*****SORY MADAM*****(60)
AGE....................................................................18+
WRITER.............................................................EDDAZARIA G.MSULWA
ILIOISHIA
TUKIWA TUNAENDELEA KUCHAGUA NGUO AKAINGIA MWANAYUME MMOJA AKIWA AMEBEBA MKOBA WA KIKE, AKASIMAMA AKITIZAMA TIZAMA BAADHI YA NGUO, AKATOA SIMU YAKE AMBAYO INAITA NAKUZUGUMZA NA SIMU, KISHA AKAIKATA NA AKASIMAMA AKITAZAMA NJE.BAADA YA MUDA AKAINGIA MDADA ALIYE JITANDA BAIBUI LILILO FUNIKA HADI MACHO YAKE HUKU TUMBO LAKE KIDOGO LIKIWA NI KUBWA AKIONEKANA NI MJAMZITO, DADA HUYO AKAVUA BAIBUI LAKE NDIPO MACHO YANGU YAKAMSHUHUDIA DORECY AKIWA AMESIMAMA KIUVIVU, HUKU MIMBA ALIYO NAYO IKIONEKANA KUMPELEKESHA SANA, NA KWABAHATI MBAYA HAKUNIONA MIMI NILIPO
ENDELEA
Nikamtazama kwa makini jinsi anavyo zungumza na mume wake, hadi Phidaya akanigusa bega
"Mbona unamtazama sana yule dada wa watu?"
"Ninamfahamu"
"Unamfahamu?"
"Ndio"
"Ni nani?"
"Anaitwa Dorecy"
Tulizungumza kwa sauti ya chini huku, tukimtazama Dorecy akichagua chagua nguo na mume wake
"Huyu ndio yule msichana, aliye nipiga na kuondoka na kiasi kikubwa cha madini yangu"
"Ahaaa"
"Ngoja kwanza, nisubiri hapa"
Nilizungumza huku nikizunguka upande wa pili alipo Dorecy na mumuwe, nikajibanza kwenye moja ya kabati lenye nguo, simu ya mume wa Dorecy ikaita na kumlazimu kutoka nje kuzungumza na simu hiyo.Nikapiga hatu za umakini, hadi sehemu alipo simama Dorecy na kumgusa kwa nyuma.Akageuka, na kujikuta akinitazama kwa macho yaliyo jaa mshangao mkubwa kwani hakutarajia kuniona nikiwa katika eneo hili.Nikamvuta hadi kwenye sehemu ambayo si rahisi kwa watu kutuona, hii ni kutokana na wingi wa nguo zilizo pangwa
"Eddy..nisamehe"
"Sikia sina haja ya kuombwa msamaha, ninacho kihitaji ni madini yangu, la sivyo nitalitumbua tumbua hili jitumbo lako kama sikujui"
Nilizungumza kwa sauti nzito iliyo jaa hasira pamoja na msisitizo mkali, mwili mzima wa Dorecy ukawa na kazi ya kutetemeka mithili ya mtu aliyepo kwenye baridi kali sana
"Yaaa, yaapo kulee"
Nikatazama juu kuchunguza kama kuna kamera yoyote ya ulinzi, ila sikuona, nikamtndika Dorecy kofi moja la kumuweka sawa
"Nimekuambia nahitaji madini yangu sawa?"
"Ndio, yapo kwa kule kule kwangu"
"Nitayapataje?"
"Eeheee?"
Nikaona Dorecy anababaika sana na kunipotezea muda, nikamtandika kibao cha pili ambacho nikizoto kuliko hata cha mara ya kwanza, hadi kuna dada mmoja akachungulia, nikajifanya nikimkumbatia Dorecy kama mpenzi wangu, dada aliye chungulia akaachia tabasamu na mimi, nikatabasamu kinafki ili airudishe sura yake alipo itoa.Alipo irudisha nikamuachia Dorecy na kumkuta sura yake imejaa machozi mengi
"Usijidai unalia kinafki, sasa leo nitakuzalilisha mbele ya mume wako"
"Hapana Eddy usifanye hivyo, mume wangu ni mtu mwenye pesa sana, atakudhuru wewe"
"Haaa na anidhuru kwahiyo pesa zake ndio unadhani kwamba ninaziogopa, si ndio"
Nilizungumza kwa hasira huku nikiwa nimeshika kiganja cha mkono wa kuliwa wa Dorecy na kukiminya kwa nguvu zangu zote.Dorecy akaanza kutoa kilio cha maumivu, simu yake aliyo ishika mkono wakushoto ikaita na kuona jina mume wake
"Pokea sasa"
Nilimuamrisha huku nikimuachia mkono, kabla ya kupokea nikamuona mume wake akija nyuma ya Dorecy
"Mumeo huyo hapo, ole wako uropoke"
Dorecy akajifuta machozi haraka, hadi mume wake anafika sehemu tuliyopo, sura yake imejaa uchangamfu wa gafla, wakazungumza kiarabu ambacho sikukielewa, nikashangaa mume wake akinipa mkono huku akiwa na tabasamu
"Eddy huyu ni mume wangu, anaitwa Khalid, nimemuambi kwamba tumesoma wote"
Nikatingisha kichwa, nikilipokea tabasamu la mume wake, tukaachiana mikono, kitu ambacho mume wake alikifanya na kuzidi kuniboa ni kumkumbatia Dorecy kwa nyuma na kuanza kumchezea chezea tumbo lake huku akizungumza maneno nisiyo yaelewa, Dorecy akanitazama machoni, na kugundua nilivyo kasirika
"Anasema, kwamba mtoto nitakaye mzaa atamleta Tanzania"
Dorecy alitafsiri maneno aliyo yazungumza mume wake
"Muambie hatutaki watoto kama wake, na utazaa Zombi kama sijakusoa"
Mume wa Dorecy akatabasamu baada ya Dorecy kumtafsiria nilicho kizungumza, na nina uhakika kwamba Dorecy alicho kizungumza sicho nilicho muambia
"Nataka, madini yangu, la sivyo nitakufanyia oparesheni bila ganzi ya hilo jitumbo lako"
Nilizungumza na kuachia tabasamu pana, kumfanya mume wa Dorecy kuto kuelewa kitu ninacho kimaanisha, nikawapa mikono na kuondoka zangu kurudi sehemuu nilipo muacha Phidaya
"Eddy umemaliza?"
"Ndio, ila kuna kazi nahitaji kuifanya peke yangu"
"Kazi gani?"
"Tutazungumza"
Phidaya akawa amesha maliza kununia alichokuwa anahitaji kukinunua, tukatoka nje na kuingia ndani ya gari
"Usiondoke kwanza, nataka tuwafwatilie Dorecy na mumewe sehenu wanapo ishi"
"Eddy mbona unanipa shuhuli nyingine"
"Zipi?"
"Hizo za kufwatilia hao watu, ujue kwamba tumekuja kutafuta nini huku"
"Powa nipatie pesa nikodo taksi"
"Utapakumbuka ninapo ishi"
"Wewe nipatie pesa"
Phidaya akanipatia kiasi cha kutosha cha pesa, nikashuka kwenye gari na yeye akaondoka, sikucheza mbali na mlango wa duka walipo Dorecy na mume wake, baada ya dakika kumi na tano nikawaona wakitoka kwenye duka, huku mumewe akiwa amebeba mzigo mkubwa wa nguo.Gari ya kifahari yenye milango sita ikasimama pembeni yao, akashuka jamaa aliye valia suti yenus na miwani nyeusi, akawafungulia mlango na wote wakaingia ndani ya gari na wakaondoka
Nikapiga mluzi kwa dereva taksi mmoja aliye kuwa ameisimisha gari yake upande wa pili wa barabara, akaja nilipo simama haraka, na nikaingia ndani ya gari
"Nilugha gani unayo tumia kuzungumza?"
Nilimuulizwa kwa kingereza, dereva taksi ambaye ni mzee wa makomo kidogo na kichwani mwake amejifunga kilemba
"Zote duniani, kiarabu, kingengereza, kiswahili, kichina na kadhalika"
Alinijibu kwa kingereza, nikamuomba alifwate gari la kifahari lilolo ondoka muda mchache sehemu hii, akatii, akafungulia mziki wa kihindi na kuanza kuimba huku akitingisha tingisha kichwa chake
"Mzee hembu kuwa makini na kazi yako. Utaipoteza hiyo gari"
Kijana mimi ile gari naijua hadi sehemu inapo elekea, ni gari la tajiri Khalid Bin Suley, baba yake alikuwa ni gavana wa hili jimbo"
"Kwa hiyo unamjua?"
"Vizuri sana, tangu akiwa mdogo, na nimwezi ulio pita amefunga ndoa na binti mmoja kutoka Afrika"
"Tuachane na hizo habari za ndoa, yeye anafanya kazi gani?"
"Ahaaa yule kijana, ni mshenzi kweli.Tangu baba yaka afariki basi yeye amekuwa ni muuzaji mkubwa sana wa madawa ya kulevya, kutokana ananguvu kubwa, wala hakuna mbweha polisi hata mmoja anaye msogelea"
"Ahaaa"
"Ahaaa, jamaa anamkono mrefu sana, akimtaka mtu kumchomoa duniani basi ni kitendo cha muda mfupi sana"
Maneno ya dereva taksi yakaanza kuniogopesha na kubaki nikiwa ninamtazama kwa umakini, ila nikajipa moyo kwamba shida yangu si yeye bali nimadini yangu tu.Tukaendelea kuifwatilia gari yake kwa ukakini, gafla dereva akaisimamisha gari yake
"Mbona umesimamisha?"
"Kijana hapa ndio mwisho wa mimi kufika, nikivuka tu hicho kibao hapo ujue haturudi"
"Haturudi kivipi?"
"Namaanisha tutakwenda kuuawa huho, ila jumba lake lile pale mbele"
Tukaishuhudia gari ya Khalid ikiingia kwenye gat kubwa ya jumba lake kifahari, hadi inazama ndani, nikajikuta nikishusha pumzi.Sehemu nzima tuliopo imependezeshwa na miti mirefu, pamoja na majani marefu kiasi yaliyo kolea kijani kikali, kiasi kwamba, ukipatazama lazima macho yafarahie mandhari ya eneo zima
"Ndio hivyo tena, gari imesha zama ndani kijana sasa sijui tunarudi pamoja, au unataka kwenda kudumbukizwa kwenye bwawa la mamba?"
"Turudi?"
Dereva taksi akasigeuza gari lake taratibu, kabla hajaliweka sawa barabarani, gari mbili nyeusi zikasimama barabarani na kuifunga barabara
"Ohoo nilikuambia kijana"
Dereva taksi alizungumza huku akianza kutetemeka mwili mzima.Wakashuka watu sita walio valia suti nyeusi huku mikononi mwao wakiwa na bunduki aina ya short gun.Mzee wa watu akaanza kuomba sala yake ya mwisho huku kajasho kembaba kakimwagika.Jamaa mmoja akaanza kupiga hatua za kuja lilipo gari letu, na kutuomba tushuke ndani ya gari, huku mikono yetu ikiwa juu.Nikajikuta nikiwa ninajiamini kupita maelezo, nikafungua mlango na kutoka nje huku mikono yangu ikiwa nimeinyoosha juu, akafwatia dereva taksi naye akafanya kama nilivyo fanya mimi
"Nyinyi ni kina nani?"
Jamaa alituuliza kwa lugha ya kingereza
"Sisi ttumepotea njia tu"
Nilimjibu jamaa kwa kujiamini, kiasi kwamba nikawa nimejiandaa kwa chochote ambacho kitakwenda kutokea.Jamaa akanisogelea na kuanza kunipapasa kuanzia chini hadi juu, akatoa kiasi cha pesa nilicho kuwa nacho mfukoni na kukitupa pembeni
"Inama kwenye gari"
Aliniamuru na nikafanya hivyo bila ya wasiwasi wa aina yoyote, nikamtazama mzee wa watu jinsi anavyo tetemeka hadi haja ndogo ikaanza kulowanisha surali yake aina ya panjabi aliyo ivaa.Jamaa akaanza kumpapasa mzee wa watu, hawakumuona na kitu chochote
"Ingieni kwenye gari lenu na muondoke haraka sana"
Asante sana baba yangu"
Mzee alijibu kwa haraka na kuingia kwenye gari, nikataka kuokota pesa zangu ila jamaa akanizuia na kuniamuru niingie kwenye gari huku akiwa ameninyooshea bunduki yake, wakazitoa gari zao barabarani na sisi tukaondoka, kwa mwendo wa kasi, njia nzima tukawa kimya, macho yangu nikayashusha sehemu ya mbele ya mzee wa watu na kujikuta nikianza kuchake kimoyomoyo
"Kufa kubaya?"
Nilijisemea huku nikicheka, hata mziki ambao mzee alikuwa anausikiliza akaona unampigia kelele, akaizima redio yake.Nikashangaa kuona mzee akisimamisha gari yake kwenye duka ambalo nilikuwepo
"Shuka kijana kwenye gari yangu, sitaki tena oda yako ya safari"
Mzee alizungumza huku akibabaika, nikashuka kwenye gari, hata pesa hakunidai, akaondoka kwa kasi na kutokomea mbele ya macho yangu.Nikabaki nikiwa nimesimama sikujua ni wapi nielekee, nikastukia nikiguswa bega kwa nyuma kugeuka nikakutana na Phidaya
"Wewe si umeondoka, mbona upo hapa?"
Phidaya alizungumza huku mkononi akiwa ameshika mfuko wa nguo zangu
"Nimerudi bwana"
"Una bahati kweli, nilisahau huu mfuko wako wa nguo, sijui ungerudije nyumbani na ubishi wako"
Phidaya akaita taksi na sote tukaingia ndani ya gari
"Gari umeiacha wapi?"
"Nimeiacha gereji, ina badilishwa rangi na kuwekwa kioo cha nyuma kipya"
"Umeshanunua hivyo vitu?'
"Ndio, vyote vipo kwenye gari"
Tuakfika hadi gereji na kukuta gari ikimaliziwa kufungwa kioo cha nyuma, huku rangi ikiwa imesha malizwa kupakwa
"Hii gereji ninaipenda kutokana huduma zao ni zaharaka, pia wanamitambo mingi"
"Ahaaa, ila ni kubwa"
"Ndio, vipi ulifanikiwa kufika lilipokuwa linakwenda lile gari?"
"Ndio, ila hatukufika kwenye jumba lenyewe, tulisimama kwa mbali"
Sikumuambia Phidaya kitu kilicho tupata kwa maana ningempa wasiwasi mwingi.Tukasubiri kwa masaa mawili, rangi iliyo pakwa kukauka, tukakabidhiwa gari yetu ikiwa katika muonekano mzuri na wakupendeza, tukaingia ndani ya gari safari ya kurudi nyumbani ikaanza
***
Nikaanza kuchukua mazoezi yangu binafsi, ya kuuweka mwili sawa, sikutaka kumuambia Phidaya lengo la mimi kufanya mzoezi hayo, kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyo jisni mwili wangu ulivyo zidi kuwa mwepesi na kuhimarika kwa mazozi, nikaingia kwenye mazoezi ya matumizi ya bunduki, katika kulenga shabaha, hadi nikajiamini kwa matumizi ya silaha
"Eddy mbona kipindi hichi unajiweka bize kwa mazoezi hadi naogopa"
Phidaya alizungumza huku akinipa taulo, nijifute jasho linalo nimwagika baada ya kufanya mazozi makali ya kupiga push up na kukimbia kwenye milima muda huu wa asubuhi
"Mwanaume siku zote ni mlinzi wa mwanamke, na ninatakiwa kukulinda mke wangu"
"Mmmm kweli?"
"Ni kweli, ndio"
Phidaya akanivuta karibu yake na kunikumbatia kwa furaha huku akitoa mihemo mizito
"Ninafurahi kuwa na mume kama wewe"
"Hata mimi ninafurahi kuwa na mke kama wewe"
"Ila Eddy kuna kitu nahitaji kukuambia"
"Kitu gani?"
"Nimeanza kuziona dalili za ujauzito"
"Kweli….!!?"
"Ndio"
Ni habari nyingine mpya ya kunifurahisha kwenye maisha yangu, kwani kitu ambacho kitanipa furaha kwenye maisha yangu ya baadaye ni mtoto
"Itabidi uende kwa Tanzania, ukailee hiyo mimba"
"Eddy….niende Tanzania nikafanya nini?"
"Uende ukailee hiyo mimba, sitaki mwanagu azaliwe hapa"
"Na wewe?"
"Mimi nitakuja, pia ninataka ukaagalie hali halisi ya usalama Tanzania kwamba ninatafutwa au laa"
"Eddy siwezi kwenda sehemu yoyote bila ya kuwa na wewe, kumbuka nimeacha kazi kwa ajili yako, na hii hali nahitaji kuwa nawe karibu kila mara na kila dakika"
Hatukufikia muafaka na Phidaya, na akakataa kabisa kurudi Tanzania.Usiku wa saa nne baada ya Phidaya kulala, nikaamka taratibu kitandani, nikachukua bastola yangu na kuhakikisha ina risasi za kutosha, nikavaa nguo nyeusi ambazo si rahisi kwa usiku kuonekana vizuri pamoja na saa yangu ya mkononi, kisha nikachikua na koleo(playz).Kitu kilicho anza kunichelewesha ni funguo ya gari, ambayo sikujua ni wapi ilipo
"Huu mwanamke ameiweka wapi hii funguo?"
Nilijiuliza huku nikiendelea kuitafuta kwenye droo ambazo nilihisi inaweza kuwepo, nikatoka nje bila ya Phidaya kugundua kitu chochote, nikafungua kweye gari kwa bahati nzuri nikaikuta funguo ikiwa kwenye gari.Kuhofia Phidaya kusikia mlio wa gari, nikaanza kuisukuma taratibu hadi nikafika umbali kidogo wa shamba lilipo.Nikaingia kwenye gari na kuiwasha na kuondoka, safari ya kuelekea kwenye jumba analo ishi Dorecy na mumewe ikaanza huku njia nzima nikiwa ninahasira kali iliyo zidi kunisukuma kuliendesha gari kwa kasi kuwahi kufika katika jumba hilo
Nikaisimamisha gari yangu kwenye kichaka kimoja, mbali kidogo na lilipo jumba hilo, nikashuka na kuanza kutembea msituni kwa kujiamini huku nikiwa makini sana, mwanga wa mbalamwezi ndio ulio nisaidia kuona mbele na shemu ninayo kanyaga.Nikafanikiwa kufika kwenye fensi ya nyaya, nikatoa kuleo na kuanza kukata moja baada ya nyingine hadi nikapata upenyo wa mimi kupita.Nikaendele kutembea hadi kwenye ikuta mrefu kiasi, nikatazama pande zote na sikuona dalili ya kumuona mtu.
Nikarudi nyuma, nikavuta kasi ya kupanda kwenye ukuta, kutokana na wepesi wa mwili wangu, halikuwa zoezi gumu la mimi kupanda juu ya ukuta huu, nikajivuta hadi nikafikia juu kasisa ya ukuta na kujilaza ili nisionekane, hapo ndipo nilipoanza kuona eneo zima la jumba la Khalid likiwa limetawaliwa na taa nyingi pamoja na ulinzi mkali wa askari walio na mbwa pamoja na bunduki nyingi.Nikamshuhudia mtu mmoja akiwa anapigwa na walinzi wapatao watano huku pembeni akiwa amesimama Khalid na Dorecy.Mtu huyo aliendelea kuomba msamaha ila walinzi hao hawakumsikiliza zaidi ya kuendelea kumshushia kipigo kitakatifu
Khalid akachomoa bastola yake na kumnyooshea mtu huyo, ila kabla hajafyatua akamkabidhi Dorecy bastola na kumuomba amuue mtu huyo, Dorecy bila ya huruma akafyatua risasi zilizo tua juu ya kichwa cha mtu huyo na kumsababishia kifo, nikashusha pumzi nyingi, kwani Dorecy amekuwa katili kiasi cha kuua mtu pasipo kuwa na huruma ya aina yoyote, nikiwa nifikiria cha kufanya nikastukia kitu kigumu kikinigusa kichwani mwangu, na kusikia sauti ya mwanaume ikiniamrisha nilale kama nilivyo na nisifanye kitu chochote la sivyo atauchangua ubongo wangu, taa kubwa lenye mwanga mkali likageukia sehemu ya sisi tulipo, juu ya ukuta na kuwafanya Khalid, Dorecy na watu wake kutuona.Na Khalid akaagiza mtu huyo kunishusha kwenye ukuta.
ITAENDELEA