Hoteli ya nyota Tatu inajengwa Chato, Wana-CCM mnafurahishwa na kitendo cha kupeleka kila mradi wa ujenzi Chato?

Hoteli ya nyota Tatu inajengwa Chato, Wana-CCM mnafurahishwa na kitendo cha kupeleka kila mradi wa ujenzi Chato?

Tena kwa lipi? Maana duniani kote watalii wana kwenda kuona Kilimanjaro, Ngorongoro, Meru, Serengeti na Zanzibar tu! Wakienda Rwanda wanafuata hivyo, wakienda Malawi ni kuona Kilimanjaro tu! Chato wanafuata nini?
Hiyo hoteli ingejengwa Kilimanjaro au Arusha, kwa nini Chato?
Miaka mingi sana kulikuwa na mpango wa kujenga Hotel ya Nyota Tano maeneo ya KIA ili Watalii wakija Kanda ya Kaskazini wafikie kwenye Hotel hiyo ndo waende Mbugani au Kilimanjaro na waondokee hapo. TANAPA wanajua mpango huo lakini walivyo na Akili finyu za kuongeza wanakwenda kujenga Chato ambako itachukua miaka 50 kufikia hali ya Mbuga ya Arusha, ndogo kuliko zote nchini. Burigi ni Mbuga kubwa lakini wanyama wadogowadogo waliohamashiwa huko mpaka wawe wengi kama Tarangire itachukua hata miaka 100 wasipomalizwa na Simba na Wasukuma. Kwa sababu Arusha hakuna Hotel za Nyota 5 za kutosha, Watalii wengi wanafikia Nairobi ndo waje kwetu kwa magari na waondokee tena Nairobi. Maviongozi wetu yalivyo majinga yanalalamika Wakenya wabaya wanadai vivutio vyetu vya Watalii ni vyao, Mtalii toka Ulaya mpaka Nairobi, City in the Sun toka pale apelekwe Kilimanjaro au Serengeti halafu arudishwe Nairobi aondokee Uwanja uleule mkubwa kuliko yote Afrika Mashariki, akifika kwao eti aseme alikuwa Tanzania. Kwani nyie Watanzania pamoja na ujinga wenu mkitangazia ulimwengu kuwa Nairobi ni Jiji lenu na likawa linawaingizia fedha kuna shida gani kama hamjalihamisha? Biashara ni akili siyo sawa na kuchunga mifugo!
 
View attachment 1715798
Maelezo ya Picha: Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja(Kulia) akikagua hoteli ya nyota tatu inayojengwa na Hifadhi za Taifa Tanzania inayojengwa Wilayani Chato mkoani Geita.
Mwalimu Nyerere akijua kabisa kuwa kuku wa taifa lazima aliwe na wote, aliamua almasi inayochimbwa Shinyanga Mwadui ikakatwe Iringa, ili Wanyalu nao wafaidike na madini hayo.

Hakupeleka kiwanda Cha Tancut Almasi Mara wala Butiama.
Magufuli amekuwa ni mtu wa kupendelea kwao tu utadhani Tanzania ni Chato tu.

1. Uwanja wa ndege mkubwa umejengwa Chato
2. Wanyama wamesombwa huko Serengeti, wamepelekwa Chato.
3. Uwanja mkubwa wa michezo kujengwa Chato.
4. Hospitali ya Kanda ya Ziwa imejengwa Chato.
Je, wanaccm mmeshindwa kukemea upendeleo huu?

Mjulisheni Mwenyekiti wenu kuwa anachokifanya sio uzalendo, ila ni ubaguzi. Anawabagua watu wasio wa Chato.

Kuku wa Taifa lazima aliwe na wote, hata watu wa Ileje na Tandahimba wanahitaji kwao kujengwe, sio kila kitu Chato tu
Huko kumejaa fisi tupu,hujaona juzi wananchi wameua fisi 28 geita,hiyo hotel watalala fisi
 
WaTanzania tunachezewa akili mwaka huu mpaka zikae sawa
 
Waziri anatetea tumbo.The guy is there for is own life not people's life
 
View attachment 1715798
Maelezo ya Picha: Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja(Kulia) akikagua hoteli ya nyota tatu inayojengwa na Hifadhi za Taifa Tanzania inayojengwa Wilayani Chato mkoani Geita.
Mwalimu Nyerere akijua kabisa kuwa kuku wa taifa lazima aliwe na wote, aliamua almasi inayochimbwa Shinyanga Mwadui ikakatwe Iringa, ili Wanyalu nao wafaidike na madini hayo.

Hakupeleka kiwanda Cha Tancut Almasi Mara wala Butiama.
Magufuli amekuwa ni mtu wa kupendelea kwao tu utadhani Tanzania ni Chato tu.

1. Uwanja wa ndege mkubwa umejengwa Chato
2. Wanyama wamesombwa huko Serengeti, wamepelekwa Chato.
3. Uwanja mkubwa wa michezo kujengwa Chato.
4. Hospitali ya Kanda ya Ziwa imejengwa Chato.
Je, wanaccm mmeshindwa kukemea upendeleo huu?

Mjulisheni Mwenyekiti wenu kuwa anachokifanya sio uzalendo, ila ni ubaguzi. Anawabagua watu wasio wa Chato.

Kuku wa Taifa lazima aliwe na wote, hata watu wa Ileje na Tandahimba wanahitaji kwao kujengwe, sio kila kitu Chato tu

===

Naibu Waziri wa Utalii Mary Masanja akagua miradi ya utalii Geita​


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja amefanya ziara katika Mkoa wa Geita ambapo pamoja na mambo mengine amekagua miradi mbalimbali ya kiutalii inayotekelezwa na taasisi za Wizara ya Maliasili na Utalii mkoani humo, anaripoti John Bera (WMU) Geita.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (katikati) akiwasili kukagua hoteli ya Nyota 3 ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania ( TANAPA) inayojengwa wilayani Chato mkoani Geita wakati wa Ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi mbalimbali ya Wizara ya Maliasili na Utalii ya mkoani Geita. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Chato, Eng. Charles Kabeho na kulia ni Kamishna Mwandamizi wa Uhifadhi Kanda ya Magharibi, Martin Loibooki.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (kushoto) akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhe. Robert Gabriel kuhusu mpango wa Wizara ya Maliasili na Utalii wa kutaka kuanzisha Utalii wa Madini katika mkoa huo wakati wa Ziara yake ya Kikazi mkoani humo.

Akiwa katika ziara hiyo amefanya mazungumzo na viongozi wa Serikali wa mkoa na wale wa taasisi zilizo chini ya wizara kuhusu namna bora ya kutangaza vivutio vya utalii vinavyopatikana katika mkoa huo.

Aidha, Mhe. Masanja ametembelea Mradi wa Ujenzi wa hoteli ya Kitalii ya Nyota 3 inayojengwa wilayani Chato mkoani Geita na kuagiza ujenzi wa hoteli hiyo ukamilike haraka ili watalii waanze kupata fursa ya kutumia huduma za malazi katika hoteli hiyo na kutembelea hifadhi mbalimbali zilizopo Kanda ya Ziwa.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (kulia) akiwa anashuka kwenye hoteli ya Nyota 3 ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania ( TANAPA) inayojengwa wilayani Chato mkoani Geita wakati wa Ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi mbalimbali ya Wizara ya Maliasili na Utalii ya mkoani Geita. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Chato, Eng. Charles Kabeho.

Amesema, Wizara ya Maliasili na Utalii itaendelea kushirikiana na uongozi wa Mkoa wa Geita kuhakikisha shughuli za utalii zinasonga mbele huku akitoa rai kwa viongozi hao kuweka mkazo katika zao la asali ambalo amesema likisimamiwa vizuri litaongeza mapato.

"Tuhamasishe zao la asali linalotokana na nyuki, sasa hivi kuna mnyororo mkubwa wa thamani ambao Serikali inaendelea kuupigania kwenye mazao ya misitu, hii itasaidia wananchi kuongeza kipato pia pato la Taifa,"amesema Mhe.Mary.
Aidha, ameongeza kuwa Wizara ya Maliasili na Utalii iko katika mpango wa kuanzisha Utalii wa Madini ambao kwa Kanda ya Ziwa utasaidia kuongeza idadi ya watalii na mapato.
Ni kweli inakera sana
 
Akili Utopolo ndio hizi Serengeti na Tarangire hifadhi zinazoingizia TANAPA mapato ya kutosha kwa miaka kadhaa wadau wamekua wakiiomba TANAPA ijenge hotels ili kuwezesha Mtanzania wa kawaida aweze pata huduma za malazi yaliyobora. Ila hakukua na kitu kama hicho zaidi ya public campsites ambazo usalama ni zero ila leo wanaenda kufanya uwekezaji sehemu ambayo hata kujiendesha kwa faida haijaanza. Huu ni zaidi ya Utopolo.
Haswaaaa, ni ujinga mkubwa. Mobutu style.
 
Mbunge ndio financer? Niko hapa Isoko, na ninatembea almost kila Kijiji kwa ajili ya biashara zangu za minadani, usafiri ni wa hovyo, maji hamna, huduma za afya ni za hovyo, watu wanatolewa hospital wanapelekwa kwa waganga na kwenye maombezi.

Hiyo miradi iko wapi? Sisi watu was pande hii tumeikosea nini serikali?

Mnasema wapinzani wametuchelewesha Sana. Mbona hili Jimbo halijawahi kuwa chini ya upinzani?
Utawala wa jiwe ni utopolo mtupu. Hauna tofauti na wa Mobutu.
 
Labda mbunge ni mbwiga hujawaona wenzake Taletale wa Morogoro na Mtemvu wa Kibamba walivyochangamka!
Mkuu Wa mkoa Wa mbeya anasimamia miradi ya kuhakikisha zahanati zote zilizojengwa zinapata wagonjwa Wa kutosha kwa kuwa zilijengwa kwa ajili yao .
 
Mbuga ya Arusha, ndogo kuliko zote nchini.
Uongo. Saa Nane, iko Mwanza.
Kwa sababu Arusha hakuna Hotel za Nyota 5 za kutosha, Watalii wengi wanafikia Nairobi ndo waje kwetu kwa magari na waondokee tena Nairobi. Maviongozi wetu yalivyo majinga yanalalamika Wakenya wabaya wanadai vivutio vyetu vya Watalii ni vyao, Mtalii toka Ulaya mpaka Nairobi, City in the Sun toka pale apelekwe Kilimanjaro au Serengeti halafu arudishwe Nairobi aondokee Uwanja uleule mkubwa kuliko yote Afrika Mashariki, akifika kwao eti aseme alikuwa Tanzania.
Hii hapa umeshangilia mno hadi ikakutoa akili zote.

Wewe husikii shemeji zako hao vilio vyao wanapozuiwa kuingia huku?

Ulianza vizuri, kwa kuwashutumu viongozi wasiokuwa na dira kichwani, lakini ukapitiliza hadi kuwa kama mshangiliaji wa ubovu huo!
Kwani nyie Watanzania pamoja na ujinga wenu mkitangazia ulimwengu kuwa Nairobi ni Jiji lenu na likawa linawaingizia fedha kuna shida gani kama hamjalihamisha?
Ona unavyokuwa mtupu kichwani. Tanzania inauhitaji gani na kuwa tapeli kama mlivyo huko kwenu. Hapa hatuna uhitaji wa namna hiyo. Tatizo ni hawa maviongozi tu, lakini Arusha pekee inatosha kuikabili hiyo Nairobi yako.
Biashara ni akili siyo sawa na kuchunga mifugo!
Unaendelea kujionyesha ukilaza. "Kuchunga mifugo" kwa akili yako unadhani hakuhitaji akili? Kwani biashara hakuna zinazoshindwa kwa kukosa akili kwa wanaoziendesha; kama ilivyo kwa wafugaji wanaofanikisha ufugaji kwa kutumia akili?

Bure kabisa.

Mwisho nimekudharau.
 
Back
Top Bottom