Tetesi: Hotel ya Ryan Bay Mwanza kubomolewa

Ngoja nikitoka hapa kibaruani kwangu saa tisa na nusu nitapita hapo kupata uhakika.
Hoteli ina bei kubwa ya vyakula, vinywaji na vyumba!!
Nitaleta mrejesho leo hii hii
mie ndie CHIKIRA MTABARI mmbeya mwandamizi katika jiji la Miamba
...Pia usisahau kama ina uhusiano wowote makamanda wa CDM
 
Yaani maajabu haya unayaona kwetu tu eti vunja kupitisha mradi mwingine.
Only in TZ
Ni uonezi kama ni kweli.
Kwanini tusijifunze dunia zingine au Ina maana hawa mawaziri hawajaona wanapokwenda nje ya nchi.

Nikiwa napita Cornwall huwa najiuliza kwanini tuna roho mbaya?
48ccc79b364aa695346ed393ad549257.jpg
 
...Pia usisahau kama ina uhusiano wowote makamanda wa CDM
ndugu si kila jambo ulipeleke kisiasa. kama umejenga ndani ya eneo la miundo mbinu ya barabara n.k utabomolewa tu. ndiyo maana watabomoa vic fish ambacho ni kiwanda wala hakihusiana na CDM ama CCM. ukiwa unawaza siasa tu kila muda utakuwa haupo sahihi.
 
Mimi naona hiyo reli wange ipeleka nje ya mji kidogo mfano buhongwa ili kutanua mji na maendeleo maana jiji la mwanza linazidi kuongezeka pia huko buhongwa kuna tambarare
 
Wanajukwaa kwa masikitiko makubwa, habari zisizo rasmi "tetesi" ni kuwa Hotel ya kitalii ya RYANS BAY iliyopo jijini Mwanza itabomolewa kupita eneo la Reli.

Mwenye habari kamili atuhabarishe...

Mbona iko umbali mrefu kutoka railway station? Ni zaidi ya mita 60.
Chikira utanisaidia kama nimekosea.
 
Wakidaivert kwa akili yao wanaona reli itavunjika

Wangeidivert na mwenye hotel achangie gharama, ila jamani ndo maana huwa tunarogwa watumishi wa umma unazeeka domo limepinda hukoo , we fikiri hao watu wa ardhi waliomuuzia hilo eneo halafu jamaa angie hasara hiyo,hata mimi ningemtoa mtu roho aisee
 
Mimi naona hiyo reli wange ipeleka nje ya mji kidogo mfano buhongwa ili kutanua mji na maendeleo maana jiji la mwanza linazidi kuongezeka pia huko buhongwa kuna tambarare
reli inaenda kigoma hiyo haiishii hapo mwanza
 
Wangeidivert na mwenye hotel achangie gharama, ila jamani ndo maana huwa tunarogwa watumishi wa umma unazeeka domo limepinda hukoo , we fikiri hao watu wa ardhi waliomuuzia hilo eneo halafu jamaa angie hasara hiyo,hata mimi ningemtoa mtu roho aisee
Unadivert vipi train ya umeme kwenye kaplot kadogo hivyo??? Alignments za standard gauge ni tofauti na metre gauge ile train ili kuwa na high speed sharti number moja ni lazima inyooke no corners no pumps.
 
Hapo serikali ichangine gharama aiseee,, huu siyo uungwana haki ya nani!! Wamlipe 90% ya usumbufu wa kuuziwa eneo lisilo!!
 
Unadivert vipi train ya umeme kwenye kaplot kadogo hivyo??? Alignments za standard gauge ni tofauti na metre gauge ile train ili kuwa na high speed sharti number moja ni lazima inyooke no corners no pumps.
Kwani steshini ya standard gauge lazima iwe katikati ya mji? Waiache huko Mwanza south huko kuwe na terminal kubwaaaa watu wanashukia huko wanapanda mwendo kasi!!
 
hahahahah, sasa misosi shost si mpaka niagize! misosi ya pale bei iko juu utadhani unanunua sijui kitu gani tu! Pale huwa ninaenda kama "nina offer" sio pesa yangu. hahahahahahahahahahah
Umenikumbusha enzi hizo niko mwnz ndo bado mpya mpya tumeenda hapo bwana jioni jioni nkaagiza sambusa skumbuki bei halisi ila ilinishtua.
 
Unadivert vipi train ya umeme kwenye kaplot kadogo hivyo??? Alignments za standard gauge ni tofauti na metre gauge ile train ili kuwa na high speed sharti number moja ni lazima inyooke no corners no pumps.

Okey
 
Kwani steshini ya standard gauge lazima iwe katikati ya mji? Waiache huko Mwanza south huko kuwe na terminal kubwaaaa watu wanashukia huko wanapanda mwendo kasi!!
Station ya mwanza bado ni kubwa mno Inahitaji eneo kidogo la kuongeza kuliko kuanzisha station mpya nyingine
 
Back
Top Bottom