Hot story

Hot story

hahahah!!!!hizo hapo ila jamaa akija kushtaki inabidi twende wote!!

Huwezi kuamini nilijificha sehemu nimsome Eddy kwa undani nasasa ndio Nimetoka machimbo, Huyu mtunzi wahii story nampongeza sana mkuu tupia zingine kama 5 zakutafutia usingizi
 
hahahah!!!!hizo hapo ila jamaa akija kushtaki inabidi twende wote!!

Hawezi kushtaki, maana ww unafata vigezo ma masharti, alichokuwa anataka eddy ni kuwa, kuwe na jina la mwandishi wa hyo hadithi, nawe waliweka, hakuna tatizo mkuu, tupia nyingine za kupatia usingizi, big up Nyaluhusa87
 
Huwezi kuamini nilijificha sehemu nimsome Eddy kwa undani nasasa ndio Nimetoka machimbo, Huyu mtunzi wahii story nampongeza sana mkuu tupia zingine kama 5 zakutafutia usingizi
Umeona eeee, yaani cjui inaishaje hii story, nitatamani iwe na pt 2
 
*****SORY MADAM*****(56)

AGE....................................................................18+
WRITER.............................................................EDDAZARIA G.MSULWA
ILIOISHIA
"VITA ILIYUPO MBELE YETU NI KUBWA SANA"
"KIVIPI?"
"MBASA KWANZA UNA UMRI GANI?"
"MIAKA ISHIRINI"
NIKATABASAMU, TABASAMU LILILO JAA UCHUNGU KWA KUMUONEA HURUMA
"ADUI YAKO NDIO ADUI YANGU"
NILIMUAMBIA MBASA NA KUMFANYA ABAKI AMENITUMBULIA MIMACHO,

ENDELEA
"Kaka Eddy sijakuelewa bado?"
"Kwa sasa sio rahisi sana wewe kunielewa, ila utakuja kunielewa muda ukiwadia"
Sikutaka kumfafanulia kila kitu Mbasa, zaidi ya kuwa makini sana kwa kila jambo ninalo lizungumza, hii ni kutokana na moyo wangu kupoteza uaminifu juu ya kila anaye nisaidia.
***
Nikakaa nyumbani kwa Mbasa siku mbili mfululizo pasipo kutoka nje, na kila siku Mbasa akawa na kazi ya kunihadisia hali halisi inavyo endelea nje kuhuasiana na polisi wanao nitafuta, siku ya tatu nikaamua kutoka nje mida ya saa tatu usiku, nikiwa nimevalia nguo za mbasa ambazo kidogo kwangu ni ndogo, ila kutokana sikuwa na lakufanya nikaamua kufanya hivyo.Nikavalia kofia iliyo yaficha macho yangu na moja kwa moja nikaelekea kwenye moja ya baa inayo itwa kilimani, lengo langu ni kupata bia japo mbili ili kuiweka akili yangu sawa
Kama kawaida muhudumu mmoja akanisogelea huku akinitazama machoni mwangu, akisubiria nini niagize,
"Niletee, kilimanjaro ya moto"
"Sawa, naomba pesa"
Nikatoa noti ya elfu tano aliyo nipatia Mbasa mida ya jioni alipokuwa akielekea kazini kwake, kuingia katika zamu ya usiku.Muhudumua akaondoka na haikuchukua dakika nyingi akarejea akiwa na chupa bia niliyo muagiza
"Utatumia glasi?"
"Hapana, asante"
Taratibu nikaanza kuporomosha mafumba kadhaa ya bia, huku sehemu niliyo kaa inakigiza kidogo na nisehemu ambayo ninaweza kuwaona wanao ingia na kutoka kwenye hii baa.Baada ya muda kidogo nikawaona wasicha wawili wa kiarabu wakiingia kwenye baa hii, huku mmoja akiwa amevalia baibui na mwengine akiwa amevalia suruali ya jinzi pamoja tisheti iliyo mbana, wakasimama na kuanza kutazama tazama ni sehemu gani ambayo waneweza kupata viti na kwabahati nzuri meza niliyo kaa mimi ina viti viwili, na sehemu nyingine zimajaa watu.Wakapiga hatua za taratibu hadi sehemu niliyo kaa mimi
"Sahamani, tunaweza kuketi hapa?"
"Ndio munaweza"
Wakaa na mimi nikaendelea kunywa bia yangu ambayo, ninaishuhudia ikielekea ukingoni na muda wangu wa kukaa kwenye hii baa utakuwa umekwisha, ukimya ukatawala kati yetu na hakuna ambaye alimsemesha mwenzake, baada ya wao kugizia vinywaji wakawa na kazi ya kuchezea masimu yao makubwa ya kugusa na kidole
"Muhudumu"
Msichana mmoja alimuita muhudumu aliyekuwa anakatiza karibu yetu
"Mletee huyu kaka,kinywaji atakacho kihitaji yeye"
"Ahaa jamani mimi, hii moja inanitosha"
"Hapana, dada mwaya lete kinywaji kama anacho kitaka huyu kaka"
Sikuwa na jinsi zaidi ya kukubaliana nao,
"Mimi naitwa Rajiti na mwenzangu anaitwa Sashah"
"Nashukuru kuwafahamu"
"Jamani hatupaswi kukujua jina lako?"
Nikatabasamu kidogo, huku nikiwa ninawatazama kwa macho ya uamakini kila mmoja kwenye sura yake
"Ninaitwa Thoma"
Niliwaongopea kuhofia jina langu la Eddy kuwa ni miongoni mwa majina yanayo tajwa kila siku katika vyomba vya habari
"Kuna kaka umefanana naye"
Sashah alizungumza, huku akiliiknja vizuri mikono ya baibui lake
"Nani?"
"Anaitwa Eddy"
Moyo ukaanza kunienda mbio huku mapigo ya kawaida yakibadilika na kuwa ya kasi sana kiasi kwamba nikaanza kujihisi vibaya
"Ahh….haaa sio mimi?"
Wakanitazama kwa umakini
"Samanani ninaomba niende msalani"
Nikawaaga na kunyanyuka, nikatamani kutoka nje ya baa ila macho yao yote tapo kwangu, nikamuuliza muhudumu ni wapi kilipo choo, akanielekeza na bahati mbaya kipo ndani ya baa hii na kama kingekuwa ni nje ingekuwa ni nafasi nzuri ya mimi kuwakimbia.Nikaingia chooni na kusimama kwenye moja ya kioo kilichomo humu ndani, nikaivua kofia yangu na kujitazama vuzuri
"Sijabadilika chochote usoni mwangu"
Nilizungumza kwa sauti ya chini, nikajiweka sawa na kuivaa kofia yangu na taratibu nikaanza kuelekea ulipo mlango, nikakishika kitasa cha mlango huku nikiwa ninahema sana, nikashusha pumzi nyingi na kuufungua mlango, nikapiga hatua mbili, gafla nikastukia nikizibwa pua na kitambaa chenye harufu ambayo tangu nizaliwe sikuwahi kuinusa, mtu aliye nikaba kwa nyma sikujua ni nani, na nilipo jaribu kuminyana naye, ndvyo naye alivyozidi kukikandamiza kitambaa puani mwangu na taratibu nikajikuta nguvu zikiniishia na nikapoteza fahamu.
***
Kwa mbali nikaanza kuona kitu nikiwa kinazunguka juu yangu, nikajaribu kuyakaza macho yangu, ila bado nikashindwa kuyafumbua, nikutokana na uchomvu mwingi ulio ambatana na usingizi mzito, nikajaribu kuinyanyua mikono yangu ila nikaihisi kuwa ni mizito sana, nikakigeuza kichwa changu upande wa kushoto na kukuta jamaa lenye miraba miine likiwa limekaa kwenye kiti, huku sura yake ikiwa na mindevu mingi sana.Hapa ndipo nilipo anza kugundua kwamba nimelala chali juu ya kindanda, sikuona kitu chochote kilicho ufunga mkono wangu, na sikuelewa ni kwanini nimekuwa mchovu kwenye mikono kiasi hichi
Nikaendelea kuvuta kumbukumbu ya nimefika vipi katika eneo hili, ila ubongo haukusoma kitu chochote zaidi ya kukumbuka kwamba nilikuwa nipo baa.Baada ya masaa kadhaa nguvu za mwili wangu zikaanza kurejea taratibu, nikapata nguvu hata ya kuyafumbua macho yangu hapo ndipo nikagundua kitu kinacho zunguka juu yangu ni feni
"Nipo wapi?"
Nilimuuliza jamaa, hakunijibu chochote zaidi ya kunitazamaa kwa macho makali, hukua akiendelea kuzichezea ndevu zake nyingi nyingi
"Nipo wapi?"
"Wee koma"
Jamaa alizungumza huku akininyooshea kidole, akionekana kukasirishwa na swali langu nililo tumia sauti ya ukali kumuuliza.Akasimama na kuitoa simu yake ya mfukoni
"Mtu wenu ameamka"
Sikujua anazungumza na nani, mapigo ya moyo yakaanza upya kudunda huku yakiandamana na wasiwasi mwingi, wazo la kwanza kunijia kichwani nikajua tarari nimeingia kwenye mikono ya Mzee Godwin, nikajaribu kusimama ila jamaa kwa haraka akaniwahi kunisukuma kitandani
"Ukilete ujinga jombaa nitakupoteza duniani?"
Nikazidi kuchanganyikiwa, baada ya muda wakaingia Rajiti na Sashah, wote wawili wamevalia suruali nyeusi na tisheti nyeusi, huku miguni wakiwa wamevaa, buti nyeusi
"Habari yako, Eddy?"
Rajiti alinisalimia, hapo ndipo nikadata kabisa na kutambua kwamba hawa si watu wazuri kwangu, kutokana niliwatambulisha kwa jina la Thomas, inakuwaje wananiita mimi Eddy
"Kamletee chakula"
Jamaa likatoka na kutuacha ndani ya chumba
"Eddy ninaimani utajiuliza imekuwaje hadi upo hapa" Sashah alizungumza
"Ndio"
Rajit akatoa picha mfukoni na kunirushia mimi kitandani nilipo lala, picha aliyo nirushia ina sura yangu na mama yangu zikiwa zimeambatanishwa kwa pamoja na kuitoa picha moja
"Usishangae sana, na kujiuliza ni wapi tumeitoa picha yako, kwa ufupi sisi tulikufwatilia kwa siku nyingi hadi jana tulipo fanikiwa kukupata" Rajit alizungumza
"Munataka nini kutoka kwangu?"
"Kikubwa tunacho kihitaji sisi ni wewe kukusaidia"
"Kunisaidia kivipi?"
"Utaelewa"
"Sisi ni wanajeshi wa kikundi cha Al-khaida, na kazi yetu kubwa ni kutafuta vijana wenye matukio makubwa kama yako, pia isitoshe tunahitaji kukupa msaada wa kumpata mama yako"
Baunsa akaingia huku akiwa amebeba sahani kubwa yenye vitu mbali mbali vya kufungua kinywa, akaviweka kwenye meza na kutoka nje
"Tunahitaji tukupeleke Iraq, yalipo makazi yetu kisha ukirudi Tanzania tukusaidia kwenye kazi moja tu"
Rajit alizungumza
"Kazi gani, unajua hadi sasa hivi sijawaelewa?"
"Eddy fungua akili yako, Tanzania nzima unatafutwa wewe, Je ukikamatwa ni wapi utapelekwa?"
"Gerezani" Nilimjibu Rajit
"Je upo tayari kuishi, gerezani?"
Swali la Rajiti likanifanya nikae kimya pasipo kumjibu chochote
"Hapa kwani nilipo ni wapi?"
"Hapa ni Mombasa, nchini Kenya.Jana tulisafiri usiku kucha hadi hapa"
"Kwa nini muniteke?"
"Ilitulazimu"
Rajiti na Sashah wakendelea kunishawishi hadi nikakubali kwenda nao Iraq kwani nikiangalia kwa jinsi maisha yangu yalivyo ya kuruka ruka kama ndege nikaona ipo siku nitanaswa kwenye jumba bovu.Akaja daktari mwenye asili ya kiarabu, waliye niambia anahusika na kazi ya kuchonhesha sura bandia, dakatari akanifanyia vipimo vya haraka na kazi ya kuchongesha sura nyingine itakayo kaa sawa kwenye uso wangu ikaanza mara moja.Ndani ya masaa sita tarari daktari akawa ameikamilisha kazi aliyo agizwa na Sashah.Kazi ya kupandikizwa sura bandia ikaanza mara moja, huku daktari akiifanya kwa umakini wa hali ya juu, haikuchukua muda mwingi sana kuvishwa sura bandia, nikaa lisaa moja kwenye kifaa ambacho daktari aliniambia kinaghusika na swala zima la kuikausha sura yangu mpya
Baada ya zoezi zima la kubadilishwa sura kuisha, Rajiti akanipa kioo niitazame sura yangu niliyo pandikizwa juu ya sura yangu halisi, sikuyaamini macho yangu kwani nimebadilika kupita maelezo hata mimi mwenyewe nikajisau
"Ebwaane eheee ni mimi kweli au naota?"
"Ni wewe, mbona hapo umetokelezea"
"Etii eheee?"
"Ndio"
"Hahaaaa"
"Sashah yupo wapi?"
"Amekwenda Mjini mara moja"
Sashah akarejea akiwa na furaha sana usoni mwake,
"Vipi kitu kimetiki nini?" Rajiti aluliza
"Ndio, chezea mimi wewe"
Rajiti akamkbidhi Sashah hati tatu za kusafiria, na akaanza kuzisoma taratibu
"Kweli wewe kiboko, kitu feki kama orijino"
"Ahaa, kila kitu kinawezekana duniani"
"Ila kipo kisicho wezekana" nilichangia mada
"Kama?"
"Kutengeneza pumzi ya mtu"
"Kweli"
"Mpe Eddy aone passport yake jinsi nilivyo itengeneza"
Sashah akanikabidhi hati yangu ya kusafiria iliyo na sura yangu mpya, huku jina langu likiwa ni Suleima Bin Yahaya
"Mbona jina ni hili?"
"Nisingeweza kuweka jina lako kutokana na wewe kuwa muhalifu, hapa mwenyewe nimetoka Jomo Kenyeata Airport na kuzikuta picha za sura yako zikiwa zemebandikwa kwamba unatafutwa"
"Mmmm"
"Unaguna? Tutakwenda na utaziona"
"Sawa bwana"
"Eheee umekata tiketi ya ndege ya saa ngapi?" Rajit aliuliza
"Saa sita uskuku"
"Ipo powa"
Tukaendelea kupiga stori za hapa na pele na nikawasimulia mkasa mzima wa nyuma uliopita kwenye maisha yangu, hadi ninamaliza wote machozi yakawa yanawamwagika
"Eddy pole sana"
"Asante"
Sashah na Rajiti wakabadilisha mavazi na kuvalia sketi ndefu nzuri na kuwafanya wapendeze sana, huku na mimi nikivalia suti kali waliyo nipa cha kushukuru Mungu imenikaa vizuri mwilini mwangu na kunifanya nionekane kama muheshimiwa wa kitengo fulani cha serikali.Tukaanza safari kwa kutumia usafiri wa gari yao ndogo, inayokwenda kwa kasi sana, kutokana ni usiku hapakuwa na magari mengi sana barabarani,Tukafika katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyata, sote tukashuku na zimesalia dakika ishirini kabla ya ndege tunayo ondoka nayo kupaa angani.Moja kwa moja tuakelekea sehemui ya ukaguzi wa hati za kusafiria, Rajiti akawa wa kwanza kukaguliwa hati yake pamoja na mwili wake kwa kutumia kifaa cha ulinzi, akapita na kupewa hati yake iliyo tiwa muhuri na muhudumu wa kike anaye ifanya kazi hiyo huku akionekana kuwa makini sana, akafatia Sashah akakaguliwa kama alivyo fanyiwa Rajit na akafanikiwa kupia
Nikamkabidhi msichana hati yangu ya kusafiria cha kwanza akanitazama machoni, kisha hati yangu ya kusafiria akaiweka kwenye mashine inayotoa ripoti kwenye kioo kikubwa cha ‘computer'.Askari anaye kagua akaanza kazi yake ya kukipitisha kifaa chake kuanzia miguuni, msichana akanitazama kwa macho makali kisha akatazama tena kwenye kioo cha kumputer yake, nikatazama pembeni na kuwaona askari wawili walio shika mbwa wakubwa weusi wakianza kunisogelea, huku wakiwa na bubduki zao mikononi, kifaa cha ukaguzi kikaanza kutoa mlio wa kelele huku kikiwaka taa nyekundu kilipo fika maeneo ya shingoni
ITAENDELEA
 
*****SORY MADAM*****(57)

AGE....................................................................18+
WRITER.............................................................EDDAZARIA G.MSULWA


ILIOISHIA
Nikamkabidhi msichana hati yangu ya kusafiria cha kwanza akanitazama machoni, kisha hati yangu ya kusafiria akaiweka kwenye mashine inayotoa ripoti kwenye kioo kikubwa cha ‘computer'.Askari anaye kagua akaanza kazi yake ya kukipitisha kifaa chake kuanzia miguuni, msichana akanitazama kwa macho makali kisha akatazama tena kwenye kioo cha kumputer yake, nikatazama pembeni na kuwaona askari wawili walio shika mbwa wakubwa weusi wakianza kunisogelea, huku wakiwa na bubduki zao mikononi, kifaa cha ukaguzi kikaanza kutoa mlio wa kelele huku kikiwaka taa nyekundu kilipo fika maeneo ya shingoni

ENDELEA
"Vua cheni yako"
Askari anaye nikagua aliniambia na kunifanya niivue cheni, niliyo ivaa shingoni mwangu.Akaendelea kukipitisha kifaa chake kwenye mgongo hadi chini kwenye miguu,
"Safari njema"
Dada aliyekuwa anaikagua hati yangu ya kusafiria alizungumza huku akinikabidhi hati yangu ya kusafiria, huku usoni mwake akiwa ameachia tabasamu pana lililo pendezeshwa na mwanya wake mwembamba.
"Asante na wewe pia kazi njema"
Nikapita kwenye kizuizi na kuwafanya Sashah na Rajiti kushusha pumzi nyingi kwani walihisi kwamba tayari nimeingia kwenye mikono ya askari, tukaingia ndani ya ndege, cha kushukuru Mungu, siti zetu tatu zipo sehemu mmoja, hatukukaa hata dakika nyingi, rubani akatuomba tufunge mikanda yetu kwani ndege itajiandaa kuruka muda sio mrefu.Ndani ya dakika kadhaa tukaanza kuiacha ardhi ya nchini Kenya
"Eddy" Rajiti aliniita
"Naam"
"Unajua kwamba unaonekana tofauti sana"
Alizungumza kwa sauti ndogo
"Kweli?"
"Ndio, umekuwa bonge la handsome"
"Mmmmm"
"Kweli vile"
"Jamani acheni kelele watu wamelala" Sashah alizungumza
"Ahaaa shauri yao, bwana"
Masaa yakazidi kusongo mbele, na ndege yetu ikatua baadhi ya nchi ambapo, baadhi ya abiria walishuka na kupanda abaria wengine na safari ikaendelea.Tukafika nchini Iraq, majira ya saa moja saa tisa alasiri huku sote tukiwa tumechoka kwa uchovu wa kukaa kwenye ndege takribani masaa kumi na tano, kutokana hatukuwa na mizigo tukawahi kupanga mstari wa kutokea sehemu ya kukaguliwa, huku moyoni mwangu nikiwa ni naomba sana nisiweze kushtukiwa kwa lolote, na nikafanikiwa kutoka njee ya uwanja wa ndege pasipo mtu yoyote kunistukia kwamba nimevalia sura bandia,
Sikuwa na sehemu yoyoote ninayo itambua na wenyeji wangu wakubwa ni Sashah na Rajit.Tukapanda kwenye taksi mojawapo iliyopo kwenye maegesho ya uwanja wa ndege na Sashah akazungumza kwa lugha ya kiarabu na dereva tuliye mkuta ndani ya teksi hii, Tukafika kwenye moja ya Hotel kubwa iliyo andikwa kwa maandishi ya kiarabu na kila kitu ambacho wanakizungumza Shasha na watu wengine, sikuweza kukifahamu kutokana siitamui lugha ya kiarabu
Sashah akamaliza kuzungumza, na wahudumu na akakabidhiwa funguo moja, akatufwata sehemu tulipo simama na Rajit, tukaingia kwenye lifti iliyo tupeleka hadi ghorofa ya sita, na tukaingia kwenye chumba ambacho Sashah alikodisha
"Eddy utakaa hapa siku mbili, ili uyazoee mazingira kisha tutaelekea makao makuu"
Sashah alizungumza
"Na nyinyi munakwenda wapi?"
"Sisi, tunakwenda kufwatilia mambo muhimu, kwa ajili ya kazi zetu, kikubwa ni wewe kuwa makini katika hili eneo.Tumekulipia chakula kila mahitaji utakayo yahitaji tumegharamia"
"Sasa jam…."
"Eddy hapo hakuna cha sasa kikubwa ni wewe kuwa makini, usipende kujitokeza tokeza kwa watu kwani watu wa huku hawana huruma, wana roho za kinyama.Yaani ukitembea sana wewe mwisho wako ni kule chini kwenye sehemu ya chakula"
"Sawa nimewaelewa, je nikihitaji hudumu ya kuwapigia wahudumu wa hii hoteli?"
"Kuna kitabu pale juu ya meza kwenye ile simu basi utaweza kuitumia hiyo sawa, na kabla sijasahau chukua hizi cuppon ukienda kuchukua chakula unaonyesha, zipo za ana mbili, moja ya chakula na nyingine ya kinywaji.Ukizipoteza baba utashinda njaa hizi siku mbili"
"Powa"
Sashah na Rajit wakaondoka na kuniacha nikiwa nimesimama, nikawasindikiza kwa macho hadi walipo funga mlango ndipo na mimi nikapiga hatua hadi kweye mlango na kuufunga kabisha kwa funguo na kurudi kujilaza kwenye kitanda kikubwa kilichomo ndani ya hii hotel.Nikanyanyuka na kusimama mbele ya kioo kikubwa na kujitazama sura yangu, kusema kweli nimebadilika kwa kiasi kikubwa
Nikavua suti niliyo ivaa na kuingia bafuni, nikaoga huku kichwani kwangu nikiwa nimejawa na mawazo yaliyo ambatana na maswali mengi juu ya wapi alipo mama yangu,
"Hii ni nafasi yangu ya mwisho kupambana na Mzee Godwin, nilazima nimuue kwa mkono wangu mimi mwenyewe"
Nilizungumza huku nikiwa nimekiinamisha kichwa chwangu kwenye ukuta, huku nikiyatazama maji yanayo tiririka na kuingia kwenye kijishimo kidogo
"Ilipo fikia inatosha"
Nilizungumza huku nikishusha pumzi nyingi, nikamaliza kuoga na kurudi chumbani, saa ya ukutani inanionyesha inakwenda majira ya saa kumi na moja kasoro jioni.Nikapanda kitandani, kutokana na uchovu mwingi nikajikuta taratibu nikiwanza kusinzia hadi usingizi ukapitia kabisa
Nikastuka kutoka usingizini, na macho yangu yakakumbana na giza, nikashuka kitandani na kupiga hatua za ungalifu hadi sehemu ilipo swichi, nikawasha taa cha kwanza kukitazama ndani ya chumba ni saa iliyopo ukutani na kukuta ikionyesha ni saa nne na dakika kumi na nane usiku, nikavaa nguo zangu na kutoka nje ya chumba, nikashuka chini sehemu ya watu kujipatia chakula
Nikaa kweny moja ya meza, muhudumu akanifwata na kuniuliza kwa lugha kingereza ninatumia chakula gani, kati ya vyakula vilivyo orodheshwa kwenye Menyu yao.Kila chakula ambacho ninakisoma kwangu ni kigeni, nikaamua kuweka tiki kwenye chakula ambacho niliona jina lake linanipendeza, kinywaji nilicho kielewa kikubwa ni maji tuu ndio niliyo amua kuyawekea tiki
Muhudumu akaondoka na baada ya muda akarudi akiwa na chakula nilicho muagiza, nikajikuta nikishusha pumzi nyingi kwani chakula nilicho kiagiza, ni konokono wakiwa wamechemshwa vizuri huku wakiwa wamepambwa na nyanya zilizo katwa vizuri na kuwekwa pembezoni mwa shahani hiyo
"Mmmm, bora nirudi bongo, kwa staili hii"
Nikawatazama watu wengine kwenye meza zao, kila mmoja yupo bize na mambo yake, jamaa mmoja aliye kaa pembeni yangu nikamuona akiwekewa chakula kama changu na muhudumu aliye muagiza, bila hata ya kusita akaanza kutafuna nyama za konokono hao huku akishushia na soda.Kwa jinsi jamaa anavyo wala nikajikuta nikianza kujihisi kichefuchefu kwa mbali, kila ninapo watazama konokono wangu ndovyo jinsi kichefuchefu kinavyo ongezeka na kujikuta nikisimama na kumsimamisha muhudumu mmoja
"Where is Toilet"(Choo kipo wapi)
Nilizungumza huku kiganja cha mkono wangu wa kulia kikiwa mdomoni mwangu kuzuia kutapika, muudumu akanionyesha kwa kidole mlango wa kuelekea chooni, nikaanza kupiga hatua za kwenda kuufwata mlango huku ninatizama chini kwa bahati mbaya nikamgoga msichana mmoja mmrefu aliye nipa mgongo, na pochi yake ikaanguka
"So…."
Sikuweza hata kuimalizia samahani yangu, tayari kechefuchefu kilikolea, nikazidi kutembea kuelekea chooni, ila kwa msonyo alio uachia huyu dada ikanilazimu kugeuza kichwa kumtazama huku nikiwa ninatembea, macho yangu yakamshuhudia Dorecy akimalizia kunyanyuka huku akiwa ameshika kipochi chake kilicho anguka, kutokana na hali mbaya niliyo nayo sikuwa na budi kuingia chooni.Nikasimama kwenye moja ya sinki la kunawia mikono na kuanza kutapika, dakika tato mfululizo nikajikuta ninatapika hadi chakula nilicho kula ndani ya ndege.
Tumbo likaanza kunisokota, sikujua hata ni kitu gani kilicho nikumba kwa dakika chache hizi, ikanilazimu kujisaidia haja kubwa, kidogo nikapata nafuu ya tumbo kuniuma.Nikajiwek sawa na kunawa mikono yangu, nilipo hakikisha ninaonekana vizuri nikafungua mlango na kumkuta yule jamaa aliyekuwa anakula konokono akiwa amesimama juu ya meza huku mkoni mwake akiwa na bomu la kurusha kwa mkono, watu wote wakanza hulala chini huku wakipiga kelele, jamaa akafungua kikoti chake alicho kivaa na nikamshuhudia akiwa amejifunga mabomu mengine makubwa kama maane na akaanza kuzungumza kwa sauti ya juu kwa lugha ya kiarabu na neno nililo lielewa ni moja tu
"Walha wakhbar"
Kisha akalirusha juu bomu la mkoni, alilokuwa amelishika, huku mabomu mengine aliyo yavaa mwilini mwake yakisoma Zero nyingi zinazo onekana kwa rangi nyekundu
ITAENDELEA
 
*****SORY MADAM*****(58)

AGE....................................................................18+
WRITER.............................................................EDDAZARIA G.MSULWA


ILIOISHIA
, jamaa akafungua kikoti chake alicho kivaa na nikamshuhudia akiwa amejifunga mabomu mengine makubwa kama maane na akaanza kuzungumza kwa sauti ya juu kwa lugha ya kiarabu na neno nililo lielewa ni moja tu
"Walha wakhbar"
Kisha akalirusha juu bomu la mkoni, alilokuwa amelishika, huku mabomu mengine aliyo yavaa mwilini mwake yakisoma Zero nyingi zinazo onekana kwa rangi nyekundu

ENDELEA
Fumba na kufumbua, nikajikuta nikiwa nimerushwa na kurudishwa nyuma ndani ya choo nilipo tokea, huku sauti kubwa ya mlipuko wa bomu ikisikika, sikujua hata nini kufanya kwani akili yangu ikakakosa maamuzi ya hataka ya kuamua, hadi ninaanza kupata chakufanya, tayari nimesha chelewa kwa maana kuta za choo zilisha anza kuporomoka na kusababisha upenyo mdogo sana.Nikazidi kuchanganyikiwa kiasi kwamba sikujua ni nini niweze, gafla nikashuhuda kifusi kikubwa cha mchanga kikilifunikia sehemu zima la chooni na taratibu nikaanza kupoteza pumzi na kulegea, na giza jingi likanitawala machoni mwangu
***
Nikaanza kuhisi kitu kikinistua kwenye kifua change, sikuweza kuelewa mapema ni vitu gani.Kelele za watu za watu mchanganyiko zikazidi kunipa hamasa ya kutamani kuona ni kitu gani kinacho endelea kwenye maisha yangu kwa wakati huu.Haikuwa rahisi sana kama ninavyo hitaji mimi kuwa, kwani kila kitu kinacho endelea kwenye ulimwengu huu niliopo ni chatofuti sana, na sijawahi kukiona hata siku moja mbele ya maisha yangu.Mwanga mkali ukasimama mbele yangu, na kundi kubwa sana la watu walio valia mavazi meupe yanayo ng'aa sana, wakiwa wapo kwenye marika tofauti kuanzi watoto wadogo hadi wakubwa, wote wakiwa wapo kwenye jinsia tofauti nikimaanisha jinsia ya kiume naya kike.
Kila niliye mtazama akaanza kutingisha kichwa, akionyesha kukaataa kitu na sikujua ni kitu gani ambacho anakikata, wakaanza kuninyooshea mikono ya kuniomba nirudi ninapotoka, sikujua ni wapi nilipo taoka kutokana sehemu nzima niliyo simama imetawaliwa na mwanga mweupe mtupu ambao sikuweza kuona ni wapi popote zaidi ya hawa watu walio simama mbele yangu
"Eddy, wakati wako bado.Rudi"
Sauti nzito ya kutetemesha ilisikika masikioni mwangu, na gafla nikisikia mstuko mkali kwenye kifua change ulio nifanya nistuke na kukaa kitako huku ninahema sana, na jasho jingi likiwa linanimwagika mwilini mwangu.Watu waliopo pembeni yangu walio valia mavazi ya kijana huku sura zao wamezifunika kwa vitambaa vinavyo fanana na mavazi yao, wajanirdusha haraka kulala kwenye kitanda.Nikaanza kuminyanana nao huku nikiomba waniachie
"Niachieni nyinyi, mimi mzima sijafaaaa"
Nilizungumza kwa sauti ya juu huku nikijitahidi kunyanyuka, ila wakazidi kunishikilia na kunikandamiza nisirudi kukaa, nikamuona dada mmoja akichukua sindano na kuichoma kwenye kwenye kichupa kidogo na kuvuta dawa nyingi kwa haraka
"Haaaaa, haaa unataka kuniua eheeee, kudadadeki nitakuua kwanza wewe"
Nilizungumza huku macho yangu nikiwa nimemtumbulia dada mwenye sindano, ila wezake wakajitahidi kunishika kwa nguvu zao zote, na nikamshuhudia dada akiichoma sindano kwenye mkono wangu wa kushoto, na kadri jinsi anavyoisukuma dawa ndivyo jinsi na mimi nilivyoanza kupoteza nguvu na usingizi mzito ukaanza kunitawala kila nilivyo jaribu kufumbua macho yangu nikashindwa kabisa
***
Nikastuka na kukuta, mashine ndogo ikiwa pembeni yangu ikionyesha mishale mishale ambayo imepinda panda, kujichunguza vizuri nikajikuta nikiwa nimevalishwa kitu kilicho funika pua yangu na mdomo wangu, sikuwa na nguvu za kufanya kitu chochote zaidi ya kuendelea kujilaza kwenye kitanda nilicho lazwa.Taa mbili nyeupe za chumba hichi hazikunipa uwezo wa kugudua kama huu ni usiku au mchana.Nikajaribu kujiinua ila nikashindwa na kuendelea kulala kitandani
Baada ya muda kidogo ukaingia nesi akiwa amebeba kisinia chenye sindano, pamoja na vichupa viwili vyenye rangi tofauti tofauti
"Unajisikiaje?" Aliniuliza kwa sauti ya chini iliyo jaa upole mwingi
"Vizuri"
"Vizuri, usiwe na wasi wasi upo sehemu salama na utapona sawa kaka"
Alizungumza huku akivaa gloves nyeupe kwenye mikono yake
"Kwani hapa nilipo nipo wapi?"
"Upo hospitali, ila kwa sasa tunajitahidi kukushuhulikie ili uweze kupona haraka"
"Kwani hapa ni Tanzania?"
"Hapana hapa ni Iraq"
"Mbona unazungumza Kiswahili kizuri"
Nilimuuliza huyu nesi mwenye asili ya kiarabu, akatabasamu na kuvuta dawa kidogo kwenye kichupa, kwa kutumia sindano kisha akachukua pamba na kuipaka dawa kidogo na kunipaka kwenye mkono wa kulia sehemu ya kikunjio, akanichoma sindano yanye dawa
"Pole eheee"
Alizungumza kwa sauti yepesi sana iliyo jaa upendo na upole
"Asante"
"Ikifika asubuhi nitakuja kukuchoma sindano ya kutuliza maumivu"
"Sawa"
Akakusanya kila kilicho chake na kutoka ndani ya chumba.Masaa yakazidi kwenye na kuzidi kukatika taratibu huku nikiwa nimesongwa na msongamano wa mawazo nikijaribu kuvuta kumbukumbu za hapa kufika hospitali ila sikukumbuka kitu cha aina yoyote, jina ambalo ninalo kichwani mwangu ni Tanzania, pamoja na lugha yangu ya Kiswahili ambayo kwangu ndio lugha ya Taifa
Wakaingi madaktari wawili wote wakiwa waarabu, wakanisogelea hadi kwenye kitanda nilicho lala na kuanza kuzungumza huku mmoja akianza kunishika mashavuni na kuniminya minya.Wakaendelea kuzungumza huku mmoja akiandika kwenye kijikitabu kidogo alicho kuja nacho.Mmoja akanifunua shuka na kumuonyesha mwenye kijikitabu mkononi sehemu ya mguu wangu, mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio baada ya kuuona mguu wangu wa kulia ukiwa umefungwa kitu kikubwa cheupe.Akaingia nesi wa jana usiku na kusimama pembeni ya madaktari hawa, huku akiwa ameshika kisinia chake cha jana usiku.Nikaanza kumuona nesi akitingisha kichwa akionekana kukataa mazungumzo ya madaktari hao
Wakaanza kubishana, na sikujua ni kitu gani wanacho bishana.Hadi ikafikia daktari mmoja wa aliyekuwa anazungumza na mwenzake anaandika akataka kumzaba kibaa nesi huyo, ila mwenzake akakataa na kumtoa nje, kuepusha ugomvi kutokea ndani ya chumba hichi.Nesi akaanza kuzunguka ndani ya chumba huku akimwagikwa na machozi na kuzidi kunichanganya kwani sikujua ni kitu gani kinacho mwaga machozi kwa kiasi hichi.
"Kuna nini?"
Nilimuuliza na kumfanya asimame na kunitazama, akautazama mlango na kwenda kuufunga kwa ndani, kisha akarudi na kukaa pembeni yangu huku akinifunika na shuka
"Eti nesi, kuna nini?"
Nilimuuliza kwa sauti ya upole iliyo jaa huzuni, akanitazama na machozi yakazidi kumwagika kiasi cha kuzidi kunichanganya mimi
"Watu wa huku, wana roho mbaya sana pale wanapo waona watu wenye ngozi yeupe"
Alizungumza huku akijifuta machozi yanayo mwagika kwa kutumia kiganja chake
"Kwa nini?"
Akanitazama kwa umakini na kwamacho yaliyo jaa huzuni kiasi cha kunifanya nihisi kuna jambo baya ila sikujua ni nini
"Kiufupi hawawapendi watu weusi, ndio maana wanafanya mpango wa kukukata huu mguu wako ulio vunjika"
Nilijihisi moyoni mwangu kama nimepigwa shoti ya umeme, kila nilivyo mtazama nesi sikujua nizungumze nini.Machozi yakaanza kunimwagika kama maji,
"Usilie, nitahakikisha unapona na hakuna mtu anaye weza kukufaniyia ukatili kama huo"
"Kwani umekatika?" Nilimuuliza kwa sauti ya upole sana huku nikiendelea kulia
"Hapana haujakatika, umefunjika mara mbili, ila nashangaa ni kwanini hapa wanapanga kuukata"
"Ila usilie, nipo radhi nipoteze kila kitu kwangu, ila si kukubali kuuona ubaguzi wa rangi kama huu.Kwa maana wakiukata kinacho fwatia hapa ni wewe kupelekwa katika kambi ya walemavu iliyopo Bangdad na kila siku hiyo kambi, walemavu wanakufa kwa njaa kali na mateso makali, na mbaya zaidi wengi wanao pelekwa kule ni wale ambao si raia wa nchi hii"
Maneno ya nesi yakazidi kuniogopesha na kuendelea kunipa wasiwasi mkubwa ulio zidi kunimwaga machozi yangu.
"Jikaze usilie, ngoja nikuchome sindano ya kutuliza maumivu na kukausha kidonda.Wakikuletea chakula tafadhali usile hadi nikuletee mimi"
"Sawa"
"Wanaweza kukupa sumu, ufe bure mtoto wa watu bila ya sababu maalumu"
Nesi alizungumza na kuendelea kunichoma sindano alizo niambia,
"Sasa hivi ninatoka, kazidi ninakwenda nyumbani kukuandalia chakula, hadi saa sita nitakuwa nimesha rudi kukuletea chakula na nikija nitakuja tuzungumze mengi.Ila vumilia njaa yako, usile chakula wala kunywa maji yoyote utakayo letewa na mtu wa aina yoyote sawa"
"Sawa, nashukuru kwa msaada wako nesi"
"Hata wewe nashukuru kwa uelewa wako, niite neshi Phidaya"
"Naitwa Eddy"
"Mungu mkubwa utapona na vua hiyo mashine"
Nikakivua kifaa nilicho kuwa nimevalishwa kwenye uso kisaha, nesi Phidaya akaondoka na kila kitu chake, baada ya muda kidogo akaingia nesi akiwa amebeba sahani nyenye chakula pamoja na maji kwenye glasi, akaviweka pembeni ya meza yangu na kunitazama usoni.Akawa anatamani kuzungumza na mimi ila anashindwa na nikahisi lugha zetu zipo tofauti sana.Akanza kunionyesha kivitendo kwamba chakula kipo mezani ninaweza kula, na mimi nikamjibu kivitendo kwamba nitakula, akatoka na kuniachia chakula mezani. Harufu ya chakula ikazidi kunitamanisha kuweza kukila kwani inavutia sana, ila kila nilipo jaribu kukumbuka maneno ya nesi Phidaya nilijikuta nikuwa ninakidharau
Baada ya muda mrefu kidogo nesi Phidaya akarudi akiwa emeshika mfuko mweupe wenye vyombo,
"Nani kakuletea chakula?"
"Nesi mmoja mfupi, mwarabu"
Nesi Phidaya akaachia msunyo mkali baada ya kumuambia nesi aliye niletea chakula hicho
"Ndio wale wale"
Akakisogeza chakula nilicho letewa akaniwekea chakula chake mezezani, akaanza kuninywesha taratibu uji alio uweka kwenye kikombe
"Watu wa huku hawana ubinadamu, ndio maana kila siku wanakazi ya kujitoa muhanga na mabomu yao"
"Hivi ni kwa nini?"
"Uchizi tu ndio unao wasumbua, kuna wanao amini kwamba ukijitoa muhanga, mbele za watu mbinguni utaingia moja kwa moja wakati ni uongo mtupu"
"Hivi unakumbuka kitu chochote cha nyuma?"
"Hapana"
"Ona sasa, wamekuchoma sindano ya kukupotezea kumbu kumbu, ndio maana nakuambia watu wa huku hawana maana"
"Wamenichoma sindano?"
"Ndio, na kuna kitu kinacho endelea, na ile siku ya oparesheni kama nisinge kuwepo ninaimani wangekumalizia, nikutokana katika watu walio okolewa wakiwa hai kwenye lile jingo wewe ni mmoja wao na idadi kubwa ya waarabu walikufa pale"
"Kwenye jengo, jengo gani?"
"Usiwe na haraka, hapa itabidi nifanye mpango wa kukutorosha la sivyo watakupoteza"
Maneno ya nesi Phidaya yakazidi kunipotezea imani moyoni mwangu na kunijaza moyo wa woga kwani imani ya kuwaamini madaktari wengine ikaanza kunipotea moyoni mwangu.Nesi Phidaya akamaliza kunilisha chakula alicho niletea na kunihaidi atarudi usiku kisha akaondoka zake
***
Masaa yakazidi kusonga, huku moyoni mwangu nikiomba sana nesi Phidaya atokee aje kunisaidia kwa maana kila daktari kwangu sikuweza kumuamini, kila nilipojaribu kuvuta subira sikuweza kumuona nesi Phidaya akiingia kwenye chumba change, mlango ukafunguliwa na kujikuta nikianza kutabasamu, macho yangu yakiwa na shauku ya kuweza kumuona nesi Phidaya.Nikashangaa kuwaona wale madaktari wa asubuhi wakiingia na kusimama pembeni yangu
Mmoja akafungua kitabu chake kilicho andikwa na maandishi ambayo akanionyesha na sikumuelewa ni maandishi ya lugha gani, akaniandikia tarehe kwenye kijikitabu chake na kuniambia kwamba hii ni tarehe ya leo, kish akaniandikia tarehe nyingine ambayo ni siku inayo fwata.Kisha akachora kijimguu na kukiwekea alama ya ‘X' akiashiria kwamba kesho ndio siku ya mimi kukatwa mguu wangu.Alipo maliza kunionyesha kwa ishara wakatoka huku wakiwa wanacheka sana.
Hadi kunapambazuka sikuweza kumuona nesi Phidaya, hali ya hatari ikaanza kunijia kichwani mwangu na kuhisi nesi Phidaya anaweza kuwa amekutwa na matatizo, mlango ukafunguliwa na wakaingia manesi wawili pamoja na madaktari wale wawili.Wakaanza kufungua kitandana na kukishusha chini kidogo hadi kikafikia usawa mzuri wa kuweza kusukumwa.Pasipo hata ya kunisemesha wakaanza kunisukuma na kunipeleka nisipo pajua huku nyuso zao zikiwa na tabasamu ambalo sikuliewewa nini maana yeke
ITAENDELEA
 
*****SORY MADAM*****(59)

AGE....................................................................18+
WRITER.............................................................EDDAZARIA G.MSULWA


ILIOISHIA
HADI KUNAPAMBAZUKA SIKUWEZA KUMUONA NESI PHIDAYA, HALI YA HATARI IKAANZA KUNIJIA KICHWANI MWANGU NA KUHISI NESI PHIDAYA ANAWEZA KUWA AMEKUTWA NA MATATIZO, MLANGO UKAFUNGULIWA NA WAKAINGIA MANESI WAWILI PAMOJA NA MADAKTARI WALE WAWILI.WAKAANZA KUFUNGUA KITANDANA NA KUKISHUSHA CHINI KIDOGO HADI KIKAFIKIA USAWA MZURI WA KUWEZA KUSUKUMWA.PASIPO HATA YA KUNISEMESHA WAKAANZA KUNISUKUMA NA KUNIPELEKA NISIPO PAJUA HUKU NYUSO ZAO ZIKIWA NA TABASAMU AMBALO SIKULIEWEWA NINI MAANA YEKE

ENDELEA
WAKAZIDI KUKISUKUMA KITANDA NILICHO LALIA HADI HADI TUKAFIKA KWENYE MAJA YA MLANGO AMBAO JUU KUNA MAANDISHI YA KIHARABU AMBAYO SIKUWEZA KUYAELEWA, NESI MMOJA AKAUSUKUMA MLANGO NA KUFUNGUKA, NA WAKANIINGIZA NDANI NIKIWA JUU YA KITANDA CHANGU, MWANGA MWEKUNDU WA TAA ULIOO NDANI YA CHUMBA UKAZIDI KUNIOGOESHA.CHUMBA KIZIME KIMEZUNGUKWA NA MASHINE MBALIMBALI AMBAZO SIKUJUA ZINAKAZI GANI.DAKTARI MMOJA AKACHUKUA MASHINE YENYE KIMVIRINGO MBELE, KISHA AKAKIWASHA NA KUANZA KUZUNGUKA, AKACHUKUA MOJA YA MIWANI KUBWA AMBAYO NI NYEUPE AKAIVAA NA KUANZA KUCHEKA KITU KILICHOO ZIDI KUNIOGOPESHA ZAIDI.
GAFLA TAA YA MWANGA MWEUE IKAWASHWA NA KUWAFANYA MADAKTARI NA MANESI, KUSTUKA, MACHO YETU WOTE TUKAYAELEKEZEA MLANGONI NA KUMUONA NESI PHIDAYA AKIWA AMESHIKA, BASTOLA HUKU JASHO JINGI LIKIWA LINAMWAGIKA USONI, AKAANZA KUZUNGUMZA KWA KIARABU NA TARATIBU MADAKTARI WAKANYOOSHA MIKONO JUU WAKITETEMEKA, AKAZUNGUMZA NENO LILILO WAFANYA MADAKTARI KUANZA KURUDI NYUMA KUTOKA KILIO KITANDA CHANGU.
"EDDY, WAMEKUFANYA CHOCHOTE KIBAYA?"
"HAPANA"
"POWA"
NESI PHIDAYA AKAZUNGUMZA NENO JENGINE LILILOWAFANYA MADAKTARI NA MANESI KULALA CHINI, SAKAFUNI HUKU MIKONO YAO WAKIWA WAMEIWEKA JUU YA VICHWA VYAO.NESI PHIDAYA AKANIFWATA HADI KITANDANI NA KUUITISHA MKONO WAKE MMOJA KWENYE, MGONGO WANGU NA KUNIOMBA NIWE KUSHUKA CHINI, JAPO NINAJIHISI MAUMIVU ILA NIKAJIKAZA KIUME KWANI KUENDELEA KUKAA HAOA KUTAHATARISHA MAISHA YANGU.
"JIKAZE BABA YANGU"
NESI PHIDAYA ALIZUNGUMZA HUKU AKIENDELEA KUNISHUSHA KWENYE KITANDA, AKANISAIDIA KUSIMAMA VIZURI, HUKU MUHIMILI WANGU WOTE WA KUSIMAMA NIKIUTEGEMEA KUTOKA KWAKE, NESI PHIDAYA AKAWATAZAMA WATU MADAKTARI WALIO LALA CHINI, AKAZUNGUMZA NENO LA UKALI LILILO WAFANYA MADAKTARI NA MANESI KUZIDI KUZIFUNIKA SURA ZAO CHINI PASIPO KUZINYANYUA JUU.TUKAFANIKIWA KOTOKA NJE YA CHUMBA WALICHO NIINGIZA, NESI PHIDAYA AKAFUNGA MLANGO KWA NJE NA SOTE TUKAANZA KUONDOKA TARATIBU HUKU NESI PHIDAYA AKIIFICHA BASTOLA YAKE NA BAADHI YA WAHUDUMU WAKABAKI WAKIWA WANATUSHANGAA.TUKATOKA NJE NA KUKUTA GARI AINA YA TAKSI IKIWA INATUSUBIRIA
"AHAAAA"
NILITOA MGUNO WA MAUMIVU BAADA YA MGUU WANGU NILIO VUNJIKA KUGONGWA KWENYE MLANGO NILIPOKUWA NINAJIAANDAA KUINGIA NDANI YA GARI, SITI YA NYUMA
"POLE EDDY"
"ASANTE"
NESI PHIDAYA AKANISAIDIA KUINGIA NDANI YA GARI NA KUFUNGA, KISHA YEYE AKAINGIA KWENYE SITI YA MBELE KWA DEREVA NA KUMUONGELESHA DEREVA KIARABU NA AKALIONDOA GARI LAKE KWA KASI.
"ASANTE SANA, NESI PHIDAYA"
"USIJALI NIPO KWA AJILI YAKO, ILA NINGEPENDA UNIITE PHIDAYA TU NA SI NESI PHIDAYA"
"SAWA"
NIKAENDELEA KUJILAZA KWENYE SITI YA NYUMA YA TAKSI TUIYO IPANDA, ILA KUNA MWANGA MKALI WA TAA UKAWA UNAINGIA KWENYE GARI LETU, IKANILAZIMA KUNYANYUA KICHWA CHANGU KUTAZAMA NYUMA, NIKAONA GARI NDOGO IKIJA KWA KASI SANA,
"PHIDAYA KUNA WATU WANATUFWATA NYU……"
KABLA SIJAMALIZIA SENTESI YANGU NIKASTUKA RISASI IKIPIGA KWENYE KIOO CHA NYUMA NA KUNIFANYA NIRUDI CHINI, NA KULALA KWENYE SITI YANGU.DEREVA AKAANZA KULALAMIKA, NA PHIDAYA AKAANZA KUMUHIMIZA DEREVA KUONGEZA MWENDO KASI WA GARI,RISASI ZIPATAZO NNE ZIKAINGIA KWENYE KIOO CHA NYUMA CHA GARI NA KUSHANGAA RAGI IKIAANZA KUYUMBA HUKU DEREVA AKIWA AMEULALIA MSKANI WAKE,
"SHIT DEREVA AMEPIGWA RISASI YA KICHWA"
PHIDAYA ALIZUNGUMZA KWA KUCHANGANYIKIWA KIASI KWAMBA NA MIMI NIKAANZA KUCHANGANYIKIWA, RISASI ZIKAENDELEA KUMIMINIKA NDANI YA GARI NA KUZIDI KUNICHANGANYA
"MTOE HUYO DEREVA"
NILIZUNGUMZA KWA SAUTI YA JUU, PHDIAYA AKAFANYA KAMA NILIVYO MUAGIZA, AKAUFUNGUA MLANGO WA DEREVA NA KUMSUKUMIA KWA NJE, KISHA AKAFUNGA MLANGO NA KUKAA KWENYE SITI YA DEREVA
"NIPE BASTOLA YAKO"
PHIDAYA AKANIRUSHIA KWA NYUMA BASTOLA YAKE, NIKAUCHUKUA MKANDA WA SITI WA SITI YA NYUMA NA KUANZA KUUVUTA NIKIJARIBU KUUKATA ILA NIKASHINDWA.NIKAMTAZAMA
"EDDY UNATAKA KUFANYAJE?"
"NATAKA KUKATA HUU MKANDA NIUFUNGE MGUU WANGU UNAVUTA SANA"
PHIDAYA AKAFUNGUA KWENYE KISANDUKU KILICHOPO PEMBENI YA SITI YA DEREVA, NA KUANZA KUTOA VITUVITU, VILIVYOMO NDANI YA KISANDUKU, AKABAHATIKA KUPATA MKASI NA KUNIKABITHI.NIKAUCHUKUA MKASI NA KUUKATA MKANDA WA SITI NA KUUFUNGA MGUU WANGU ULIO VUNJIKA, MAENEO YA MAPAJANI, HADI NILIPO HAKIKISHA KWAMBA NIMEUNGUZA MISULI KUVUTA, NIKAJILAZA VIZURI KWENYE SITI NA KUTOA MAGAZINE YA BASTOLA NA KUKUTA IKIWA NA RISASI ZA KUTOSHA.NIKAITAZAMA GARI INAYO TUFWATILIA, NIKASHUHUDIA JINSI INAVYO KUJA KWA KASI, AKACHOMOKA JAA MAA MMOJA KWENYE KIOO CHA GARI LAO HUKU AKIWA NA BUNDUKI AKIJIANDAA KUFYATU RISASI NYINGINE KWENYE GARI LATEU.NIKAANZA KUHESABU MOJA HADI TATU KIMOYO MOYO HUKU BASTOLA NIKIWA NIMEISHIKA KWA UMAKINI MKONONI MWANGU, NIKABANA UMZI KWA NGUVU, KISHA NIKAFYATUA RISASI TATU MFULULIZO KUELEKEA ALIPO JAAMA, KWA BAHATI NZURI RISASI ZOTE LILIATA KIFUANI NA KUSABABISHA KUNING'INIA TU
NIKAFYARUA RISASI NYINGINE MBILI KWENYE KIOO CHA DEREVA NA KULISABABISHA GARI LAO KUYUMBA, JAMBO LILILO PELEKEA GARI KUANZA KUSHUKA CHINI KWENYE KORONGO LILILO EMBEZONI MWA BARABRA, NA KUANZA KUBINGIRIA KWENDA CHINI.PHDAYA AKAZIDI KUONGEZA MWENDO WA GARI TUKIKATIZA KWENYE MILIMA, SIKUJUA NI WAPI TUNAPO ELEKEA ILA IKANILAZIMU KUWA MTULIVU
"UPO FRESHI EDDY?"
"NDIO NIPO POWA, TUNAELEKEA WAPI?"
"HUKU TUNAPO ELEKEA NI KWENYE SHAMBA LANGU, LA PAMBA"
"AHAA SAWA"
NDANI YA DAKIKA AROBAINI NA TANO TUKAWA TUMEFANIKIWA KUFIKA KWENYE SHAMBA LAKE, LENYE MITI MINGI YA PAMBA, TUKAINGIA NDANI YA SHAMBA HADI TUKAKUTA NYUMBA MOJA NZURI IKIWA KATIKATI YA SHAMBA NA IMEZUNGUKWA NA PAMBA NYINGI
"KARIBU"
PHIDAYA ALIZUNGUMZA HUKU AKISIMAMISHA GARI LAKE, AKAFUNGUA MLANGO NA KUSHUKA, AKAFUNGUA MLANGO WA SITI YA NYUMA AMBAPO NIPO, KISHA AKANISAIDIA KUSHUKA NDANI YA GARI, AKAENDELEA KUNISAIDIA KUTEMBEA HADI NDANI YA NYUMBA YAKE, NDOGO ILA IMETENGENEZWA KWA USTADI WA HALI YA JUU, AKAWASHA TAA NA TARATIBU AKANIKALISHA KWENYE MOJA YA SOFA KUBWA LILILOPO NDANI YA NYUMBA YAKE
"POLE SANA EDDY"
"NASHUKURU, HAPA UNAISHI NA NANI?"
"HUWA NINAISHI PEKE YANGU, MUDA WA MAPUMZIKO, KAMA LIKIZO na huwa ninanunua vyakula vinavyoweza kudumu hata kwa miezi sita pasipo kuharibika na kama unavyo ona, umbali kutoka huku hadi mjini"
"Ahaaa sawa"
Phidaya akaingia kwenye moja ya chumba kisha akarudi akiwa amebadilisha nguzo alizo kuwa amezivaa na kukaa kwenye moja ya sofa ambalo lipo karibu na sofa nililo jilaza
"Eddy kuna kitu nahitaji kukuuliza"
"Uliza kama huto jali"
"Wewe haswa ni nani?"
"Kivipi?"
"Nahitaji kujua ukweli kuhusu wewe, juu ya maisha yako na kazi zako"
Phidaya alizungumza huku akinitazama machoni, kwa umakini.Nikaanza kumuelezea Phidaya juu ya maisha yangu ya nyuma, kuhusiana na machafuko yanayo endelea kwenye familia yangu, japo kuna baadhi ya vitu sikuviweka wazi kwake, kama swala la kumuua Derick kikatili sana.
"Pole sana Eddy"
"Asante"
Sikuona haja ya kuendelea kukaa na sura bandia, ikanilazimu kuvua sura bandia nilivyo pandikizwa juu ya sura yangu japo inasababisha maumivu mengi, ila nilijikaza, na ikawa ndio mara ya kwanza kwa Phidaya kuiona sura yangu halisi
***
Hali ya mguu wangu kuendelea kuimarika huku vidonge vya kurudisha kumbukumbu anavyo nipa Phidaya vikaanza kufanya kazi, na taratibu kumbukumbu zangu zikaanza kurudi moja hadi nyingi, hali iliyoa anza kuleta matumaini kati yangu na Phidaya ambaye anaendelea kunipatia matibabu kila kukicha, kwa dawa na mazoezi ambayo Phidaya, ananipatia nikajikuta mguu ukianza kupona, hadi nikaanza kuacha kutembele gongo lililo kuwa likinisaidia kutembelea.Baada ya miezi minne nikawa nimepona kabisa hata maumivu ambayo nilikuwa nikiyapata yakawa yamekwisha kabisa
Katika kipindi ambacho tumeishi kwenye hili shamba la pamba, haikutokea hata siku moja mimi na Phidaya tukazungumzia swala zima la mahusiano ya kimapenzi, kwani heshima niliyo jijengea kwa Phidaya ni kama, dada na kaka
"Eddy hivi, una mchumba?"
"Hapana"
"Unamipango gani kwa sasa"
"Nahitaji kurudi, Tanzania kujua kama mama yangu yupo hai au lah"
"Nitakusaidia katika hilo pia"
Phidaya alizungumza huku akinitazama kwa macho malegevu, yaliyo jaa hisia kali za kimapenzi, akanisogelea sehemu nilipo simama na kunikumbatia kwa nguvu.Ikachukua kama dakika tano, Phidaya akiwa amenikumbatia mwilini mwangu.Phidaya akaanza uchokozi wa kama mwanamke akiwa anahitaji kitu muhimu kutoka kwa mwanaume.Kutokana na uzoefu wangu wa kuwajua wanawake, haikunia shida sana ikanilazimu na mimi kuanza kuonyesha makeke yangu ya mikono yangu kupita sehemu mbali mbali za mwili wa Phidaya, na taratibu tukajikuta tukizama kwenye dimbwi kuwa la mapenzi, na kadri ya jinsi tulivyozidi kupeana raha, ndivyo jinsi, hisia kali za upendo zilivyo zidi kukua kati yetu
Siku ya pili tukakubaliana kwenda mjini kufanya baadhi ya manunuzi ya vitu vya kuweka ndani, ikiwemo chakula kwani kinakaribia kuisha.Alfajiri na mapema tukaingia kwenye taksi ambayo tulikuja nayo kipindi tunatoroka kutoka mjini.Phidaya akawa ni dereva wa kuendesha hadi tukafika mjini, tukapitia benki ambapo Phidaya alichukua kiasi kikubwa cha kutosha kwa manunuzi tulio yapanga kisha, tukaingia kwenye maduka ya nguo, na akaninunulia nguo mpya
"Kuna duka flani la kike ninahitaji nikanunue nguo"
Phidaya alizungumza huku akiendelea kunichagulia nguo ambazo alihisi kwamba zitaupendezesha mwili wangu
"Lipo wapi?"
"Upande wa pili wa barabara, ili kufidia muda wewe chagua nguo utakazo ona zinatosha, nikuachie pesa, na utanikuta kwenye hilo duku"
"Nitalijuaje?"
"Ukivuka tu barabara upande wa kulia kwako, utakuta duka lina masanamu mengi yamevalishwa nguo za kike"
"Ahaaa powa"
Phidaya akaniachia kiasi cha kutosha na kuvuka upande wa pili wa barabara, mimi nikachagua nguo zangu kisha nikaelekea kwenye duka alipo Phidaya, nikamkuta akiwa anachagua nguo,
"Eddy hii inanifaa?"
"Ndio inakufaa"
Tukiwa tunaendelea kuchagua nguo akaingia mwanayume mmoja akiwa amebeba mkoba wa kike, akasimama akitizama tizama baadhi ya nguo, akatoa simu yake ambayo inaita nakuzugumza na simu, kisha akaikata na akasimama akitazama nje.Baada ya muda akaingia mdada aliye jitanda baibui lililo funika hadi macho yake huku tumbo lake kidogo likiwa ni kubwa akionekana ni mjamzito, dada huyo akavua baibui lake ndipo macho yangu yakamshuhudia Dorecy akiwa amesimama kiuvivu, huku mimba aliyo nayo ikionekana kumpelekesha sana, na kwabahati mbaya hakuniona mimi nilipo
ITAENDELEA
 
*****SORY MADAM*****(60)

AGE....................................................................18+
WRITER.............................................................EDDAZARIA G.MSULWA


ILIOISHIA
TUKIWA TUNAENDELEA KUCHAGUA NGUO AKAINGIA MWANAYUME MMOJA AKIWA AMEBEBA MKOBA WA KIKE, AKASIMAMA AKITIZAMA TIZAMA BAADHI YA NGUO, AKATOA SIMU YAKE AMBAYO INAITA NAKUZUGUMZA NA SIMU, KISHA AKAIKATA NA AKASIMAMA AKITAZAMA NJE.BAADA YA MUDA AKAINGIA MDADA ALIYE JITANDA BAIBUI LILILO FUNIKA HADI MACHO YAKE HUKU TUMBO LAKE KIDOGO LIKIWA NI KUBWA AKIONEKANA NI MJAMZITO, DADA HUYO AKAVUA BAIBUI LAKE NDIPO MACHO YANGU YAKAMSHUHUDIA DORECY AKIWA AMESIMAMA KIUVIVU, HUKU MIMBA ALIYO NAYO IKIONEKANA KUMPELEKESHA SANA, NA KWABAHATI MBAYA HAKUNIONA MIMI NILIPO

ENDELEA
Nikamtazama kwa makini jinsi anavyo zungumza na mume wake, hadi Phidaya akanigusa bega
"Mbona unamtazama sana yule dada wa watu?"
"Ninamfahamu"
"Unamfahamu?"
"Ndio"
"Ni nani?"
"Anaitwa Dorecy"
Tulizungumza kwa sauti ya chini huku, tukimtazama Dorecy akichagua chagua nguo na mume wake
"Huyu ndio yule msichana, aliye nipiga na kuondoka na kiasi kikubwa cha madini yangu"
"Ahaaa"
"Ngoja kwanza, nisubiri hapa"
Nilizungumza huku nikizunguka upande wa pili alipo Dorecy na mumuwe, nikajibanza kwenye moja ya kabati lenye nguo, simu ya mume wa Dorecy ikaita na kumlazimu kutoka nje kuzungumza na simu hiyo.Nikapiga hatu za umakini, hadi sehemu alipo simama Dorecy na kumgusa kwa nyuma.Akageuka, na kujikuta akinitazama kwa macho yaliyo jaa mshangao mkubwa kwani hakutarajia kuniona nikiwa katika eneo hili.Nikamvuta hadi kwenye sehemu ambayo si rahisi kwa watu kutuona, hii ni kutokana na wingi wa nguo zilizo pangwa
"Eddy..nisamehe"
"Sikia sina haja ya kuombwa msamaha, ninacho kihitaji ni madini yangu, la sivyo nitalitumbua tumbua hili jitumbo lako kama sikujui"
Nilizungumza kwa sauti nzito iliyo jaa hasira pamoja na msisitizo mkali, mwili mzima wa Dorecy ukawa na kazi ya kutetemeka mithili ya mtu aliyepo kwenye baridi kali sana
"Yaaa, yaapo kulee"
Nikatazama juu kuchunguza kama kuna kamera yoyote ya ulinzi, ila sikuona, nikamtndika Dorecy kofi moja la kumuweka sawa
"Nimekuambia nahitaji madini yangu sawa?"
"Ndio, yapo kwa kule kule kwangu"
"Nitayapataje?"
"Eeheee?"
Nikaona Dorecy anababaika sana na kunipotezea muda, nikamtandika kibao cha pili ambacho nikizoto kuliko hata cha mara ya kwanza, hadi kuna dada mmoja akachungulia, nikajifanya nikimkumbatia Dorecy kama mpenzi wangu, dada aliye chungulia akaachia tabasamu na mimi, nikatabasamu kinafki ili airudishe sura yake alipo itoa.Alipo irudisha nikamuachia Dorecy na kumkuta sura yake imejaa machozi mengi
"Usijidai unalia kinafki, sasa leo nitakuzalilisha mbele ya mume wako"
"Hapana Eddy usifanye hivyo, mume wangu ni mtu mwenye pesa sana, atakudhuru wewe"
"Haaa na anidhuru kwahiyo pesa zake ndio unadhani kwamba ninaziogopa, si ndio"
Nilizungumza kwa hasira huku nikiwa nimeshika kiganja cha mkono wa kuliwa wa Dorecy na kukiminya kwa nguvu zangu zote.Dorecy akaanza kutoa kilio cha maumivu, simu yake aliyo ishika mkono wakushoto ikaita na kuona jina mume wake
"Pokea sasa"
Nilimuamrisha huku nikimuachia mkono, kabla ya kupokea nikamuona mume wake akija nyuma ya Dorecy
"Mumeo huyo hapo, ole wako uropoke"
Dorecy akajifuta machozi haraka, hadi mume wake anafika sehemu tuliyopo, sura yake imejaa uchangamfu wa gafla, wakazungumza kiarabu ambacho sikukielewa, nikashangaa mume wake akinipa mkono huku akiwa na tabasamu
"Eddy huyu ni mume wangu, anaitwa Khalid, nimemuambi kwamba tumesoma wote"
Nikatingisha kichwa, nikilipokea tabasamu la mume wake, tukaachiana mikono, kitu ambacho mume wake alikifanya na kuzidi kuniboa ni kumkumbatia Dorecy kwa nyuma na kuanza kumchezea chezea tumbo lake huku akizungumza maneno nisiyo yaelewa, Dorecy akanitazama machoni, na kugundua nilivyo kasirika
"Anasema, kwamba mtoto nitakaye mzaa atamleta Tanzania"
Dorecy alitafsiri maneno aliyo yazungumza mume wake
"Muambie hatutaki watoto kama wake, na utazaa Zombi kama sijakusoa"
Mume wa Dorecy akatabasamu baada ya Dorecy kumtafsiria nilicho kizungumza, na nina uhakika kwamba Dorecy alicho kizungumza sicho nilicho muambia
"Nataka, madini yangu, la sivyo nitakufanyia oparesheni bila ganzi ya hilo jitumbo lako"
Nilizungumza na kuachia tabasamu pana, kumfanya mume wa Dorecy kuto kuelewa kitu ninacho kimaanisha, nikawapa mikono na kuondoka zangu kurudi sehemuu nilipo muacha Phidaya
"Eddy umemaliza?"
"Ndio, ila kuna kazi nahitaji kuifanya peke yangu"
"Kazi gani?"
"Tutazungumza"
Phidaya akawa amesha maliza kununia alichokuwa anahitaji kukinunua, tukatoka nje na kuingia ndani ya gari
"Usiondoke kwanza, nataka tuwafwatilie Dorecy na mumewe sehenu wanapo ishi"
"Eddy mbona unanipa shuhuli nyingine"
"Zipi?"
"Hizo za kufwatilia hao watu, ujue kwamba tumekuja kutafuta nini huku"
"Powa nipatie pesa nikodo taksi"
"Utapakumbuka ninapo ishi"
"Wewe nipatie pesa"
Phidaya akanipatia kiasi cha kutosha cha pesa, nikashuka kwenye gari na yeye akaondoka, sikucheza mbali na mlango wa duka walipo Dorecy na mume wake, baada ya dakika kumi na tano nikawaona wakitoka kwenye duka, huku mumewe akiwa amebeba mzigo mkubwa wa nguo.Gari ya kifahari yenye milango sita ikasimama pembeni yao, akashuka jamaa aliye valia suti yenus na miwani nyeusi, akawafungulia mlango na wote wakaingia ndani ya gari na wakaondoka
Nikapiga mluzi kwa dereva taksi mmoja aliye kuwa ameisimisha gari yake upande wa pili wa barabara, akaja nilipo simama haraka, na nikaingia ndani ya gari
"Nilugha gani unayo tumia kuzungumza?"
Nilimuulizwa kwa kingereza, dereva taksi ambaye ni mzee wa makomo kidogo na kichwani mwake amejifunga kilemba
"Zote duniani, kiarabu, kingengereza, kiswahili, kichina na kadhalika"
Alinijibu kwa kingereza, nikamuomba alifwate gari la kifahari lilolo ondoka muda mchache sehemu hii, akatii, akafungulia mziki wa kihindi na kuanza kuimba huku akitingisha tingisha kichwa chake
"Mzee hembu kuwa makini na kazi yako. Utaipoteza hiyo gari"
Kijana mimi ile gari naijua hadi sehemu inapo elekea, ni gari la tajiri Khalid Bin Suley, baba yake alikuwa ni gavana wa hili jimbo"
"Kwa hiyo unamjua?"
"Vizuri sana, tangu akiwa mdogo, na nimwezi ulio pita amefunga ndoa na binti mmoja kutoka Afrika"
"Tuachane na hizo habari za ndoa, yeye anafanya kazi gani?"
"Ahaaa yule kijana, ni mshenzi kweli.Tangu baba yaka afariki basi yeye amekuwa ni muuzaji mkubwa sana wa madawa ya kulevya, kutokana ananguvu kubwa, wala hakuna mbweha polisi hata mmoja anaye msogelea"
"Ahaaa"
"Ahaaa, jamaa anamkono mrefu sana, akimtaka mtu kumchomoa duniani basi ni kitendo cha muda mfupi sana"
Maneno ya dereva taksi yakaanza kuniogopesha na kubaki nikiwa ninamtazama kwa umakini, ila nikajipa moyo kwamba shida yangu si yeye bali nimadini yangu tu.Tukaendelea kuifwatilia gari yake kwa ukakini, gafla dereva akaisimamisha gari yake
"Mbona umesimamisha?"
"Kijana hapa ndio mwisho wa mimi kufika, nikivuka tu hicho kibao hapo ujue haturudi"
"Haturudi kivipi?"
"Namaanisha tutakwenda kuuawa huho, ila jumba lake lile pale mbele"
Tukaishuhudia gari ya Khalid ikiingia kwenye gat kubwa ya jumba lake kifahari, hadi inazama ndani, nikajikuta nikishusha pumzi.Sehemu nzima tuliopo imependezeshwa na miti mirefu, pamoja na majani marefu kiasi yaliyo kolea kijani kikali, kiasi kwamba, ukipatazama lazima macho yafarahie mandhari ya eneo zima
"Ndio hivyo tena, gari imesha zama ndani kijana sasa sijui tunarudi pamoja, au unataka kwenda kudumbukizwa kwenye bwawa la mamba?"
"Turudi?"
Dereva taksi akasigeuza gari lake taratibu, kabla hajaliweka sawa barabarani, gari mbili nyeusi zikasimama barabarani na kuifunga barabara
"Ohoo nilikuambia kijana"
Dereva taksi alizungumza huku akianza kutetemeka mwili mzima.Wakashuka watu sita walio valia suti nyeusi huku mikononi mwao wakiwa na bunduki aina ya short gun.Mzee wa watu akaanza kuomba sala yake ya mwisho huku kajasho kembaba kakimwagika.Jamaa mmoja akaanza kupiga hatua za kuja lilipo gari letu, na kutuomba tushuke ndani ya gari, huku mikono yetu ikiwa juu.Nikajikuta nikiwa ninajiamini kupita maelezo, nikafungua mlango na kutoka nje huku mikono yangu ikiwa nimeinyoosha juu, akafwatia dereva taksi naye akafanya kama nilivyo fanya mimi
"Nyinyi ni kina nani?"
Jamaa alituuliza kwa lugha ya kingereza
"Sisi ttumepotea njia tu"
Nilimjibu jamaa kwa kujiamini, kiasi kwamba nikawa nimejiandaa kwa chochote ambacho kitakwenda kutokea.Jamaa akanisogelea na kuanza kunipapasa kuanzia chini hadi juu, akatoa kiasi cha pesa nilicho kuwa nacho mfukoni na kukitupa pembeni
"Inama kwenye gari"
Aliniamuru na nikafanya hivyo bila ya wasiwasi wa aina yoyote, nikamtazama mzee wa watu jinsi anavyo tetemeka hadi haja ndogo ikaanza kulowanisha surali yake aina ya panjabi aliyo ivaa.Jamaa akaanza kumpapasa mzee wa watu, hawakumuona na kitu chochote
"Ingieni kwenye gari lenu na muondoke haraka sana"
Asante sana baba yangu"
Mzee alijibu kwa haraka na kuingia kwenye gari, nikataka kuokota pesa zangu ila jamaa akanizuia na kuniamuru niingie kwenye gari huku akiwa ameninyooshea bunduki yake, wakazitoa gari zao barabarani na sisi tukaondoka, kwa mwendo wa kasi, njia nzima tukawa kimya, macho yangu nikayashusha sehemu ya mbele ya mzee wa watu na kujikuta nikianza kuchake kimoyomoyo
"Kufa kubaya?"
Nilijisemea huku nikicheka, hata mziki ambao mzee alikuwa anausikiliza akaona unampigia kelele, akaizima redio yake.Nikashangaa kuona mzee akisimamisha gari yake kwenye duka ambalo nilikuwepo
"Shuka kijana kwenye gari yangu, sitaki tena oda yako ya safari"
Mzee alizungumza huku akibabaika, nikashuka kwenye gari, hata pesa hakunidai, akaondoka kwa kasi na kutokomea mbele ya macho yangu.Nikabaki nikiwa nimesimama sikujua ni wapi nielekee, nikastukia nikiguswa bega kwa nyuma kugeuka nikakutana na Phidaya
"Wewe si umeondoka, mbona upo hapa?"
Phidaya alizungumza huku mkononi akiwa ameshika mfuko wa nguo zangu
"Nimerudi bwana"
"Una bahati kweli, nilisahau huu mfuko wako wa nguo, sijui ungerudije nyumbani na ubishi wako"
Phidaya akaita taksi na sote tukaingia ndani ya gari
"Gari umeiacha wapi?"
"Nimeiacha gereji, ina badilishwa rangi na kuwekwa kioo cha nyuma kipya"
"Umeshanunua hivyo vitu?'
"Ndio, vyote vipo kwenye gari"
Tuakfika hadi gereji na kukuta gari ikimaliziwa kufungwa kioo cha nyuma, huku rangi ikiwa imesha malizwa kupakwa
"Hii gereji ninaipenda kutokana huduma zao ni zaharaka, pia wanamitambo mingi"
"Ahaaa, ila ni kubwa"
"Ndio, vipi ulifanikiwa kufika lilipokuwa linakwenda lile gari?"
"Ndio, ila hatukufika kwenye jumba lenyewe, tulisimama kwa mbali"
Sikumuambia Phidaya kitu kilicho tupata kwa maana ningempa wasiwasi mwingi.Tukasubiri kwa masaa mawili, rangi iliyo pakwa kukauka, tukakabidhiwa gari yetu ikiwa katika muonekano mzuri na wakupendeza, tukaingia ndani ya gari safari ya kurudi nyumbani ikaanza
***
Nikaanza kuchukua mazoezi yangu binafsi, ya kuuweka mwili sawa, sikutaka kumuambia Phidaya lengo la mimi kufanya mzoezi hayo, kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyo jisni mwili wangu ulivyo zidi kuwa mwepesi na kuhimarika kwa mazozi, nikaingia kwenye mazoezi ya matumizi ya bunduki, katika kulenga shabaha, hadi nikajiamini kwa matumizi ya silaha
"Eddy mbona kipindi hichi unajiweka bize kwa mazoezi hadi naogopa"
Phidaya alizungumza huku akinipa taulo, nijifute jasho linalo nimwagika baada ya kufanya mazozi makali ya kupiga push up na kukimbia kwenye milima muda huu wa asubuhi
"Mwanaume siku zote ni mlinzi wa mwanamke, na ninatakiwa kukulinda mke wangu"
"Mmmm kweli?"
"Ni kweli, ndio"
Phidaya akanivuta karibu yake na kunikumbatia kwa furaha huku akitoa mihemo mizito
"Ninafurahi kuwa na mume kama wewe"
"Hata mimi ninafurahi kuwa na mke kama wewe"
"Ila Eddy kuna kitu nahitaji kukuambia"
"Kitu gani?"
"Nimeanza kuziona dalili za ujauzito"
"Kweli….!!?"
"Ndio"
Ni habari nyingine mpya ya kunifurahisha kwenye maisha yangu, kwani kitu ambacho kitanipa furaha kwenye maisha yangu ya baadaye ni mtoto
"Itabidi uende kwa Tanzania, ukailee hiyo mimba"
"Eddy….niende Tanzania nikafanya nini?"
"Uende ukailee hiyo mimba, sitaki mwanagu azaliwe hapa"
"Na wewe?"
"Mimi nitakuja, pia ninataka ukaagalie hali halisi ya usalama Tanzania kwamba ninatafutwa au laa"
"Eddy siwezi kwenda sehemu yoyote bila ya kuwa na wewe, kumbuka nimeacha kazi kwa ajili yako, na hii hali nahitaji kuwa nawe karibu kila mara na kila dakika"
Hatukufikia muafaka na Phidaya, na akakataa kabisa kurudi Tanzania.Usiku wa saa nne baada ya Phidaya kulala, nikaamka taratibu kitandani, nikachukua bastola yangu na kuhakikisha ina risasi za kutosha, nikavaa nguo nyeusi ambazo si rahisi kwa usiku kuonekana vizuri pamoja na saa yangu ya mkononi, kisha nikachikua na koleo(playz).Kitu kilicho anza kunichelewesha ni funguo ya gari, ambayo sikujua ni wapi ilipo
"Huu mwanamke ameiweka wapi hii funguo?"
Nilijiuliza huku nikiendelea kuitafuta kwenye droo ambazo nilihisi inaweza kuwepo, nikatoka nje bila ya Phidaya kugundua kitu chochote, nikafungua kweye gari kwa bahati nzuri nikaikuta funguo ikiwa kwenye gari.Kuhofia Phidaya kusikia mlio wa gari, nikaanza kuisukuma taratibu hadi nikafika umbali kidogo wa shamba lilipo.Nikaingia kwenye gari na kuiwasha na kuondoka, safari ya kuelekea kwenye jumba analo ishi Dorecy na mumewe ikaanza huku njia nzima nikiwa ninahasira kali iliyo zidi kunisukuma kuliendesha gari kwa kasi kuwahi kufika katika jumba hilo
Nikaisimamisha gari yangu kwenye kichaka kimoja, mbali kidogo na lilipo jumba hilo, nikashuka na kuanza kutembea msituni kwa kujiamini huku nikiwa makini sana, mwanga wa mbalamwezi ndio ulio nisaidia kuona mbele na shemu ninayo kanyaga.Nikafanikiwa kufika kwenye fensi ya nyaya, nikatoa kuleo na kuanza kukata moja baada ya nyingine hadi nikapata upenyo wa mimi kupita.Nikaendele kutembea hadi kwenye ikuta mrefu kiasi, nikatazama pande zote na sikuona dalili ya kumuona mtu.
Nikarudi nyuma, nikavuta kasi ya kupanda kwenye ukuta, kutokana na wepesi wa mwili wangu, halikuwa zoezi gumu la mimi kupanda juu ya ukuta huu, nikajivuta hadi nikafikia juu kasisa ya ukuta na kujilaza ili nisionekane, hapo ndipo nilipoanza kuona eneo zima la jumba la Khalid likiwa limetawaliwa na taa nyingi pamoja na ulinzi mkali wa askari walio na mbwa pamoja na bunduki nyingi.Nikamshuhudia mtu mmoja akiwa anapigwa na walinzi wapatao watano huku pembeni akiwa amesimama Khalid na Dorecy.Mtu huyo aliendelea kuomba msamaha ila walinzi hao hawakumsikiliza zaidi ya kuendelea kumshushia kipigo kitakatifu
Khalid akachomoa bastola yake na kumnyooshea mtu huyo, ila kabla hajafyatua akamkabidhi Dorecy bastola na kumuomba amuue mtu huyo, Dorecy bila ya huruma akafyatua risasi zilizo tua juu ya kichwa cha mtu huyo na kumsababishia kifo, nikashusha pumzi nyingi, kwani Dorecy amekuwa katili kiasi cha kuua mtu pasipo kuwa na huruma ya aina yoyote, nikiwa nifikiria cha kufanya nikastukia kitu kigumu kikinigusa kichwani mwangu, na kusikia sauti ya mwanaume ikiniamrisha nilale kama nilivyo na nisifanye kitu chochote la sivyo atauchangua ubongo wangu, taa kubwa lenye mwanga mkali likageukia sehemu ya sisi tulipo, juu ya ukuta na kuwafanya Khalid, Dorecy na watu wake kutuona.Na Khalid akaagiza mtu huyo kunishusha kwenye ukuta.
ITAENDELEA
 
*****SORY MADAM*****(61)

AGE....................................................................18+
WRITER.............................................................EDDAZARIA G.MSULWA

ILIOISHIA
Khalid akachomoa bastola yake na kumnyooshea mtu huyo, ila kabla hajafyatua akamkabidhi Dorecy bastola na kumuomba amuue mtu huyo, Dorecy bila ya huruma akafyatua risasi zilizo tua juu ya kichwa cha mtu huyo na kumsababishia kifo, nikashusha pumzi nyingi, kwani Dorecy amekuwa katili kiasi cha kuua mtu pasipo kuwa na huruma ya aina yoyote, nikiwa nifikiria cha kufanya nikastukia kitu kigumu kikinigusa kichwani mwangu, na kusikia sauti ya mwanaume ikiniamrisha nilale kama nilivyo na nisifanye kitu chochote la sivyo atauchangua ubongo wangu, taa kubwa lenye mwanga mkali likageukia sehemu ya sisi tulipo, juu ya ukuta na kuwafanya Khalid, Dorecy na watu wake kutuona.Na Khalid akaagiza mtu huyo kunishusha kwenye ukuta.

ENDELEA
Nikashusha pumzi taratibu, jamaa akanigusa tena na ndunduki yake kwenye kichwa changu na kuniamrisha kushuka kwenye ukuta, kwa haraka sana nikajigeuza na kuichota miguu yote ya mtu huyo na kumfanya aangukie ndani kama mzigo wa kuni, nikajirusha na kuangukia nje ya sehemu ambayo nimetokea, cha kumsukuru Mungu sijaumia sehemu yoyote ya mwili wangu ambayo itanizuia mimi kukimbia.Nikanyanyuka haraka na kuhakikisha bastola yangu ipo sehemu nilipo iweka nikaikuta ipo.Kelele za ving'ora vya hatari vikanifanya nianze kukimbia kwa kasi zangu zote na kutokomea msituni, kelele za mbwa wengi, nikaanza kuzisikia nyuma yangu, na kadri ninavyo kimbia ndivyo jinsi zilivyo zidi kuja nyuma yangu kwa kasi kubwa.Milio ya bunduki ikazidi kunipa changamoto ya kukimbia kwani watu wa Khalid wapo nyuma yangu, nikajibanza kwenye moja ya mti baada ya kuona risasi zinazidi kuwa nyingi nyuma yangu.Kundi kubwa la walinzi wa Khalid wakazidi kunifwatwa kwa nyuma.
"Mungu bariki"
Nimaneo niliyo yasema kimya kimya moyoni mwangu, kisha nikaanza kujibu mapigo ya risasi niazo rushiwa kwa fujo, nikaendelea kuwafatulia watu wa Khalid na kuwaangamiza kila ambaye nilimfyatulia risasi.
Nikastukia kuona mwanga mkali wa ukinimulika kutoka juu, nikatazama na kukuta ni Helcoptar, nikaanza kusikia sauti kutoka kwenye kipata sauti ikiniomba nijisalimishe la sivyo nitauawa kwani sehemu nzima ya msitu imezingirwa, nikaitoa magazine ya bastola yangu na kukuta imebakiwa na risasi moja tu, na nyuma yangu kundi la watu wasio pungua ishirini, wananifwata kwa kuyata, huku wengine wakiwa awanatokea mbele yangu.Mwanga wa Helcoptar ukaendelea kunimulika kiasi cha kuninyongonyeza kabisa katika kupata matumaini ya kujiokoa.Sikuwa na jinsi zaidi ya kupiga magoti chini, huku miono yangu nikiwa nimeiinyoosha juu.Jamaa wakanizingira na wawili wakanisogelea nakuanza kunipapasa na kunitoa kila kitu nilicho kuwa nacho mfukoni mwangu kisha wakaninyanyua na kunifunga waya mgumu kwenye mikono yangu na safari ya kuelekea ilipo ngome ya Khalid ikaanza.
Ilituchukua mwendo wa dakika zisizo pungua kumi hadi kufika ilipo ngome ya Khalid, nikamuona Dorecy na mume wake wakiwa wamesimama kwenye moja ya ngorofa kubwa lililopo ndani ya ngome, macho yao yote yakiwa kwangu
"Ohooo karibu bwana Eddy"
Muyo ulinistuka sana baada ya kumsikia Khalid akizungumza kiswahili kizuri tu, kwa haraka nikayafikira maneno ya kejeli niliyokuwa ninazungumza na mke wake, nikiamini kwamba Khalid aelewi kitu ambacho ninakizungumza na mke wake.
"Naona umekuja kunitembelea, za masiku bwana Eddy?"
Sikumjibu Khalid zaidi ya kumtazama kwa macho makali katika sehemu ambayo amesimama, pamoja na mke wake
"Mpandisheni huku juu"
Aliwaamuru watu wake na wakaniingiza kwenye moja ya lango kubwa, tukaanza kupandisha ngazi kuelekea ghrorofani, wasiwasi wangu mkubwa ni juu ya mke wangu Phidaya, sijui akiamka asubuhi na kunikuta sipo ndani chumbani, ataamua kufanya maamuzi gani.
"Karibu Eddy, ninafurahi sana kukuona hapa, kwa kipindi hichi kingine.Vipi ulikuwa umekosea njia ya kuja hapa?"
Macho yangu yakagongana na Dorecy aliye valia dera refu, kutokana na ujauzito wake kuwa ni mkubwa.Khalid akazitazama ishara za macho kati yangu na Dorecy kisha akatabasamu.
"Naamini, mke wangu atakuwa na furaha sana kukuona hapa mwanadarasa wake, na munavyo onekana mulikuwa munasoma sana eheee"
"Hee baby, hembu acha maneno yako, mimi huyo Eddy hatukuwa na ushirikiano kwenye masomo"
Dorecy alizungumza kwa sauti nyororo iliyo mbembeleza mumewe, na taratibu akamsogelea mumewe na kuanza kuzichezea nywele za kifua cha mume wake
"Ohh mke wangu, sawa ila vipi, sijaielewa maana ya rafiki yako kuwa hapa?"
"Hata mimi sijui"
"Eddy, ni kwanini upo hapa?"
"Dorecy nipe mali yangu niondoke"
Nlizungumza kwa sauti nzito, na kumfanya Khalid kumgeukia mke wake
"Anakudai?'
"Ahaaa hapana ila sijui kachanganyikiwa huyo"
"Eddy, unamdai nini mke wangu?"
Kwa haraka Dorecy akanikonyeza, pasipo mume wake kumuona, nakuniomba nisizungumze kitu chochote mbele ya mume wake.Nikatabasamua na kumtazama Khalid
"Hapana, ile siku nilipo kutana na nyinyi kule dukani, Dorecy aliniambia kwamba siku moja nije kuwatembelea atanipa mali ya kutosha"
"Ohhh, mke wangu ni mali gani unataka kumpa Eddy?"
"Ni mtaji wa kufungua biashara, siku ile baby si nilikuwambia kwamba kuna bishara ya hoteli nataka kwenda kuifungua Tanzania, so nikaona mtu wa kumuweka awe Eddy kama msimamizi"
"Ahahaaaa hapo nimewaelewa, kwani mulianza kunitisha.Mfungueni"
Khalid aliwaamrisha watu wake wanifungue mikono yangu na wakatii kama bosi wao alivyo agiza, wakanifungua mikono yangu na akawaomba waondoke, Khalid akanikaribisha sebleni kwake, na tukaanza kuzungumza mambo mbalimbali ya maisha, jambo ambalo lilianza kunishangaza kwani Khalid niliye adisiwa na muendesha taksi sio huyu ninaye zungumza naye mbele yangu.
"Bwana Eddy, kunabinti atakuja hapa kukuonyesha chumba cha kulala, mimi ngoja nikapumzike na mke wangu, si unamuona jinsi hali yake ilivyo?"
"Hakuna shida shemeji"
Khalid akanyanyuka na Dorecy na kupandisha ngazi kwenda juu kabisa, macho yangu yakawa na kazi ya kuwachunguza walinzi walio simama kwenye kila kona ya jumba huili kuanzia ndani hadi nje.Akaja dada mmoja aliye valia chupi aina ya bikini na sidiria
"Nifwate"
Alizungumza kwa kingereza, pasipo kuuliza ni wapi ninapo elekea nikanyunyuka na kuanza kumfwata kuelekea sehemu anapo kwenda, tukapita kwenye moja ya kordo ndefu, nyenye wingi wa vyumba kila kona, akafungungua mlango mmojana na sote tukaingia.
"Unapenda nini, whyne, shampen, wicky au juis"
Aliniorodheshea idadi ya vinywaji ambavyo sivitumii kwa wakati huu ambao nipo kwenye ngome ambayo hadi sasa hivi sijajua usalama wangu upo kaika upande gani,kati ya kutoka salama au kutokamu ndani ya ngome hii.
"Sihitaji chochote, asante sana"
"Una hitaji huduma ya mwili wangu"
"Hapana ninashukuru"
Baada ya msichana kumjibu hivyo akajizoa zoa na kutoka ndani ya chumba changu na kuniacha nikiwa ninamawazo sana, nikazima taa za chumba kizima na kuwa giza totoro, nikaanza kuchunguza kuta moja baada ya nyingine, kutazama kama kuta kuwa na kamera zilizo fichwa kwenye kuta za chumba hichi, ambazo mara nyingi baadhi huwa zinachimbiwa ukutani, na zinatoa mwanga mwekundu kila unapo ziona kukiwa na giza.Nikamaliza kukizunguka chumba kizima na sikuona kitu cha aina yoyote, nikaipanga mito mitatu kitandani kama mtu aliye lala na kuifunika kwa shuka.Nikalisogelea dirisha taratibu na kulifungua, ukimya mwingi umetawala nje, kitu kikubwa ninacho kiona ni walinzi wakikatiza katiza kila kona ya ngome hii.
Kitu ambacho kinanifanya nishindwe kushuka kwenye chumba hichi ni kutokana, chumba kipo ghorofani na chini ni mbali sana, mwanga wa jitaa kubwa ukakatiza kwenye dirisha nililo simama na kwa haraka nikajibanza kwenye ukuta ili upite vizuri na walinzi wasione.Ukarudi tena ulipo tokea, kabla sijanyanyuka mlango wa chumbani kwangu ukafunguliwa taratibu na nikamuona Dorecy akiingia huku akiwa amevalia kagauni kakulalia
"Eddy"
Aliniita kwa sauti ya kunong'oneza, huku akielekea kitandani ambapp nimepanga mito vizuri kama mtu aliye lala.Akasimama pembeni ya kitanda changu, niaamini hakuniona kwenye sehemu niliyo simama, akakitazama vizuri mwili wa mito nilio ulaza kisha akakipandisha kigauni chake juu, na kuchomoa kisu kikali alicho kuwa amekificha kwa kukifunga kwenye paja lake kwa mpira kisha kwa haraka akakishusha na kutua kwenye mito jambo lililo nistua sana kuona Dorecy akizidi kuwa katili juu yangu
ITAENDELEA
 
*****SORY MADAM*****(62)

AGE....................................................................18+
WRITER.............................................................EDDAZARIA G.MSULWA


ILIOISHIA
"Eddy"
Aliniita kwa sauti ya kunong'oneza, huku akielekea kitandani ambapp nimepanga mito vizuri kama mtu aliye lala.Akasimama pembeni ya kitanda changu, niaamini hakuniona kwenye sehemu niliyo simama, akakitazama vizuri mwili wa mito nilio ulaza kisha akakipandisha kigauni chake juu, na kuchomoa kisu kikali alicho kuwa amekificha kwa kukifunga kwenye paja lake kwa mpira kisha kwa haraka akakishusha na kutua kwenye mito jambo lililo nistua sana kuona Dorecy akizidi kuwa katili juu yangu
ENDELEA
Dorecy akastuka baada ya kuona kisu kikinyanyuka na mto, ikamlazimu kufunua shuka kwa haraka kwa ajili ya kutazama kama kitandani kwangu kuna mtu, akajikuta akistuka zaidi baada ya kukuta ni mito ndio imejipanga, kwa haraka nikamrukia na kumsukimiza kitandani na kisu chake kikaangukia pembeni, nikakiwahi kukiokota kisu chake, kisha nikamuwahi kulikamata koo lake na kuliminya kwa nguvu zangu zote huku kisu nikiwa nimekinyanyua juu kwa mkono wangu wa kulia
"Unataka kuniua ehee"
Nilizungumza kwa hasira huku nikiendelea kuliminya koo lake na kumfanya atoa mlio wa kukoroma akishiria kukata roho
"E…ddy naa…."
"Hakuna cha kuomba, malaya mkubwa wewe, leo ndio utaijua jina langu la utotoni nilikuwa ninaitwa nani"
Niliendelea kukaba Dorecy koo lake, hadi akaanza kulegea, nikamuachia na kwaharaka nikashuka kitandani na kuivuta miguu yake na akaangukia mgongo kwenye sakafu, nikamnyanyua juu na kumpiga kabali kwa nyuma huku kisu changu nikikiweka kwenye tumbo lake.
"Eddy mpenzi wangu naomba unisamehe nilikuwa ninakutania tuu"
Dorecy alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake.Sikutaka kuzisikiliza porojo zake kwa maana hakuna utani wa kuuana
"Ongoza njia"
"Eheee"
"Ongoza kwenda nje"
Nilizungumza huku nikikikandamiza kidogo kisu kwenye tumbo lake lenye mtoto ndani na kumfanya aanze kutambea huku mwili mzima ukimtetemeka, akafungua mlango, na kukutana na walinzi wawili wenye bunduki wakiwa wamesimama kwenye mlango wa chumba changu, hapo ndipo nikagundua kwamba nilikuwa ninalindwa nje nisitoke.Wakanielekezea bunduki zao, ila mimi nikazidi kumkaba kabali Dorecy huku kisu nikikikandamiza kwenye tumbo lake.
"Waambie washushe bunduki zao la sivyo nakufanyia oparesheni bila ganzi"
Dorecy akawaamuru watu wake waweze kufanya kama nilivyoa mauambia, wakatii kwa haraka, tukaanzaa kutembea kwenye kordo ndefu ya vyumba, huku walinzi wake wakitufwata kwa nyuma, sikuwa na woga wa aina yoyote kutokana bosi wao yupo chini ya mamlaka yangu.Tukafika sebleni na kukutana na walinzi wapata kumi wakiwa na bunduki zao wakitusubiria sisi kutokea kwenye seble hii.
"Eddy, sasa nimeijua rang yako"
Sauti ya Khalid ikanistua, nikamuona akitokea kwenye moja ya chumba huku akiwa amevalia nguo za kulalia na mkononi mwaka akiwa ameshika bastola
"Waamrishe watu wako kutupisha la sivyo ninamuua mke wako"
Nilizungumza kwa sauti kubwa, huku nikiendela kukikandamiza kisu kwenye tumbo la Dorecy ambaye muda wote machozi yanamwagika, kwa ishara Khalid akawaamrisha watu wake kutupisha, tukapita katikati yao huku muda wote nikiwa makini sana, nikiwatazama watu wa Khalid
"Ila Eddy unacheza makida makida kwenye nyaza za umeme"
Khalid alizungumza kwa kujiamini sana, sikujali maneno ya Khalid zaidi ya kumuamrisha Dorecy kutembea kuelekea nje.Tukafunguliwa mlango na walinzi wake baada ya Dorecy kuwaamrisha waweze kufanyan hivyo.
"Magari yenu yapo wapi?"
Nilimuuliza Dorecy kwa sauti ya ukali, taa kubwa lililopo katika jumba hili likawa na kazi ya kutumulika kila sehemu ambayo tunakwenda, macho yangu yote yakawa na kazi ya kutazama kila sehemu ya jengo hili kuangalia walinzi walio jipanga huku wote bunduki zao zikiwa kwetu, Dorecy akanionyesha moja yan jengo ambalo aliniambia kwamba ndipo yalipo magari, kwa hatua za umakini tukatembea hadi lilipo jengo hilo na kuingia ndani, ambapo nikakuta magari mengi ya kifahari takiwa yamepangwa kwa mpangilio mzuri.Macho yangu yakatua kwenye gari aina ya BMW inayo endana na gari ya Sheila aliyo pewa na wamarekani alio cheza nao filamu ya ngono.Nikaisogela huku nikiwa ninaendelea kumshika Dorecy shingo yake, nikajaribu kufungua mlango wa gari na ukafunguka, kwa bahati nzuri nikakuta funguo ikiwa kwenye siti ya dereva.
"Eddy si umesha fika sehemu uliyokuwa unahitaji, niachie sasa"
"Bado unakazi na mimi"
"Kazi gani jamani Eddy?"
"Utaijua mbele ya safari"
Nikamshukumiza Dorecy kwenye siti ya pembeni na mimi nikaingia, nikaiwasha gari na ikawaka pasipo tabu yoyote, cha kushukuru MUNGU mafuta ya gari yamejaa vizuri kwenye tanki lake, nikashusha pumzi nyingi huku nikijifunga mkanda wa gari
"Eddy Khalid atakuua"
Dorecy alizungumza kwa sauti ya chini huku, machozi yakiendelea kumwagika, sikutaka kumsikiliza sana Dorecy, nikairuduisha nyuma gari na kuiweka sawa kuelekea kwenye mlango wa kutokea kwenye jumba hili ambao ni wambao.
"Funga mkanda"
Nilimuamrisha Dorecy na akatii, nikaknyaga mafuta pamoja na breki na kuifanya matairi ya nyuma ya gari kuserereka kwa nguvu, nikaachia breki na kuifanya gari kuanza kwenda kwa mwendo wa kasi, nikaubamiza mlango na gari ikapita kwenye mlango bila ya shida.Taa kali zikapiga kwenye kioo cha gari langu na kunifanya nisione mbele vizuri, nikajikuta nikikanyaga breki kwa haraka, huku macho yangu yakikitazama ‘Kifaru' kikubwa kilichopo mbele yatu.Nikatazama pembeni na kuona kuna bustani ya maua ambayo gari linaweza kupita pasipo shida yoyote.Nikatazam kifaru hichi ambacho mara nyingi hutumika jeshini katika vita.Mwanga wa Helcoptar ukaendelea kumulia kwenye gari letu,
"Shiti"
Nikakanyaga mafuta kwa haraka, kugeuza gari kwa kasi na kuuelekezea kwenye bustani ya maua, risasi nyingi za walinzi wa Khalid zikaanza kupiga kwenye gari yetu cha kushukuru Mungu hakuna risasi hata moja ambayo inaingia kwenye gari, nikaendelea kuipitisha gari kwenye bustania ya maua hadi nikafika kwenye barabara kubwa iliyopo ndani ya hili jengo la Khalid
"Njia hapa ya kutokea ni ipi?"
"Wewe nyoosha tuu mbele"
Dorecy akanipa ushirikiano mzuri paiso kupinga, nikazidi kunyoosha kwenye barabara aliyo seme Dorecy, huku mfululizo wa risasi ukizidi kuniandama kwa nyuma, mwanga wa Helcoptar ukazidi kutumulika
"Kunja kushoto"
Dorecy alizungumza na mimi nikafanya kama alivyo seme, kazi yangu kubwa ikawa ni kubadilisha gia kwenye gari na kuongeza mwendo kasi wa gari
"Kulia"
Nikakunja kulia kwenye kibarabara kidogo ambacho kwa mbele yake kuna geti dogo lililo wazi, nikazidi kuongeza mwendo kasi wa gari na kutoka kwenye ngome ya Khalid.Tukatokea kwenye barabara iliyopo kwenye kilima, huku pembeni ya barabra kukiwa kuna maporomoka marefu mithili ya barabara ya mlima Kitonga uliopo Mkoni Iringa nchini Tanzania.
"Unaijua hii barabara?"
"Ndio wewe twende"
Umakini wote nikazidi kuuweka kwenye barabara, kwani ina kona nyingi, na endapo nitafanya ujinga wa aina yoyote gari itabingiria kwenye maporomoko na ndio utakuwa mwisho wa maisha yangu na Dorecy.Helcoptar ya watu wa Khalid ikazidi kutufwata kila sehemu ambayo tunaelekea, kutokana na uzoefu wangu wa kuendesha gari kwenye barabara zenye makona mengi, haikuwa nguma kwangu kuhimili kona za hapo kwa hapo ambazo ni nyingi sana.
"Ukimaliza kona mbili hapo mbele kuna mporomoko mrefu kuwa makini"
Dorecy alizungumza, ushirikiano wake sikuuamini sana kutokana na yote aliyo nifanyia, nikazidi kuongeza mwendo kasi wa gari huku miguu yangu, ikiwa na kazi ya kucheza na breki.Tukafika kwenye kiporomoko ambacho Dorecy anazungumza kwa mbali kidogo nikaona taa za gari kwa haraka haraka zinapata kumi zikiwa zimeziba njia, kwa jicho langu la kushoto nikamuona Dorecy akitabasamu hapo ndipo nikagundua amaniuza, kwa kutumia kisukusuku changu cha mkono wa kushoto, nikambamiza nacho Dorecy pembeni ya shingo yake na kumfanya atulie kimya na kupoteza fahamu.Nikafunga breki za gari langu, umbali kidogo kutoka zilipo gari za watu wa Khalid, nikatazama kushoto kwangu ambapo kuna maporomoko marefu, hapakuwa na nyia ya aina yoyote.Kulia kwangu kuna ukuta mkubwa wa mlima, Helcoptar ikasimama na kuzidi kutumulika,
"Nitafanyaje?"
Nilijikuta nikijiuliza swali mwenye pasipo kupata jibu, kwa kutumia kioo cha pembeni nikaona gari nyingi zikija kwa kasi nyuma yangu, huku zikaanza kushuka kiporomoko ambacho ndipo nilipo.
"Bwana Eddy jisalimishe, wewe mwenyewe"
Niliisikia sauti ya Khalid ikitokea kwenye kipaza sauti juu ya Helcoptar yake,
"Siwezi kufa kijinga"
Nilizungumza mwenyewe huku nikiitazama Helcoptar ambayo inaendelea kumulika mwanga kwenye gari yetu
"Moja jisalimishe"
Khalid alianza kuhesabu, nikatimaza pembeni upande wa kushoto nikaona tobo kubwa kwenye gemo kubwa la mlima, gari za mbele yangu zikaanza kupandisha kilima huku za nyuma zikishuka kwa kasi, nikakanyaga mafuta, pamoja na breki zote kwa pamoja na kuyafanya matairi ya nyuma yakiserereka kwa nguvu gari za nyuma zilazidi kunisogelea katika sehemu ambayo nimesimama, kwa kasi nikakunja kulia na kuifanya gari yangu kuelekea kwenye tobo lilipo kwenye gemo la mlima, sikuamini kama gari yangu inaweza kuingia ndani ya tobo hili, sikumini macho yangu baada ya kukuta barabara iliyo chongwa ndani ya shimo hili, ambayo ipo ndani ya mlima
"Waoooo"
Nilijikuta nikipiga kelele a furaha baada ya kufanikiwa kuingia ndani ya shimo hili, japo kuna giza jingi ila taa gari langu zikanisaidia kuona mbele vizuri sana.Gari za watu wa Khalid zikaendelea kunifukuzia kwa nyuma jambo lililo anza kunipa wasiwasi mwingi
"Wakinikamata watanila nyama"
Nilijisemea kimoyo moyo, nikamtazama Dorecy na kumkuta akiwa bado amepoteza fahamu, upana wabarabara hii iliyo chongwa ndani ya mlima ikazipa upenyo gari za watu wa Khalid kutanda njia nzima, huku baadhi ya gari zikijari kunipita ila niliwazui kwa kuwazibia njia kwa mbele.Wakaanza kunipiga risasi kwenye kii cha nyuma cha gari langu, nikazidi kuongeza mwendo wa gari langu, mbaya zaidi barabara hii haina hata kona zaidi ya kunyooka.
Risasi zao nyingi zikafanikiwa kutoboa kioo cha nyuma cha gari na kuzidi kunichanganya akili yangu, nikazidi kukanyaga mafuta hadi mshale wa spidi mita ukagota kwenye spidi ya mwisho ambayo ni mia mbili na hamsini.Nikazidi kwenda mbele, gafla nikakutana na kona ambayo kwa mwendo ambao ninao nikashindwa kukunja na kuisababisha gari kupiga kweney ukuta na kuvunja ukuta huu wa udongo, kufumba na kufumbua nikajikuta gari ikielea hewani, na kuanza kwenda chini kwenye miamba mikubwa ya mawe jambo ambalo lilinifanya niaanze kusali sala yangu ya mwisho kwani, ikitua chini mimi na Dorecy wote tutakuwa maiti
ITAENDELEA
 
*****SORY MADAM*****(63)

AGE....................................................................18+
WRITER.............................................................EDDAZARIA G.MSULWA


ILIOISHIA
Risasi zao nyingi zikafanikiwa kutoboa kioo cha nyuma cha gari na kuzidi kunichanganya akili yangu, nikazidi kukanyaga mafuta hadi mshale wa spidi mita ukagota kwenye spidi ya mwisho ambayo ni mia mbili na hamsini.Nikazidi kwenda mbele, gafla nikakutana na kona ambayo kwa mwendo ambao ninao nikashindwa kukunja na kuisababisha gari kupiga kweney ukuta na kuvunja ukuta huu wa udongo, kufumba na kufumbua nikajikuta gari ikielea hewani, na kuanza kwenda chini kwenye miamba mikubwa ya mawe jambo ambalo lilinifanya niaanze kusali sala yangu ya mwisho kwani, ikitua chini mimi na Dorecy wote tutakuwa maiti

ENDELEA
Gari ikazidi kwenda chini kwa kasi, gafla nikastukia gari ikiwa imekwama huku, tawi kubwa la mti likiwa limeingia dirishani la nyuma la gari na kuifnya iendelee kuninginia kwenye mti, nikashusha pumzi taratibu huku nikitazama chini, cha kumshukuru MUNGU, kutoka sehemu tulipo ning'inia hadi chini si mbali sana, nikaufungua mkanda wa gari nilio jifunga, nikamtazama Dorecy na kumuoana akiwa anainyanyua nyanyua shingo yake, akizinduka kutoka usingizini.Akanitazama kwa macho yakuchoka
"Eddy"
"Nini?'
"Yupo wapi Khalid?"
"Wee mwehu nini, jiulize mwenyewe"
Nilizungumza kwa hasira huku nikiufungua mlango wa gari, kuna tawi lipo karibu na mlango wangu, nikapiga makadirio ya macho na kuona ninaweza kuruka na kulikanyaga pasipo na wasiwasi wa aina yoyote
"Eddy unataka kwenda wapi, kwani hapa wapi?"
Dorecy alizungumza huku akitazama chini
"Hapa tupo mbinguni mama yangu"
"Mbinguni……!!?"
"Unauliza tena, hapa ukifungua mlango tuu umeshafika kwa sir God"
Nilizungumza kwa dharau, nikaruka kwenye tawi la mti, kwa bahati nzuri nikatua vizuri na kujiweka sawa mwili wangu, nikashuka kwenye mti taratibu na kufika chini pasipo shida ya aina yoyote, gafla nikasikia kelele za Dorecy akiniita jina langu, ikanilazimu nimtazame nikamuona akiwa ananing'inia, huku ameushikilia mlango wa gari uliopo upande wa siti yake
"Eddy niokoe mwenziooo, ninakufa mimi"
"Ukijiachia tuu unafika mbnguni, hapo tulikuwa kwenye geti la kuingilia mbinguni"
Nilizungumza huku nikimtazama Dorecy jinsi anavyo ning'inia huku akiirusha rusha miguu yake hewani
"Eddy nakufa mimi"
Dorecy aliendelea kuzungumza kwa sauti ya kilio, huku akiendelea kuning'inia hewani, nikatafuta sehemu yenye jiwe lililo kaa vizuri, nikakaa na kuendelea kumtazama Dorecy anaye endelea kuninginia hewani
"Eddy niokooe"
"Nikuulize kitu Dorecy?"
"Ehee" Alijibu huku akiwa amening'inia
"Hivi huku ulifikaje?"
"Nikuulize wewe, tumefikaje huku?"
"Ahaa unaniuliza mimi tena kwamba tumefikaje huku, unadhani kwamba mimi nilikuwa ni ndege iliyo kufikisha kwenye hii nchi?"
"Eddy tuachane na hayo, ninakuomba unisaidiea"
Dorecy alizungumza kwa sauti ya unyong, akiashiria kwamba amechoka sana
"Madini yangu yapo wapi?"
"Edd siwezi kukujibu hadi nishuke"
"Basi wewe si mjeda wa mzee Godwin, jishushe mwenyewe"
Nilizungumza huku nikinyanyuka kwenye jiwe, nikiendelea kulichunguza aneo zima la hii sehemu, nilipo hakikisha lipo salama na hakuna uwezekana na watu wa Khalid kufika katika sehemu tulipo nikarudi sehemu alipo Dorecy akiendelea kuning'inia huku akitoa kilio kwa mbali akilalamika kwamba anakufa
"Jiachie"
Nilizungumza huku nikiwa nimesimama chini yake nikimtazama
"Ehee?"
"Hujasikia, jiachie nitakudaka na hilo jitumbo lako"
"Kweli Eddy?"
"Kama hutaki basi bwana"
"Basi najiachia"
Nikaitega mikono yangu usawa wa sehemu anayo ning'inia Dorecy, nikahesabu moja hadi tatu, Dorecy akajiachia na kutua kwenye mikono yangu, cha kushukuru MUNGU ametua vizuri kwenye mikono yangu, nikamsimamisha chini na kumuacha akiendelea kuhema kwa nguvu, kama bata mzinga.Nikaanza kupiga hatua za kuondoka katika eneo hili pasipo kusubiria asante ya Dorecy huku moyoni mwangu nikijikuta nikianza kusamehe kuhusiana na madini yangu, kwani hakuna uwezekano wowote wa mimi kuyapata kutokana na Khalid kujizatiti vizuri katika swala la ulinzi
"Edd….y"
Nilisikia sauti ya Dorecy ikiniita kwa unyonge nyuma yangu, nikasimama pasipo kutazama nyuma, nikashusha pumzi nyingi na kugeuka taratibu, nikamuona Dorecy akianza kukaa chini taratibu huku akiwa amelishika tumbo lake
"Eddy nakufa mimi, tumbo langu"
Dorecy alilalamika huku akiwa amelishika rumbo lake, nikaanza kupata mstuko baada ya kagauni kake ka kulalia alicho kivaa kukiona kikiwa kimelowa kwa damu sehemu zake za siri.Machozi ya uchungu yakaendelea kumtoka Dorecy, vilio vya Dorecy vikazidi kuongezeka, ikanilazimu kurudi kwa haraka katika sehemu alipo
"Eddy mtoto anatoka"
Dorecy alizungumza huku akipanua mapaja yake, wazo la kwanza kunijia kichwani mwangu, ni kukata nguo ya ndani aliyo ivaa Dorecy, macho yangu yakaendelea kumtazama Dorecy jinsi anavyo toa mayowe ya uchungu
"Eddy mwanangu uwiiiiiii"
"Yupo wapi?"
Nikastukia kofi zito ikitua kwenye shavu langu, kutoka kwa Dorecy ambaye anaonekana kukasirika, macho yake ameyatoa huku jasho jingi likimwagika kutoka na maumivu makali anayo yapata.
"Jikaze uzae"
Nilizungumza huku nikiishikilia miguu ya Dorecy ambayo ameichanua kwa kiasi fulani, nikaendelea kumuhimiza ajitahidi kumsukuma mtoto, kwani nilisha anza kuona dalili ya majimaji yanayotangulia kabla ya mtoto kuzaliwa.Taratibu nikaanza kuona kichwa cha mtoto kikianza kuchomoza
"Push kwa nguvu"(Sukuma…&#8230😉
Nikaendelea kumuhimiza Dorecy kwa sauti ya juu, akaendelea kujitahidi kumsukuma mtoto wake atoke nje, nikaiweka mikono yangu karibu na kichwa cha mtoto na kuanza kukipokea kichwa chake taratibu
"Endelea mama, mabega yameshaanza kuchomoza"
Hadi mimi mwenyewe jasho likaanza kunitoka kwani si kazi ndogo ya kumzalisha mwanamke
"Eddyyyyyyyyyyyyyyyy"
Dorecy alizungumza kwa nguvu, huku akijikamua kwa nguvu zake zote na kumfanya mtoto wake kutoka na kuangukia mikononi mwangu, sikuisikia tena sauti ya Dorecy, katoto kake ka kiume, kenye mwili mdogo kakaanza kutoa kimlio kwa mbali, nikajikuta nikifurahi mimi mwenyewe, huku jasho likiendelea kunimwangika uso mzima, nikabaki nikimtazama mtoto huku kitomvu chake kikiwa bado kimeshikana na mama yake, ambaye amepotezafahamu kutokana na maumivu makali ya kujifungua
"Huyu mtoto amezaliwa kabla ya siku zake"
Nilijisemea kimoyo moyo huku nikiendelea kumtazama mtoto kwani ni mdogo kupindukia, kwa elimu yangu ya sayansi watoto wa aina hii huwa tunawaita njiti kutokana hajatimiza umri halisi wa yeye kuzaliwa kama watoto wengine wanaotimiza miezi tisa
Nikamtazama Dorecy kwa macho yaliyo jaa uchovu mwingi, kifua chake kwa mbali kinanyanyuka taratibu na kurudi chini, nikamsogelea na kumtingisha kidogo, ila hakuzinduka
"Hichi kitovu kinakatajwe?"
Nilijiuliza swali huku nikikitazama kitovu kilicho ungana kati ya mama na mtoto, nikamuweka vizuri Dorecy na kumlaza chali, nikamuweka mtoto wake juu ya tumbo lake kisha nikanyanyuka na kuanza kutafuta ni wapi ninapoweza kupata kitu chenye ncha kali cha kukikata kitomvu cha mtoto, kutokana kumesha pambazuka vuzuri ninaweza kuona kila kitu ambacho kinaweza kuwa chini, nikazunguka aneo la karibu na alipo Dorecy ila sikuona kitu kinachoweza kunisaidia kwa muda huu.Ikanilazimu kurudi sehemu nilipo muacha Dorecy, macho yangu yakangonana na macho ya chui, ambaye yupo hatua chache kutoka sehemu alipo lala Dorecy, ambaye muda wote hajitambui kutokana nakupoteza fahamu
"Mungu wangu"
Nilijisemea kimoyo moyo huku nikiendelea kumtazama chui ambaye anatoa mingurumo ya chini chini huku akilamba lamba mdomo wake wenye meno makli yenye ncha kali sana, nikachuchumaa chini taratibu pasipo kuyapepesha macho yangu, nikimtazama chui huyu, nikaokota kipande cha jiwe ambacho nimekikanyanga kwa mguu wangu wa kushoto, kisha nikasimama huku nikiendelea kumtazama chui huyu
"Shiiiii"
Nilitoa mlio huo, nikimfukuza chuki huyu ambaye taratibua alichaanza kupiga hatua za kumfwata Dorecy na mwanaye katka sehemu ambayo wamelala chini, chui akasita kidogo na kunitazama kwa macho yake makali
"Toka opo"
Niliendelea kuzungumza huku nikimtishia kwa jiwe ambalo nimelishika mkononi mwangu, mwili mzima ukaanza kunitetemeka baada ya chui kubadilisha muelekeo wake na kuanza kunifwata mimi kwa mwendo wa madaha katika sehemu ambayo nimesimama, kikataka kupiga hatua moja nyuma, gafla nikajikuta nikianguka chini kama mzigo, kitendo cha kujaribu kunyanyuka tayari Chui amenirukia kifuani kwangu, kichu cha kwanza kukiwahi katika kukishika ni shingo yake, nikakizuia kichwa chenye mdomo wake ulio jaa meno makali, usinidhuru kwenye mwili sura yangu,
Chui huyu akaendelea kunikwaruza na kucha zake, sehemu mbali mbali za mwili wangu, huku akijitahidi kuushusha mdomo wake kuing'ofoa pua yangu, nikaendelea kujikaza kwa juhudi zangu zote, uzito wa chui huyu ni mara mbili ya uzito alio nao mke wangu Phidaya, mikono yangu ikaanza kutetemeka kwa kuchoka, huku taratibi nikiendelea kujikaza kizuia shingo ya Chui huyu.
"Mungu wangu nisaidie mimi"
Niliendelea kuzungumza, huku mikono ikianza kuchuka taratibu chini, ikizidiwa uzito na kichwa cha chui huyu anaye onekana ananjaa kali, sikujali jinsi anavyo nikwaruza sehemu za mwili wangu kwa kutumia miguu yake ya nyuma na yambele yenye kucha kali sana, kikubwa ni kujitolea maisha yangu kwa ajili ya Dorecy na mwanaye niliye mzalisha
"Siwezi kufa kijinga"
Nikaanza kujitutumua kiume, huku nikiipandisha mikono yangu juu nikijitahidi kumtoa Chui huyu mwilini wangu, juhudi na nguvu zangu taratibu zikaanza kuzaa matunda, kwani nikafanikiwa kumgeuza chui na kumuegemesha kando.Mwili wangu mzima unavuja damu kataika sehemua alizo nikwaruza chui huyu, mikono yangu sikuiruhusu kutoka mikononi mwa chui huyu.Nikaanza kukidundiza kichwa chake chini, kwenye jiwe kubwa.Chui akazidi kupandisha hasira na kutoa pumzi kali iliyo anza kuyafanya macho yangu kumwagika machozi mithili ya mtu aliye pigwa bomu la machozi na askari wa kutulizaghasia
"Eddyyy"
Niliisikia sauti ya Dorecy ikiita kutoka katika sehemu alipo lala, nikageuza shingo yangu kumtazama sehemu alipo, nikamuona amekaa chini huku amemshika mwanaye, kitendo cha mimi kumtazama Dorecy kikawa ni kosa kubwa kwangu kwani chui, akanibinua kwa nguvu zake zote akaanza kunikwaruza huku meno yake akijaribu kuyakita kwenye paja langu la mguu wa kulia.Maumivu yasiyo na kifani yakaanza kuutesa mguu wangu, machozi ya uchungu yakanimwagika.Nikaokot kipande cha jiwe lilicho chongoka na kuanza kumkita nacho Chui cha kichwani mwake
Chui akazidi kuyakita meno yake kwenye paja langu, nia yake kuu ikiwa ni kunikata mguu wangu, nikazidisha kumbabiza kwa jiwe langu nililo lishika, kelele za maumivu zikaniendana na kasi yangu ya kukikita kicha cha chui kwa ncha ya kipande cha jiwe, kichwa cha Chui kikaanza kufumuka damu huku fuvu lake la kichwa likipasuka na ubongo wake kutoka nje, ikawa ni mwisho wa maisha yake
"Ahaaaa"
Nilizungumza huku nikilia kwa uchungu mkali, nikaushika mdomo wa Chui na kikauachanisha mdomo wake wenye meno yaliyo kita kwenye paja langu, japo maumivu ni makali sana ila nikajitahidi hivyo hivyo hadi paja langu nikalitoa kwenye kinywa cha Chui na kujilaza pembeni,Nikamtazama Dorecy sehemu aliyo kaa nikamuona akijitahidi kusota kuja sehemu niliyo jilaza mimi, huku sura yake ikiwa imejaa machozi mengi
"Usije"
Nilizungumza kwa sauti iliyo kwaruza sana huku nikimnyooshea mkono asifike katika sehemu nilipo mimi, nikajinyanyua taratibu huku damu zikendelea kuvuja kwenye paja langu.Chakumshukuru Mungu, Chui huyu meno yake, hayakufanikiwa kukutana na kutoa kipande cha nyama kwenye paja langu, au kuukata kabisa mguu wangu, nikaanza kutembea huku nikiuburuza mguu wangu ulio jeruhiwa hadi nikafika sehemu alipo kaa Dorecy
"Mtoto yupo hai?"
Nilimuuliza Dorecy huku nikimtazama mtoto wake aliye yafumba macho yake
"Ndio"
"Ohhh asante Mungu"
Nilizungumza kwa sauti ya kukwaruza sana huku damu zikiendelea kunimwagika mwilini mwangu, machozi yafuraha yaliyo changanyikana na uchungu yakaendelea kunitiririka usoni mwangu
"Eddy ninakupenda sana, samahani kwa yale yote niliyo kufanyia, ninaamini kwamba mimi ni binadamu ninaye weza kuhadaika kwa vitu vidogo sana.Sikustahili unisaidie, ilikuwa ni haki yangu kutafunwa na huyo chui mimi na mwanangu, ila wewe uliweza kujitolea maisha yako kwa ajliya yangu na mwanangu"
Dorecy alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake, nikamtazama kwa muda jinsi anavyo endelea kulia kwa uchungu sana
"Usilie, nimekusamehe muda mwingi sana, hali yangu inazidi kuwa mbaya na hapa niporini, ninjua sinto weza kutoka nikiwa hai, kifo kitakuwa juu yangu, ninakuomba umtafute msichana mmoja anaitwa Phidaya, anamimba yangu nakuomba unisaidie kwa hilo pale nitakapo kuwa nimeshakufa"
"Hapana Eddy, huwezi kufa nakuomba usizungumze hivyo"
"Dorecy, damu nyingi inanitoka nilazima…."
"Edddyyuuu tazama nyuma yako"
Sauti kali ya Dorecy ikaniomba kugeuka nyuma na mimi nikafanya kama alivyo niambia, ila tayari nimeshachelewa risasi mbili kutoka kwa watu wa Khalid waliofika kwenye eneo hili, zikatua kifuani mwangu, na taratibu nikaanza kwenda chini, nikapiga magoti na kumtazama Dorecy, aliye yatoa macho yake huku akishangaa, kuto kuamini kitu anacho kiona
"Bye…."
Nikaanguka chini, huku nikilalia tumbo na giza nene taratibu likaanza kuyafunika macho yangu, na kwambali nikaanza kuisikia sauti ya Dorecy ikiliita jina langu kwa uchungu
ITAENDELEA
 
****SORY MADAM*****(64)

AGE....................................................................18+
WRITER.............................................................EDDAZARIA G.MSULWA


ILIOISHIA
"Bye…."
Nikaanguka chini, huku nikilalia tumbo na giza nene taratibu likaanza kuyafunika macho yangu, na kwambali nikaanza kuisikia sauti ya Dorecy ikiliita jina langu kwa uchungu
ENDELEA
Sikuweza kusikia kitu chochote kinacho endelea kwenye masikio yangu
***
Kwa mbali nikaanza kuhisi sauti za watu wakizungumza taratibu, nikajaribu kuyafumbua macho yangu kutazama ili nione ni kina nani, ila ukungu mwingi uliojaa machoni mwangu sikuweza kuwaona vizuri.
"Eddy"
Nilisikia sauti ikiniita masikioni mwangu, ambayo inaendana na sauti ya mke wangu Phidaya, nikageuza shingo yangu kutazama sehemu inapo tokea sauti hiyo, nikawaona watu wawili wakiwa wamesimama huku mmoja akiwa amevalia mavazi meupe huku wapili nguo zake zikiwa na rangi mchangayiko.
"Eddy mume wangu upo salama?"
Sauti ya Phidaya ikaendelea kupenya masikioni mwangu, nikajaribu kuzungumza ila kinywa changu nikakikuta kikiwa ni kizito sana, Nikabaki nikimtazama Phidaya mke wangu, aliye valia gauni lenye rangi machanganyiko, mkono wa Pihidaya ukapita kwenye sura yangu, kisha mwanaume aliye valia nguo nyeupe akamshika na kumuondoa ndani ya chumba
Hali yangu ya afya ikazidi kuhimarika siku hadi siku, nikiendelea kupatiwa huduma na madaktari ambao sikuwafahamu, zikapita siku kadhaa nikiwa kitandani nikiendelea kuuguza majeraha yangu ya mwili mzima huku Phidaya akija kunitembelea kila siku, ila kitu kikubwa ambacho ananificha ni jinsi ya mimi kufika katika hospitali hii
"Baby ngoja mimi nirudi hotelin"
Phidaya alinyanyuka kiuvivu huku tumbo lake likiwa kubwa kiasi, kutokana na ujauzito wake alio kuwa nao
"Ngoja kwanza"
Nilimuambia Phidaya huku nikimshika mkono wake wa kushoto, uliokuwa karibu yangu
"Kwa nini huniambii ukweli, juu ya kufika kwangu hapa"
"Eddy nilisha kueleza kwamba, nitakujibu mume wangu siku ukiwa umepona vizuri, hili swala halina haja ya wewe kulijua kwa wakati huu
"Hata kama, kwani kukuuliza jinsi ya mimi kufika hapa imekuwa ni shida, si ndio?"
"Hapana mume wangu, ila kikubwa ni wewe afya yako kuwa katika hali ya uzima"
"Powa kama hutaki kuniambia chochote ninakuomba uende zako"
Nilizungumza kwa hasir huku nikimtazama Phidaya aliye simama pembeni ya kitanda changu,
"Baby umekasirika?"
"Hapana, wewe nenda"
Phidaya akaanza kupiga hatua za kuondoka kuelekea ulipo mlango wa kutokea katika chumba cha hospitalini, kabla hajaufikia nikamstua
"Na usipo nikuta, usijilaumu"
Ikamlazimu Phidaya kugeuka na kunitazama kwa macho ya mshangao mwingi, taratibu akarudi na kukaaa kwenye kiti, huku sura yake ikiwa na huzuni kidogo
"Mume wangu ni kwanini unazungumza maneno kama hayo, unajua ni jinsi gani unavyo utesa moyo wangu"
"Tatizo sio kuutesa moyo wako ila tatizo ni kwanini hutaki kuniambia ukweli juu kufika kwangu hapa, kwa mtazamo wangu hapa si Iraq, siwezi kuendelea kukaa sehemu ambayo siijui ni wapi nikifa j…?"
"Eddy inatosha…"
Phidaya alinikatisha na kuzungumza kwa sauti kubwa ya ukali huku machozi yakimwagika usoni mwake, akanitazama na macho yake makubwa kiasi ambayo tayari yalisha anza kubadilika rangi na kuwa mekundu kiasi
"Eddy unajua ni jinsi gani, tabu niliyo ipata hadi kukuleta hapa eheeeee? Ulikuwa ni mfu wewe usiye jitambua, umeyafanya maisha yangu kuwa ni yakuwindwa kama kitu cha thamani kwa ajili yako"
Phidaya alizungumza kwa sauti ya ukali iliyo jaa hasira
"Utaka kujua kwamba hapa ni wapi si ndio?"
Swali la Phidaya likaniacha mdomo wazi huku nikishindwa kujua ni jinsi gani nimjibu
"Si unataka kujua, mbona uzungumzi?"
"Ndio"
Nilijibu kwa unyonge baada ya kumuona Phidaya akinijia juu
"Hapa Manila, Philipines"
"Ndio wapi?"
"Ndio hapa"
Phidaya alinijibu kwa ufupi huku akinitazama machoni, akanyanyuka na kupiga hatua za haraka hadi shemeu ulipo mlango akafungua na kutoka, nikajikuta nikishusha pumzi nyingi, huku nikuutazama mlango aliotoka Phidaya.Kitu kikubwa ambacho kunaniumiza kichwa ni juu ya kwanini Phidaya hataki kunieleza ukweli jinsi ya yeye alivyo fika hapa
Siku mbili zikapita pasipo kumuona Phidaya, jambo lililoanza kuzua wingi wa maswali kichwani mwangu, huku nikijiuliza ni nikwanini sijkumbili hizi hajatokea.
"Au hao watu wanao muwinda ndio wamemteka?"
Niswali jingine lililotokea kuniumiza kichwa change, kutokana nimeshaanza kuruhusiwa kutoka nje ya maeneo ya hii hospitali iliyojaa watu wenye asili ya bara la ulaya na asia.Sikuwa na rafiki zaidi ya kuzunguka kila eneo la hospitali huku nikiwa nimevalia nguo nyeupe zinazo fanana na wangonjwa wengine wanao zunguka zunguka katika eneo hili la hospitlini
Baada ya kuhisi kuchoka nikaamua kurudi kwenye chumba change, kabla sijakifikia nikawaona jamaa wawili walio walia nguo nyeusi pamoja na miwani wakiingia ndani ya chumba change, ikanilazimu kujibanza kwenye moja ya kona ya ukuta kutazama kujua ni kitu gani amacho kitaendelea, baada ya dakika kama tatu hivi jamaa wakatoka na kuondoka, jambo lililo anza kunipa mashaka mengi
"Niende au nisiende?"
Nilijiuliza huku mwili mzima ukinitetemeka, nikatazama mlango wa chumba changu kisha nikajipa matumaini mimi mwenye kwamba hakuna kitu kibaya kitakacho tokea juu yangu, nikaanza kupiga hatau za kwenda kilipo chumba change, nikafika kwenye mlango na kukishika kitasa, nikashusha pumzi na kufungua mlango taratibu.Nikamkuta Phidaya akiwa amekaa kwenye kiti pamoja na mwanamke aliye valia baibui jeusi, huku usoni mwake akiwa amejiziba na kubakisha macho yake, nikawatazama kwa muda huku nao wakinitazama, msichana aliye vaa baibui akajifungua uso wake na kujua kwamba ni Dorecy
"Mbona unashangaa?"
Dorecy aliniuliza huku akinyanyuka kwenye kiti nilicho kikalia
"Hapana"
"Karibu ndani ukae"
Nikapitiliza moja kwa moja na kukaa kitandani mwangu, na kuwatazama Phidaya, aliye nunu na Dorecy ambaye sura yake ipo kawaida tu
"Ninafuraha kukuona tena ukiwa hai Eddy"
"Asante"
"Niliwaagiza watu wangu wakakutafute huko nje, kutoka tulilkuja muda mrefu hatukuona, ila tulivyo wauliza manesi wakadai kwamba upo kwenye maeneo ya viwanja vya michezo"
Dorecy aliendelea kuzungumza huku akiwa amesimama akinitazama kitandani sehemu nilipo kaa
"Ila vipi bado unamaumivu ya vidonda vya risasi?"
"Hapana vimesha kauka"
Ukimya ukatawala ndani ya chumba huku kila mmoja akiwa yupo kimya akimtazama mwenzake aanze kuzngumza.Phidaya akasimama na kutaka kutoka ndani ya chumba ila Dorecy akamkamata mkono
"Shoga yangu ninakuomba utulize hsira usiondoke"
"Sioni sababu ya mimi kuendelea kukaa hapa"
"Ndio ninatambua ya kwamba unahasira sana, ila ninakuomba utulie kwani kuendelea kuwa na hasira haitasaidia kupatana kwenu"
Dorecy aliendelea kuzungumza huku akiwa ameushika mkono wa Phidaya aliye vimba kwa hasira, sikujua ni kitu gani ambacho kimemkasirisha Phidaya hadi ikafikia hatua ya yeye kunichukia kupita maelezo.Phidaya akarudi na kukaa kwenye kiti chake alichokuwa ameka
"Eddy natambua ya kwamba hujui ni kitu gani ambacho kinaendelea kwa wakati huu, ila utaelewa tuu"
"Kwani mke wangu unatatizo gani?"
"Nani mke wako?"
"Haaaa"
Ilinibidi kushangaa tu kwani sikulitarajia jibu kama hili la Phidaya kunijibu mimi, kwaishara Dorecy akaniomba ninyamaze kimya kwamaana ananijua mimi vizuri sana pale ninapokuwa nimekasirika
"Eddy ile siku ambayo ulipigwa risasi kule porini, mume wangu alinichukua mimi pamoja na mtoto, akiamini kwamba wewe umeshafariki.Walinipeleka hadi nyumbani, ila kwa siri sana nilizungumza na hawa walinzi wangu wawili nilio kuja nao huku"
"Walienda kukuchukua kule porini nakunipele kwenye moja ya hospitali pasipo Khalid kugundua kitu cha aina yoyote.Kwa kipindi chote ulipokuwa kwenye hospitali ya siri, ukifanyiwa matibabu ya kuyaokoa maisha yako, niliendelea kulifanyia kazi ombi lako la wewe kumtafuta mke wako, hadi nikafanikiwa kimpata"
Tulinyamaza kimya mimi na Phidaya tukimuacha Dorecy akizungumza,
"Baada ya kukutana na bibie hapa, nilimueleza kila kitu juu yako, na maisha yetu ya nyuma, kitu ambacho sikukijua ni kwamba kunabadhi ya mambo ambayo wewe hukumuadisia mkeo na mimi nikajikuta nikumuadisi"
"Phidaya alikasirika sana, na kukiri kwamba hakufahamu wewe, ila nileiendele kumbembeleza ili asifikie hatua ya kukutenga wewe, nashukuru Mungu kwamba alinielewa, kumbe kunakipindi kunatukio ambalo mulilifana wewe na yeye, ambalo kule Iraq hadi leo munatafutwa na serikali ya kule"
"Ngoja kwanza, tukio la mimi kutoroshwa hospitali ndilo lilolofanya sisi kutafutwa?"
Nilimuuliza Dorecy na kumfanya Phidaya kunitazama kwa jicho kali lililo jaa hasira
"Ndio, ila kuna ishu Khalid alitaka kukufanyia wewe na Phidaya akaiingilia kati na kuwa adui namba mwengine wa Khalid"
"Jambo gani hilo?"
Hata kabla Dorecy hajanijibu tukasikia milio mingi ya risasi kwenye kordo yetu huku kelele za watu wagonjwa na manesi wakike zikisikia jambo lililo tustua sote ndani ya chumba
ITAENDELEA
 
Back
Top Bottom