Hoteli ya nyota Tatu inajengwa Chato, Wana-CCM mnafurahishwa na kitendo cha kupeleka kila mradi wa ujenzi Chato?

akina Mabutu bado wapo hai aisee !!
 
Kujenga hoteli ya nyota tatu ni kitu kimoja. Lakini kuwapata watalii wa kuweza kulala hapo ni kitu kingine kabisa na hasa hali hii tuliyo nayo ikiendelea ilivyo.
Ngoja tuangalie huenda chini ya kapeti wana kampango fulani hivi amazing kuleta watalii wa kulala hapo
 
Safi sana Magufuli. Uzalendo huanzia nyumbani. Kama wengine hawakuona umuhimu wa kwao hilo ni tatizo lao. Kuna mmoja sasa hivi marehemu alihama mpaka kwao akaenda kuijenga kwa wenzake. Wamemrudisha kwao akiwa ni mfu. Sasa hiyo ndiyo akili?! After all huko nako ni Tanganyika tukawahi viwanja jamani
 
Kwio.

Tano tena
 
Sawa kama hili ni sahihi kufanyika , basi ifike mahali tuwe na utaratibu huu , Tz tuna mikoa kaa 26 hivi ( kama sijakosea ) . kila mkoa utoe raisi basi ili kunyanyua maendeleo ya mkoa husika .

Ukweli mambo anayoyafanya mwenzetu yanachukiza tena yanaleta ubinfsi na ukanda wa hali ya juu .
Kwa hali hii sitoshangaa raisi ajae naye akaporomosha viwanja vya ndege , viwanda na barabara za viwango vya juu au kufanya uwekeza mkubwa usio na tija kwa taifa sehemu aliyotokea. Maana kila mtu anaona mambo anayofanya huyu bwana .
 
Hii hoteli ni muhimu sana,hasa kimkakati maana kila rais akienda huko itajaza wageni balaa
 
Ni swali tu ' hivi ile hospitali yenye hadhi ya hospitali ya Taifa ya Muhimbili ipo wilaya na mkoa gani nchini Tanzania?

Tuwe tunakumbuka yaliyotendeka awamu zilizotangulia kwa ajili ya hoja kuntu. Hakuna dhambi wala kosa lolote kupeleka miundo mbinu ya hospitali, hoteli za kitalii, huduma za kibenki na mambo mengine kama hayo Chato; Chato nayo ni sehemu ya Tanzania na kwa Kiongozi Mkuu wa Nchi yetu. Rais ameekeza katika maeneo mbalimbali kama vile hospitali, miundo mbinu ya Barabara na reli, umeme mfano SGR na bwawa la Mwl. Nyerere maarufu kama stiglers gorge, hospitali za rufaa za mikoa na wilaya, vituo vya afya, interchange za mfano kama ubungo interchange na miundo mbinu mingine muhimu nchi nzima. Cha ajabu na kinachosikitisha ni kwamba miradi hii mikubwa na iliyobadilisha taswira ya Tanzania ilipoanza kutekelezwa ilikumbumbana na upinzani toka kwetu sisi tunaopenda kupinga kila jambo bila sababu za msingi na yakinifu. Hima JPM songa mbele ukikumbuka kuwa mti wenye matunda ndio hushambuliwa na amini kuwa ukistaafu utasikia maneno kama ''nafuu JPM mara tumemkumbuka JPM".
 
Kidogo niseme kinachokuwasha nini? Nikidhani huyo ni mtu binafsi, hata angekuwa rais mwenyewe! Ila hili kufanywa na serikali kwa kweli limevuka mpaka. Hongera watu wa Chato. Mtakuwa Wilaya ya kwanza Tanzania kuwa na employment 100%
 
Yaelekea huna ufahamu. Hivyo ulivyovitaja kujengwa sehemu mbali mbali ni kwa vile vinahitajika zaidi huko na metokea baada ya majadiliano na kuonekana viwekwe huko. Zaidi ya hayo, vingi ni aidha ilani ya Cham au mipango ya serikali ya siku nyingi ikingojea pesa.
Ndiyo tofauti na hili ambalo dhahiri linafanyika kwa utashi wa mtu mwenye nguvu na Mwaziri kutaka kujipendekeza. Hatuna sababu yeyote ya kuichukia Chato. Chato ni Tanzania. Ila uwazi lazima uwepo. Bada ya miaka 60 ya Uhuru hata kusema hatuwezi?
 
Asipofanya hivyo majengo mengi Chato yatageuka magofu ndani ya miaka 5 baada ya kutoka.
 

Niko Mapogoro nawatibu hata Corona
 
Yatabaki kama magofu nakwambia, time will tell!
 
Ujasema hospital gani kuwa wazi au unamaanisha mloganzila hospital Kama ni hii ipo kibamba daressalaam.na lililokuwa jiji halijatoa RAIS.kinachowatatiza watu ni mfulilizo wa miradi ktk WILAYA moja.hapo tunajiaanda na ujenzi wa chuo Cha utumishi wa umma soon mh Mkuchika atatembelea mradi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…