Hoteli ya nyota Tatu inajengwa Chato, Wana-CCM mnafurahishwa na kitendo cha kupeleka kila mradi wa ujenzi Chato?

Hoteli ya nyota Tatu inajengwa Chato, Wana-CCM mnafurahishwa na kitendo cha kupeleka kila mradi wa ujenzi Chato?

Ni swali tu ' hivi ile hospitali yenye hadhi ya hospitali ya Taifa ya Muhimbili ipo wilaya na mkoa gani nchini Tanzania?

Tuwe tunakumbuka yaliyotendeka awamu zilizotangulia kwa ajili ya hoja kuntu. Hakuna dhambi wala kosa lolote kupeleka miundo mbinu ya hospitali, hoteli za kitalii, huduma za kibenki na mambo mengine kama hayo Chato; Chato nayo ni sehemu ya Tanzania na kwa Kiongozi Mkuu wa Nchi yetu. Rais ameekeza katika maeneo mbalimbali kama vile hospitali, miundo mbinu ya Barabara na reli, umeme mfano SGR na bwawa la Mwl. Nyerere maarufu kama stiglers gorge, hospitali za rufaa za mikoa na wilaya, vituo vya afya, interchange za mfano kama ubungo interchange na miundo mbinu mingine muhimu nchi nzima. Cha ajabu na kinachosikitisha ni kwamba miradi hii mikubwa na iliyobadilisha taswira ya Tanzania ilipoanza kutekelezwa ilikumbumbana na upinzani toka kwetu sisi tunaopenda kupinga kila jambo bila sababu za msingi na yakinifu. Hima JPM songa mbele ukikumbuka kuwa mti wenye matunda ndio hushambuliwa na amini kuwa ukistaafu utasikia maneno kama ''nafuu JPM mara tumemkumbuka JPM".
Unaijua Butiama?! Ni makao makuu ya wilaya, ambako mwasisi wa taifa letu katokea, nipe orodha ya miradi na thamani kwa miaka 5 iliyopita linganisha.Yanayofanyika Chato ni maamuzi magumu na ya kipekee.
 
Kila mradi Chato kivipi? Hizi barabara za sinza, mwenge, mbezi, stieglers gorge, stands mpya kila mkoa, nazo zipo Chato?
Nitajie wilaya zaidi ya chato waliohamishia wanyama kwa ma malory ili kuanzisha mbuga ya wanyama.Ukimaliza taja na wilaya zilizojengwa viwanja vya ndege kwenye awamu hii ya tano
 
Wacha apeleke tu. Mimi nikiwa Rais 2030 yanayofanyika Chato yataonekana takataka. Ni Kweli huko kwetu Usoke, Tabora nitaweka yote yaliyowekwa Chato ie internaional airport, hospital ya rufaa, uwanja wa michezo, mbuga ya wanyama, n.k. Huyo wa Chato nitamzidi kwa yafuatayo:
1. Nitafikisha SGR hapo
2. Chuo Kikuu
3. Bandari.
Ndiyo, bandari! Nitachimba mfereji mkubwa wa kupitisha meli kutoka pwani ya bahari ya Hindi hadi Usoke. Kama mfereji wa Suez au wa Panama ulijengwa basi hata wa Usoke unaweza kujengwa, elevation ya Usoke above sea level notwithstanding. Hapo ndo ulimwengu utashangaakuhusu engineering feat ya watanzania. Tena nitajitahidi kijiji cha usoke kiwe jiji nani y miaka 10. Nikione miaka 10 inaisha lengo langu halijafanikiwa, nitapiga ndogo ndogo niongezewe miaka mingine, ili flagship projects zangu zikamilike. Charity begins at home!
 
Hayo mahotel yatageuka kuwa magofu mara tu atakapotoka madarakani.

Mtalii gani ataenda CHATO? Kwa lipi?
Dah.....atoke kwenda wapi? ,[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji2960]
 
Ulivyotaja Tancut Almasi tu, Kampuni ya uwekezaji ya mtu binafsi, iliyo jifia miaka ya 90, nikajua tayari wewe ni mchekeshaji tu.
 
Eti huo ni uzalendo. Ila siku wakishtuka hao wanaojiita chawa wa chama: walah watapiga mtu mawe hadharani tena kweupeeee
Najua unaandika huku moyo unakuuma sana yani concious yako inakusuta
 
Kweni Chato wanaishi waGanda au waKenya? Yani wabongo bana
 
View attachment 1715798
Maelezo ya Picha: Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja(Kulia) akikagua hoteli ya nyota tatu inayojengwa na Hifadhi za Taifa Tanzania inayojengwa Wilayani Chato mkoani Geita.
Mwalimu Nyerere akijua kabisa kuwa kuku wa taifa lazima aliwe na wote, aliamua almasi inayochimbwa Shinyanga Mwadui ikakatwe Iringa, ili Wanyalu nao wafaidike na madini hayo.

Hakupeleka kiwanda Cha Tancut Almasi Mara wala Butiama.
Magufuli amekuwa ni mtu wa kupendelea kwao tu utadhani Tanzania ni Chato tu.

1. Uwanja wa ndege mkubwa umejengwa Chato
2. Wanyama wamesombwa huko Serengeti, wamepelekwa Chato.
3. Uwanja mkubwa wa michezo kujengwa Chato.
4. Hospitali ya Kanda ya Ziwa imejengwa Chato.
Je, wanaccm mmeshindwa kukemea upendeleo huu?

Mjulisheni Mwenyekiti wenu kuwa anachokifanya sio uzalendo, ila ni ubaguzi. Anawabagua watu wasio wa Chato.

Kuku wa Taifa lazima aliwe na wote, hata watu wa Ileje na Tandahimba wanahitaji kwao kujengwe, sio kila kitu Chato tu

===

Naibu Waziri wa Utalii Mary Masanja akagua miradi ya utalii Geita​

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja amefanya ziara katika Mkoa wa Geita ambapo pamoja na mambo mengine amekagua miradi mbalimbali ya kiutalii inayotekelezwa na taasisi za Wizara ya Maliasili na Utalii mkoani humo, anaripoti John Bera (WMU) Geita.


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (katikati) akiwasili kukagua hoteli ya Nyota 3 ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania ( TANAPA) inayojengwa wilayani Chato mkoani Geita wakati wa Ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi mbalimbali ya Wizara ya Maliasili na Utalii ya mkoani Geita. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Chato, Eng. Charles Kabeho na kulia ni Kamishna Mwandamizi wa Uhifadhi Kanda ya Magharibi, Martin Loibooki.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (kushoto) akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhe. Robert Gabriel kuhusu mpango wa Wizara ya Maliasili na Utalii wa kutaka kuanzisha Utalii wa Madini katika mkoa huo wakati wa Ziara yake ya Kikazi mkoani humo.

Akiwa katika ziara hiyo amefanya mazungumzo na viongozi wa Serikali wa mkoa na wale wa taasisi zilizo chini ya wizara kuhusu namna bora ya kutangaza vivutio vya utalii vinavyopatikana katika mkoa huo.

Aidha, Mhe. Masanja ametembelea Mradi wa Ujenzi wa hoteli ya Kitalii ya Nyota 3 inayojengwa wilayani Chato mkoani Geita na kuagiza ujenzi wa hoteli hiyo ukamilike haraka ili watalii waanze kupata fursa ya kutumia huduma za malazi katika hoteli hiyo na kutembelea hifadhi mbalimbali zilizopo Kanda ya Ziwa.


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (kulia) akiwa anashuka kwenye hoteli ya Nyota 3 ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania ( TANAPA) inayojengwa wilayani Chato mkoani Geita wakati wa Ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi mbalimbali ya Wizara ya Maliasili na Utalii ya mkoani Geita. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Chato, Eng. Charles Kabeho.

Amesema, Wizara ya Maliasili na Utalii itaendelea kushirikiana na uongozi wa Mkoa wa Geita kuhakikisha shughuli za utalii zinasonga mbele huku akitoa rai kwa viongozi hao kuweka mkazo katika zao la asali ambalo amesema likisimamiwa vizuri litaongeza mapato.

"Tuhamasishe zao la asali linalotokana na nyuki, sasa hivi kuna mnyororo mkubwa wa thamani ambao Serikali inaendelea kuupigania kwenye mazao ya misitu, hii itasaidia wananchi kuongeza kipato pia pato la Taifa,"amesema Mhe. Mary.

Aidha, ameongeza kuwa Wizara ya Maliasili na Utalii iko katika mpango wa kuanzisha Utalii wa Madini ambao kwa Kanda ya Ziwa utasaidia kuongeza idadi ya watalii na mapato.
Kwa ujinga wako ulitaka ijengwe wapi ndo ulidhike?
Mapato ya kodi ya watu wa chato ulishayakataa yasitumike sehemu nyingine?
Ni upumbavu kutaka kuonyesha kuwa kuna sehemu tanzania haihitaji kuendelezwa.
 
Asipofanya hivyo majengo mengi Chato yatageuka magofu ndani ya miaka 5 baada ya kutoka.
Ni kweli. lakini hata hivyo majengo kugeuka magofu ni suala la muda tu. Ataishi milele? Jibu ni hapana. Na siku akiwa hayuko tu mambo yataanza kugeuka. Kitu kama ule uwanja wa ndege ni nani atautumia?
 
CCM wanalilia ndani kwa ndani na ole wako machozi yaonekane
 
Back
Top Bottom