu na kurudisha mfukoni kisha akaniangalia machoni na kutabasamu.Akamshika mtoto vizuri na kuanza kumbembeleza huku akizunguka huku na huku ndani ya sable.Mlango ukafunguliwa na akaingia Madam Mery akiwaavalia vizuri na ule uzuri wake umezidi kuongezeka na baada ya kunioana akaonekana akistushwa.Akapitiliza hadi kwa mume wake na kumpiga busu la shavu kama ishara ya salamu
"Nenda kakae kule"
"Ehee"
"Nenda kakae kwa mshenzi mwenzako"
Jamaa alizungumza kwa hasira hukua akimsukuma Madam Mery kuja kukaa kwenye sofa ambalo nimekaa
"Jamani Derick mume wangu si tulisha lizungumza na limeisha mbona unataka kuanzisha ugomvi?"
"Nyamaza Malaya mkubwa wewe,hivi unajua uchungu nilio kuwa nao wewe,Au unadhani kukaa siku zote kulea kiumbe kisicho changu hivi unajua ni maumivu gani ambayo ninayo moyoni mwangu"
Derick alizungumza huku machozi yakimwagika na mtoto wetu akiwa amemshika mikononi mwake.Madam Mery machozi yaakanza kuutawala uso wake
"Derick nakuomba unisamehe kwa mara nyingine sito rudia tena kukusaloti mume wangu"
"Ahaaa chagua mawili kati yangu au huyu panya wako?"
Macho yakanitoka nilipomuona Derick akifanya kitendo cha mara ya kwanza cha kumshika mwanangu kichwa chini miguu juu huku akiwa amemuinua kwa mkono mmoja
"Derick nyote ni muhimu sana kwangu ninakuomba mume wangu unisamehe nina kupenda sana mume wangu"
"Wewe manamke ni muuaji,kumbuka mimi ndio nilikufanya kupata elimu yako hadi akawa mwalimu ukaona haitoshi ukanisaliti mara ya kwanza nikakusamehe......Baba yako alifariki mikononi mwangu tukimuwahisha nchini India kwa matibabu na zote zilikuwa gharama zangu senti tano kwenu mulikuwa hamuna nimevunja vibanda vyenu na kuwajengea nyumba nzuri ili nanyi muonekane watu kati ya watu ila bado umeona hatoshi kabla ya ndoa yetu umebeba mimba ambayo si yangu ni ya uyo paka hapo."
"Ni mara mia ungetembea na mtuu aliye kuzidi umri ila wewe ukachukua Serengeti Boy unadhani atakusaidia nini huyo mwehu wako"
Derick aliendelea kuzungumza kwa hasira huku machozi yakiendelea kumwagika na mwanangu akiendelea kulia kwa maumivu anayo yapata.Madam Mery kapiga magoti na kuanza kuburuzika taratibu akimfwata mumewe sehemu aliyo simama
"Rudi huko huko la sivyo ninamuua huyu paka wenu."
Madam Mery akaanza kurudi nyuma taratibu huku akiendelea kumwagikwa na machozi mengi.Kelele za mwanangu kulia kwa maumivu zikanifanya nishindwe kuvumilia huku hasira ikinipanda nikanyanyuka huku nikiwa nimeushika mkono nilio vunjika na kupiga hatua mbili mbela za kuikwepa miguu ya madam mery
"Wewe rudisha miguu yako huko la sivyo ninamuachia huyu mtoto"
Derick aliniambia akionekana kutokuwa na huruma kabisa na maumivu anayo yapata mwanangu,nikashindwa kuizuia miguu yangu na kujikuta nikizidi kupiga hatua kwa hasira kali iliyo nitawala mwili mzima.Derick akampiga mwanagu chini kwa nguvu na kumfanya mtoto wangu kunyamaza kimya na kelele kali ikatoka kwa madama Mery pamoja na mfanyakazi wa ndani ambaye alikuwa amejificha kwenye ukuta akishuhudia kila kinacho endelea.
Sikujali kama mkono wangu mmoja umevunjika kwa hasira nikamrukia Derick ambaye akanikwepa na kunisindikiza kwa teke kali la mgongoni na kujigongwa kwenye uso kwenye ukuta na kuangukia pembeni ya miguu ya mfanyakazi wa ndani ambaya mkononi mwake ameshika kisu na kitunguu.Nikamuomba mafanyakazi wa ndani kisu kabla hajanipa Derick akauwahi mkono wa mfanyakazi wa ndani ulio shika kisu ikanilazimu na mimi kuuwahi mkono wa mfanyakazi kwa kuutumia mkono wangu mmoja usio vunjika.Derick akatuzidi nguvu na kumshika mfanyakazi wa ndani na kusukumia pembeni na kisu kikaanguka chini.Kabla Derick ajakiokota nikampiga teke na kuifanya miguu yake yote miwili kunyanyuka chini na akaangukia mgongo.
Nikajisogeza kwa haraka na kabla sijakiokota kisu akanikanyaga vidole vya mkono wangu wa kulia nilio unyoosha kukiokota kisu.Derick akakipiga kisu mbali kido na eneo ambalo nililo angukia akanipiga teke la mbavu lilinifanya nijikunje huku nikigumia kwa maumivu makali.
"Derick utamuua mtoto wa watu"
Madam Mery alizungumza huku akimwagikwa na machozi na mikpono yake ikiwa imejaa damua na vitu vyeupe vyeupe na kugundua kuwa mwanangu amepasuka kichwa chake.Nikanyanyuka huku meno yangu nikiwa nimeyang'ata kwa nguvu.Nikajaribu kuuyanyua mkono wangu wa kushoto ulio vunjika na kuufanya kuuma kwa maumivu makali yaliyonifanya nitoe ukelel wa kuumia kwani kuna kitu kinanichoma kwa ndani.Derick akayashusha macho yake hadi kwenye mkono wangu kisha akayarudisha machoni mwangu na kwa haraka akanitisha kama ananipiga teke kwenye mkono na kuufanya niukinge mkono wangu kwa kugeuka na kumpa mgongo na kushtukia akininyanua miguu yangu na kuivuta na kuanguka kifudifudi huku mkono ulio vunjika nikiwa nimeulalia
Derick akanikalia mgongoni na kuishika mikono yangu yote miwili na kuivuta kwa nyuma.Maumivu ninayo yapata sikuwahi kuyapata tangu nizaliwe.Madam Mery akauweka chini mwili wa mtoto wetu na kukimbilia sehemu tuliyupo na kumsukuma Derick na akaanguka kwa mbele yangu.Sikuwa na uwezo wa kunyanyuka kuokana na maumuzi makali na kubaki nikilia kwa uchungu.
"Ni binadamyu gani usiye na huruma wewe,umenilia mwanangu kikatili ila bado unataka kumuu huyu kijana wa watu"
"Niliapia ni lazima nimuue huyu kijana pamoja na wewe na leo ndio mwesho wenu"
Derick alizungumza huku akinyanyuka kwa haraka na akamshika madam Mery nywele zake na kumbwaga chini kwa nguvu na kumfanya madam mery kutoa ukulele wa kulia kwa maumivu
"Shemeji mikono yako nyoosha juu"
Niliisikia sauti ya mfanya kazi kwa nyuma yangu na kunifanya nigeuke nyuma na kumkuta akiwa ameshika kisu huku mwili mzima ukimtetemeka.Derick akacheka kwa dharau na kumfwata mfanyakazi kwa kasi na kupiga kabali ya gafla na kumpokonya kisu na pasipo kuwa na huruma Derick akamchoma mfanya kazi wa ndani kisu cha tumbo na kumtupa chini.Derick akanisogelea huku kisu chake kikiwa kinavuja damu za mfanyakazi,akaniinamia na kunitazama kwa umakini huku akicheka
"Nilikuumbia siku nikikutia mikononi mwangu nilazima nikuue"
Maneno ya Derick hayakuhafikiana na moyo wangu kuyakubali kiharaka na kirahisi kama anavyo fikiria.Kwa haraka nikainyanyua miguu yangu kuikaba shingo ya Derick na kwa nguvu zote.Madam Mery akamuwahi kumshika Derick mkono ulio shika kisu na kumpokonya,Kila nilipo kumbuka jinsi mwangu alivyo anguka chini ndivyo jinsi nilivyozidi kumkaba Derick shingo yake ambaye akaanza kunishindilia ngumi za mbavu na akaubana mkono wangu uliovunjika na kuzidi kunifanya niachie ukele mkali
"Madam nisaidieeeeeee"
Madam akabaki akiwa ameshika kisu asijue nini afanye,Nikamuomba tena anisaidie ndipo akastuka kama yupo sehemu ya tukio la hatari,akatutizama tena kwa umakini na kwaharaka kisu akakishusha na kikatua kwenye bega la Derick na kumfanya aniachie na kunyanyuka kama mbogo na kumsukuma Madam Mery ambaye akaangukia mwili wa mtoto wetu na kutulia chini
"Nitaendelea kukusaka"
Derick alizungumza huku akiingia ndani kwa haraka na kutoka akiwa na begi la kuburuza na akanitazama kwa muda kisha akanipiga teke la kichwa na kizunguzungu kikali kikanitawala kikiambatana na giza kubwa lililo tanda kwenye macho yangu na nikatulia tuli
***
Milio ya ndege pamoja na mwanga mkali vikanistua na kujikuta nipo kwenye chumba chene kitanda kimoja tuu.Pembeni ya kitanda kuna meza ndogo pamoja na kiti,Kila ninapojaribu kuitadhimini sehemu hii ninashindwa kujua ni wapi.Mbaya zaidi sehemu hii haifanani na hospitalini kwani kitanda nilicho lala kinaukubwa zaidi ya kitanda cha hospitalini.Nikajichunguza vizuri na kuukuta mkon wangu ukiwa umefungwa bandeji gumu(P.O.P.O).Nikashuka kitandani na kwenda dirishani na kufungua dirisha nikaona migomba mingi nikstukia kwa nyuma mlango ukifunguliwa na akaingia mama mmoja mtu mzima
"Umeamka mwanangu?"
"Shikamoo"
"Marahaba,unajisikiaje?"
"Vizuri tuu"
Akanishika mkono na kuugeuza geuza kisha akanitazama usoni huku akiwa ameachia tabasamu pana
"Mimi ninaitwa Mama Natujwa na hapa ulipo ni Moshi"
"Nimefikaje?"
"Umeletwa na rafiki yangu anaitwa Mery na tangu uje hapa huna hukuwahi kuyafumbua macho yako na ulikuwa ni mgonjwa mahututi sana"
Ikanibidi kurudi kitandani na kukaa kwani niliaza kuhisi kizungu zungu,Mama Natujwa akakaa pembeni yangu huku akinishika shika kichwa changu na kunigeuza huku na huku
"Mimi ni daktari wa mifupa ninamiliki hospitali yangu hapa Moshi,na kipindi Mery alipo kuleta nilikufanyia oparesheni hospitalini kwangu na tukakulaza kule kwa kipindi cha mwezi mzima huku tukikulisha kwa mipira maalumu.Nilipo kuleta hapa nyumbani kwangu tatizo lililo kuwa kubwa ni wewe kurudi katika hali yako ya kawaida"
"Ni kipindi gani kimepita?"
"Unakwenda mwezi wa tatu sasa,Japo Mery alikata tamaa ya kudaidi kuwa huto weza kurudi katika hali yako ya kawaida"
"Na yeye sasa hivi yupo wapi?"
"Yupo Arusha anaendelea na kazi...tena ngoja nimpigie simu nimjulishe kuwa umezinduka?"
Nikamzia mama Natujwa kumpigia simu Madam Mery
"Kwa nini unanizuia?"
"Sihitaji alijue hili sawa"
"Je akija?"
"Nimekuambia sihitaji aweze kugundua jambo hilo"
Akili na wazo juu ya mauaji ya mwanangu likanijia kichwani mwangu,Picha niyingine ya jinsi nilivyo teseka kwenye pango nchini Afrika kusini likanijia kichwani mwangu na sura ya baba yangu mkubwa Mzee Godwin ikanijia kichwani huku ikifwatiwa na sura ya Derick.
"HII KAZI NITAIFANYA MIMI MWENYEWE"
Nilizungumza kwa sauti ya chini na kumfanya mama Natujwa kuniuliza ninasemaje
"Hapana sijazungumza kitu"
Nikaka nyumbani kwa mama Natujwa kwa wiki moja,Nilipo ridhika afya yangu ipo kamili nikamuomba ruhusa ya kuondoka na akanikubalia ila kwa kipindi chote sikumuomba asizungumze chochote kwa Madam Mery,Nikapanda basi hadi Dar es Salaam na sikufikizia nyumbani kwetu nikelekea nyumbani kwa Sheila na kukuta geti lake likiwa wazi na gari yake ikiwa imesimamishwa nje.Nikapata matumaini ya uwepo wake na moja kwa moja nikaufungua mlango wake na sikuamini macho yangu baada ya kumkuta akiwa ananyonyana denda na mwanaume mwengine ambaye kwa haraka nikamtambua ni Derick mume wa madam Mery
ITAENDELEA