Mkuu FMES,
Nimeeleza kuwa kuna mambo mawili ambayo siafikiani nayo kwenye hiyo makala ambayo ni sababu za kukosana hawa wawili, na sababu ya kurudi nyumbani bila shahada. Nakumbuka kusoma maandiko yako siku za nyuma na nakubaliana na wewe kuwa Kambona alikamatwa na masanduku yaliyosheheni dola za US pale Nairobi lakini mwalimu akaruhusu wamwache aende zake. Mbali na kazi yake, hakuwa na shughuli nyingine yoyote ambayo ingehalalisha utajiri aliojipatia haraka haraka. Sasa kama kuzuia wizi mwalimu alikuwa anazuia maendeleo ya wananchi, hiyo iko juu ya uelewa wangu. Kwangu mimi kilichowakosanisha ni ufisadi ambao rangi yake ni sawa kabisa na huu unaopigiwa kelele na kina Slaa ambao sijui kama ni waumini wa azimio la Arusha. Fisadi ni fisadi tu, awe Balali, Nyerere, Kambona...
Kuhusu kurudi bila shahada, naamini kuwa wewe FMES una access ya information toka kwenye sources ambazo ni very reliable. Ukifanya utafiti kidogo utagundua kuwa huyu bwana masomo yalimshinda. Sina sababu yoyote ya kumchukia huyu mzee, lakini nasikitika sana ukweli unapogeuzwa kuwa uongo na uongo kuwa ukweli. Mwalimu anayo madhambi yake na moja ni lile la kukumbatia watu wakiharibu sehemu moja na kupelekwa sehemu kuharibu sehemu nyingine. Lakini pia lipo lile la kutorudi nyuma baada ya kumchukia mtu.