Hot story

Hot story

oooooohoooooo..kumekucha...subilini basi hadithi iishe maoni mwisho jamani msije tukatishia buleeeee
 
Kitu munacho nikera nyinyi muoana ichukua story yangu na kuipost sehemu ni, kufuta jina langu mimi muandishi, hivi jina likisomeka EDDDAZARIA G.MSULWA, wewe uliye ichukua utapungua nini?

Pole ilo nikawaida kwa wabongo kujimilikisha au kuonyesha hakina mwenyewe. Tunaosoma pia umetupa somo tuulize hayo yasipokuwepo. Imalizie basi mana sijui kama wataweza imalizia.
 
Jamani Mbona mpoo kimya shusheni basi

Kuzipata kwenye account yake Ya Facebook ni kazi kidogo inachukua muda maana hazipo kwenye mpangilio mzuri ila nikiweza nitaziweka hapa ingawa mwenyewe story
 
Mimi ndio mmiliki halali wa hiyo story, na sijajua chanzo cha kuifuta jina la muandishi ni nini?

Sorry kaka hii story inasambaa watsap bila jina jinsi nilivyoipost ndivyo hivyo hivyo inavyo sambaa watsap so wala usinihukumu

but baada ya jamaa aliyeendelea kupost ndipo nilipo kufahamu ndio maana nikakutafuta

mimi ndie niliyekutafuta na kukutaarifu juu ya huku jamii forum
so mimi GOOGLE 2014 Ndie niliekuwa na chart na wewe watsap jana jioni.
 
Mimi ndio mmiliki halali wa hiyo story, na sijajua chanzo cha kuifuta jina la muandishi ni nini?

Kaka usikasirike, hata sisi tunajua hawa si wamiliki halali wa hii hadithi, ila nakupongeza sana kwa hasidhi kama hii, na naomba utuambie vitabu vyako vinapatikana wapi ili tuweze kununua
 
Hahaha mwenye Mali kaja kwanza Nitumie nafasi hii kukupongeza wewe nihodari Sijapata kuona mtunzi Mzuri kama wewe
 
Bora umekuja naomba utuwekee mwenyewe hii story kwasababu tumeteseka sana kuwaomba watu hapa kumbe story yenyewe hawajatunga wao
 
Kwahiyo ndo conflict of interest imezuia further publication?
 
*****SORY MADAM*****(37)

AGE…………………………………….18+
WRITER………………………………EDDAZARIA G.MSULWA


ILIPOISHIA
Roho ya huruma ikaniingia na kujikuta nikianza kukimbia na kuwakumba watu waliopo mbele yangu na kujikuta nikisimama gafla huku macho ni kiwa nimeyatoa kiasi kwamba hasira ikazi kunipanda hii ni baada ya kumkuta ni mama yangu ndio anaye pigwa na askari hawa wanao onekana hawana huruma kabiasa wa watumwa walipo ndani ya hili pango.

ENDELEA
Nikajirusha juu ya mwili wa mama yangua na kumkumbatia kitendo kilicho zidisha hasira ya askari hawa na wakaanza kunishambulia mimi kwa kunipiga,Sikaanza kusikia uzito mwengine ukija juu yangu na nikagundua kuwa watumwa wengine wamepatawa na roho ya huruma na wao mwaneamua kufanya kama nilivyo fanya mimi na kwa umoja wetu ikawalazimu askari kusitisha zoezi lao la kutupiga.Wakatuamuru tuweze kurudi kwenye kazi za kuvunja miamba,nikamnyanyua mama taratibu huku uso wake ukiwa umejawa na damu zilizo changanyikana na machozi mengi.Nikamshika mama huku akiwa hatambui ni nani aliye mshika na kabla sijamsemesha kitu cha ina yoyote askari mmoja anisukuma ili nimuechie mama kisha akamshika mama mkono na kuanza kumburuza kitendo kilicho zidi kunipandisha hasira ila kabla sijhamfwata nikastukia nikichapwa na fimbo aina ya mkia wa taa iliyo jizungusha kwenye tumbo langu na kunirudisha nyuma baada ya askari aliye nichapa kafanya hivyo bila ya huruma
Nikamshuhudia mama akipotelea gizani kwenye pango pamoja na askari aliye mchukua na sikuwa na lakufanya zaidi ya kuendelea kupokea kichapo cha kuchapwa nikiamrishwa kwenda kufanya kazi upasuaji wa mame.Nikaokota moja ya nyundo huku nikiwa na hasira na uchungu mwingi na kuaza kuvunja mwamba amabao wenzangu wanaendelea kuuvunja.Kitu ambacho nimegundua ni kwamba watu wengi waliomo humu ndani wamelishwa makaa ya mawe moto ambaya sio rahisi kwa mtu kuweza kuzungumza chocheta zaidi ya kutoa miguno.Hali ya maisha ikazidi kuwa ngumu kwa upande wangu kadri ya siku zinavyo zidi kwenda sikuweza kumuona mama yangu japo ninaendelea kufanya juhudi ya kuchunguza ni wapi alipo mama na sikuwa ninafahamu kama yupo hai au tayari amesha fariki,mwili wangu ukazidi kudhohofika kutokana na chakula finyu tunacho pewa asubuhi na jiono,Asabuhi tunakunywa kikombe kidogo cha uji usio na kadha ya aina yoyote na usiku tunapewa viazi viwili vilivyo chemshwa na huo ndio mlo wa siku moja na mbaya zaidi chakula ni chakugombani usipo fanya hivyo unaweza kukaa siku mbili hadi tatu pasipo kula
Watu wengi wanazidi kufa kutokana na njaa inayo andamana na kazi ngumu kwa upande wangu kifua kianza kuniuma sana ikafikia hatua nikaanza kukohoa na makohozi yangu yamechanganyikana na damu nyingi,
“Hapana siwezi kufa humu ndani”
Nimawazo ambayo yakawa yanajirudia rudia kichwani kwangu kadri siku zinavyo zidi kwenda,mbaya zaidi sikuweza kujua upi ni usiku na upi ni mchana hii ni kutokana na muda wote tuliopo ndani ya pango mataa makubwa yanawaka,Kila ninapo jitazama mwili wangu ninajikuta nikimwagikwa na machozi kwani mbavu zangu unaweza kuzihesabu,mikono na miguu yangu imekondeana sana.Nyele zangu zimekosa uhusiano mzuri kichwani vidonda vingi ambavyi vingine vimefikia hadi hatua ya kutoka na funza vikaendelea kunitesa mwili wangu.
“Mungu wangu ninaomba unipe nguvu na juhudi katika hili”
Nikaanza kufanya kazi ya kutafuta ni wapi ninaweza kupata njia ya kutokea na kwa bahati nzuri katika uvunjaji wangu wa miamba nikaona sehemu yenye ufana wenye kijisihimo kidogo,nikawatazama askari waliopo ndani humu na hakuna aliye nifwatiliza nikapiga hatua za taratibu na kuchungulia kwenye shimo na kuona mwanga kwa mbali na akili yangu ikatambua utakuwa ni mwanga wa jua.Kengele ya kwenda kupata chakula cha jioni ikagongwa na nikatupa sururu niliyo nayo chini na kuchomoja kwa kasi kuwania chakula ambacho nikikosa leo itakuwa siku yangu ya pili kukosa chakula.Japo mwili wangu umedhohofika nikajikaza katika kugombani viazi na kupata viazi vitatu,Nikakaa kwenye sehemu ambayo siku zote huwa ninapenda kukaa na kuanza kuvisakamia viazi kwa fujo
Nikastukia nikiguswa mguu na binti mdogo na akaniwekea mkono kwa ishara ya kuniomba kiazi kimoja ambacho nimebaki nacho mkononi.Nikamtazama kwa jinsi alivyo kondeana hadi sura yake imejaa vishimo shimo vilivyo kosa nyma kwa kukondeana.Taratibu nikampa kijikiazi nilicho nacho na chote akakiweka mdomoni na kuanza kukitafuna kwa haraka na inavyo onyesha ana njaa kuliko mimi.Akanishukuru kwa kuikutanisha mikono yake kwa pamoja huku akiinama na akanyanyuka taratibu na kuondoka
Tukuruhusiwa kwenda kulala kwenye mapango yetu ambayo milango yake ni ya chuma na katika chumba kimoja cha pango tunalala watu si chini ya thelathini na tangu niingie kwenye hili pango sikuwahi kuona hata siku moja watu wakienda kuoga kwahi maji tunayo kunywa ni machafu sana na yapo kwenye kijikisima kimoja kidogo.Harufu ya uchafu wa miili yetu siku zote inanikusesha raha ya kulala na hususani loe kidogo ninajambo la kuliwazia kichwani kwangu kutokana na ufana nilio uona ninaimani utanisaidia katika kutoroka ndani ya hili pango.
Muda wa kuamshwa ukawadia na tukatoka ndani ya vyomba vyetu na kuelekea sehemu za utendaji wetu wa kazi na kitu cha kwanza kufika kwenye sehemu yangu nikawa na kazi ya kuvujunya ufa nilio uona,ugumu wa mwamba huu hakunifanya nife moyo zaidi ya nilicho kifanya ni kuendelea kuvunja hadi ikafikia kipindi matumaini yakaaza kuja,Filimbi ya dharura ikapangwa na tukakusanyika kwenye eneo la moja na askari wakaanza kutupanga mistari mitatu na tukasubiria nini tunacho taka kuambiwa.Nikawaona watu wanne walio valia vizuri na nikamgundua mmoja wao ambaye ni baba yangu mkubwa Mzee Godwin akiwa ameongozana na watu wengine watatu ambao sikuwajua.Mukuu wa askari wa eneo hili akawapokea kwa unyeyekevu mkubwa na kuanza kuwapitisha kwa kwenye mistari mmoja baada ya mwengine kama vile raisi anaye kagua gwaride la wanajeshi.
Sura yangu nikaiinamisha chini ili asiweze kunijua kwa haraka na kabla ya kunifikia mimi akahamia kwenye mstari wa nyuma yetu na kuendelea kuwatazama watumwa wezangu tuliopo kwenye eneo hili,Wakamaliza kazi hii na wakapanda kwenye ofisi ya mkuu wa eneo hili huku wakizungumza na kucheka kwa furaha.Uchungu na maumivu makali yakaendelea kuutesa moyo wangu ila sikuwa jinsi,tukarudi kwenye sehemu zetu na kuendelea na kazi hata kengele ya uji ilivyo gonga sikuwa na haja ya kwenda kugombania uji.Nikaendelea kupasua mwamba huu na kugundua mawe haya nikiyagonganisha kwa pamoja yanaweza yakazalisha moto kutokana na chechezake.Nikawaona askari wanao tusimamia wakielekea walipo kwenda baba na wezake wakionekana kujawa na furaha hapa ndipo nikaamini kuwa baba mkubwa ndio mmiliki wa hili eneo.
Kwa bahati nzuri nikaona kamba moja ambayo hutumia katika kubutia mawe makubwa,Nikaichukua na kwenda moja kwa moja kwenye mapipa yenye mafuta ya petrol ambayo yanatumika kuendeshea majenereta yanayo washa taa za humu ndani,Kwa haraka nikaichovya kamba kwenye pipa lenye mafuta na kabla sijaondoka eneo lenye mapipa nikaona kidungu kidogo cha maji ya lita moja na nusu.Nikakiokota na kuchota mafuta nusu na kurudi katika eneo lenye ufa,kwa uzuri ni kwaba sehemu yenye ufa juu yake ndipo zilipo ofisi za wakuu wa hii sehemu na haikuw ni raisi kwa wao kuniona kutokana nipo chini shana na pameingia ndani.Wezangu tayari wamesha toka kunywa uji na wanaendelea na kazi zao za upasuaji wa mawe na kelele za upasuaji wa mawe zikazidi kunipa moyo wa kwamba sio rahisi kwa maaskari kuweza kusikia kitu cha aina yoyote.Nikaiingiza kamba kwenye mdomo wa kidungu nilicho kiokota japo kamba ni nene kiasi ila nikajitahidi kuigandamiza hivyo hivyo na ikaingia kiasi kidogo.Nikakichomeka kidungu sehemu yenye ufa na kabla sija ondoka kwenye eneo hili msichana aliye niomba kiazi jana usiku akanifwata na kunigusa mkono na kwa ishara akaanza kunielekeza kitu ambacho haikuwa si raisi kwa mimi kuielewa
Nikaivuta kamba yangu hadi sehemu yenye umbali kidogo na eneo lenye ufa na kuokota mawe mwili ya mwamba na kuanza kuyagonganisha kwa nguvu.Kila ninavyo endelea kuyagonganisha ndivyo jinsi msichana anavyo nisumbua kwa kunishika mkono na kunionyesha kwa ishara umbo la binadamu na kudai kuwa lipo kwenye sehemu ya pili ya sehemu ninayo ipasua.Japo ninamuelewa ila sikuwa na haja ya kusikiliza sana na nikazidi kujitahidi kuyagonganisha mawe yangu kwa nguvu na kasi ya kubwa hadi chche zikaanza kutoka na kwabahati nzuri cheche baadhi zikanasa kwenye kamba yenye mafuta ya petrol na kwa kasi ikaanza kuwaka huku ikielekea sehemu yenye kidungu cha maputa.Msichana anakigeuza ili nisome kitu alicho kiandika sehemu ya ukutani kwenye mwamba kwa kutimia jiwe.Nikakutana na maandishi yenye herufi kubwa na zilizo kaa bila mpangilio zinazosomeka
{MAMA ULIYE MTETEA SIKU ZILEEEE YUPO SEHEMU YA PILI YA SEHEMU AMBAYO UNAPASUA HUO MWAMB…..}
Kabla sijamalizia kusoma maandishi hayo nikastukia mlipuko mkubwa ulio sababisha mwamba kupasuka na kuanza kudondosha mawe makubwa ambayo yameanza kuwaangukia watumwa wezangu pamoja na kuta za ofisi zilizopo juu kuanza kumeguka taratibu na kuporomoka chini

ITAENDELEA
 
*****SORY MADAM*****(38)

AGE…………………………………….18+
WRITER………………………………EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA
{MAMA ULIYE MTETEA SIKU ZILEEEE YUPO SEHEMU YA PILI YA SEHEMU AMBAYO UNAPASUA HUO MWAMB…..}
Kabla sijamalizia kusoma maandishi hayo nikastukia mlipuko mkubwa ulio sababisha mwamba kupasuka na kuanza kudondosha mawe makubwa ambayo yameanza kuwaangukia watumwa wezangu pamoja na kuta za ofisi zilizopo juu kuanza kumeguka taratibu na kuporomoka chini

ENDELEA
Mawe yakazidi kuporomoka huku vilio na kelele zikitawala kwenye pango zima,Binti niliye naye akanishika mkono na kuniomba nimfwate huku tukijaribu kuyakwepa mawe yanayo endelea kuanguaka,tukafanikiwa kufika kwenye moja ya kijiuchochoro na tukapita na kutokea kwenye moja ya kijimlango cha mbao na akaniomba nichungulie ndani kupitia nondo mbili zilizopo kwenye mlango.Nikamuona mama akiwa amelala chini huku panya na wadudu wengi wakiwa wanamtambalia,hali yake imedhoohofika sana mimi kidogo ninanafuu.Nikatafuta kipande cha jiwe kikubwa na kuanza kupiga kwenye mlango huu ambao ni wa mbao.Nikaendelea kusaidiana na binti niliye kuwa naye na tukafani kiwa kuipasua mbao moja ya mlango,kutokana na wembamba wangu nikafanikiwa kupennya ndani na kumkuta mama akikoroma sana akiwa anaelekea kwenye hatua za mwisho mwisho za maisha
"Mama…..mama mama"
Nimuita mama na akayafumua macho yake taratibu na kunitazama na hakuamini kama ni mimi ndio ninaye muita,akaachia tabasamu pana nikamnyanyua na kuanza kumpitisha kwenye kijiuwazi japo ni kwashida sana ila ikanilazimu kufanya hivyo.Tetemeko la ardhi likaanza kutikisika na woga ukazidi kunitawala,nikafanikikiwa kimtoa mama kwenye kijiupenyo cha mlango kisha na mimi nikaanza kupenya ila kabla sikamalizia kutoka nikajikita nikipiga kelele ya uchungu hii ni kutokana na jiwe lenye ncha kali kutua juu ya mguu wangu wa kushoto.Mama na msichana mdogo wakaanza kunivuta nje japo kwa mama kidogo hakuwa na nguvu sana.
Nikatoka nje ya kijishimo na kuutazama vizuri mguu wangu na kuundua kuwa umetobolewa vibaya maeneo ya kigimbi na kipande kidogo cha jiwe kimekatikia ndani ya mguu.Kila nilipo jaribu kunyanyuka nikajikiya nikishinda na kukaa chini.Tetemeko kubwa la ardhi likaendelea kutetemesha kila eneo na mawe yakazidi kuanguka
"E…ddy…mwan…gu jiiikazeee"
Maneno ya mama yakanipa matumaini mapya ya kujiokoa,nikasimama wima huku meno yangu nikiwa nimeyang'ata nikisikilizi maumivu jinsi yanavyo vuta kwenye mguu wangu.Tukaanza kusikia mlio mkubwa wa maji na gafla tukastukia maji mengi yakija nyuma yetu kwa kasi kubwa na moja kwa moja nikatambua kuwa sehemu ambayo tupo kuna mwamba wa maji umepasuka.Mama akanikumbatia kwa nguvu na binti mdogo niliye kuwa naye ananing'ang'ania mkono na sote maji yakatunyanyua na tukaungana na watu wengi waliobebwa kwenye maji haya.
Ikawa ni kazi ya kumuomba Mungu tunapo elekea tusikutane na kitu ambacho kitaweza kutudhuru.Mama wala binti mdogo hakuna aliye niachia na kila mmoja akajitahidi kwa uwezo weke kunishikilia kwa nguvu zake zote.Ikawa ni kazi yangu kujitahidi kupata muhumili wa kuendana na maji haya kwani watu wengine waliojiachia walijikuta wakikigonga vichwa kwenye mawe ambayao yanaendelea kupasuka na ikawa ni safari ya maisha yao japo miili yao iliendelea kuendelea kupelekwa na maji kama tunavyo pelekwa sisi.Maji yakazidi kutupekeka kwa kasi cha kumshukuru Mungu nikafanikiwa kushika maja ya jiwe lililo simama kama nguzo,Kila nilipo mtaza mama usoni nikajikuta nikipata moyo wa kuuendelea kumsaidia mama kwa moyo mmoja na wakaendelea kunishikilia japo ninapata maumivu kwenye viganja vyangu ambaco hadi kwa sasa vimeota sugu kutokana na upasuaji wa mawe ila nikajikaza kama mwanaume.
"Bora nife mimi ila si mama yangu"
Nilijisemea kimoyo moyo huku nikijitahidi kuikanza mikono yangu ili maji yasizidi kutupeleka mbele zaidi,Kwa bahati mbaya mwili wa mtu ukaja kutua kwenye jiwe nililo lishikikilia na kuvigandamiza viganja vyangu kwa nguvu hadi nikajihisi vidole vinaweza kukatika na taratibu nikajikuta nikachina na safari ya maji ikaanza kutupeleka huku tukiwa tumetanguliza miguu.Nikaanza kuona mwanga kwa mbali kidogo ambapo ndipo maji yanapo tokea.Wasiwasi mwingi ukaanza kuniingia na nikiwa katikati ya mawazo hayo nikastukia tukuchomolewa ndani ya pango na kuanza kwenda chini ambapo ndipo maji yanapo elekea.Nikagundua sehemu tunayo kwenda kuangukia ni kwenye bahari
Sote tukaingia ndani ya bahari na kushuka chini kidogo na nikajihisi wepesi na nikaanza kuogelea kurudi juu,hadi ninatokeza kwenye usawa wa bahari nikajikuta nipo peke yangu sikumuona mama wala msichana mdogo.Baridi kali ikazidi kunitesa na mbaya zaidi sehemu kubwa ya bahari imezungukwa na milima mingi.Nikavuta pumzi nyingi ya kutosha na kurudi ndani ya maji na kuangaza kila sehemu ila sikuweza kumuona mama wala masichana mdogo.Nikarudi tena juu na kumuona msichana mdogo akinywa maji kwa mkupuo,kwa haraka nikaanza kuogelea hadi sehemu alipo na nikamuacha kudogo nguvu zimuishie ndipo nikaipitisha mikono yangu chini na kuushika mgongo wake ili aelele juu kidogo na macho yangu yakawa na kazi ya kutazama ni wapi alipo mama.Nikamuona mama akiibuka kwenye maji kwa mbali kidogo na kutokana na kuchoka sana sikuwa na hata na uwezo wa kumuita kwa sauti yajuu.Mama akaanza kupiga mbizi taratibi hadi nillipo mimi na akanisaidia kuipitisha mikono yake chini na ikakutana na mikono yangu kwa chini na tukashikana tukiwa hatujua nini cha kufanya kwa maana sehemu tuliyopo ni mbali sana kinho za bahari
Jua likaanza kuzama taratibu huku baridi ikizidi kuongezeka na kwabahati nzuri tukaona boti ndogo inayo kwenda kwa kasi ikipita maeneo ya karibu nasi.Kwa hungu nikapiga kelele za kuomba msaada huku nikisaidiana na mama,Ikatupita na kujikuta tukinyamaza tukiiangalia jinsi inavyo tokomea kwenye maji na matumaini ya kuokolewa ikakata
"Kama MUNGU aliye tusaidia tukatoka pangoni na kutufikisha hapa ninaimani yeye pia atatusaidia kupata msaada"
Mama alizungumza huku akiutasama usawa wa biti ilipo elekea kisha akanigeukia na mimi huku machi yakianza kumlenga lenga.Unene wa kiasi wa mama yangu umepota wote,uzuri na taswira yake ya kuvutia imepotea na sura yake imeingia uzee wa gafla huku akiwa amekondeana sana
"Haki ya Mungu nikirudi hai lazima nilipize kisasi kwa Mzee Godwin"
Nilijiapiza kimoyo moyo huku nikimuangalia mama kwa huruma sana,msichana mdogo hali yake ikaanza kuwa mbaya.Mwili wake ulianza kutetemeka huku kmapovu mengi yakimwagika mdomoni
"Mama ana nini huyu"
"Ni kifafa hambe jikaze kidogo mikono yako mimi ninaachia"
Nikafanya kama mama anavyo nihitaji na nikaikaza mikono yangu na mama akaitoa mikono yake na kuushika mdomo ya mtoto mdogo na kuanza kuziachanisha taya zake ili asiung'ate ulimi wake,Gafla kwa mbali sana nikaanza kuona kitu kikija kwa kasi huku kikiwa kimejitokeza upanga mmoja na kwaharaka nikatambua ni papa
"Ma…"
"Nini?"
"Ona huko nyuma"
Mama akatizama nyuma na nikastukia akiacha alichokuwa akikifanya kwa msichana na kwa haraka akaniomba niogelee na nimuache msicha.
"Mama"
"Fanya kama nilivyo kuambia okoa maisha yako kwanza huyo binti muache"
Mama alizungumza huku akiendelea kupiga mbizi akielekea upande mwengine,roho ya huruma ikanijaa moyoni mwangu na ninakafikiria mambo machache aliyo nifanyia huyu binti kwani isinge kuwa ni yeye nisingeweza kumuona mama na kwa haraka nikamuweka mgongoni kisha nikaivua suruali yangu iliyo chakaa na kubakiwa kama nilivyo zaliwa na kumfunga vizuri ili asianguke na kuanza kuogelea kuelekea kwa haraka alipo mama.Japo kuna uzito ila nikaendelea kujikaza kama mwanaume.Na jinsi ninavyo ogelea mbele ndivyo jinsi papa aliyozidi kunikaribia na safari hii akajitokeza vizuri na kuhakikisha kweli ni papa samaki mwenye meno makali ya kumrarua binadamu anaye ingia kwenye kumi na nane zake ndio anaye nifwata kwa mwendo wa kasi na kujikuta nikipiga picha ya jinsi atakavyo nirarua pamoja na huyu msichana mdogo

ITAENDELA
 
*****SORY MADAM*****(39)

AGE………………………………………….18
WRITER……………………………………..EDDAZARIA G.MSULWA


ILIPOISHIA
Na jinsi ninavyo ogelea kwenda mbele ndivyo jinsi papa aliyozidi kunikaribia na safari hii akajitokeza vizuri na kuhakikisha kweli ni papa samaki mwenye meno makali ya kumrarua binadamu anaye ingia kwenye kumi na nane zake ndio anaye nifwata kwa mwendo wa kasi na kujikuta nikipiga picha ya jinsi atakavyo nirarua pamoja na huyu msichana mdogo

ENDELEA
Gafla nikasikia milio mingi ya risasi iliyoanza kunichanganya hata mfumo wa kuogelea ukabadilika nikatamani maji ya bahari yabadilike na kuwa mchanga ili miguu yangu ipate uwezo wa kukimbia ila hikuwa hivyo zaidi ya milio kuzidi kuongezeka kwa kasi ya ajabu na kwakiweza sikujua hata ni wapi inapo tokea,Maji yakabadilika na kuanza kuwa na rangi nyekundu nikageuka nyuma na kukutana na boti iliyo wabeba watu wapatao wanne wenye bunduki na pembeni nikamuona papa aliyekuwa akinifwata akielea elea juu ya maji akiwa amekufa.Jamaa wenye boti yao wakaisogeza hadi pembeni na kunitazama kwa muda kisha wakanipa mkono na kunivuta kwa nguvu huku buinti mdogo akuwa mgongoni,wakanipa kitaulo cha kujifunga na kunza kumfwata mama ambaye tayari alisha fika mbali kutoka sehemu ambayo nilikuwepo mimi.Jamaa mmoja alizungumza na simu na sikuielewa luga yake kutokana anazungumza kikabila kisha akakata simu.Wakaisogeza boti yao hadi alipo mama na wakamvutia ndani ya maji.Nikawaona jamaa wakinong'onezana na kisha wakagongeana mikono ikatubidi mimi na mama tutazamane
"Asanteni ka masaada wenu"
Mama alizungumza huku akiwatazama usoni
"Musijali kwa hilo"
Jamaa wakaonekana kutawaliwa na furaha ambayo hadi wakati huu sikujua ni ya nini
"Mbona munafurahi?"
"Tunafurahi kwa maana tumesha kuwa ni matajiri"
"Matajiri wa nini?"
"Kuna tangazo lilikuwa linatolewa kwa mtu atakaye fanikisha kukupata wewe atapewa dola milioni mbili za kimarekani na baba yako na sasa ni mwezi wa tatu ndio sisi tumekupata"
Nikatabasamu ila ikawa ni tofauti kwa mama ambaye nahisi kuwa anajua ni mume wake mzee Godwin
"Eddy waambie wanipige risasi ili nife sipi tayari kurudi tena mikononi mwa baba yako"
"Mama sio baba wa Tanzania?"
"Unataka kusema wewe baba yako yupi huyo mwenye roho ya kibinadamu atakaye toa pesa yake ili amzawadie mtu?"
"Mama sio baba unaye mjua wewe…tambua kuwa ukweli wote ninauju na ninamshukuru Mungu kuwa nimempata baba yangu ambaye yeye ndio damu yeke japo amepitia yaliyo mengi ila ninamshukuru Mungu yupo hai"
Mama akabaki kimya huku macho yake yakiwa chini akimtazama mtoto tuliye mlaza chini,Tukaona boti nyingine kubwa ikija na kusimama karibu na sehemu ilipo boti hii ndogo,wakatuwekea kingazi na tukaanza kupanda na kuingia kwenye boti kubwa iliyo kuja na jamaa watatu wakingia na kumuacha mwezao mmoja kwenye boti ndogo.Ndani ya boti wakatupa makoti makubwa kwa ajili ya kuzui baridi kali iliyo kuwa ikitukung'uta.Wakampa msichana mdogo huduma ya kwanza na sisi wakatupatia vyakula na chai ya moto kutoa njaaa tumboni.Mimi wakanihudumia kwenye sehemu niliyo jeruhiwa na jiwe kisha wakanipa suruali mpaya,nikavua kitaulo nilicho pewa na kuivaa suruali hii.Boti ikazidi kusonga mbele huku moyoni mwangu nikijawa na amani tele ya kuweza kumpata mama yangu na kilicho salia ni kuwaunganisha baba mzazi na mama.
"Samahani kaka nyinyi ni kina nani?"
"Sisi ni wavuvi wa samaki wakubwa sasa yule papa tuliye muua tulikuwa tunamkimbiza alitusumbua sana na pale tumemuacha yule mwezetu akilinda sisi tutamrudia kumchukua na boti nyingine"
"Sawa"
Tukafika ufukweni na jamaa wakatupeleka kwenye moja ya Hotel isiyo mbali sana na bahari na kutuchukulia chumba,wakamchukua daktari maalumu na kuja kutuhudumia.Tukakaa hotelini kwa wiki moja tukijitahidi kuirudisha miili yetu katika afya zake za kawaida kwani kwa muonekano tulio nao ninaweza kujifananisha na misukule.Mudu wa wiki moja kukatika Afya yangu ikarejea kama awali japo sio sana ila kidogo niliweza kusimama mbele ya mtu au watu na kujiona ni mtu.Gharama zote zikalipwa na mama kutokana na kuwa na akaunti yake ya siri iliyopo huku Afrika kusini na kwakipindi chote hatukuwasiliana na mtu yoyote zaidi ya jamaa walio tuokoa ambao nao mama aliwakanya wasizungumze ummbea wa aina yoyote kwa mtu yoyote ili waweze kupata donge lao nono wanalo lisubiria kwa hamu kubwa kutoka kwa baba yangu mzazi
Msichana mdogo alilazwa kwenye moja ya hospitali na madaktari wanaendelea na juhudi za kuweza kumtibu kama ataweza kuzungumza tena ili awe miongoni mwa mashaidi wa kumuhukumu baba Mzee Godwin katika kesi ya kuwatumikisha watu kikatili na kuwakatili katika kuzungumza nao
"Mama unampango gani na baba?"
"Nitahakikisha ninamfunga hadi magereza yanabomoka"
"Sawa mama je baba yangu mzazi naye una mpango gani naye?"
"Mmmm sijui hata ni wapi nitaanzia kwa maana kwa niliyo mfanyia baba yako kidogo yananipa hata ugumu wa kusema ninaanzi wapi"
"Ninafurahi kusikia hivyo mama ila kwa hilo ninaomba uniachie mimi kwa maana baba ananipenda sana"
"Ila Eddy roho yangu imejawa na dukuduku kubwa ambalo sielewi siku ninamkamata Godwin nitamfanya kitu gani?"
"Hilo mama wala lisikutie mawazo sana cha msingi ni kuweza kumuomba msamaha baba yangu ili kama ni maisha yaweze kuendelea kwa amani"
"Sawa mwanangu nitafanya hivyo"
"Je umewasiliana na serikali ya Tanzania?"
"Mmmm siwezi kufanya hivyo kwanza kutokana huwezi jua baba yako ana mtandao mkubwa kiasi gani ila nitarudi kimya kimya"
"Hapo umesema ila yule daktari wako ni mnoko sana na kama unaweza awe miongoni mwa watu wa kushuhulikiwa"
"Kwa nini?"
"Ana vitu vingi sana ambavyo wewe ukimuambia humuambia baba,kwa mfano swala la kuwa mimi sio mwanaye wewe siku ulipokuwa unamwambia pale sebleni kama sisi.Yeye kaenda kuyang'aza kwa lile jijambazi ndio maana likatumia uwezo wake wa kijeshi kufanya mambo ya ajabu kama haya"
"Kumbee hapa ndio ninaanza kupata picha kwa maana siku ambayo waliniteka hospitali baba yako akawa analalamika kuwa nimemdhalilisha na lazima na mimi anidhalilishe"
"Ndio hivyo mama je ile siku walikupeleka wapi?"
"Walinipeleka sehemu moja hivi wala sikujua ni wapi ila nikaja kukutana na binti mmoja aliniambia anaitwa nani vileee….."
"Nani…..?"
"Jina lake limenitoka mara moja alisema na yeye anatokea Tanzania na anakufahamua sana wewe na mumeshirikiana sana kwenye mambo mengi"
"Sheila"
"Eheee huyo huyo….yule binti alinisaidia sana kipindi nipo matesoni kweni baba yako alinipeleka kwenye jijumba chakavu msituni huko wakanifungia…cha kushukuru Mungu yule binti alikuwa akiniletea chakula kila siku usiku kwani wao walikuwa wakinipa vyakula vibaya?"
"Kina nani?"
"Si hilo jibaba lako na watu wake"
"Ahaaa ila sio baba yangu"
"Basi siku kama mbili zilipita sikumuona Sheila sasa sikujua ni wapi walimpeleka binti wa watu sijui walimuua au"
"Hawakumuua….nilikutana naye hapa kipindi cha katikati akiwa amelishwa makaa ya mawe hawezi kuzungumza"
"Weeee ndio maana baba yako akaamua kunipeleka kwenye lile jipango na kuniambia kuwa nitalisha keki za moto"
"Ndio"
"Basi nakumbuka kipindi ninaingizwa mule sikubahatika kulishwa hayo makaa na walinipiga na kuninyanyasa sana hadi ikafikia kipindi wakanitenga na wezanu na kunifungia kwenye kile kijichumba"
"Unajua siku ya mwisho unapigwa mimi ndio niliye kusadia kuuziba mwili wako ili nipigwe mimi badala yako"
Mama akabaki akiwa mdomo wazi na taratibu chozi likamtoka na akanivuta na kunikumbatia kwa uchungu na machozi yakaendelea kumtoka hadi akalowanisha bega langu alilo pitishia bega
Niambembeleza mama hadi akanyamaza na akaniaga na kuingia chumbani kwake kulala na mimi nikabaki nikitazama Tv na nikapitiwa na usingizi kwenye sofa nililo kaa.Asubuhi kama ilivyo kawaida daktari maalumu anayetuhudumia akaja kututembelea na kutupa maelezo ya nini tuweze kufanya ili afya zetu ziweze kuhimarika.Nikwasiliana na jamaa walio tuokoa kili waje kutuchukua na watupeleke nyumbani kwa baba.Baada ya nusu saa jamaa wakawa wamefika na sisi tukawa tayari kwa safri,njia nzima ndani ya gari mama akawa amenishika mkono huku akiwa na futaha sana.Tukafika kwenye jumba la baba na nikamuona mama akitazama tazama kila sehemu
"Mama mbona unashangaa?"
"Hili jumba lote ni la kwake?"
"Ndio"
"Amejitahidi"
Walinzi wakazungumza na dereva anaye endesha gari letu na baada ya kuniona mimi wakaturuhusu.Nikawa mtu wa kwanza kushuka na nikamuomba mama kusubiri ndani ya gari hadi nitakapo kuja kumuita wenyewe wazungu wanasema kumfanyia Suprize baba.Nikafungua mlango ndani huku nikiwa na shuuku kubwa sanaya kumuona baba,
"Nimesema sitaki kumona huyo kinyago wako humu ndani"
"Lazima……."
Nilizisikia kelele za baba na mke wake wakibishana ila sentesi ya baba haikumalizika na kwakasi kubwa nikashuhudia akinguka kutoka juu gorofani alipo sukumwa na mke wake na akatua kwenye meza ya kioo na kutulia kimya

ITAENDELEA
 
*****SORY MADAM*****(40)

AGE………………………………………….18
WRITER……………………………………..EDDAZARIA G.MSULWA


ILIPOISHIA
"Nimesema sitaki kumona huyo kinyago wako humu ndani"
"Lazima……."
Nilizisikia kelele za baba na mke wake wakibishana ila sentesi ya baba haikumalizika na kwakasi kubwa nikashuhudia akinguka kutoka juu gorofani alipo sukumwa na mke wake na akatua kwenye meza ya kioo na kutulia kimya

ENDELEA
Nikabaki nikiwa nimesimama kama sekunde kadhaa huku macho yangu nikimtizama baba kisha ninayahamishia kwa mke wa baba ambaye hakuzungumza kitu cha aina yoyote,Akaondoka na kukimbilia ndani kwa haraka nikamsogelea baba na kumuwekea mkono kifuani na sikuyasikia mapigo yake ya moyo yakifanya kazi,Nikapiga kelele za kuomba msaada na walinzi wa baba wakaingia akiwemo mama na akaonekana kustuka baada ya kumkuta baba katika hali kama hii
"Eddy amefanya nini?"
Sikumjibu mama zaidi ya kunyanyuka na kuanza kupandisha ngazi za kuelekea gorofani na nikakutana uso kwa uso na mke wa baba akiwa ameshika begi la kuburuza huku mkono wake mmoja akiwa na bastola,Akiwa anababaika kuikoki bastola kwa haraka nikamrukia na kusukuma na akaanguka chini na bastola yeka ikaangulia pembeni.Nikamuwahi kumshika kifuani kwenye shati alilo livaa na nikamnyanyua hadi akasimama na nikumvuta karibu yangu na ngumi mbili za haraka zikatua usoni mwake,Akainama huku akiwa ameizima pua yake kwa mikono yake miwili na damu nyingi zikaanza kumtoka,sikuhitaji kumuonea huruma zaidi ya kuiacha mikono yangu kufanya kazi ya kuzichomoa ngumi zenye kasi kubwa na kutua katika mwili wa mke wa baba ambaye aliendelea kulia kama mtoto mdogo
Mke wa baba akaanguka chini na kunipa fursa nzuri ya kuanza kumpiga mateke ya tumbo yaliyo mfanya ajikunje kama samaki mbichi huku damu zikiwa zinamwagika puani na mdomoni.Nikaikota bastola yake na kuikagua kwa haraka na kugundua kuwa ina risasi za kutosha na nikaielekeza kwake kwa hasira
"Eddy......Eddy"
Nikaisikia sauti ya mama ikiniita kwa nyuma
"Eddy mwangu ninakuomba usifanye hivyo baba yangu nakuomba tena sana mwanangu mpendwa usifanye hilo mwanangu"
"Mama huyu mwanamke ndio chanzo cha baba kuanguka kutoka juu na kufa,na hana haki ya kuishi duniani kwahiyo niache nifanye ninacho kitaka kukifanya"
Nilizungumza kwa sauti nzito na nne iliyo jaa uchungu na hasira na machozi yakiwa yametapakaa kwenye sura yangu kiasi kwamba hata mimi mwenyewe nikajishangaa ni wapi hii sauti imetokea
"Eddy nakujua mwangu....nakuomba utulize hasira zako nakuomba mwanangu tafadhali"
Mama alizungumza huku akinisogelea taratibu huku walinzi watutu wa baba wakiwa nyuma yake,Nikamtazama mke wa baba jinsi anavyo hema kwa tabu nikayakaza meno yangu kwa kuyang'ata na kwa hasira nikaipiga risasi moja chini karibu na eneo alilo lala na bastola yake nikaitupa pembeni na mama kwa haraka akanikumbatia na kuanza kunibembeleza huku akinipiga piga mgongoni
"Shiii....nyamaza baba yangu usilie baba hajafa tumemuwahisha hospitalini"
Milio miwili ya risasi ilinistua na nikatizama nyuma yangu na kumshuhudia mlinzi wa baba aliyekuwa na mahusiano na mke wa baba akianguka chini na damu nyingi zikiwa zimetapakaa kifuani mwake huku bastola ya yule mama ikiwa mkononi.Mlinzi aliye mfyatulia risasi mwenzake ni yule ambaye alinipeleka bank
"Aitaka kuwaua"
Jamaa alizungumza huku akiusogelea mwili wa mwezake na kuuchunguza kama kweli amefariki dunia,Mke wa baba akazidisha kulia baada ya kumuona mpenzi wake akiwa amelala chini.Mama akanishika mkono na kuniondoa katika eneo la tukio na kunitoa nje huku akiendelea kunituliza hasira hadi nikarudi katika hali yangu ya kawaida
"Baba anaendeleaje?"
"Wamemuwahisha hospitalini"
"Nani amempeleka?"
"Amepelekwa na wafanyakazi wake pamoja na wale vijana walio tusaidia,tuwasubiri warudi ndio tutajua ni hospitali gani ambayo wamempeleka"
"Ahaa sawa"
"Yule uliye kuwa unampiga ni nani?"
"Si ni mke wa baba"
"Ahaa na yule mwengine aliye pigwa risasi?"
"Ni mshenzi mwenzake ambaye walikuwa wakitembea pamoja na kumzunguka baba"
Tukiwa katika mzungumza ya kawaida tukazishuhudia gari mbili za polisi pamoja na gari moja za wagonjwa zikiingia kwenye geti kuu la jumba la baba na kusimama sehemu ya magari ya kusimama,Wakaingia ndani na baada ya muda madaktari wakatoka wakiwa na kitanda cha matairi na juu yake wakiwa wamemlaza mke wa baba na kumuingiza kwenye gari lao na wakaondoka huku wakiwa wanapiga ving'ora.Askari wawili wakatufwata sehemu tuliyo simama na mama na kutusalimia kwa utaratibu
"Tunaimani na nyinyi ni miongoni mwa wahusika kwenye hii nyumba?"
Askari mmoja alizungumza huku akituangalia usoni na mama akanitizama kisha akajibu
"Ndio labda tuwasaidie nini?"
"Kwa jina ninaitwa Afande Lawnrance ninawaomba kuwafanyia mahojiano ya nini kilicho tokea muda mfupi uliopita"
"Mimi ninaitwa Afande Martin
Kitu ambacho nimekigundua kuwa askari huyu anaukarimu mkubwa na nitofauti na baadhi ya askari wa Tanzania ambaye kwenye tukio kama hili atataka kukutingisha tingisha ilimradi iwe ni shida,Mama akashusha pumzi na kumtazama askari Lawnrence
"Kilicho tokea kwa ufupini kwamba yule mama aliye wahishwa hospitalini alimsukuma baba wa huyu kijana kutoka gorofani hadi chini ninaimani mumeona meza ya kioo iliyo pasuka?"
"Ndio nimeiona"
"Yaa hilo ndio kubwa ambalo limetokea na mengine mukawahoji wale wafanyakazi wa humu ndani"
"Asante mama je kijana una lolote la kuzugumza"
Kwa haraka mama akaniminya mguu pasipo askari kuono tukio hilo
"Hapana sina la kuzungumza"
"Haya asanteni kwa maelezo yenu"
Wakatupa mikono na wakaondoka na kuniacha nikiwa na wasiwasi mwingi juu ya tukio hili na sheria za hapa Afrika kusini hata kama una pesa kiasi gani ila kama umefanya kosa lazima ustakiwe
"Mama si watanikama wakiujua ukweli?"
"Ndio..ila cha kufanya sasa hivi nikupeleke kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo hapa na urudi Tanzania na mimi uniache nishuhulikie hili swala"
"Mama wewe ubaki.....!?"
"Ndio nahitaji kulishuhulikia kwanza hili swala la baba yako la sivyo wataanza usumbufu tena wa kukupeleka mahakamani na ikiwa hivyo ujue ni ishu nyingine tena ya kukuweka mmatatani"
"Sasa mama...."
"Hakuna cha sasa tena ngoja nizungumze na vijana wa hapa kazi hiyo ifanyike sasa hivi"
Mama akamuita mmoja wa walinzi wa baba na kuwaomba atupeleke ulipo ubalozi wa Tanzania
"Si unapajua?"
"Ndio mama ila mimi sihusiki na maswala ya usafiri na funguo zote za magari zipo ndani"
"Eddy si unajua sehemu zinapokaa funguo za magari?"
"Ngoja nikatazame ndani kwa baba"
Nikaingia ndani na kuwakuta askari wakipiga picha sehemu za matukio yalipo tokea,moja kwa moja nikaingia chumbani kwa baba na kuanza kufungua kabati moja baada ya jengine na sikufanikiwa kuona funguo hata moja.Nikafungua droo ya kitanda na kukuta funguo mbili za gari pamoja na saa mbili za dhahabu.Nikaziingiza mfukoni saa na kuzichukua funguo na kutoka nje,nikiwa ninashuka ngazi askari mmoja akanifwata na kunizuia
"Angalia usikanyange hiyo kwenye hilo sehemu lililo chorwa"
Alinielekeza nisipite kwenye sehemu ambayo wameichora kama ushaidi,Nikapita pembeni na kutoka nje na kuwakuta mama na mlinzi wakitusubiria.Tukafika sehemu yenye magari ya baba na kuitoa funguo moja na kuminya kitufe kilichopo kwenye gari kikiwa na matumizi ya kulifungua gari husila la funguo hiyo.Gari moja likatoa mlio na sote tukajua ndio gari husika la funguo hii.Nikamkabidhi mlizi funguo na sote tukaingia ndani ya gari na kuondoka.
Tukafika kwenye ofisi za ubalozi wa Tanzania na mama akashuka na kuniomba nibaki ndani ya gari na baada ya muda akatoka na kuniita kwa ishara na sote tukangozana hadi ndani ambapo akaanza kunitambulisha kwa balozi wa Tanzania Afrika kusini bwana Marki Msuya na baadi ya wafanyakazi wa ofisi hii.
"Tena mumekuja muda mzuri kwa maana leo ndio siku ya wale vijana wa Tanzania walio zamia huku na kukamata ndio wanarudishwa"
"Wanatumia usafiri gani?"
"Serikali ya hapa imetupa ndege tuwarudishe vijana wetu wapo kama 248 hivi"
"Si kijana wangu anaweza kupata nafasi kwa maana mimi ninahitaji kubaki huku kuna ishu nitaishuhulikika kabla ya kurudi nchini"
"Ndio nafasi zipo.....Za masiku dada yangu kwa maana ninayo taarifa kuwa umetekwa na Al Shabab?"
"Ahaa tutazaungumza baadaye kaka yangu ila kikubwa kwanza tumshuhulikie huyu kijana wangu"
Mipango ya mimi kurudi Tanzania ikaanza kushuhulikiwa na jina langu likawa ni miongoni mwa majinina ya vijana wanao rudishwa Tanzania kwa kuingia nchini Afrika kusini pasipo kuwa na kibali maalumu.Mida ya saa nane mchana tukafika uwanja wa ndege wa O.R. Tambo International uliopo Johannesburg na nikajumuishwa na baadhi ya vijana nilio wakuta katika sehemu za kusubiria ndege muda wa kuondoka huku wakiwa chini ya ulinzi mkali wa askari.Mama akanikumbatia kwa ishara ya kuniaga
"Ukirudi hakikisha humuambii mtu yoyote ni wapi nilipo na hakikisha kuwa unafwatilia nyendo zima za baba yako na utakuwa unawasiliana na mimi"
"Nitawasilia vipi na wewe kwa maana sina simu?"
Mama akamuita balozi wa Tanzania na akamuoma namba yake ya simu ambayo akaiindika kwenye kikaratasi na kunikabidhi mimi
"Hiyo utaitumia kuwasiliana na mimi kwa maana mama atakuwa kwangu"
"Sawa"
Muda wa kuondoka ukawadia na tukaongozwa hadi kwenye ndege ambayo ndi maalu kwa sisi kuondoka na tukaanza kuingia kwa majina na mimi nikawa mtu wa mwisho kwenye orodha ya majina na kuingia ndani ya ndege na kukuta wezangu wote wamekaa kwenye siti zao.Nikaanza kutafuta siti niliyoa ambiwa na muhudumu nikae.Kila abiria akawa ananitazama na macho yangu yakagongana na macho ya Sheila akiwa amejifunga kitambaa kichwani na pembeni yake amekaa jamaa mwengine
"Sheila?"
"Bee"
Nikampa mkono nikataka kuanzisha mazungumzo ya kujua ni nini kimempata ila muhudumu akaniomba nikakae kwenye siti yangu iliyopo nyuma kabisa kwani ndege imebakisha dakika chache kabla ya kuondoka.Nikakaa kwenye siti yangu na kujufunga mkanda na nisita ambayo pembeni hapakuwa namtu yoyote na mashine za ndege zikawashwa taratibu,Kwa kupitia kwenye kiio nikazishuhudia gari sita za polisi zikija katika eneo ilipo ndege na kuizuia isiondoke na katika kuchungulia vizuri nikamuona Askari Lawrance akizungumza na waongozaji wa ndege wa chini akiwaomba ndege isiondoke na wakihitaji kumshusha mmoja wa abairia wa ndege hii na kwa haraka nikajua ni mimi ndio wamenifwata na kuyafanya mapigo yangu ya moyo kuanza kwenda kasi na amani ikanitoweka moyoni mwangu

ITAENDELEA
 
*****SORY MADAM*****(41)

AGE....................................................................18+
WRITER.............................................................EDDAZARIA G.MSULWA


ILIPOISHIA
Kwa kupitia kwenye kiio nikazishuhudia gari sita za polisi zikija katika eneo ilipo ndege na kuizuia isiondoke na katika kuchungulia vizuri nikamuona Askari Lawrance akizungumza na waongozaji wa ndege wa chini akiwaomba ndege isiondoke na wakihitaji kumshusha mmoja wa abairia wa ndege hii na kwa haraka nikajua ni mimi ndio wamenifwata na kuyafanya mapigo yangu ya moyo kuanza kwenda kasi na amani ikanitoweka moyoni mwangu

ENDELEA
Kutokana tayari injini za ndege zilishaanza kuata moto haikuwa rahisi kwa kuisimamisha ndege ambayo taratibu ilishaanza kuondoka kuzipisha ndege nyingine ambazo zinasubiri kutua na kila kitu katika uwanjwa huu wa ndege vinakwenda na muda wanao jipangia.Macho yangu yakashuhudia jinsi tunavyo ziacha gari za polisi na ndege inavyo ongeza mwenza na kuitafuta njia ya kurukia
"Ehee mola niokoe mimi mja wako kwa maana mmmm"
Nilijizungumza kimoyo moyo na kweli ndege ikakaanza kunyanyuka taratibua na kuiacha ardhi ya Afrika kusini hadi ndege inakaa sawa angani ndio nikapata amani na kajasho taratibu kakanishuka huku kwa mbali nikijasikilizia jinsi mapigo ya moyo yanavyo punguza kasi yake,safari ikaendelea kwa amani na kutokana na uchovu mwingi nikajikuta nikilala fofofo pasipo na kitu kilicho nistua ni kipaza sauti cha rubani akituomba tufunge mikanda yetu vizuri kwani ndege inajiandaa kutua katika uwanja wa Jomo Kenyata nchini Kenya
"Mmmmmmm"
Nikajikuta nikiguna kwani sijazoea kuziona ndege zinazo toka nchini Afrika kusini kutua Kenya ili kwenda Tanzania na isitoshe kwa maelezo niliyo yasikia wakizungumza mama na balozi wa Tanzania ni kwamba ndege inakwenda moja kwa moja Tanzania.Moyo wangu ukaanza kupoteza amani tena ikanilazimu kumiya muhudumu wa ndege na hakusita kunifwata sehemu nilipo na kunisikiliza haja yangu niliyo muitia
"Sijui nimesikia vibaya au....? Ni kweli tutatu Kenya?"
"Ndio kuna mzigo tunaishusha kwanza na pia kuna mmoja wa abiria nanhitajika kurudisha Afrika kusini kwahiyo tunaiwahi ndege ya shirika letu inayo ondoka Kenya saa sita usiku na tutamkabidhi abiria huyo kwa askari."
Moyo ukawa kama umelipuliwa na bomo,kuzungumza nikajikuta nikishindwa na kubaki nikimtazama muhudumu kama sanamu la kushangaza
"Halloo mr"
Nikastuka na kumtazama muhudumu wa ndege ambaye alikuwa akinipungia mkono mbele ya uso wangu baada ya kuniona nikiwa nimegandishwa kama sanamu
"Umesema kuna mtu anashushwa?"
"Ndio hiyo ni taarifa tuliyo powa tukiwa njiani"
"Ni mwanume au mwanamke"
"Kusema kweli hatujatajiwa ni jinsia gani?"
"Nashukuru"
"Na wewe pia"
Muhudumu akaondoka na kuniacha nikitawaliwa na mawazo na laiti ingekuwa nipo kwenye gari nigeweza kuruka na kufilia mali.Kitu cha ndege ni ngumu sana kujirusha,rubani akatutangazia kuwa zimesalia dakika tano kwa ndege kutua na kila mto ahakikishe kuwa amejifunga vizuri mkanda wake hapo ndipo nikakumbuka na mimi kujifunga mkanda.Ndani ya dakika tano ambazo rubadi alisema ndivyo jinsi iliyo kuwa na ndege nikaanza kushuka chini kwa kasi na matairi yake yakaanza kukanyaga ardhi ila gafla tukasikia mlio wa ‘KWAAA' kama kitu kilicho katika na kuifanya ndege kuegemea upande wangu niliopo na wezangu tulio kaa upande huu.Milio ya vyuma kukatika katika tukazidi kuisikia na si mimi mwenye niliye anza kupiga kelele za kumuomba Mungu ila hadi wezangu nao wakafanya hivyo huku kila mmoja akiomba kwa lugha anayo ijua yeye mwenyewe
Ndege ikazidi kulala upande wetu na kazidi kuserereka na mbaya zaidi moto mwingi ukaanza kuwaka sehemu ya nyuma mita chache kutoka ilipo siti yangu na kunilazimu kuufungua mkanda ili kuyaokoa maisha yangu kama wanavyofanya wezangu.Nikawahi kuishika siti ya mbele yangu ili kujizuia na upepo mwingi unao nivuta nyuma kutoka katika sehemu ulipo moto ambao umepasua sehemu nzima ya nyuma.Nikajikaza kwenda mbele na watu walio shidwa kujishikilia walivutwa nyuma kwenye moto.Kelele na vilio vikazidi kutawala na kila sehemu na watu wengi wakawa wamebanwa na siti zao kiaisi kwamba baadhi yao walijigonga vibaya kwenye vyuma na vichwa vyao kupasuka vibaya na wengine kukatika viungo vya miili yao
Ndege ikagonga sehemu na kusababisha mtikisiko mkubwa na kupinduka kichwa chini miguu juu jambo lililosababisha mikono yangu kushindwa kuhimili kuishikilia siti niliyo kuwa nimeishika na nikajikuta nikiachia na kuanza kuvutwa nyuma na upepo mkali uliochanganyika na moto ambao ni mkali sana,Gafla nikastukia nikidakwa mkono na kuangalia vizuri nikamkuta ni Sheila ambaye amenishika mkono huku na yeye akiwa amekaa kwenye siti yake na kuzuiwa na mkanda alio jifunga na huku mkono mmoja akiwa ameushika kwenye siti iliyopo pembeni.Nikamtazama kwa macho ya huzuni na kumuona akishindwa kuhimili uzito wangu kwani tegemezi lote la mwili wangu ni mkono wake na sikuwa na sehemu yingine ya kushikilia
"Sheila niachie nife"
"Eddy unasemaje?"
"Niachie."
Nilizungumza huku nikimtazama Sheila machoni ambaye anatumia nguvu nyingi kunizuia nisichomolewe nje ya ndege na mbaya zaidi pembeni yangu hakuna kitu ambacho ninaweza kusema kuwa nitakishika ili kinizuie nisichomolewe nje kwani siti zote za nyuma zimechomoka na watu wake.Ndege ikaendelea kugonga majengo yaliyopo ya hapa uwanja wa ndege hadi ikasimama ndipo Sheila akaniachia mkono na mimi nikaanguka chini na kujigonga mkono wangu wa kushoto kwenye upande wa pili wa ndege.Sheila akaaanza kupata shida ya kujifungua mkanda wa siti yake na mbaya zaidi kwa jinsi ndege ilivyo anguka imemfanya awe kichwa chini miguu juu
Nikaanza kusikia ving'ora vya gari za zimamoto zikija katika eneo la tukio na kuazna kuuzima moto unaoendelea kuiteketeza ndege,moshi mwingi ulio tawala ndani ya ndege ukanifanya nianza kukohoa na taratibu nikaanza kujivuta nje ya ndege huku mkono wangu ukitawaliwa na maumivu makali.Niavutwa nje na waokoaji na gafla mlipuko mkubwa wa ndege ukatokea na kuturusha mbali mimi pamoja na waokoaji na nikajzidi kuuegemea mkono wangu ambao ninahisi unamaumivu
"No Sheila?"
Nikajinyanyua na kuanza kutembea huku nikiyumba na kujitahidi kurudi kwenye ndege ila baadhi ya waaokoaji na askari wakanizuia,Machozi mengi yakaanza kunitawala kwani moja kwa moja ninatambua kuwa Sheila ni miongo mwa walio lipuka na ndege.Wazo la kwamba ninatafutwa na polisi na ninahitajika kurudishwa Afrika kusini kujibu mastaka yangu likanijia kichwani.Nikawatazama askari na waokoaji nikaona kila mmoja yupo na mihangaiko ya kuwaokoa majeruhi wengine na taratibu nikaanza kutembea kwa kujikaza pasipo kutazama pembeni wala nyuma zaidi ya kwenda mbele huku mkono wangu wa kushoto nikiwa nimeushikilia vizuri.Machela moja ikapitishwa kwa haraka pembeni yangu na waokoaji huku wakikimbia kwa kwasi na mtu waliye mmbeba juu ya machela nikamtambua ni Sheila japo mwili wake umeharibika sana kwa moto kitu kilicho nifanya nimtambue kwa haraka ni nguo zake alizo zivaa,wakamuingiza ndani ya gari ya wagonjwa na wakaondoka
Nikabaki nikiwa na mshangao sikujua ni nini nifanye,Nikiwa ninaendelea kushangaa nikwaona askari wawili wakinifwata sehemu niliyo simama.Nikaanza kutembea kwa mwendo wa haraka huku nikigeuza geuza shingo yangu nyuma na kuwatazama askari na kuwoana nao wakiongeza mwendo wa kunifwata.Moto mkali ulio andamwa na upepe mkali ukaanza kushika majengo mengine ya uwanja wa ndege na kuwafanya watu waliopo kweye eneo hili kuaanza kukimbia kimbia ovyo kuyaokoa maisha yao.Nikajichomka katikati ya watu wanaokimbia kuokoa roho zao na nikafanikiwa kutoka nje ya uwanja wa ndege.Nikaendelea kukimbia hadi nikafanikiwa kutoka nje ya uwanja wa ndege na nilipo tizama nyuma yangu sikuweza kuwaona askari wakinifwata.Mauivu ya mkono yakazidi kunitawala na sikuwa na jinsi zaidi ya kujikaza kiume na kuendelea kutembea nisipo pajua na kunyoosha barabara ya lami ambayo nikatembea kwa umbali mkubwa na kukuta kibao kilicho andikwa Athi River na kutokana na uchovu mwingi nikatafuta sehemu nikajipuumzisha pembezoni mwa barabara,Nikapata sehemu nikajipumzisha hadi kulipo pambazuka mida ya saa kumi na moja alfajiri nikasimama barabarani na kuanza kusimamisha magari yanayo pita.Nikafanikiwa kuahatisha gari moja la watalii aina ya Landrover ikasimama
"Where are you going young boy?"(Unakwenda wapi kijana?)
"Am going Tanzania"(Ninakwenda Tanzania)
"Are you a Tanzanian?"(Wewe ni mtanzania?)
"Yes"(Ndio)
Mama wa kizungu alinihoji maswali hayo kisha akazungumza na mume wake kwa lugha ya kireno,ambaye ni dereva wa gari lao na akanikubalia kupanda ndani ya gari lao na safari ikaanza.Ndani ya gari ukimya ukatawala huku nikiyasikilizia maumivu ya mkono wangu ambao unavuta kwa kiasi kikubwa na sikuhitaji waweze kujua juu ya kuvunjikwa kwangu mkono kwani wangenihoji maswali mengi yasiyo na msingi wowote kwangu
"What's your name?"(Jina lako ni nani?)
"My name is Eddy"(Jina langu ni Eddy)
"You have a good name as our soon"(Unajina zuri kama mtoto wetu wa kiume)
"Thanks"(Asante)
"My name is Madam Loren we are going Moshi"(Jina langu ni Madam Loren,tunakwenda Moshi)
Sikutaka kujua wanakwenda Moshi kufanya nini kwani mkono wangu unaniuma kupita maelezo,Hadi tunafika Arusha Tanzani mida ya saa sita mchana hatukuweza kusimamishwa na askari njiani na tuliingilia kwa njia ya Monduli hadi tunafika Arusha mjini nikawaomba wanishushe na nikawashukuru kwa masaada wao kisha wakaendelea na safari yao kwani walinieleza wanaelekea Moshi.Nikaanza kupandisha barabara ya Old Moshi na moja kwa moja nikaenda nyumbani kwa Madam Mery.Nikafika nyumbani kwa madam Mery na kukuta mabadiliko kidogo kwani rangi ya ukuta na gati lake vilikuwa vimebadilishwa
Niikaanza kugonga kwa kutumia mkono wa kulia na nikasikia sauti ya kike ikisema inakuja kufungua,Nikasimama kwa dakika kadhaa na gati likafunguliwa na akasimama msichana akiwa amemshika mtoto mdogo mkononi mwake akiwa anasura inayo endana na mimi
"Nikusaidie nini kaka?"
"Ehee madam Mery nimemkuta?"
"Hayupo amekwenda kazini"
"Wapi?"
"Shuleni hapo juu...Karibu ndani"
Nikatazama pande zote za nje kisha nikaingia ndani huku nikimtazama mtoto aliye bebwa na mtoto msichana ambaye ninahisi ni msichana wa kazi na kusema kweli kila kitu ambacho mimi ninacho kwenye sura yangu kipo kwa huyu mtoto mdogo.Binti akatangulia kuingia sebleni na akanikaribisha kwenye masofa mapya niliyo yakuta ndani ya sable hii kidogo nikashusha pumzi,Gafla macho yangu yakagongana na mume wa Madam Mery ambaye siku zote ni adui yangu na mara ya mwisho nakumuka nilimpiga kichwa na akanitolea bastola na jamaa sura yake ikabadilika gafla akanitazama kwa umakini kisha macho yake akayahamishia kwa mtoto aliye bebwa na mfanyakazi wake

ITAENDELEA
 
*****SORY MADAM*****(42)

AGE....................................................................18+
WRITER.............................................................EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA
Gafla macho yangu yakagongana na mume wa Madam Mery ambaye siku zote ni adui yangu na mara ya mwisho nakumuka nilimpiga kichwa na akanitolea bastola na jamaa sura yake ikabadilika gafla akanitazama kwa umakini kisha macho yake akayahamishia kwa mtoto aliye bebwa na mfanyakazi wake

ENDELEA
"Waooo ni muda sasa sijakuona naona umekuja kuchukua kiumbe chako si ndio?"
Mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio huku nikimtazama mume wa Madam Mery na kajasho kembamba kakaanza kunimwagika
"Nipe huyo mtoto"
Mfanyakazi wa ndani akamkabidhi mume wa madam Mery mtoto ambaye tayari nimegundua kuwa ni mwanangu.
"Nenda ndani?"
Mfanyakazi wa ndani akaondoka na kutuacha na mume wa Madam,Japo ninamaumivu ya mkono nikajaribu kunyanyuka ila niweze kujiokoa,mume wa madam Mery akamshika mwanangu kichwa chini miguu juu na kumfanya mtoto kuanza kulia kwa sauti
"Kaa hapo hapo la sivyo huyu paka wako ninamwangamiza mbele ya macho yako"
Nikamangalia jinsi mtoto wangu anavyolia na kujikuta roho ya huruma ikinitawala na nikakaa chini nikimtazama mume wa Madam Mery,Akatoa simu na kuipiga
"Njoo nyum bani"
Jamaa akakata simu na kurudisha mfukoni kisha akaniangalia machoni na kutabasamu.Akamshika mtoto vizuri na kuanza kumbembeleza huku akizunguka huku na huku ndani ya sable.Mlango ukafunguliwa na akaingia Madam Mery akiwaavalia vizuri na ule uzuri wake umezidi kuongezeka na baada ya kunioana akaonekana akistushwa.Akapitiliza hadi kwa mume wake na kumpiga busu la shavu kama ishara ya salamu
"Nenda kakae kule"
"Ehee"
"Nenda kakae kwa mshenzi mwenzako"
Jamaa alizungumza kwa hasira hukua akimsukuma Madam Mery kuja kukaa kwenye sofa ambalo nimekaa
"Jamani Derick mume wangu si tulisha lizungumza na limeisha mbona unataka kuanzisha ugomvi?"
"Nyamaza Malaya mkubwa wewe,hivi unajua uchungu nilio kuwa nao wewe,Au unadhani kukaa siku zote kulea kiumbe kisicho changu hivi unajua ni maumivu gani ambayo ninayo moyoni mwangu"
Derick alizungumza huku machozi yakimwagika na mtoto wetu akiwa amemshika mikononi mwake.Madam Mery machozi yaakanza kuutawala uso wake
"Derick nakuomba unisamehe kwa mara nyingine sito rudia tena kukusaloti mume wangu"
"Ahaaa chagua mawili kati yangu au huyu panya wako?"
Macho yakanitoka nilipomuona Derick akifanya kitendo cha mara ya kwanza cha kumshika mwanangu kichwa chini miguu juu huku akiwa amemuinua kwa mkono mmoja
"Derick nyote ni muhimu sana kwangu ninakuomba mume wangu unisamehe nina kupenda sana mume wangu"
"Wewe manamke ni muuaji,kumbuka mimi ndio nilikufanya kupata elimu yako hadi akawa mwalimu ukaona haitoshi ukanisaliti mara ya kwanza nikakusamehe......Baba yako alifariki mikononi mwangu tukimuwahisha nchini India kwa matibabu na zote zilikuwa gharama zangu senti tano kwenu mulikuwa hamuna nimevunja vibanda vyenu na kuwajengea nyumba nzuri ili nanyi muonekane watu kati ya watu ila bado umeona hatoshi kabla ya ndoa yetu umebeba mimba ambayo si yangu ni ya uyo paka hapo."
"Ni mara mia ungetembea na mtuu aliye kuzidi umri ila wewe ukachukua Serengeti Boy unadhani atakusaidia nini huyo mwehu wako"
Derick aliendelea kuzungumza kwa hasira huku machozi yakiendelea kumwagika na mwanangu akiendelea kulia kwa maumivu anayo yapata.Madam Mery kapiga magoti na kuanza kuburuzika taratibu akimfwata mumewe sehemu aliyo simama
"Rudi huko huko la sivyo ninamuua huyu paka wenu."
Madam Mery akaanza kurudi nyuma taratibu huku akiendelea kumwagikwa na machozi mengi.Kelele za mwanangu kulia kwa maumivu zikanifanya nishindwe kuvumilia huku hasira ikinipanda nikanyanyuka huku nikiwa nimeushika mkono nilio vunjika na kupiga hatua mbili mbela za kuikwepa miguu ya madam mery
"Wewe rudisha miguu yako huko la sivyo ninamuachia huyu mtoto"
Derick aliniambia akionekana kutokuwa na huruma kabisa na maumivu anayo yapata mwanangu,nikashindwa kuizuia miguu yangu na kujikuta nikizidi kupiga hatua kwa hasira kali iliyo nitawala mwili mzima.Derick akampiga mwanagu chini kwa nguvu na kumfanya mtoto wangu kunyamaza kimya na kelele kali ikatoka kwa madama Mery pamoja na mfanyakazi wa ndani ambaye alikuwa amejificha kwenye ukuta akishuhudia kila kinacho endelea.
Sikujali kama mkono wangu mmoja umevunjika kwa hasira nikamrukia Derick ambaye akanikwepa na kunisindikiza kwa teke kali la mgongoni na kujigongwa kwenye uso kwenye ukuta na kuangukia pembeni ya miguu ya mfanyakazi wa ndani ambaya mkononi mwake ameshika kisu na kitunguu.Nikamuomba mafanyakazi wa ndani kisu kabla hajanipa Derick akauwahi mkono wa mfanyakazi wa ndani ulio shika kisu ikanilazimu na mimi kuuwahi mkono wa mfanyakazi kwa kuutumia mkono wangu mmoja usio vunjika.Derick akatuzidi nguvu na kumshika mfanyakazi wa ndani na kusukumia pembeni na kisu kikaanguka chini.Kabla Derick ajakiokota nikampiga teke na kuifanya miguu yake yote miwili kunyanyuka chini na akaangukia mgongo.
Nikajisogeza kwa haraka na kabla sijakiokota kisu akanikanyaga vidole vya mkono wangu wa kulia nilio unyoosha kukiokota kisu.Derick akakipiga kisu mbali kido na eneo ambalo nililo angukia akanipiga teke la mbavu lilinifanya nijikunje huku nikigumia kwa maumivu makali.
"Derick utamuua mtoto wa watu"
Madam Mery alizungumza huku akimwagikwa na machozi na mikpono yake ikiwa imejaa damua na vitu vyeupe vyeupe na kugundua kuwa mwanangu amepasuka kichwa chake.Nikanyanyuka huku meno yangu nikiwa nimeyang'ata kwa nguvu.Nikajaribu kuuyanyua mkono wangu wa kushoto ulio vunjika na kuufanya kuuma kwa maumivu makali yaliyonifanya nitoe ukelel wa kuumia kwani kuna kitu kinanichoma kwa ndani.Derick akayashusha macho yake hadi kwenye mkono wangu kisha akayarudisha machoni mwangu na kwa haraka akanitisha kama ananipiga teke kwenye mkono na kuufanya niukinge mkono wangu kwa kugeuka na kumpa mgongo na kushtukia akininyanua miguu yangu na kuivuta na kuanguka kifudifudi huku mkono ulio vunjika nikiwa nimeulalia
Derick akanikalia mgongoni na kuishika mikono yangu yote miwili na kuivuta kwa nyuma.Maumivu ninayo yapata sikuwahi kuyapata tangu nizaliwe.Madam Mery akauweka chini mwili wa mtoto wetu na kukimbilia sehemu tuliyupo na kumsukuma Derick na akaanguka kwa mbele yangu.Sikuwa na uwezo wa kunyanyuka kuokana na maumuzi makali na kubaki nikilia kwa uchungu.
"Ni binadamyu gani usiye na huruma wewe,umenilia mwanangu kikatili ila bado unataka kumuu huyu kijana wa watu"
"Niliapia ni lazima nimuue huyu kijana pamoja na wewe na leo ndio mwesho wenu"
Derick alizungumza huku akinyanyuka kwa haraka na akamshika madam Mery nywele zake na kumbwaga chini kwa nguvu na kumfanya madam mery kutoa ukulele wa kulia kwa maumivu
"Shemeji mikono yako nyoosha juu"
Niliisikia sauti ya mfanya kazi kwa nyuma yangu na kunifanya nigeuke nyuma na kumkuta akiwa ameshika kisu huku mwili mzima ukimtetemeka.Derick akacheka kwa dharau na kumfwata mfanyakazi kwa kasi na kupiga kabali ya gafla na kumpokonya kisu na pasipo kuwa na huruma Derick akamchoma mfanya kazi wa ndani kisu cha tumbo na kumtupa chini.Derick akanisogelea huku kisu chake kikiwa kinavuja damu za mfanyakazi,akaniinamia na kunitazama kwa umakini huku akicheka
"Nilikuumbia siku nikikutia mikononi mwangu nilazima nikuue"
Maneno ya Derick hayakuhafikiana na moyo wangu kuyakubali kiharaka na kirahisi kama anavyo fikiria.Kwa haraka nikainyanyua miguu yangu kuikaba shingo ya Derick na kwa nguvu zote.Madam Mery akamuwahi kumshika Derick mkono ulio shika kisu na kumpokonya,Kila nilipo kumbuka jinsi mwangu alivyo anguka chini ndivyo jinsi nilivyozidi kumkaba Derick shingo yake ambaye akaanza kunishindilia ngumi za mbavu na akaubana mkono wangu uliovunjika na kuzidi kunifanya niachie ukele mkali
"Madam nisaidieeeeeee"
Madam akabaki akiwa ameshika kisu asijue nini afanye,Nikamuomba tena anisaidie ndipo akastuka kama yupo sehemu ya tukio la hatari,akatutizama tena kwa umakini na kwaharaka kisu akakishusha na kikatua kwenye bega la Derick na kumfanya aniachie na kunyanyuka kama mbogo na kumsukuma Madam Mery ambaye akaangukia mwili wa mtoto wetu na kutulia chini
"Nitaendelea kukusaka"
Derick alizungumza huku akiingia ndani kwa haraka na kutoka akiwa na begi la kuburuza na akanitazama kwa muda kisha akanipiga teke la kichwa na kizunguzungu kikali kikanitawala kikiambatana na giza kubwa lililo tanda kwenye macho yangu na nikatulia tuli
***
Milio ya ndege pamoja na mwanga mkali vikanistua na kujikuta nipo kwenye chumba chene kitanda kimoja tuu.Pembeni ya kitanda kuna meza ndogo pamoja na kiti,Kila ninapojaribu kuitadhimini sehemu hii ninashindwa kujua ni wapi.Mbaya zaidi sehemu hii haifanani na hospitalini kwani kitanda nilicho lala kinaukubwa zaidi ya kitanda cha hospitalini.Nikajichunguza vizuri na kuukuta mkon wangu ukiwa umefungwa bandeji gumu(P.O.P.O).Nikashuka kitandani na kwenda dirishani na kufungua dirisha nikaona migomba mingi nikstukia kwa nyuma mlango ukifunguliwa na akaingia mama mmoja mtu mzima
"Umeamka mwanangu?"
"Shikamoo"
"Marahaba,unajisikiaje?"
"Vizuri tuu"
Akanishika mkono na kuugeuza geuza kisha akanitazama usoni huku akiwa ameachia tabasamu pana
"Mimi ninaitwa Mama Natujwa na hapa ulipo ni Moshi"
"Nimefikaje?"
"Umeletwa na rafiki yangu anaitwa Mery na tangu uje hapa huna hukuwahi kuyafumbua macho yako na ulikuwa ni mgonjwa mahututi sana"
Ikanibidi kurudi kitandani na kukaa kwani niliaza kuhisi kizungu zungu,Mama Natujwa akakaa pembeni yangu huku akinishika shika kichwa changu na kunigeuza huku na huku
"Mimi ni daktari wa mifupa ninamiliki hospitali yangu hapa Moshi,na kipindi Mery alipo kuleta nilikufanyia oparesheni hospitalini kwangu na tukakulaza kule kwa kipindi cha mwezi mzima huku tukikulisha kwa mipira maalumu.Nilipo kuleta hapa nyumbani kwangu tatizo lililo kuwa kubwa ni wewe kurudi katika hali yako ya kawaida"
"Ni kipindi gani kimepita?"
"Unakwenda mwezi wa tatu sasa,Japo Mery alikata tamaa ya kudaidi kuwa huto weza kurudi katika hali yako ya kawaida"
"Na yeye sasa hivi yupo wapi?"
"Yupo Arusha anaendelea na kazi...tena ngoja nimpigie simu nimjulishe kuwa umezinduka?"
Nikamzia mama Natujwa kumpigia simu Madam Mery
"Kwa nini unanizuia?"
"Sihitaji alijue hili sawa"
"Je akija?"
"Nimekuambia sihitaji aweze kugundua jambo hilo"
Akili na wazo juu ya mauaji ya mwanangu likanijia kichwani mwangu,Picha niyingine ya jinsi nilivyo teseka kwenye pango nchini Afrika kusini likanijia kichwani mwangu na sura ya baba yangu mkubwa Mzee Godwin ikanijia kichwani huku ikifwatiwa na sura ya Derick.
"HII KAZI NITAIFANYA MIMI MWENYEWE"
Nilizungumza kwa sauti ya chini na kumfanya mama Natujwa kuniuliza ninasemaje
"Hapana sijazungumza kitu"
Nikaka nyumbani kwa mama Natujwa kwa wiki moja,Nilipo ridhika afya yangu ipo kamili nikamuomba ruhusa ya kuondoka na akanikubalia ila kwa kipindi chote sikumuomba asizungumze chochote kwa Madam Mery,Nikapanda basi hadi Dar es Salaam na sikufikizia nyumbani kwetu nikelekea nyumbani kwa Sheila na kukuta geti lake likiwa wazi na gari yake ikiwa imesimamishwa nje.Nikapata matumaini ya uwepo wake na moja kwa moja nikaufungua mlango wake na sikuamini macho yangu baada ya kumkuta akiwa ananyonyana denda na mwanaume mwengine ambaye kwa haraka nikamtambua ni Derick mume wa madam Mery

ITAENDELEA
 
Back
Top Bottom